Sunday, December 17, 2017

WEWE BWANA, NDIWE BABA YETU!

*WEWE BWANA, NDIWE BABA YETU!*

_*Mwl Proo*_
0762879363

Amani ya Mungu ipitayo akili zote, iwahifadhi!. Nawasalimu nyote kwa jina kuu la Yesu Kristo, Aliye Baba wa milele....

Mungu anaweza kujifunua kwako kulingana na ulivyo au unavyomjua (Zab 18:25-26). Leo Bwana alinijaza kweli hii, kuwa Yeye ni Baba (Our Abba Father). Nilipokuwa katika maombi ya usiku wa manane, nilitumia dakika tano kutamka sentensi *_"Wewe ni Baba yangu"_*, niliitamka until all my situations were inundated by the Truth, kuwa ninaye Baba. Niliamua kumtaja mpaka nafsi, roho na mwili vyote vijawe na hiyo kweli. Nilimtaja Baba yangu mpaka yale mambo yaliyotendeka hivi karibuni na kunishusha moyo, nayo yaka-salute👋🏾👋🏾. Na ingawa huwa ninakuwa na ratiba, nikimaliza maombi, huwa naanza vita katika ulimwengu wa roho, lakini leo nilipoenda kwa Mungu kama Baba, nilimaliza kuomba sikusikia haja tena, ya kufanya vita vya rohoni, My Papa is greater than all enemies out there (1Yoh 4:4), I just relaxed, nikaendelea kumfurahia Baba yangu.

Katika utamaduni wa kiyahudi, Baba/mababa ni kitu kina-matter mno. Na hivyo watu hutaja mababa as an ID, na kiburi kikuu ni pale wanapogundua kwa jinsi ya mwili wako connected na Ibrahimu na yale maagano (Abrahamic covenant).

Luka 19 : 9
*_............Leo wokovu umefika nyumbani humu, kwa sababu huyu naye ni mwana wa Ibrahimu._*

Mathayo 3 : 9
*_wala msiwaze mioyoni mwenu kwamba, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba Mungu aweza katika mawe haya kumwinulia Ibrahimu watoto._*

Yohana 8 : 39a
*_Wakajibu, wakamwambia, Baba yetu ndiye Ibrahimu!._*

YAANI WAYAHUDI ILIKUWA NONGWA, KILA UNACHOWAAMBIA, WAO DEFENCE YAO NI MOJA, TUNAYE BABA!! INGAWA HUYO BABA SI WA MILELE, WALA HAWEZI KUWA NAO KILA MAHALI. BILA SHAKA NA WEWE MSOMAJI UNAYE BABA WA KIROHO, HUENDA ANAKUGUSA MNO, KIASI KWAMBA UKIGUSWA TU UNAMTAJA HUYO FASTA, WELL AND GOOD!! HUENDA UNAYE BABA WA KIMWILI, ULIZALIWA KWAKE, KAMA AMBAVYO MIMI NILIKUWA NAYE, PAMOJA NA KUMPENDA NA KUMFURAHIA KAMA AMBAVYO UNAMFURAHIA SASA ULIYE NAYE, HUYO NAYE SI WA MILELE. SIKU NILIPOSIMAMA MBELE YA JENEZA⚰ NIKIMTAZAMA SURA YA BABA MZAZI, NDIPO NIKAJUA KUMBE NILIKUWA NAKUFURAHIA HAPA NYUMBANI, TUNAPIGA STORI ZA BIBLIA, KUMBE UNANIACHA, MAANA NAYE HAKUWA WA MILELE  (KAMA AMBAVYO ULIYE NAYE SI WA MILELE, HATA KAMA HE LOOKS SO YOUNG AND ENERGETIC 👨🏾💪🏾, IPITE MIAKA 20,30 ETC HE WILL GO), HII SIO KUKUTISHIA, BUT I WANT TO MAKE A TRADE-OFF, ILI TUMTAMBUE MWENYE UBABA WA MILELE YESU KRISTO, MUNGU MKUU NA MWOKOZI WETU (Isaya 6:9), AMETAJWA KAMA *_EVERLASTING FATHER_*

*MOYO WA SOMO*

Pamoja na kile kiburi cha Wayahudi, juu ya kuwa wana wa baba yao ibrahimu kwa jinsi ya mwili, nabii Isaya katika roho akatoa ukiri ambao mimi niliposoma, nafsi yangu ilivutwa kwa nguvu. Tusome;

Isaya 63 : 16
*_Maana wewe ndiwe Baba yetu, ijapokuwa Ibrahimu hatujui, wala Israeli hatukiri; wewe, Bwana, ndiwe Baba yetu, mkombozi wetu tangu milele ndilo jina lako._*

Isaya 64 : 8
*_Lakini sasa, Ee Bwana, wewe u baba yetu; sisi tu udongo, nawe u mfinyanzi wetu; sisi sote tu kazi ya mikono yako._*

HUYU NDIYE BABA TUNAWEZA KUJIJENGEA KIBURI KWA ADUI ZETU, MZEE WA SIKU AMBAYE HANA MWISHO WAKE. HATA WAZEE VIKONGWE 👴🏾👵🏿WA MIAKA 100/90 KWA HUYU NAO WANAJIVUNIA KUWA TUNAYE BABA.  ISAYA ANASEMA, KUWA HUYU IBRAHIMU TUNAYEJIVUNIA WALA HATUJUI, WALE YULE BABA WA TAIFA LETU ISRAEL(YAKOBO) HATUKIRI. MUDA ANAANDIKA HAYO ILIKUWA IMEPITA MIAKA 1300 TANGU IBRAHIMU AFE, LAKINI AKAJUA YUKO MUNGU ALIYE BABA, ANAYETUJALI HUYO NDIYE BABA YETU👈🏾.

*MUNGU KWA ROHO MTAKATIFU AMETUFANYA WANA (WE ARE ADOPTED AS SONS)*

Warumi 8 : 15
*_Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba._*

USIKUBALI KUISHI, NA MUNGU AKIWA KAMA BABA WA KAMBO KWAKO. HUYU NI BABA...FEEL HIM, UKIENDA KUFANYA MAOMBI UKIITA TU JINA BABA/AV/ABBA, UMHISI NDANI YAKO KABISA, UKIIMBA WIMBO WA KUABUDI AU KUSIFU, UKITAMKA BABA, MOYO WAKO UCHOMWE💘 NA FURAHA YA BWANA, KWAMBA UNAYE BABA. INFACT NIMESOMA MAFUNDISHO YA DINI ZOTE KUU ZA DUNIA ZILE 19, IDEOLOGY YA MUNGU KUWA BABA,TUNAIPATA HUKU KWETU TU; YAANI HAKUNA MUNGU ALIYE BABA ILA HUYU YEHOVAH BWANA ALIYEJIFUNUA KWETU KWA YESU KRISTO (YOH 1:18).

🔊 *HUYU BABA YETU, MACHO YAKE HAYATULII, YANAKIMBIA KIMBIA, ILI KUTULINDA* 👁👁
2 Mambo ya Nyakati 16 : 9a
*_Kwa maana macho ya Bwana hukimbia-kimbia duniani mwote, ili ajionyeshe mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake._*

Zekaria 4 : 10
*_naam, hizi saba ndizo macho ya Bwana; yapiga mbio huko na huko duniani mwote._*

AS THE MATTER OF FACT, MUNGU NI ROHO, YUKO KILA MAHALI (OMNIPRESENT GOD), LAKINI AMEAMUA KUTUMIA LUGHA YA KIBINADAMU (ANTHROPOMETAPHORIC LANGUAGE), ILI KUTIA MKAZO WA KAZI YAKE KAMA BABA. HUTASAHAULIKA HATA UTUPWE KIJIJINI, HUTAFICHIKA EVEN IN THE DEAD OF THE NIGHT. YEYE NI BABA, USIWE NA HOFU ✋🏾

🔊 *KWA NAMNA ILE-ILE BABA ANAYOMBEBA MTOTO MIKONONI, PIA MUNGU HUTUBEBA, MAANA YEYE NDIYE BABA YETU*

Kumbukumbu la Torati 1 : 31
*_na huko jangwani, ulipoona alivyokuchukua Bwana, Mungu wako, kama mtu amchukuavyo mwanawe, njia yote mliyoiendea, hata mkafikilia mahali hapa._*

BABA, HUYU AKIONA NJIA UIENDEAYO IKO ROUGH, IKO CROOKED, IMEJAA VALLEYS AND HILLS, ANAKUCHUKUA MIKONONI KWA NAMNA ILE-ILE AMBAYO BABA ANAKANYANYUA KATOTO KAKE👶🏽, ATATEMBEA YEYE ILI WEWE UEE SALAMA.

🔊 *BABA YETU, ANATUBEBEA MIZIGO, KILA SIKU, ILI TUSIWE OVERWHELMED*

Zaburi 68 : 19
*_Na ahimidiwe Bwana, Siku kwa siku hutuchukulia mzigo wetu; Mungu ndiye wokovu wetu._*

KUNA WATU, UNAKUTANA NAO, WAMEOKOKA, ILA WAKO HOI KIMAISHA NA KILA ANGEL YA MAISHA, MAANA MIZIGO YAO WAMEIBEBA WENYEWE, INAWALEMEA, LAKINI HUYA BABA ANASEMA, NJOONI KWANGU NINYI WENYE KULEMEWA....ANAZUNGUMZIA AINA ZOTE ZA MIZIGO, UMTWIKE YEYE ALIYE BABA, TENA YUKO BIZE MNO, AKIJISHUGHULISHA NA MAMBO YETU (1PET 5:7).

UKIISHA KUSOMA HUU UJUMBE, PATA DAKIKA HATA 10, JIFUNGIE UTANGAZIE MAZINGIRA YAKO YOTE NA HALI ZAKO ZOTE, KUWA UNAYE BABA. YAAMBIE MAGONJWA KUWA NINAYE BABA AITWAYE JEHOVAH RAHA (KUT 15:26), KIAMBIE KIFO, KUWA UNAYE BABA ANAITWA MKUU WA UZIMA NAAM YEYE NDIYE UFUFUO NA UZIMA (Mdo 3:15),
ZUNGUMZA NA HUZUNI, KUWA UNAYE BABA, ANAITWA MUNGU WA FARAJA YOTE (2KOR 1:3-11), ZUNGUMZA NA UMASKINI, KUWA UNAYE BABA, ANAITWA MCHUNGAJI MWEMA, HUTAPUNGUKIWA!

ANZA LEO KUMFURAHIA MUNGU, PEKEE ALIYE BABA. TEMBEA NJIANI UKIIMBA KUHUSU BABA YAKO HUYU, UKIMJUA HUYU UNARUHUSIWA KUJIVUNA (YER 9:24, 1KOR 1:31). YAANI HAPA WARINGISHIE MAADUI, NA MATAIFA WOTE, KUWA UNAYE BABA!!!! YAANI NIKIMTAMKA MUNGU NI BABA NAONA SURA YANGU INATENGENEZA SMILE 😊,NINASHUSHA PUMZI YA KUHISI RAHA 😉.

Lyrics By Don Moen 🎤🎼🎹🎸

*_I have known the Father's Cares for me. He's been goodX2,Through it all He is always there for me, God's been good to me.Through the storm, through the night,come what may, everything will be alright..._*

MUNGU BABA WABARIKI..

Mwl Proo
(Prosper Kadewele)
0762879363(ATG whatsapp group)

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment