Friday, December 8, 2017

MWILI NI WA KRISTO

*BིAིLིIི MིWིIིLིIི NིIི WིAི KིRིIིSིTིOི*

_*Mིwིlི Pིrིoིoི*_
*0762879363*

Shalom Shalom!
Hii ndiyo jumla ya maneno, yote yamekwisha sikiwa, imewafaa leo kuwaandikia hili. Nyakati hizi zimekuwa na shida kubwa ya wataabishaji, wenye juhudi ya kubeza na kutafuta kuwaweka watu katika kuchanganyikiwa kwa hoja zisizo na elimu (2Timotheo 2:23). Kuna watu wenye masikio ya utafiti, wanatamani kufanya midahalo tu (debating), wao ni watu wa kubeza tu mafundisho mengine, hali hawafundishi hiyo wanayoidai ndiyo kweli. Watu hawa wata-challenge kunena kwa lugha mpya (Speaking in tongues/new languages), kwamba mbona wanavyonena hawa wa sikuizi inafanana duniani kote, mbona hawatafsiri, lakini wao hawaoneshi hiyo ya kunena halisi ikoje, iko wapi? na je! waliisikia hiyo ya kwanza ilikuwaje? na je! kunena kwa lugha kupo kwa aina ngapi?. Nilikutana na wakristo wa kanisa fulani, wao walini-challenge kuhusu kukemea&kutoa pepo wachafu, kwamba ni kwa andiko lipi naagizwa kufanya hivyo? wakaniambia hii Marko 16:17 iliwahusu wale mitume, na ilitimia tayari katika Marko 16:20, kwa hiyo wakasema tunachofanya waamini wa leo ni *exorcism* ya kupunga pepo kama wana wa Skewa tu. Kwa wakati mmoja hawa wanaodai nikitoa pepo kwa jina la Yesu siko sahihi, wao walijinadi kuwa wafuasi wa moja ya wahubiri wa kiuamsho W.M Branham wa mwanzoni mwa karne ya 20, nikashangaa wanayedai kumwamini kama mjumbe wa Mungu kuwa ndiye malaika wa 7, huyo alitenda kazi hizi, wao wana-challenge miujiza, ila wanayemwamini alitumiwa kwa hizo kazi. Si hawa tu, bali kumekuwa na uvumi mkali wa watu ambao ni kama wana lengo zuri, maana watainuka wakikosoa kwa kubeza kila fundisho, kila kazi inayofanywa na waamini, kila matendo ya ibada, ila wao wenyewe hawatendi, hawaoneshi hiyo halisi/kweli ni ipi, kwa namna ileile ya mafarisayo (Luka 11:52ff). Paulo mtume katika zama zake, alikutana pia na mafundisho na mambo mengine yasiyo sahihi, kama Mwalimu wa mataifa, hakujihusisha kufanya hii kazi inayofanya na hawa wakosoaji na wabezaji wa leo. Paulo mtume alijadili hoja yenye shida kwa kuufundisha usahihi wake. Kwa mfano kulikuwa na watu wanafundisha hakuna kiama ya wafu, na kulikuweko na wengine mahala pengine walifundisha kwamba kiama ya wafu tayari. Mtume Paulo alifundisha usahihi wake, ili watu wayapime hayo kwa yale mengine (1Korintho 15:12-58). Hii ndiyo njia naitazamia kwa mtu ambaye kweli anafanya kazi kama kwa Bwana. Nitarudi hapa kuja kuendelea....

Nimesukumwa kuyaandika haya nilipokutana na andiko moja katika Wakolosai.

Wakolosai 2 : 17
_*mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.*_

Andiko hili limebeba mambo makubwa sana, ingawa lina muunganiko na vitu vilivyotajwa juu vya Torati na kweli ya Agano lililo bora, lakini ngoja nikuoneshe kitu kingine. Hapa panapotajwa mwili ni wa Kristo, katika tafsiri za asili za Kiyunani zimetaja neno *πραγματικότητα* linalosomeka  *pragmatikótita* yaani *KITU HALISI/Reality*  ni Kristo, na katika Strong Greek Concordance imeeleza neno hili lina maana sawa kimatumizi na Neno *ἀλήθεια* linalosomeka *alétheia* yaani *TRUTH/Kweli*, neno hili ndilo linaloitaja ile Kweli ya Mungu, kwa kusema hivyo kuna vivuli *skia*, na kuna Kweli yenyewe ambayo ni Kristo, yaani kutakuwa na blabla zingine lakini mwili/real substance yenyewe ni Kristo.

Hapa sasa hakuna mwamba, maana ni wazi tu kwamba mafundisho ya madhehebu mbalimbali yanaweza kuwa na makosa fulani fulani, either kwa kukosa ufunuo kamili, au fundisho kujengwa juu ya *Dogmas* zenye makosa, Yeye aliye wa ile Kweli, atafundisha usahihi, na walio wa ile Kweli wataisikia tu (Yohana 18:37b), wanaopendezwa na midahalo, go on debating, endeleeni tu  juu ya mizozo ya mambo ya kidini , lakini mimi kwa uzoefu wa kiimani, kweli ya Mungu haifikiwi kwa debates (Ni tofauti ni ile ishu ya Baraza la Yerusalem katika Matendo 15). Hata mimi nikiona kuna hoja yenye utata nitajitahidi kutumia kwa halali neno la kweli kuifundisha. Sasa nyakati hizi kumeinuka watu ambao kwa nje ni kama wana nia njema, lakini watu hawa wanatumiwa tu kuleta *Confusion*, maana wakiisha kubeza hawafundishi hiyo kweli, unfortunately wachache wanaojaribu kufundisha nao unaona wazi wame-base kwenye dogmatic ideologies ambazo pia hazina msingi wowote. Mmoja kati ya watu ambao alijaribu kutuaminisha kuwa hapa duniani kuna uzao wa nyoka, uliotokana na Kaini, kwa madai kwamba Eva alisex na Nyoka 👧🏽❤🐍 akazaliwa Kaini, alijitahidi kutumia maandiko mengi kutuaminisha hilo. Badae nikafikiri hivi hiyo wasted energy ya mdahalo inazaa nini. Katika kutafakari nikapata hoja ya msingi sana, kwamba ipo kweli kamili, kipo kitu halisi cha imani hii. Hilo ni la muhimu kuliko hizo debates zisizo zaa matunda, hawa wapenda Debate mara nyingi hawana habari za Kristo, hawana maneno ya uzima, hawana ile kweli, wengine tangu nikutane nao nikiwa shule ya sekondari miaka ya 2004 mpaka leo nikikutana naye bado anahoja kuwa unaabudu siku ya jumapili,ni siku ya Mnyama yule wa Ufunuo 13, Nilikwisha achaga debates na watu hawa, maana cha ajabu ukikaa na wabezaji wote, humwoni Kristo kwao, huoni akijidhihirisha kwao kwa lolote, maana kama wanayoyakazinia ndio mwili halisi basi tumwone Mungu akitembea kati yao, sasa hawa watu in their practical ministry hamna uhai wowote,mtu akipagawa hata pepo, inabidi tuwasaidie tena kutoa. Mitume wa Yesu hawakuwa na elimu dunia, hawakuwa na ujuzi mkubwa wa Torati kuwazidi mafarisayo na wakuu wa dini, hawangeweza kushindana nao kidini, lakini wakuu wa dini walisaliu amri,kwamba hawa watu aisee wako na Yesu haswaaa (Matendo 4:13). Maana wanafunzi hawakudili na vivuli,walikuwa na mwili wenyewe, hivyo enyi wabezaji tunatamani tumwona Kristo na kazi zake kwa mafundisho yenu basi.

Hata sasa kunaweza kuwa na mambo mengi ya ujuzi, kama ambavyo wale wakosoaji na wabezaji, hata ikitokea wanafundisha kidogo ni kwa majivuno makuu (1Korintho 8:1b), lakini mengi ya yale yanayoshindaniwa si Mwili wenyewe. Kuna watu wataurithi Ufalme wala hawakupoteza muda na mashindano ya maneno (Debates), Ila walimpata Kristo (Mwili wenyewe, aliye Kweli kitu halisi), wakatembea naye huyo, wakafika!. Wanaweza kuwa hawakuweza kueleza kwa kina mambo mengine ya dini na ya madhehebu na mabishano yake.

Huenda bado hujajua nalenga nini katika andiko langu hili. Nisemalo ni hili ni vyema kuendelea kujifunza,kutafuta kuijua kweli,lakini usipotezewe muda na wataabishaji, ambao wao wenyewe hawamwoni Mungu, wamesalia na akili za kidhehebu tu, kweli haipo kwenye dhehebu wala mdahalo, Wewe uliyeamini katika Kristo Yesu kabisa kabisa, Yesu akajifunua kwako, akakujaza na Roho wake Mtakatifu unacho kitu halisi, mwili wenyewe.... Kwa njia hiyo unafanyika mtoto wa Mungu (Yoh 1:12, Rumi 8:16-17), Hicho ulicho nacho ndicho cha kushikwa haswaaa. Usirudishwe nyuma kutilia mashaka mambo uliyoyapokea kwa Bwana. Kwa mfano mimi sihitaji debate ya kujadili kunena kwa lugha ili ninene au niache kunena, maana tukio lililotokea kwangu tarehe 29/8/2004 nilipojazwa Roho Mtakatifu kwa nguvu kubwa na nikaanza kunena kwa lugha mpya bila maelekezo wala debate, ila niliuhakikisha uwezo ule kwa namna zote ndilo lile nilisomalo katika maandiko mtakatifu. Kwa hiyo kama Mungu alinipa kipawa bila mdahalo, nitaanzaje leo kujadili kwa mdahalo ili kupata usahihi wa ninene au nisinene. Na hata hawa wtaabishaji wanaojaribu kuweka kikwazo kwa sehemu kubwa wamekosa ufunuo, maana haya mambo tumeyapata kwa kufunuliwa (Efeso 3:3), and the other side wamekosa hata elimu tu ya kuyafasiri maandiko, mtu anayehoji mbona kanisani kwenu mnanena wengi, Paulo Mtume alisema wanene wawili watatu na mwingine afasiri.... Hoja hizi zisiwanyamazishe, tatizo ni  hao wabezao walikosa elimu tu. Hawana ujuzi wa msingi wa kutafsiri maandiko kujua kuwa Paulo aliandika barua kwa Wakorintho akijibu barua zenye maswali alizokwisha tumiwa,and Paulo was trying to settle some disputes katia kanisa hilo, ili kuweka harmony, je! tunayo hali ileile iliyoikuta kanisa la Korintho? ili kukopi kila kitu? Je kila kunena kwa lugha kunahitaji tafsiri? mtayatupa wapi maandiko kama (1Kor 14:2, 14)?, tjnawezaje kupachika maandiko out of context huku tukidhani tunaelekeza ukweli?. Niwavunje tu moyo wataabishaji ambao furaha yao ipo kwenye ku-challenge kila kitu, huku wenyewe wakijiona ni waberoya eti, ha ha ha ha😁, kwanza wangeelewa tabia ile ya waberoy ilijengwa na msingi upi, wasingejisifu kwa kujipachika jina la uberoya, Mji wa Berea uliopo Macedonia, Kaskazini mwa Ugiriki, kulikuwa na falsafa nyiiingi zilizo waundia worldview ya namna ile, wiki wemo zile za skepticism,zilizowafanya wa-doubt kila kitu,of which haiendani sana na maana ya maisha ya imani. Ni kweli si vyema kuwa ni watu wa kujibu Ameeeen,kwa kila kitu, lakini pia hatuishi kwa kuwazia maneno ya ushindani, huku ukijidhania nafsi yako imefika. Mimi nayajua mafundisho yenye makosa hata yaliyo katika madhehebu ya kipentoste, lakini hata hayo sio mwili wenyewe, kukiwaa fundisho ambalo halijabalansi linaweza kuwa kwazo, likapunguza sehemu ya utendaji, lakini Mungu yuko Hai, na amemwachilia Roho Mtakatifu wa kututia katika kweli yote, hapo napo kuna process (Yohana 16:13).

So to say ni kazi yako leo,kujua kuwa mwili (kitu halisi/kweli) ni wa Kristo. Kama tukianza kuassess mafundisho yote ya madhehebu na dogmas zao, lazima tutapata makandokando mengi tu, Ni dhehebu gani basi, litajinadi kuwa wao ndio sahihi peke yao kwa mafundisho? hata wale wanaodai kwamba Protestant Churches are not pure Protestant,ila wao ndio halisi, nao wana maudambudambu kibao ya kimafudisho, ila kama kuna jambo linaweza kuwa na maana ni Kristo mwenyewe. Na ninajua jinsi iivyo kazi kubadili doctrine ambayo tayari imemezwa. Ila wale wabezaji pokeeni maarifa mapya, cha msingi ni kuifundisha kweli, ila hiyo ajira ingine wala hata sio kazi ya Mungu... iko jamii ya watu wa Mungu, inaitwa jamii ya waaminio. kuna mambo ya msingi yanaiunganisha jamaii hii (Efeso 4:4-5), wala usitarajie kwamba kuna wakati mtafanikiwa kufanya *MERGING* ya all dogmas and doctrines, Never! Kanisa la Korintho lilikuwa na divisions fulani,wengine wakijinadi ni wa Paulo, wengine wa Kefa, wengine wa Apolo etc,ni wazi kwamba kuna namna hawa watumishi mababa walitofautiana vitu fulani.

2 Timotheo 2 : 14
*Uwakumbushe mambo hayo, ukiwaonya machoni pa Mungu, wasiwe na mashindano ya maneno, ambayo hayana faida, bali huwaharibu wasikiao.*

1 Timotheo 6 : 4
*amejivuna; wala hafahamu neno lo lote; bali ana wazimu wa kuwazia habari za maswali, na mashindano ya maneno, ambayo katika hayo hutoka husuda, na ugomvi, na matukano, na shuku mbaya;*

Mwl Proo
0762879363
alltruth5ministies@gmail.com

No comments:

Post a Comment