Sunday, December 17, 2017

KAA NA LADHA YAKO WALA HARUFU ISIBADILIKE

🇦 🇱 🇱     🇹 🇷 🇺 🇹 🇭

*KAA NA LADHA YAKO WALA HARUFU ISIBADILIKE*

_Mwl Proo_
*0762879363*
0718922662

Haleluya!
Bwana analo Neno kwa ajili yetu leo, na neno lake kwako ni hili *_"kaa na ladha yako,wala harufu yako isibadilike"_*

*Yeremia 48 : 11*
*_Moabu amestarehe tangu ujana wake, naye ametulia juu ya sira zake, wala hakumiminwa kutoka chombo kimoja kutiwa chombo kingine, wala hakwenda kufungwa; kwa hiyo ladha yake anakaa nayo, wala harufu yake haikubadilika._*

UNAJUA SISI NI MATAWI TULIOPANDIKIZWA KTK SHINA JEMA YESU KRISTO(INGRAFTED BRANCHES) Warumi 11:11-24  Sasa ule umwitu unaondoka,kila mtu akikutana na Yesu anakuwa na *taste* na *smell* mpya ya namna yake,hiyo ladha na harufu imetokana na shina Yesu Kristo,Sasa Mungu anatazamia hiyo ladha yako ukae nayo na ile harufu isibadilike,bila kujalisha mabadiliko ya mazingira au mambo mengine.

Mimi ni mwalimu wa Jiografia,kuna kitu tunakiita *_River Regimes_* haya ni mabadiliko ya ujazo wa maji ya mto na tabia zingine za mto,kwa mfano mto Nile umeanzia ktk Ziwa Victoria,unasafiri mpaka Misri unakoenda kumwaga maji yake ktk bahari ya Mediterania. Huu mto ktk safari yake unabadili sifa(ladha na harufu) Ukienda kuupima huu mto hapo Uganda una kuwa na properties(sifa) tofauti na zile ambazo mto huu unazo unapofika Sudan(yaani hata Chemical composition yake hubadilika) ,unaweza kupima kiasi cha asidi/alkali kwa kutumia pH-scale ukahisi ni mto mwingine tena usiotoka Ziwa Victoria.

*MUNGU ANASHANGAA AKIONA UMEBADILIKA LADHA NA HARUFU*

*Yeremia 2 : 21*

*_Nami nalikuwa nimekupanda, mzabibu mwema sana, mbegu nzuri kabisa; umegeukaje, basi, kuwa mche usiofaa wa mzabibu-mwitu machoni pangu?_*

*Isaya 1 : 21*

*_Mji huu uliokuwa mwaminifu umekuwaje kahaba! Yeye aliyejaa hukumu ya haki; haki ilikaa ndani yake, bali sasa wauaji!_*

*UKIACHA KUKAA NA LADHA YAKO, NA HARUFU YAKO IKABADILIKA,HAUBAKI NA UTUKUFU SAWA*

1.Shetani alikuwa anakaa na ladha na harufu fulani ila akaacha kukaa nayo hata kubadili harufu yake

*Isaya 14*

*_11 Fahari yako imeshushwa hata kuzimu,Na sauti ya vinanda vyako;Funza wametandazwa chini yako,Na vidudu vinakufunika._*
*_12 Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni,Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi!Jinsi ulivyokatwa kabisa,Ewe uliyewaangusha mataifa!_*

*Ezekiel 28*

*_13 Ulikuwa ndani ya Adeni, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako, akiki, na yakuti manjano, na almasi, na zabarajadi, na shohamu, na yaspi, na yakuti samawi, na zumaridi, na baharamani, na dhahabu; kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako; katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari._*
*_14 Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto._*
*_15 Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako._*

2.Taifa la Israel lilipoteza ladha na kubadili harufu wakati fulani

*Maombolezo 4*

*_1 Jinsi dhahabu ilivyoacha kung'aa?,Na dhahabu iliyo safi ilivyobadilika!Mawe ya patakatifu yametupwa mwanzo wa kila njia._*
*_2 Wana wa Sayuni wenye thamani,Walinganao na dhahabu safi,Jinsi wanavyodhaniwa kuwa vyombo vya udongo,Kazi ya mikono ya mfinyanzi!_*
*_3 Hata mbwa-mwitu hutoa matiti,Huwanyonyesha watoto wao;Binti ya watu wangu amekuwa mkali,Mfano wa mbuni jangwani._*
*_4 Ulimi wa mtoto anyonyaye wagandamana na kaakaa lake kwa kiu;Watoto wachanga waomba chakula,Wala hakuna hata mmoja awamegeaye._*
*_5 Wale waliokula vitu vya anasa wameachwa peke yao njiani;Wale waliokuzwa kuvaa nguo nyekundu wakumbatia jaa._*

*_7 Wakuu wake walikuwa safi kuliko theluji,Walikuwa weupe kuliko maziwa;Miili yao, walikuwa wekundu kuliko marijani,Na umbo lao kama yakuti samawi._*
*_8 Nyuso zao ni nyeusi kuliko makaa;Hawajulikani katika njia kuu;Ngozi yao yagandamana na mifupa yaoImekauka, imekuwa kama mti._*

PIA KTK MAANDIKO TUNASOMA WENGI WALIOACHA KUKAA NA LADHA ZAO NA KUBADILI HARUFU. LAKINI SASA TUYATATHMINI MAISHA NA SAFARI YETU, JE TUMEKUWA NA VARIATIONS KAMA ZA ULE MTO _"RIVER REGIME"?_ ,WENGI TASTE/SMELL ZIMEBADILIKA/SHWA ATI NA NDOA,KADIGRII KAMOJA ETC,HUYU ALIYEKUWA NGUZO YA HUDUMA FULANI CHECH AMEOA TU AKABADILI HARUFU,KUNA MABINTI WALIKUWA WAKIIMBISHA MAKANISANI ILA HIYO HUDUMA ILISITISHWA NA KUOLEWA,HUPASWI KUACHA KUIHUDUMIA NDOA KWA SABABU ZA KIHUDUMA NA PIA HAUNA SABABU YOYOTE YA KUACHA HUDUMA(MAMBO YOTE YAFANYIKE KWA UZURI NA KWA UTARATIBU-1kor 14:40),KUNA VIJANA WALITUMIKA VIZURI SANA WAKIWA TAASISI ZA ELIMU,ETI WALIPOPATA KAZI *_WAMEKOMAA HADI WAMEKOMA_*  WALISHASAHAUGI KAMA KUNA KITU KINAITWA HUDUMA NA KUJITOA KWA BWANA. WAMEBAKI NA HISTORIA TUU,TULIWAHI KUFANYA GOSPEL OUTREACHES MAENEO YENYE NGOME ZA UCHAWI,TULIKUWA TUNAFUNGA SANA AISEE TUKIWA CHUONI,MWINGINE ALIKUWA MWALIMU MZURI WA NENO,ILA KWA SASA HAKUMBUKI MARA YA MWISHO NI MWAKA GANI ALISIMAMA KUHUDUMU,ULIPOKUWA UNAHUDUMU ILIKUWA NJIA NYEPESI YA KUJIJENGA NAFSI YAKO PIA,KWA WALE WAHUBIRI NI MASHAHIDI KUWA KUNA MUDA UPO KWENYE DALADALA🚌LAKINI KWA KUWA KIKOMBE CHA ROHONI KIMEFURIKA UNAJISIKIA NAFSI YAKO UNAENDELEA KUHUBIRI, SASA HAYO UKAYAACHA NDIO MAANA IJAPOKUWA ULIZALIWA UPYA ILA UNAJIJUA UNAVYOSHINDANA NA MWILI,😃YAANI NGOMA YA DIAMOND PLATINUMS 🎤🎼🎹🎸IKIGONGA UNAANZA KUTIKISA KAMGUU THEN KAKICHWA THEN MOYO,KISHA UNAUDAUNLOD,KWELI WEWE KAKA MWINJILISTI ULIKUWA NI WA KUKAA NA WIMBO WA ALI KIBA KWENYE SIMU📱 YAKO? *UMEACHA KUKAA NA LADHA YAKO. HIVI SI WEWE ULIJAA MISTARI YA MOYO KAMA ULILISHWA BIBLIA,SASA MBONA LEO HATA KIFUNGU CHA MATHAYO 5:8 HUKIKUMBUKI KILE KIFUNGU ULICHOKIKARIRI TOKA MWAKA 1986 KWENYE SUNDAY SCHOOL YA WATOTO👶🏾,. YOU ARE NOW A BUSY BUSINESS MAN😱😱😱 WITO WAKO MKUBWA NI MAFANIKIO YA DUNIA HII🌍,NA KWA KUWA UMEKUWA MATERIALIST SASA UNAWAHI KUTUMA ZAKA KWA M-PESA ILI KUMVUNGA MCHUNGAJI ASIKUHOJI SANA KUHUSU YOUR ABSENTISM. NA MAKANISA YALIBADILI HARUFU, YAANI MSHIRIKA HAI SIO MWENYE KIROHO SAFI BALI ANAYETOA ZAKA HATA KWA KUTUMA TUU KWENYE NAMBA YA SIMU HUKU NI DODGER MZURI IBADANI,WAPENZI HII NI AJABU SANA. NILIENDA KANISA FULANI NIKAKUTA WALE WENYE AJIRA RASMI WAKO EXEMPTED KUJA IBADA ZA MID-WEEK DAYS, AKU😕 NANI KASEMA?? MIMI NI MTUMISHI WA
SERIKALI, ILA SIJAWAHI PATA SABABU YA KUHALALISHA KUKOSA IBADA YOYOTE, WEWE UNAYEFANYA FANYA OVERTIME ILI UPATE KALE KAELFU 40 USISINGIZIE KAZI WALA SERIKALI, NI WEWE ULIPOFANYA OPPORTUNITY COST YA IBADA NA ILE POSHO YA OVERTIME, .MUNGU ALIZIDIWA KETE.

NI NANI MTU YULE AMBAYE BAADA YA KUINULIWA ATABAKI NA QUALITIES ZAKE(LADHA/HARUFU)?  .MWAKA 2006 NILITEMBELEA IRINGA NIKAKUTANA NA JAJI MMOJA (LATE JUDGE UZIAH) WA MAHAKAMA YA RUFAA, ANAHUDHURIA IBADA ZOTE ZA MID WEEK DAYS, HADI MIKESHA YA VIJANA ANAKUJA ILI APATE MUDA WA KUTOSHA NA MUNGU TENA STYLE YAKE YA KUOMBA ILIKUWA ANALALA FLAT KIFULIFULI🚼,HUKU NJE YA KANISA KUNA SHANGINGI🚘ZILE ZA HERUFI MOJA SIJUI J25 NA MAASKARI. SASA HUYU JAJI ALIMENTEINI LADHA NA HARUFU PAMOJA NA KUINULIWA SANA MAANA  KIKWETE ALIMTEUA CHEO FULANI HIVI.

NB
UNAPOACHA LADHA YAKO NA KUBADILI HARUFU KAMA ULIKUWA SILVER OBJECT(CHOMBO CHA FEDHA UNAWEZA KUBADILISHWA UKAWA CLAY OBJECT (CHOMBO CHA UDONGO)  NA KUMBUKA THAMANI NA HESHIMA YA VYOMBO HAIFANANI (2TIM 2:20-21)

*PATA MUDA UTAFAKARI KUHUSU LADHA YAKO UNAKAA NAYO NA JE HARUFU YAKO HAIJABADILIKA?*

UNAYO NAFASI YA KUMLINGANA MUNGU, ILI AREJEZE ILE LADHA NA HARUFU YAKO.

Mwl Proo
0762879363(Whatsapp#)

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment