Friday, June 5, 2026

IMANI YA DINI IPI NI SAHIHI?

*IMANI KATIKA MUNGU-JEHOVAH NA BWANA YESU KRISTO NDIYO ILIYO YA KWELI NA TAKATIFU SANA*

*_By Mwl Proo_*
0762879363

©2014

Bwana Yesu asifiwe sana! Nakukaribisha ktk mfululizo wa somo hili ambalo ni ufunuo nilioupata kama zao/product baada ya kujifunza kwa kina kuhusu misingi ya dini kuu 19 za dunia (19 world major religions) na matabaka(subdivisions) 270 ya kidini duniani. Na ingawa mimi ni Mkristo ila ktk kutafuta kuzijua,nilifanya kama mwanafalsafa anayesimama kati/nje ili afanye upembuzi sahihi (Radical Objectification of Reality),Ingawa pia niliimulika imani hii in the light of other religions,Nikatoka na hitimisho hili *_The faith in God-Jehovah and the LORD Jesus Christ is the most trustworth and most holy faith_*

*IMANI HII NINAYOITAJA KUWA NDIYO YA KWELI NA TAKATIFU SANA*

*Yuda 1 : 20*-
*_Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo TAKATIFU SANA, na kuomba katika Roho Mtakatifu,_*

✝Imani hii ilikuwepo kabla ya anguko la mwanadamu (Mwanzo 1&2)
✝Imani hii Mungu aliiahidi siku ile ya anguko (Mwanzo 3:15/Gal 4:4) kwa kuahidi uzao wa mwanamke yaani Yesu
✝Baada ya anguko imani hii ilikuwepo,maana kuna kizazi cha walioliitia jina la BWANA (Mwanzo 4:26)
✝Imani hii ilikuwepo wakati wa Nuhu. Katika 2Petro 2:5 ,Nuhu anatajwa kuwa ni mjumbe wa haki(Preacher of Righteousness) Aliihubiri haki ya Imani hii,
๐Ÿ”ดKulitokea imani/dini nyingi  nyakati hizi kuelekea wakati wa Ibrahimu na yule Babu Africa a.k.a (Nimrod) Mwanzo 10:8-12 anatajwa kama mwanzilishi wa ibada za sanamu(idolatry)
✝Mungu akaitenga imani hii kwa kupitia Ibrahimu na vizazi vyake(Mwanzo 12:1ff)
✝Imani hii ilibaki kwenye kusanyiko la watumwa waliokuweko  huko Gosheni,na kwa kuwa inakuwa ndani ya watu haikubaki Kanaani.
✝Imani hii ilikuwa na kusanyiko la watu laki 6(wanaume)approximately milioni 2 waliosafiri jangwani
✝Imani hii iliendelea nyakati zote za wafalme na manabii(Ndani ya kapu kubwa la dini ya Kiyahudi/Judaism)
✝Hii ndiyo Imani ambayo Yesu alikuja kuieleza kwa ufasaha,na mataifa tukaipokea imani hiyo kwa neema tu

*SIFA ZA IMANI HII*
Ni muhimu kutambua kuwa,imani zote ambazo mwanzilishi wake si JEHOVAH BWANA/YESU KRISTO,basi hiyo imani ni kazi ya Adui Shetani aliyeitwa Lucifer hapo mwanzo kwa kupitia idara yake ya "FALME NA MAMLAKA" ngazi ya pili ya cheo toka kwake, Na Shetani huyu ni mmoja tu anayejidhihirisha tofauti tofauti, NI HUYO HUYO NDIYE ALIYEJIFUNUA KAMA *ALLAH* KTK UISLAMU,LAKINI NDIYE HUYO HUYO ALIYEJIFUNUA KAMA *KAMI* KTK DINI YA SHINTO,NI HUYO HUYO ALIYEJIFUNUA KAMA *VISHNU* NA PIA GODESS OF INDIA KTK DINI YA HINDUISM, NI HUYO HUYO ALIYEJIFUNUA KWA *Deo De Jing (Tao Te Ching)* kwenye TAOISM dini kubwa ya China, Ni yeye Shetani huyohuyo aliyejifunua kwenye dini ya SIKHISM kwa wale *GURUS*  na kama *TIRTHANKARAS* ktk BAHA'I na kadhalika na kadhilika. Najua it sounds so harshy, kisa tunakariri kuwa Mungu ni mmoja katika kutafuta amani kijamii ecumenically.

✝Ni imani pekee yenye *kweli yote*(Yohana 16:13) Haina utata(innerate and infalliable faith)

*TUILINGANISHE NA IMANI ZINGINE* 
Imani hii imeeleza vizuri kuhusu uumbaji wa Mungu(Genesis 1&2)  lakini ktk Dharmic faiths kuna historia ya uumbaji (Babylonian Creation story) iitwayo *_Enuma Elish_*
Ambapo wanaaeleza kulikuwa na Two giants mmoja aliitwa Marduk(Merodaki mungu wa Babeli/ Yeremia 50:2) na mwingine aliitwa Tiamat ,na kwamba hawa waligombana ila huyo Marduk akamshinda Tiamat akamkata ๐Ÿ—กvipande viwili na kipande  cha juu ndiyo mbingu/anga na kipande cha chini ardhi yaani dunia. Huu ni mfano mmoja tu wa namna Imani hii imetakasika sana kwa habari ya kuwa na Kweli yote.

✝Ni imani pekee yenye tumaini la kweli
>Hatujaachwa bila taarifa yakini,Mungu wetu ametujulishaa yote,Tunajua tutokako na tuendako

Imani nyingine hazina tumaini la kweli
Mfano imani nyingi ktk Dharmic faiths hazina fundisho la Mbinguni na Kuzimu. Mfano hai ni Hinduism wao wana fundisho lao la *_SAMSARA_* yaani rebirth/reincarnate .Wanaamini mtu akifa anazaliwa tena. Mara nyingi ule mwili wa kwanza wanauchoma moto,Ila wanafundisha kwamba ukiishiaisha mema,basi ukifa unazaliwa tena ukiwa ni mwanadamu mwenye viwango vya  juu,kama ulikufa huna utajiri kabisa ila ulitenda mema,basi ukizaliwa tena unakuwa hata waziri mkuu etc,lakini kama uliishi maisha maovu ya ubakaji uuaji n.k basi unaweza zaliwa ukiwa paka๐Ÿˆ nyau๐Ÿ‘‰๐Ÿพ๐Ÿ˜พ Au mdudu๐Ÿœ etc etc
Sasa sisi ktk Imani hii tumetanabaishwa vyema kwa habari ya yote baada ya maisha haya(Ukweli ambao kama maandishi ya Biblia hayatoshi,Basi Bwana anawaonesha watu hata kwa maono ya wazi)

✝Ni imani pekee yenye kuushinda ulimwengu,tamaa zake na maovu yote
*1John 5:4*

*_Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, HIYO IMANI YETI._*

✝Ni imani hii pekee ndiyo inayoufanya ulimwengu/dunia iendelee kuwa salama(it sustains the world)
Earth Science proves that the world is not static,its existence us uncertain,mambo kama natural catastrophes,global warming,nuclear threats etc etc yanatishia uwepo wa planet  earth

MAMBO MATATU
*Kiapo cha Mungu kwa mtu mmoja aliyeishika imani hii (Mwanzo 8:21)
*Watu wa imani hii kwa kuwa bado wapo duniani (Mathayo 24:22,2Thes 2:6)
*Mungu ameiweka๐ŸŒakiba kwa moto,so inalindwa (2Petro 3:7)

*TUKIINGIA KTK IMANI TUNAPASWA KUFANYA NINI?*

✝Kujijenga na kuongezeka hata kufikia kwenye kimo cha cheo ch utimilifu wa Kristo (xv✝Kuendelea kumjua Bwana (Hosea 6:3,Ayu 22:21)
✝Kuishindania Imani hii(Yuda 1:3)

*FAIDA ZA KUWA KTK IMANI HII*

✝Ni watu wa imani hii pekee ndio wanaoingia mbinguni (Kondoo wa zizi lolote lingine sharti waletwe ktk zizi la imani hii๐Ÿ‘‰๐ŸพYohana 10:16)
✝Ni watu wa imani hii pekee ambao mbingu zina *_full control_* juu ya yao. Ufalme wa giza hauwagusi ili kuwadhuru Mathayo 10:29-30,1Yohana 5:18-19
>Hawawezi kufa *_prematurely_* kwa mapenzi ya Shetani,kwani wako malaika(wakalimani) mmoja kati ya elfu wanazuia hatari zote juu yao (Ayub 33:23-25) Maana duniq yote hukaa kwa yule mwovu(1yoh 5:18-19) ,mara baada ya anguko,Shetani alitawala vyote juu ya mwanadamu, .Yesu aliitangua hiyo mamlaka kwa wamwaminio. 
So to say,watu wa imani hii ndio wali salama kuliko yeyote ktk dunia hii mbovu(Gal 1:4)

Dini kuu zote  19 na matabaka ya kidini 270 yanagawanywa ktk makundi  manne kimsingi yaani kulingana na namna wanavyoamini kuhusu Mungu/Uungu
1.DEISM;wanaamini Uungu/Mungu aliuumba ulimwengu,akaufanya uanze kazi zake(functioning),lakini haendelei kujishughulisha nao
2.PANENTHEISM; Huamini uungu ni sifa ya kiroho ya kila kitu duniani lakini pia ipo nje ya dunia
3.PANTHEISM;Huamini kila kitu ulimwenguni kina sifa ya kiroho ya uungu ila hiyo sifa haipo nje ya ulimwengu.
4.THEISM;Huamini Mungu aliumba ulimwengu na anaendelea kujihusisha na shughuli za dunia na wanadamu.

Hili kundi la nne(THEISM) lina matabaka matano pia yaani
1.DUOTHEISM; Wanaamini ktk miungu wawili wenye  kukadiriwa kuwa na nguvu sawa.
2.HENOTHEISM; Wanaamini Mungu mmoja mwenye miungu wasaidizi wengi
3.MONOTHEISM; Wanaamini ktk Mungu mmoja ambaye ni Mungu mme/Male Deity
4.POLYTHEISM; Huamini miungu wengi wake/waume male and female deities
5.TRINITY; Huamini nafsi tatu ktk Mungu mmoja,hii ni aina ya ile Monotheism pia

NB:
YAKO MAKUNDI MATATU YALIYO KINYUME NA MISINGI YOTE YA IMANI TAJWA HAPO JUU

A.)AGNOTICISM;Hili ni kundi ambalo halijafanya maamuzi kuamini kwamba kuna uungu au la .
B.)ATHEISM; hawaamini chochote kuhusu Mungu
C.)STRONG ATHEISM; Hawa wako extremely and fanatic ktk kukataa kuhusu kuwepo kwa Mungu

*DINI MBALIMBALI NA MISINGI YA IMANI ZAO*
Pamoja na makundi tajwa hapo juu,kuna makundi mawili zaidi ambayo yanatokana na wapi imani hiyo iliasisiwa ikiwa na mshikamano(affiliation) na mzizi gani.Kwa hiyo tunazo 
Abrahamic Faiths(Judaism,Islam and Christianity)  na pia tunayo Dharmic Faiths.Ingawa asili yake ni India (Hinduism) lakini neno hilo linatumika kuzieleza dini zote za mashariki ya kati na mbali (Buddhism Hinduism,Jainism,Shinto,Taosm,Sikhism) Etc etc

TAKWIMU ZINAONESHA KATI YA DINI KUBWA 19 THE MOST POPULAR   
NI HIZI, KATI YA WANADAMU WANAOKADIRIWA KUZIDI BILIONI 6.5 , BILIONI 2.1 NI WAKRISTO, BILIONI 1.6 NI WAISLAMU NA DINI YA TATU KWA WINGI WA WATU NI CTR (CHINESE TRADITIONAL RELIGIONS) YENYE WATU MILIONI 780

*TAOISM*☯

Hii ni dini most popular huko China,inaamini ktk mamia ya miungu (watu wasiokufa/immortal people) ,iliasisiwa na Deo De Jing(inatamkwa Tao Te Ching) Imani imejengwa juu ya kuamini nguvu/nishati isiyobadilika,inayojitosheleza,isiyo na muundo/kuumbwa ilikuwepo kabla ya ulimwengu na inaendelea kuwepo ktk kila kitu,imebezi ktk zoezi liitwalo Qi gong/Tai Chi-exercise na falsafa yao kuu ni hii *_"Kama unaamini kitu fulani basi ni halisi"_*

*SIKHISM๐Ÿ•Ž๐Ÿ•‰*

Dini yenye asili yake yake India,inatokana na neno sikh (sanskrit/sisya-student/disciple) 
Neno hilo sanskrit ni mtu yeyote anayeamini uwepo wa nafsi isiyokufa (๐ŸฆLion-Sikh)
Falsafa yao ni _Ishi kwa namna ambayo Mungu angependa._
*Mungu hawezi kubainishwa jinsia yake,Ni wa milele,anajitegemea,naye amefunuluwa na Guru (Gurus ni walimu waliokuwa na asili ya kiroho na kibinadamu (walikuwepo miak 239 kati ya 1469 na 1708)
*Wanaamini Mungu mmija wa dini zote na kuwa hakuna dini moja inayoweza kudai Mungu ni wa kwao

*SHINTO*
Wanaamini katika kuwaabudu 'Kami' yaani roho,kuwa hizo roho zipo karibu na wanadamu na wanasikia dua zao,wanazo nguvu za kuathiri nguvuza aili na matukio ktk maisha ya mwanadamu ,wanawesa kutoa uzima na kuwaweka watu vizuri (Musubi) na mapenzi mema (Makoto),Sio kami wote ni wazuri wapi waovu

*BAHA'I*
Yatokana na neno Baha'ullah mwanzilishi wake i Abdu-Baha ilijitokeza toka ktk dhehebu la Shia karne ya 19 huko Iran.Wanaamini Mungu hawezi julikana (Unkowable God) ,Ni kweli yeye ni muumba mwenye sifa zote,Lakini haiwezekani mwanadamu amfahamu,yaani ufahamu wa kiumbe kinachoweza kufa hakiwezi kumfahamu Muumbaji. Pia husema kila tunachofikiri kuhusu Mungu sio Mungu halisi,yeye hajulikani,hafikiriki.

*JAINISM*
Hawa hawaamini kuhusu Mungu,wala miungu ,Ila wanaamini ktk ukiroho/uungu(au ukamilifu wa viumbe vinavyohitajiwa/stahili kuheshimiwa,wao wanaweza kueleza kwa wepesi swala la uovu kwa kuwa hawaamini kuhusu Mungu. Wanaamini kila kiumbe kinaweza kuwa mungu kwa sababu kinaweza kuwa *perfect*
Jainists hawana sala na maombi ya kuomba kwa Mungu (God-focused prayer),wao maombi yao ni kwa nja ya kujikumbusha matendo mema na sifa nzuri za tirthankaras,hawaamini uumbaji wa dunia.

*TUNAWEZA KUFANYA SURVEY KTK DINI ZOTE ZINA MAMBO YA KUFANANA, NA HIZO NDIZO DINI AMBAZO MATAIFA YALE YANAJISIFU NI DUNIA YA KWANZA WAMEYASHIKA NA KUYAAMINI, LAKINI SISI KUPITIA KWA YESU KRISTO TUMEKIRIMIWA KUMFAHAMU MUNGU PEKEE WA KWELI*

*Yohana 17*

*_Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma_*

*KAMA MPAKA SASA HUJAINGIA KTK NJIA HII (IMANI HII) YA MUNGU HUYU ALIYEJIFUNUA MWISHO WA SIKU HIZI KATIKA YESU KRISTO (HEBREWS 1:1-3) BASI HUU NI WAKATI SAHIHI, HAKUNA WOKOVU KWA MWINGINE AWAYE YEYOTE,HAKUNA JINA JINGINE,HAKUTA TUMAINI LINGINE, HAKUNA POPOTE KWENYE KWELI YOTE ILA KWA HUYU MUNGU MKUU NA MWOKOZI YESU KRISTO*

Mwl Proo 
0762879363 (whatsapp)
0718922662(calls/texts)

alltruth5ministries@gmail.com

Thursday, November 6, 2025

KULITUMIA KWA HALALI NENO LA KWELI (PART 8)

*KULITUMIA KWA HALALI NENO LA KWELI*
_*Rightly Dividing The Word of Truth*_ (2Timothy 2:15b)

*SEHEMU YA NANE*

*A.) MWAMINI AMEITWA KUWA HURU*

Mwandishi: *Mwl Proo*


Maandiko: Wagalatia 5:13, Yohana 8:32, 36

Salaam wapendwa katika Bwana na Mwokozi, Yesu Kristo! Nawakaribisha kuendelea kujifunza kweli ya neno la Mungu. Kila mhudumu wa kweli wa injili, atafurahishwa daima na kazi ya kuwaelekeza waamini katika kweli. Wapenda sarakasi, hata wakiijua kweli mioyoni mwao, hawataisema, kwani ni wanufaika wa ujinga wa waamini. Wiki chache zilizopita nimemsikia mhubiri wa kilokole anafundisha somo, "Jinsi waamini wanavyologwa kieneo". Katika ufafanuzi wake alisema unaweza kuwa umeokoka vizuri, lakini kibiashara ukiwa mkoa fulani haufanikiwi, ukiwa mkoa mwingine unafanikiwa, kwa sababu umelogwa kieneo. Vyovyote tu vile atakavyoipamba...!!! Vipi na yeye mhubiri amelogwa kieneo? ๐Ÿ˜‚. Kama kuna jambo alilifanya likasaidia yeye asilogwe kieneo, basi afundishe mara moja jambo hilo, ili hawa waumini wake wasilogwe tena kama yeye ambavyo halogwi, kisha aachane na hizo jumbe.... Lakini jumbe na mafundisho haya, mara nyingi huambatana na kutoa fedha na mali kama namna ya kusindikizia maombi ili kuwaepusha na kulogwa kieneo.... The same the same message, itarudiwa tena ikiwa na sura tofauti ikionesha kwa nini pesa zinapotea, kwa nini unapoteza kibali, kwa nini watoto wanafeli.... (jumbe fukunyuzi, za kutafuta wapi mwamini atapumbazwa, asahaulishwe msalaba wa Kristo). Wenzetu mnahubiri Ukristo gani? Mmeyapata hayo kwa Yesu yupi? Mnachofundisha na kuhubiri mnakutana nacho kwenye nyaraka 21 za mitume popote? Au ndio mafunuo binafsi?

Ukristo, mikononi mwa watu wasio imara kwenye mafundisho, kwenye kupuuza kabisa kanuni za kutafsiri maandiko, umekuja kuwa kama *CULT* kama  *VOODOOISM*, yaani ni ki-movement fulani hivi cha ubabaishaji... mahali tu unapokuja kuoneshwa wewe ni mfungwa, tegemezi, upo katika hatari daima, mnusurika wa daima, mlaaniwa ambaye laana zitaendelea kuondolewa taratibu, kwa kadri kiongozi wako wa dini atakavyoendelea kufunuliwa..!. Huwa nasikiliza mafundisho ya Ukristo kwa TV, mpaka nahoji sasa kama Ukristo ni zigo zito hivi... mnahubiri nini sasa? Mnawakaribisha watu waje wafanye nini? Mbona ni kama wao wapagani wako huru kuliko ninyi huku? Mnawaalika waje walogwe pamoja nanyi?


*B. KUMFAHAMU SANA MWANA WA MUNGU*

Efeso 4:13-16, Kolosai 1:26-28
Waamini wanaweza wakakoseshwa shabaha, kama baada ya kuamini watafundishwa elimu zingine.. huku wakiamini kwamba wamezaliwa na Mungu ili wawe matajiri wa kumiliki mali mengi, kwamba sasa wao watakuwa wajasiriamali nambari moja, watakuwa wawekezaji kwenye uchumi namba moja... Na hapa ndipo maandiko kama 2Korintho 8:9, kwamba Yesu alifanyika masikini ili wao wawe matajiri, mara Mwanzo 12 & 15, baraka za Ibrahim bla bla, kwa bahati mbaya sana kule kupuuzia kanuni za kutafsiri maandiko ndiko kumefanya maandiko hayo hapo juu yahusishwe na utajiri wa kumiliki mali (Kanuni ikizingatiwa tu juu ya hayo maandiko, kinachotajwa ni kuhesabiwa haki bure kwa njia ya imani, kuokolewa kwa kumwamini Yesu tu). Mwamini, anapaswa amfahamu sana, sana, sana, Mwana wa Mungu. Siri zote, utimilifu wote wa Mungu, unakaa katika Yeye, Yesu. Unampofunzwa sana kuhusu Mwana wa Mungu, ili umfahamu sana, ndipo sasa na wewe utajifahamu sana. Utakuwa mtu mkamilifu, aliyekuwa kiroho, mwenye kimo cha cheo, kama Kristo, kwa kuwa umemfahamu sana Mwana wa Mungu... Utakuwa huru, mbali na vifungo, mbali na kuonewa, mbali na giza lote kwa sababu umemfahamu sana Yesu. Struggles za kupambana na mwili, na matendo yake, maisha ya kujazwa hofu, kutembea tena kama mtumwa baada ya kuzaliwa na Mungu, ni product ya mafundisho...  Hakuna mwamini aliyejifunza kwa ufasaha kuhusu Yesu, atakaa kwenye kiti ๐Ÿช‘ afundishwe tena namna alivyologwa kieneo... Afundishwe tena namna kitovu chake kilichawiwa na mabibi, namna alivyoibiwa nyota yake, namna wachawi wanavyoyafunga maisha yake sijui aje aje... Kusikiliza tu fundisho kama hilo ni kuyatia maarifa giza... Giza haliiwezi nuru (Yohana 1:4-5), hakuna siku balbu ya umeme yenye 100 watts, itawashwa chumbani  kisha giza ligome, kwamba taa waka, na mimi giza nabaki kama kawaida... Yesu ni nuru, amewafanya waamini nao kuwa nuru (Mathayo 5:13-14), mnakuwaje nuru mkiwa mnafundishwa vitu vya kuwatia utumwa? Mtafunguaje watu wa mataifa iwapo ninyi daima ni manusura wa hivyo vifungo, mnaoponea chupu-chupu kwa kudra za huyo mhubiri wa kwenu? Yaani kwamba asingekutabiria tu juu ya shida zako, kwishaaaaaaa! ilikuwa nawe usombwe na maji... Akakutabiria kwamba anaona umelogwa, anaona mikwamo, anaona majanga, mambo hayasogei, anaona umepoteza kibali... Haya yalikukuta yote ukiwa wapi mwenzetu??? Au labda ndio umekuja kuisikia injili? Yaani umezaliwa na Mungu, unakaliwa na Roho wake milele, Mungu amechagua kwa hiari yake afanye makao ndani yako milele, una ushirika naye milele, umeketishwa na Yesu juu sana, lakini pamoja na hayo hapa kati umeibiwa nyota, umepoteza kibali, umelogwa kieneo, umefungwa usiolewe na kuoa... Kama hili ni kweli, basi Ukristu unakuwa ni matakataka kabisa... Kama ukiwa na Mungu ndani yako, una ushirika naye, umefanyika mfalme na kuhani, lakini kuna mwizi mchawi, bado anakuibia kibali na nyota, ni nini sasa kitazuia asikuibie tena? Aliwezaje mwanzo, atashindwaje baadaye.... Haya yanashamiri kwa sababu kuna wanufaika wa ujinga wa waamini, kuna  mtu anajijenga kiuchumi in the expense of believers' ignorance.. Yeye peke yake haibiwi nyota, hafungwi, halaaniki, halogwi (mkingiwa wa majanga yote) lakini anaowaongoza kiroho pekee wako _prone and vulnerable to all sorts of disasters_ (HUU NI UTAPELI TU WA KAWAIDA). Imagine mhubiri kwenye TV anaelekeza watu, kuwa kinachofanya wanapitia matatizo ya kwenye ndoa yao, ni kwa sababu ile mahari iliyolipwa kabla waowane, hawakuitolea fungu la kumi... ๐Ÿ˜ฅ๐Ÿ˜ฅ๐Ÿ˜ฅ !!!  Huyu ndiye mwamini wa nyakati hizi na chakula anacholishwa kiroho. Mimi pia kuna nabii alipoona nakawia kuoa, aliniambia, akiwa katika maombi, Mungu alimfunulia kuwa kuna sadaka maalumu ilitolewa kwenye madhabahu ya kuzimu, kuzuia ndoa yangu, kuhakikisha kwamba sioi... Hiyo siku aliyoniambia hivyo kwa njia ya WhatsApp, niliweka tu emoji za kulia (๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ) wala sikuandika kitu kingine, maana nilikuwa na safari siku ya kesho yake kwenda kulipa mahari... Na nikaoa miezi mitatu baadaye bila kuhangaika na kafara maalumu kwenye madhabahu ya kuzimu... Fikira kama nisingejenga msingi imara kwenye kweli ya Kristo, na namna ambavyo ningeanza kukimbizana na kafara ya kuzimu inayozuia ndoa...!



*BIBLIA INASOMWA, NA INAFUNDISHWA KIFUNDISHO*

Bila kusahau msisitizo wa kanuni za kutafsiri maandiko (Hermeneutics), zilizodadavuliwa kwa upana sehemu ya I, II, & III, ya mfululizo huu, jambo jingine la msingi la kujua ni kwamba Biblia inasomwa na inafundishwa kifundisho. 
Watu wanaotafuta uvumbuzi wao kwenye maandiko (Eisegesis), wanaweza kusoma Ufunuo wa Yohana 8:13 (Kuhusu tai ๐Ÿฆ… arukaye), na wakahitimisha huyu tai anawakalisha taifa la Marekani, kitu ambacho hata mtume Yohana aliyeandika hakuwahi kuwaza. Ni uchaguzi wa kutoisoma Biblia, na kuifundisha kifundisho...

KUISOMA BIBLIA KIFUNDISHO...  ni kuiangalia yote kwa pamoja (synoptically), kutazama kiini cha ujumbe, ushabihisho kimuktadha, na ya KUIFUNDISHA KIFUNDISHO ni kujiuliza, hiki nilichosoma, kilifundishwa hivyo kwa waamini?. Hapa utakuwa salama!
Wiki chache zilizopita nimeona tangazo la ibada maalumu, ya kuwatenganisha waumini walokole, na malkia wa mbinguni, pamoja na kuondoa laana za kwenye majina yao zilizowaingia kupitia vyakula. Nilistuka kuona tangazo kubwa limerembwa vizuri kwa rangi za kuvitia, na wahubiri kama 7, lakini maombi maalum ni kuwatenga kwa maombezi, washirika na malkia wa mbinguni.... Hawa watu walisoma vifungu vitano katika Yeremia, ambaye yeye peke yake alimtaja mungu mke wa kipagani (isthar) kwa kificho, kama malkia wa mbinguni .. ambapo wana wa Israel waliwahi kumwabudu kwa kuCopy utamaduni wa kipagani na kumfanyia ibada kwa kukanda unga, kutengeneza kaki (keki) na kumwaga vinywaji. Swali linakuja; hawa waamini wa injili ya Yesu Kristo, waliozaliwa na Mungu, na kukaliwa na Roho wa milele... Waliunganishwa lini na Isthari au Ashtorethi (pagan goddesses), kiasi cha kuhitaji maombi ya kuwatenganisha nao? Mlipata wapi giza la kuwapaka waamini wanaoonekana kama mianga, hawa ambao ni nuru ya ulimwengu? Mshirika wa Kikristo, ambaye anakuja kanisani akiwa ameelekezwa tayari ameunganishwa na malkia wa mbinguni (labda niite falme za giza, majini/mapepo), huyu atashindwaje kupata uvamizi wa roho za giza? Maana fundisho hilo tayari limeunda fikra, badala atembee njiani akijijua kuwa ameketishwa juu sana, pamoja na Kristo, juu sana zaidi ya kila jina, zaidi ya kila ufalme, usultani, ubaba, juu sana kuliko majeshi ya pepo, juu sana kuliko wakuu wa giza... Anaenda kanisani na kasadaka
ka elfu 5 Tshs ziwezeshe mchakato wa kumtenganisha na malkia wa mbinguni...  Wapi mambo haya? Je! mitume wa Kristo walisahau kulitenga kanisa la kwanza na huyo mungu mke wa kipagani? Je! waliposoma Yeremia 7:18 walitoka na fundisho kama lako?
Last week, nimekutana tena na kitu cha ajabu kwenye TV... (Mhubiri wa Assemblies Of God toka Dar), amesoma Hesabu 23, kisa cha zile sadaka ambazo mchawi na mnajimu Balaamu bin Beori alimwelekeza Balaki bin Sipori kuzitoa ili yeye akakutane na Bwana, kisha akazipa jina kuwa ni *"sadaka za udhamini"*.. Baada ya hapo akasisitiza sana, kuwa ni lazima kutoa sadaka za udhamini, mtu hatatoboa asipotoa hizo sadaka za udhamini... Wapi mambo haya? Kusoma na kufundisha maandiko kifundisho ni pamoja na kuhoji, Je! ndivyo walivyofundishwa waamini? Je! inashabihiana na ujumbe wa Mungu kwa waamini katika Kristo? Fundisho kwa waamini linatazamwa synoptically throughout the Bible... ndio maana ni muhimu kujua, Biblia iko na kiini cha ujumbe (the central message).  Inaweza kujadili ujenzi wa ukuta wa mji, wala haina maana sasa Biblia ni kitabu cha architectural studies, inaweza kuwa na visa vya kusimamia biashara, wala haitakuwa na maana sasa Biblia tayari ni kitabu cha business management... Kabla hujaokoteza maandiko popote, ukihisi unapata ufunuo, ujiulize kama usomaji na ufundishaji wako upo kifundisho? Je! hauwatii waamini katika utumwa? Je! hauibatili neema ya Mungu? Je! hauufanyi msalaba wa Kristo kuwa bure na usio na maana? Je! haujiinui wewe kuwa mwokozi msaidizi, kana kwamba Yesu hakupatia sana suala la wokovu, ila unayo namna nyingine ya kuvumbua vifungu vya kupachika vifungo kwa waamini?


*MWAMINI UMEITWA UWE HURU, MFAHAMU SANA MWANA WA MUNGU UTEMBEE KATIKA UHURU KAMILI*


Tukutane kwenye sehemu ya 9 ya mfululizo wetu.
Mmebarikiwa, Shalom Aleichem! ๐Ÿ‘‹

Wednesday, October 16, 2024

MAISHA YA VIJANA WA KILEO

*NACHELEWA KIDOGO KUELEWA, AU KUAMINI MAISHA YA VIJANA WENGI WAKRISTO WA KILEO* ๐Ÿค”๐Ÿค”๐Ÿค”


_Anaandika Mwl Proo_ ✍️ 

Mwaka huu nimetimiza miaka 20 tangu nilipoamini Injili na kuokoka. Miaka ya hapa usoni, nimechunguza maisha na mienendo ya maisha ya vijana wakristo, ukiacha wachache, wengi wao (majority) maisha yao huoni tena ule ushindi, ile ladha, ule uchaji/kicho, ile bidii, ule ukiroho... Najiuliza hawa wanashindaje? wanaishije maisha ya utauwa katikati ya uchafu mwingi ulioletwa na utandawazi? Mbona hawazipigi mbio zile tulipiga? ๐Ÿค”๐Ÿค”๐Ÿค” 

Wakati ule naamini na kuwa mwongofu, hakukuwa na maendeleo makubwa ya teknolojia, Shule ya Sekondari Ya Wavulana 1,400, wenye viswaswadu tulikuwa wachache mno. Nakumbuka kule kuomba kusikokoma, nakumbuka mifungo ya lazima na hiari, iliyofanya kuwa na siku mpaka 204 za kufunga kwa mwaka, mpaka ikawa desturi ya kuwa na wastani wa siku 3 au 4 za kufunga kila wiki. Nakumbuka kuhusu gatherings & fellowships siku 6 kila wiki, ukikosa siku moja, jiandae kupokea wapendwa kibao huko kwako wakija  kujua sababu ya kukosa ibada. Nakumbuka namna tulisumbuka kuomba ruhusa ili kuhudhuria semina zote za Mwakasege, mikutano ya injili kule Biafra na Jangwani. Nakumbuka namna ambayo hakuna Joint-Mass tuliwahi kuikosa weekends zote pale DIT, IFM, UDSM na penginepo, makongamano yote ya pasaka hakuna hata moja tuliwahi kukosa kwa sababu yoyote. Nakumbuka jinsi ambavyo tulishikamana na mafundisho ya fellowship yetu kuwa hakuna mahusiano (relationship)  kwa wanafunzi wa Sekondari kidato cha kwanza mpaka cha sita.. Uhusiano halali pekee ni  'Kaka' & 'Dada' (Na watu tukaishi maisha hayo hayo) kile kinachoitwa Boyfriend &. Girlfriend kuna sisi hapa hatukuwahi jua kama kipo... Na ndio maana haikuwa ajabu, si ajabu kwa sisi wa kizazi kile na maisha yale yenye nidhamu ya kiroho kuwa tuliishi bila zinaa, haikuwahi kutajwa kwetu kamwe, tulikuwa hata hatufananii mambo hayo... (Our walk with the Lord shaped our lifestyles)... Tunao ujasiri wa kusema tulishinda tamaa za dunia na mambo yake. Yale maisha ya utauwa yalifanya hata nikiona kapicha tu kwenye gazeti au Tv kenye viashiria nudity (uchi) tachukia hapo vya kuchanwa vitachanwa, vya kufutwa vitafutwa, vya kuondolewa vitaondolewa, na nitafanyia kazi fikra zangu kuhakikisha no memories za huo uchafu zitabaki hata kwa mbali ๐Ÿง . Sasa kwa nini naandika haya.... Nimeona miaka ya usoni yale mazoezi ya kiroho yaliyotupa kuishi maisha ya wokovu yenye   ushindi, yenye usafi kimwenendo, ni kama yanakwepwa sana na vijana... Hesabu idadi ya vijana kwenye mikesha ya maombi, kwenye makusanyiko ya mifungo, na huduma nyingine...... Vijana wengi utawapata kwenye programs & events (they live too ceremonial)... Ndio najiuliza kwa lifestyle hii ya kwao, wanaweza kuishi maisha ya utauwa hawa? Na uchafu wote wa kwenye TV wanaweza kuepuka hawa kujaza vitu vichafu  kwenye nafsi zao? Nguvu zao chache watashinda kweli na ushawishi wa mitandaoni, picha za uchi kila mahali, sio Facebook, sio Instagram, sio TikTok sio WhatsApp, hata kama huja-follow kurasa mbaya utakutana tu na watoto wa Belial ambao kutwa nzima wanatengeneza contents za utupu.... Vijana wa sasa wanashindaje? Wanaepukaje uasherati? Wanaepukaje usagaji na kujichua? Mnaepukaje kuwa na mazungumzo mabaya mkiwa mnawasiliana wa jinsi mbili tofauti? Mnawezaje?  Yale ambayo yalikuwa ni sababu ya kuwapa ushindi hamyafanyi, mmeyakimbia, mnawezaje kushinda? Ni vijana wangapi wa kileo wapo serious na ratiba za kusoma na kujifunza maandiko, na wakawa strict kuhakikisha wanazifuata? Nilihitaji miezi 8 tu kwa mwaka kumaliza vitabu 66 vyote vya Biblia (tena nasoma kwa parallel-system:- English Bible juu/Swahili Bible chini)... Kijana ambaye kinachomfurahisha ni matamasha ya muziki pekee, anavukaje kwa ushindi??

_mwlproo_
Ujumbe huu ufikishwe kwa vijana. Kwamba maisha safi ya Kikristo yanahitaji nidhamu, utauwa ni wa kujizoeza, mpaka ifikie mahali mambo yote yasiyofaa unayachukia, huwezi puuzia mambo ya muhimu ya kiroho na ukabaki salama tu, ukipuuza nidhamu na bidii kwenye kujifunza maandiko, nidhamu na bidii kwenye kuomba, nidhamu na bidii kwenye kufunga, nidhamu na bidii kwenye kufanya huduma, jiandae kuwa na maisha ya hovyo, kurudi nyuma, na kutawaliwa na matendo ya mwili... Zingatia sana hayo nisemayo, inawezekana kabisa kuwa na mienendo safi, maisha yasiyo na uchafu, uadilifu kama iwapasavyo watumishi wa Kristo Yesu... Katika zama za Teknolojia hizi unaweza kuchagua kubaki kijana wa mfano, kinara kwa mambo ya kiroho, mnyoofu kabisa kiuadilifu na maadili, si tu ukiwa kwa watu, bali ukiwa sirini sana, bado uwe mnyoofu!


Asante kwa kusoma... Tuwasaidie, tuwaombee vijana!

Mwl Proo
0762879363
Bado tunatoa ofa ya vyombo vya muziki kwa makanisa kwa bei ya sadaka. Piga simu uweke oda yako

Thursday, December 22, 2022

KANUNI YA KUTAFSIRI MAANDIKO (PART 7)

*KULITUMIA KWA HALALI NENO LA KWELI*
_*Rightly Dividing The Word of Truth*_ (2Timothy 2:15b)

*SEHEMU YA SABA*

*CHANZO CHA NGUVU*

Mwandishi: *Mwl Proo*

Mmebarikiwa ninyi nyote mnaoendelea kuufuatilia mfululizo huu. Leo nimepewa kuzungumzia nguvu na chanzo chake.

Nguvu zote zilizopo, zilizokuwapo, zitakazokuja zote (za zamani zijazo) ni za Mungu, chanzo cha nguvu zote ni Mungu. Hata nguvu zinazotajwa kuwa ni za shetani (Mdo 26:18) zote ni za Mungu, na chanzo cha nguvu hizo ni Mungu. Suala la shetani ku-manipulate, au kuzitumia nguvu alizopewa kwa uovu, haibadili ukweli kama chanzo cha nguvu hizo ni Mungu. Hata zile nguvu maarufu ziitwazo za asili (natural powers), chanzo chake ni Mungu, ni za Mungu... Kama kuna nguvu inaizungusha dunia bila kupungua spidi yake, kama kuna mikandamizo ya hewa kukaleta upepo, kama kuna nyota na sayari katika miendo yake kuna aliyeamuru viwe vikawepo, alipoamuru aliruhusu nguvu zake kutekeleza na kuyashikilia mambo yote kwa uratibu wa hali ya juu (Isaya 40:26, Zaburi 8:3)

Andiko la Warumi 13:1b linatumia neno _'exousia_' kutaja uweza/nguvu/mamlaka. Neno hilo limetumika mara 29 katika Agano Jipya la Kiyunani na mara nyingine limetumika kwa kubadilishana (interchangeably) na neno dรฝnamis (dunamis ๐Ÿ‘‰ specifically to perform miracles) likitaja nguvu. Andiko hilo katika versions nyingi (mfano: KJB,  ASV, DRM) linasomeka, _Hakuna nguvu ila za kutoka kwa Mungu tu_
*For there is no power but of God: the powers that be are ordained of God.*

Nguvu za Mungu zinaweza kuwekwa katika vitu kutekeleza makusudi fulani fulani. Kwenye Biblia yote Agano Jipya na la Kale, viko visa vingi ambavyo nguvu za Mungu ziliruhusiwa kuwepo (transmit) katika vitu na vitu hivyo vikatumiwa kutekeleza kazi iliyokusudiwa. Hebu fikiria kisa cha Elisha katika 2Wafalme 4:29ff... Elisha alitransmit nguvu za Mungu kwenda kwenye fimbo yake, akampa Gehazi akamgusishe mtoto aliyefariki, ili afufuke. Nguvu za Mungu ndani ya Elisha hazikukaa tu ndani ya roho na nafsi yake hai, bali hata mwili, damu, nyama, na mifupa yake (soma 2Wafalme 13:21) utagundua mifupa yake ilisalia na nguvu zilizoweza kufufua mtu yeye akiwa amekufa kwa homa siku nyingi. Tunasoma katika Matendo 19:11, leso na nguo ambazo zilimgusa Paulo zilipelekwa kwa wagonjwa wakapona, na pepo wabaya wakawatoka. Matukio kadhaa yanaonesha nguvu za Mungu ndani ya watu zilikuwa transmitted kwa vitu (kumbuka kisa cha chumvi kwenye chanzo cha mto huko Yeriko, kumbuka kisa cha unga uliotiwa sufuriani ili kuiondoa mauti, kumbuka  pindo la vazi la Yesu, tope lenye mate ya Yesu, birika la Bethzatha na mengine mengi). _mwlproo_

Kuna upotoshaji mwingi unaotokana na kukosekana kwa maarifa. Kuna makelele mengi yanaleta aibu kama sio huzuni. Leo hii tuna watu ambao hiki kitu wamekipokea kimakosa utasikia sabuni, utasikia mafuta, utasikia maji, utasikia pipi, utasikia keki, utasikia stika, utasikia chumvi, utasikia udongo, utasikia kitambaa cheupe.... Vyote hivi vitaenda kwa jina la upako... Kwa miaka mingi vimekuwa vikiitwa visaidizi (erroneously), na miaka michache iliyopita nilimsikia mhubiri mmoja wa Dar akiviita vifaa vya kiroho, jina ambalo sasa linatumiwa na wengi. NDUGU ZANGU WAKRISTO VITU NILIVYOTAJA HAPO JUU VYOTE HAVINA NGUVU. NGUVU ZIKO NDANI YA WATU, NA WATU NDIO WANAOWEZA KURUHUSU NGUVU ZILIZO NDANI YAO ZIENDE KWENYE VITU (TRANSMISSION), NA KURUHUSU NGUVU ZIENDE KWENYE VITU KIBIBLIA NI PALE TU ROHO AMEKUPA UFUNUO (NENO LA HEKIMA) KWAMBA SHIDA HII IHUDUMIE HIVI ZIRUHUSU NGUVU ZIENDE KWENYE MAJI AU CHOCHOTE KIWE NA CONTACT NA MWENYE SHIDA TATIZO LIKAONDOLEWA, AU KWA NAMNA ILIVYO KATIKA MAZINGIRA NI NGUMU KU-ADMINISTER HUDUMA ZA KUPONYA NA MATENDO YA MIUJIZA KWA NENO LA IMANI, KWA KUOMBA, KWA KUWEKA MIKONO NA NAMNA NYINGINE YA UTENDAJI. HIZI NI NAMNA MBILI KWA MUKTADHA WA UKRISTO VITU HIVI VYAWEZA HAMISHIWA NGUVU ZILIZO NDANI YA MTU KURUHUSU VIKATENDE KAZI.

Dramas zinazoendelea leo hii Afrika ni nyingi mno. Wakristo wanakimbizana na hivi vitu kiasi cha wao kupumbazika kabisa kubakia watumwa mara billion ya walivyokuwa kwanza. Nilipewa ushuhuda wa mama aliyemwaga chumvi yake ya upako bahati mbaya na akasikitika sana na kilio juu. Nilishuhudia kwa macho yangu mhubiri mmoja huko Dar, aliivua tai yake ๐Ÿ‘”  na kuirusha kwa watu kwamba ina upako (sikatai maana upako unahamishika), lakini iligombaniwa sana na washirika, na kijana mmoja alifanikiwa kutoka nayo nje,  katika vutavuta mwingine aliikata kipande... wamama wawili wakamwomba wamlipe laki 3 awaachie kipande hicho cha tai. Dramas hizi za vile vinavyoitwa visaidizi au vifaa vya kiroho ziko Afrika kuliko mahali pengine popote palipofikiwa na pentecostal & charismatic movements, kwa nini haswa?

 Hapa Afrika vimekuwa maarufu kwa sababu ya imani za asili au za kienyeji kwa jamii ya watu wa Afrika. Maishani mwangu nilipata neema ya kusomea dini za asili za Afrika (African Traditional Religion ๐Ÿ‘‰  ATR). Kwenye dini zetu za asili na tamaduni vitu vya kuonekana, vya kushikika, manuizo, matambiko, ulozi, na mengine mengi yaliyohitaji vitu vya kuonekana yalihitajika sana. Fikiria jamii ambayo ilizoea wakitoka kwa mganga wa kienyeji,  wamechanjwa miili, wamepewa vitu vya kutia kwenye maji ya kuoga, wamepewa vitu vya kufunga mikononi, viunoni, shingoni, wamepewa vitu vya kulalia chini ya kitanda, cha kupaka ukutani, cha kumwaga na kunuiza kwenye kuta za nyumba, cha kuweka darini na kadhalika.... Haya yamekuwa mambo ya kawaida kwa karne nyingi Afrika, yamerithishwa vizazi vingi kiasi cha kuwa ni kama kitu cha kuzaliwa nacho. Kila atakayekuja Afrika akawa na vitu tangible vya kugawa kwamba vina nguvu za kusaidia atake au asitake lazima atafanikiwa kupata ufuasi mkubwa maana imegusa asili ya Afrika. Hapa sasa ndio sababu haswa ya kila mhubiri kwa sasa anakomaa na vitu hivi.. Hata mahali ambako angeweza kumgusa mgonjwa kwa mkono wake, atamwagiza ashike kitu, hata mahali ambako angetamka tu 'kansa kauka'... atatafuta kwenye briefcase ๐Ÿ’ผ  chupa cha mafuta aliyoyabeba toka Israel bila hata maelekezo ya Roho wa Yesu (mtu akiongozwa na anaweza kuthibitisha hilo hakuna tatizo) Lakini 95% ya watumiaji wa hivi vitu, hawana maelekezo yoyote ya Yesu... wanaunga-unga na kujaribu-jaribu tu, mambo yakitokea kweli wanaendeleza bila kujua nguvu zipo ndani yao.. Na matokeo yanatokea si kwa sababu wapo sahihi... Ni kama tu mtu kunywa sumu akiamini ni juisi tu, haitazuilia sumu kufanya kazi yake ya kumwua, au mtu anywe maziwa akiamini ni maji tu, haitaizuia maziwa yasimpe nutrients zinazopatikana kwenye maziwa. Lakini tatizo limekuwa kwenye kufanya waamini wasijue kuwa nguvu ziko ndani ya watu si ndani ya hivyo vitu.. Niliongea na rafiki yangu mmoja ambaye dada yake ni mhudumu (usher) kwenye huduma moja ya maombezi. Alisema waliuza maji ya uhai (katoni za kutosha) ambayo yaliombewa na mtumishi wiki nzima, yakaisha na watu bado walikuwa wengi, hivyo ikabidi maji yakanunuliwe direct toka dukani na kuuzwa kwa watu kama maji ya upako... bila hayo maombi ya siku saba. Guess what! Kwa sababu ya imani ya miujiza ndani ya hawa watu haya maji yaliyotoka dukani directly yakipelekwa kwa wenye shida yanawezaleta shuhuda pia. Lakini ufahamu wa juu kabisa kwa waamini ni kufahamu nguvu zote hizo ni za Mungu, na jamaa ya waamini (WOTE) walipobatizwa katika Roho wa Kweli nguvu hizo bila kipimo zilikuwa superimposed ndani yao. Waamini wote wanazo hizo nguvu, utendaji utatofautiana tu kulingana kiwango cha maarifa, na unafanya nini katika ufalme, na Roho Mtakatifu amekupea karama zipi, au wewe mwenyewe unatembeaje katika kutumia vilivyowekwa ndani yako tayari. KWA KUSEMA HIVYO WAAMINI HAWANA HAJA WAO WENYEWE KUKIMBIZANA NA CHOCHOTE, MAANA NGUVU ZENYEWE ZIKO NDANI YAO. KAMA KUNA NGUVU ZIPO KWENYE UDONGO WA ISRAEL, AU MAJI YA YORDAN, AU SABUNI, AU CHUMVI AU KITAMBAA KILICHOOMBEWA, NGUVU HIZO SI KWA AJILI YA MKRISTO YEYOTE MKOMAVU, MAANA YEYE MWENYEWE NDIYE MZALISHAJI WA HIZO NGUVU KUTOKEA NDANI YAKE ZIKASAIDIE WALIOFUNGWA NA ADUI HUKO NJE (YOH 7:38). MWAMINI ANAYEHISI KUWA KWA POSTI HII NINAWAPINGA WAO AU MHUBIRI YEYOTE HONGERA YAKE KWA KUCHAGUA KUWA MTUMWA WA DAIMA.. ENJOY YOUR SLAVERY, REMAIN CAPTIVE TO IGNORANCE. MIMI BINAFSI NGUVU ZIPO NDANI YANGU, NIKISTULIWA SAA NANE USIKU KUTOA HUDUMA YOYOTE YA KIROHO, NITATOKA NIKIWA NA NGUVU ZOTE BILA KUHITAJI KUTAFUTA KICHUPA FULANI ETI NIMEKIFICHA  KWA KABATI, HATA BAADA YA KUTRANSMIT NGUVU KWENDA KWENYE VITU, NIMEPEWA UWEZO KUJI-RECHARGE ๐Ÿ”Œ  ๐Ÿ”‹  MIMI MWENYEWE SI MIMI KUTEGEMEA VINGUVU NILIVYOVIHAMISHIA KWENYE KITU.


Tukutane sehemu 8, kuna mambo mazuri utayafahamu


alltruth5ministries@gmail.com

Tuesday, November 15, 2022

SWALI NA JIBU (KANUNI YA KUTAFSIRI MAANDIKO)

*KULITUMIA KWA HALALI NENO LA KWELI*

_*Majibu ya swali nililoulizwa na mchungaji mmoja kwa inbox, kufuatia sehemu ya tano ya somo letu*_

Kufuatia sehemu ya tano ya mfululizo wa somo letu la *Kulitumia Kwa Halali Neno La Kweli*, sehemu iliyojikita kuzungumzia *UTOAJI/MATOLEO* nimeulizwa na mchungaji mmoja kuwa Je! kwa namna hiyo niliyofundisha mapato hayatapungua na kurudisha kazi ya Mungu nyuma?

Niseme hivi, watu wanachofanya sasa hivi ni matokeo ya mafundisho, utoaji uliopo sasa hivi (wa kichoyo) ni matokeo ya mafundisho (tena yenye makosa). Kwa fundisho sahihi la Ukristo juu ya utoaji lililojikita juu ya ukarimu (generosity), kanisa wala wahudumu wa injili hawakupaswa kubakia na mahitaji (Mdo 4:34, 2Kor 11:9,  Mdo 20:34-35, Filipi 4:16). Tatizo tulichagua mafundisho yaliyoumodoa Ukristo na watu wakaamini katika Ukristo, utoaji kiwango chake ni kuweka ka-kakapu (kitunga ) na kupokea masilesile ๐Ÿช™๐Ÿช™๐Ÿ’ฐ๐Ÿ’ฐ, au Ukristo kiwango chake ni kutoa million 10 kila upatapo million 100. Ukristo kiwango chake cha utoaji ni kuhudumia mahitaji kwa ukarimu hata pasiwepo uhitaji. Ukipata million 100 kama kuna uhitaji wa million 85, unapambana kuondoa huo uhitaji kwa kadri cha kiasi cha ukarimu wako. Tutawatambua wakristo waliokomaa katika fundisho la Kristo kwa namna yao wanavyohudumia mahitaji ya kazi za injili, na namna wanavyosapoti wahudumu wa injili, ili kusiwe na mikwamo yoyote. Kama waamini wakifundishwa usahihi wa utoaji kiKristo wataacha uchoyo wa kutoa kidogo kwa asilimia wakati uhitaji ni mkubwa. Wakristo wakifundishwa fundisho sahihi la utoaji, mtaona ghafula tu mabadiliko, watu wataanza kutoa magari, hati za nyumba zitamiminika, viwanja vitamiminika, wafanyabiashara wakubwa na watu wenye tenda za mabilioni ya pesa wataacha uchoyo wa percents na badala yake vyombo vya matoleo vitajaa cheques (cheki) za benki zenye figures tu kubwa, mtu hataona kazi kuandika cheki yenye million 700 kuituma kanisani. Ila kwa sasa kwa kuwa mnafundishana uchoyo, mtu anaishi chini ya viwango vya ukristo huku akiamini amefika. Kwa wahudumu wa neno (mafundisho) wafundisheni waKristo mwenendo unaopatana na tabia mpya za asili yao mpya waliyoipata kwa kuzaliwa kwa njia ya Roho wa Yesu. Mapato ya kanisa hayatapungua, badala yake hakutakuwa na mahitaji tena, na itawapunguzia wahubiri kuwa na mahubiri ya mchongo ya *naona watu 50 wenye elfu 50 kwenye wallets ๐Ÿ‘›  zao, wazitoe na watapata upenyo ndani ya siku 50* ๐Ÿ˜€ Na wengine wametumia 1Samwel 9:7-9, kuweka gharama za kumwona mtumishi (consultation charges), mara ambatanisha sijui what. All sorts of kuambatanisha, kujiambatanisha kwa sadaka, kuifanya kama catalyst ichochee mchakato wa wewe kupokea ahadi au wema wa Mungu, katika Ukristo vyote hivyo ni vya mchongo. Usiulize swali juu ya haya majibu kama hujasoma sehemu ya 1, 2, 3, 4, 5 ya mfululizo huu. Ukiyakataa haya yakatae tu. Endelea kuufurahia uongo kwamba ikitokea sijui kama hujafanya jambo fulani la kimatoleo utalaaniwa, kwamba utakufa kama Anania na Safira, kwamba hutauona ufalme wa Mungu, kwamba sijui what you name them..... Hayo mmeyachagua kuyaamini kinyume na fundisho la Kristo, mitume wake na matendo yao.......

Asante! Tukutane sehemu ya 6 ambayo iko njiani

Mwl Proo- +255762879363

KANUNI YA KUTAFSIRI MAANDIKO (PART 6)

*KULITUMIA KWA HALALI NENO LA KWELI*
*_Rightly Dividing The Word Of Truth_* (2Timothy 2:15b)

*SEHEMU YA SITA*

_MwlProo-0762879363_

*KUHUBIRI NA KUFUNDISHA (Mathayo 11:1)*
 
Karibu katika mfululizo huu wa kuifahamu kweli, jitahidi usome sehemu tano zilizotangulia utaelewa zaidi hapa. Leo napiga hatua kuingia ndani zaidi. Kuna kipindi fulani hivi katika kanisa, mafundisho mengi yalijengwa juu ya shuhuda za watu waliodai kuchukuliwa mbinguni na kuzimu ma kurudishwa. Wengi wa waliotoa madai hayo hawachukuliwa na shetani, wengi katika wale encounters zao zilikuwa za kweli. Kukatokea tatizo kwa kutojua msingi kamili wa fundisho la Kristo, na hawakuwa na namna sahihi ya kuyafikisha waliyoyaona. Kwa ufinyu wa maarifa ya imani ya Ukristo waliyatafsiri mambo kinyume na kweli, ikapelekea kuwa na vitu vingi kwenye mafundisho vyenye kuwakosesha target waamini. Nyakati hizo mtu angezuka kusema nimemwona mchungaji fulani kuzimu (aliyefariki kitambo) anateseka katika moto, kosa lake alizini kwa siri. Nimemwona bibi yangu kuzimu, kosa lake alikuwa mchawi. Yesu amenionesha kwenye maono wote wanaovaa hereni, mawigi na mikufu wapo motoni wanachomwa, Yesu amenionesha wasiotoa zaka kamili hawana nyumba zao mbinguni, na wanaotoa sadaka chache nyumba zao hazijafungwa lenta au hazina canopy. Kwa hiyo waamini wakawa wakirushwa huku na huko na kila upepo wa fundisho toka katika chanzo kisicho sahihi cha mafundisho na mahubiri. Sipo kinyume na shuhuda zao, nipo kinyume na uwasilisho na tafsiri zinazokinzana na kweli ya injili, pamoja na kutumia maono na ndoto za mbinguni na kuzimu kama chanzo cha mafundisho ya msingi ya kanisa. 

Kwa nini kumetokea makosa (errors) mengi kwenye mafundisho na mahubiri mengi kwenye mwili wa Kristo? Andiko nililoliweka hapo juu (Mathayo 11:1) tunaona wanafunzi wakitumwa kufundisha na kuhubiri. Kuna watu wamepewa karama ya kufundisha, na kuna watu kuhubiri, na inawezekana vyote vikawepo. Mtu ambaye hajapewa kufundisha anapolazimisha kufundisha ni rahisi sana kuwaingiza watu katika makosa. Kuna watu walijaliwa neema ya karama za Roho za matendo ya miujiza, karama za kuponya, na karama zingine zenye mvuto tu, wakaaminika kwamba kama wanaweza kutumika kwa karama za nguvu kiasi hicho wanaweza kufundisha, kwa bahati mbaya ikawa kinyume chake. Miongoni mwa ambao waliingiza chachu nyingi za kimafundisho ni watu waliowahi kutembea katika karama za nguvu _(Rejea somo langu la Karama za Roho)_ na wakaamini pia wanaweza kufundisha, kumbe hawakupewa kufanya hilo (Unaweza ukaelewa fundisho la mtu aliyetoka kufufua mfu, linavyoweza kuwa na nguvu, hata kama lina makosa. Watu waliondaliwa na kupewa huduma ya kufundisha wanayo neema ya kufanya uchambuzi wa maandiko (exposition of  scriptures) na kuleta *BALANCE* ya mambo yote yahusuyo imani. Nimesoma kisa fulani ambapo Kenneth Hagin alimwandikia mwalimu mmoja wa neno la Mungu kwa jina Gordon Lindsay (ambaye aliwahi kuwa manager wa mhubiri wa miujiza na uponyaji aitwaye William Branham), katika ujumbe wake alimwambia nimeona maono kadhaa moja wapo ilikuwa Bwana anamwondoa Branham kwa sababu ya damage anayoileta kwenye mwili wa Kristo kimafundisho. Baada ya miezi kadhaa kupita na mhubiri huyo kupatikana katika ajali ya gari na kuwa katika comma na badae kufariki, Lindsay alimjibu Hagin kuwa mtu uliyetoa unabii juu yake amefariki. Lindsay alisisitiza kusema, nilimwambia brother Branham wewe si mwalimu, unachanganya waamini, hubiri neno kisha tumia karama za miujiza na kuponya. Majibu ya Branham kwa Lindsay yalikuwa, "najua mimi si mwalimu, lakini nataka kufundisha, na nitafundisha". Unaweza kuwa na karama kuu za kiroho zenye mvuto mwingi, ila kama hukupewa kufundisha kila ufanyapo hivyo unaweza kuwaelekeza watu katika makosa. Kabla ya Lindsay kuondoka kwenye utumishi wa Branham alisaidia kuleta balance ya mambo mengi kimafundisho (NB:- SIPO KINYUME NA HAWA WOTE NILIOWATAJA AKIWEMO HUYO BRANHAM W.M, NIMETUMIA KISA CHAO KUFUNDISHA TU).

Siku moja nikiwa naandika ufafanuzi wa sura 12 za Daniel (April 2020), nilipofika sura ya 7, 8, 9, & 12 nikajigundua nimekaa nikiwa natumia nyenzo kadhaa mpaka scientific calculator (Niliandika masomo hayo baada ya Mungu kwa Roho Mtakatifu kuniahidi katika ndoto kuwa wiki hiyo atanipa kuelewa hicho kitabu). Nikasema Mungu kama imenibidi nipitie haya ili kukielewa kitabu hiki  Je! itakuwaje kwa wengine ambao labda hawana kipawa cha hivyo, ilikusudiwa wote waelewe? hapo hapo jibu la Mungu kwangu likawa, kila mahali kuna watu waliopewa vipawa vya kufanya uchambuzi wa maandiko (Labda kama hawatatumiwa, au kunyamazishwa). Na hapa niandike ushauri tu kwa viongozi wa makanisa, wasizime vipawa vya waliopewa kufundisha, kwa kuwa unaweza kuwa senior pastor lakini labda una neema ya kuhubiri tu si kufundisha, ukawa na watu dhaifu kwa upande wa fundisho la Kristo, wakasombwa na ukengeufu wowote utakaojitokeza, kumbe hawakupata nafasi ya kufundishwa. Nimesoma andiko la mtu mmoja kasema walimu wanaofundisha masomo ya neema wanapenda sana kutumia maneno ya kiyunani na kiebrania na wanatumia ufahamu wao zaidi kuliko ufunuo wa Roho. Walimu wanaweza kuwa na neema tofauti ya kufanya uchambuzi (exposition of scriptural text), ukiwaona huko kwako *WATUMIE*, USIWAPINGE, USISIMAME NAO KINYUME. Kama unakerwa na ufafanuzi wa kutumia Kiyunani na Kiebrania ni wazi tu, hukupewa eneo hilo kutumika na approach hiyo, shughulika na mzingo na mlinganyo uliopewa utumike kwa uaminifu, lakini waliopewa kipawa cha kufundisha wapewe nafasi hiyo ili kuleta balance ya kweli yote ya injili. Ilitolewa kazi kwa wanafunzi *Wafundishe na kuhubiri*,  watu hawawezi kujengwa kwa ukamilifu kwa kuhubiriwa peke yake, kuna mahali fulani hawatafika kimaarifa ya kiroho. Waamini waliojengwa katika kuhubiriwa pekee bila kufundishwa hawawi imara kiasi cha kusimama sana wao wenyewe. Hawa ndio ambao wakipata uhamisho wa kikazi mbali na mahubiri aliyozoeaga kumpiga *handel*, hasongi mbele, hawa ndio ambao mtumishi anayewaongoza kiroho akifariki na wao hawaendelei tena mbio zao za imani, hawa ndio kukitokeza kauvumi ka roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani yanawabeba alfajiri na mapema.

Kama nilivyotangulia kusema, imani ya Ukristo sio ya mchongo. Mafundisho yasiyojengwa au kutokana na kweli ya injili  lazima yawe *terminated*, mafundisho ambayo msingi wake ulikuwa ndoto na maono binafsi ya mtu huku yakikinzana na fundisho la Kristo, na mitume wake na matendo yao sharti liondolewe lisiweke kwazo wala kongwa la utumwa kwa waamini. Waliopewa kuhubiri wahubiri tu, wasijaribiwe kufundisha waka-infuse errors kwa mafundisho yenye makosa (false indoctrination). Waliopewa kufundisha, wafundishe kwa bidii, kwa ustahimilivu, wala wasichoke. Mwili wa Kristo (kanisa) ujazwe kwa maarifa sahihi ya neno la Mungu, na kuwasaidia waamini kuweza kusimama nyakati zote, na kuwa wazoevu wa maneno ya imani. Hawa wataweza kushinda purukushani zote za masuala ya kiimani katika dunia hii mbovu.


Mungu awabariki tukutane sehemu ya 7

alltruth5ministries@gmail.com