*KULITUMIA KWA HALALI NENO LA KWELI*
_*Majibu ya swali nililoulizwa na mchungaji mmoja kwa inbox, kufuatia sehemu ya tano ya somo letu*_
Kufuatia sehemu ya tano ya mfululizo wa somo letu la *Kulitumia Kwa Halali Neno La Kweli*, sehemu iliyojikita kuzungumzia *UTOAJI/MATOLEO* nimeulizwa na mchungaji mmoja kuwa Je! kwa namna hiyo niliyofundisha mapato hayatapungua na kurudisha kazi ya Mungu nyuma?
Niseme hivi, watu wanachofanya sasa hivi ni matokeo ya mafundisho, utoaji uliopo sasa hivi (wa kichoyo) ni matokeo ya mafundisho (tena yenye makosa). Kwa fundisho sahihi la Ukristo juu ya utoaji lililojikita juu ya ukarimu (generosity), kanisa wala wahudumu wa injili hawakupaswa kubakia na mahitaji (Mdo 4:34, 2Kor 11:9, Mdo 20:34-35, Filipi 4:16). Tatizo tulichagua mafundisho yaliyoumodoa Ukristo na watu wakaamini katika Ukristo, utoaji kiwango chake ni kuweka ka-kakapu (kitunga ) na kupokea masilesile 🪙🪙💰💰, au Ukristo kiwango chake ni kutoa million 10 kila upatapo million 100. Ukristo kiwango chake cha utoaji ni kuhudumia mahitaji kwa ukarimu hata pasiwepo uhitaji. Ukipata million 100 kama kuna uhitaji wa million 85, unapambana kuondoa huo uhitaji kwa kadri cha kiasi cha ukarimu wako. Tutawatambua wakristo waliokomaa katika fundisho la Kristo kwa namna yao wanavyohudumia mahitaji ya kazi za injili, na namna wanavyosapoti wahudumu wa injili, ili kusiwe na mikwamo yoyote. Kama waamini wakifundishwa usahihi wa utoaji kiKristo wataacha uchoyo wa kutoa kidogo kwa asilimia wakati uhitaji ni mkubwa. Wakristo wakifundishwa fundisho sahihi la utoaji, mtaona ghafula tu mabadiliko, watu wataanza kutoa magari, hati za nyumba zitamiminika, viwanja vitamiminika, wafanyabiashara wakubwa na watu wenye tenda za mabilioni ya pesa wataacha uchoyo wa percents na badala yake vyombo vya matoleo vitajaa cheques (cheki) za benki zenye figures tu kubwa, mtu hataona kazi kuandika cheki yenye million 700 kuituma kanisani. Ila kwa sasa kwa kuwa mnafundishana uchoyo, mtu anaishi chini ya viwango vya ukristo huku akiamini amefika. Kwa wahudumu wa neno (mafundisho) wafundisheni waKristo mwenendo unaopatana na tabia mpya za asili yao mpya waliyoipata kwa kuzaliwa kwa njia ya Roho wa Yesu. Mapato ya kanisa hayatapungua, badala yake hakutakuwa na mahitaji tena, na itawapunguzia wahubiri kuwa na mahubiri ya mchongo ya *naona watu 50 wenye elfu 50 kwenye wallets 👛 zao, wazitoe na watapata upenyo ndani ya siku 50* 😀 Na wengine wametumia 1Samwel 9:7-9, kuweka gharama za kumwona mtumishi (consultation charges), mara ambatanisha sijui what. All sorts of kuambatanisha, kujiambatanisha kwa sadaka, kuifanya kama catalyst ichochee mchakato wa wewe kupokea ahadi au wema wa Mungu, katika Ukristo vyote hivyo ni vya mchongo. Usiulize swali juu ya haya majibu kama hujasoma sehemu ya 1, 2, 3, 4, 5 ya mfululizo huu. Ukiyakataa haya yakatae tu. Endelea kuufurahia uongo kwamba ikitokea sijui kama hujafanya jambo fulani la kimatoleo utalaaniwa, kwamba utakufa kama Anania na Safira, kwamba hutauona ufalme wa Mungu, kwamba sijui what you name them..... Hayo mmeyachagua kuyaamini kinyume na fundisho la Kristo, mitume wake na matendo yao.......
Asante! Tukutane sehemu ya 6 ambayo iko njiani
No comments:
Post a Comment