*IMANI KATIKA MUNGU-JEHOVAH NA BWANA YESU KRISTO NDIYO ILIYO YA KWELI NA TAKATIFU SANA*
*_By Mwl Proo_*
0762879363
©2014
Bwana Yesu asifiwe sana! Nakukaribisha ktk mfululizo wa somo hili ambalo ni ufunuo nilioupata kama zao/product baada ya kujifunza kwa kina kuhusu misingi ya dini kuu 19 za dunia (19 world major religions) na matabaka(subdivisions) 270 ya kidini duniani. Na ingawa mimi ni Mkristo ila ktk kutafuta kuzijua,nilifanya kama mwanafalsafa anayesimama kati/nje ili afanye upembuzi sahihi (Radical Objectification of Reality),Ingawa pia niliimulika imani hii in the light of other religions,Nikatoka na hitimisho hili *_The faith in God-Jehovah and the LORD Jesus Christ is the most trustworth and most holy faith_*
*IMANI HII NINAYOITAJA KUWA NDIYO YA KWELI NA TAKATIFU SANA*
*Yuda 1 : 20*-
*_Bali ninyi, wapenzi, mkijijenga juu ya imani yenu iliyo TAKATIFU SANA, na kuomba katika Roho Mtakatifu,_*
✝Imani hii ilikuwepo kabla ya anguko la mwanadamu (Mwanzo 1&2)
✝Imani hii Mungu aliiahidi siku ile ya anguko (Mwanzo 3:15/Gal 4:4) kwa kuahidi uzao wa mwanamke yaani Yesu
✝Baada ya anguko imani hii ilikuwepo,maana kuna kizazi cha walioliitia jina la BWANA (Mwanzo 4:26)
✝Imani hii ilikuwepo wakati wa Nuhu. Katika 2Petro 2:5 ,Nuhu anatajwa kuwa ni mjumbe wa haki(Preacher of Righteousness) Aliihubiri haki ya Imani hii,
🔴Kulitokea imani/dini nyingi nyakati hizi kuelekea wakati wa Ibrahimu na yule Babu Africa a.k.a (Nimrod) Mwanzo 10:8-12 anatajwa kama mwanzilishi wa ibada za sanamu(idolatry)
✝Mungu akaitenga imani hii kwa kupitia Ibrahimu na vizazi vyake(Mwanzo 12:1ff)
✝Imani hii ilibaki kwenye kusanyiko la watumwa waliokuweko huko Gosheni,na kwa kuwa inakuwa ndani ya watu haikubaki Kanaani.
✝Imani hii ilikuwa na kusanyiko la watu laki 6(wanaume)approximately milioni 2 waliosafiri jangwani
✝Imani hii iliendelea nyakati zote za wafalme na manabii(Ndani ya kapu kubwa la dini ya Kiyahudi/Judaism)
✝Hii ndiyo Imani ambayo Yesu alikuja kuieleza kwa ufasaha,na mataifa tukaipokea imani hiyo kwa neema tu
*SIFA ZA IMANI HII*
Ni muhimu kutambua kuwa,imani zote ambazo mwanzilishi wake si JEHOVAH BWANA/YESU KRISTO,basi hiyo imani ni kazi ya Adui Shetani aliyeitwa Lucifer hapo mwanzo kwa kupitia idara yake ya "FALME NA MAMLAKA" ngazi ya pili ya cheo toka kwake, Na Shetani huyu ni mmoja tu anayejidhihirisha tofauti tofauti, NI HUYO HUYO NDIYE ALIYEJIFUNUA KAMA *ALLAH* KTK UISLAMU,LAKINI NDIYE HUYO HUYO ALIYEJIFUNUA KAMA *KAMI* KTK DINI YA SHINTO,NI HUYO HUYO ALIYEJIFUNUA KAMA *VISHNU* NA PIA GODESS OF INDIA KTK DINI YA HINDUISM, NI HUYO HUYO ALIYEJIFUNUA KWA *Deo De Jing (Tao Te Ching)* kwenye TAOISM dini kubwa ya China, Ni yeye Shetani huyohuyo aliyejifunua kwenye dini ya SIKHISM kwa wale *GURUS* na kama *TIRTHANKARAS* ktk BAHA'I na kadhalika na kadhilika. Najua it sounds so harshy, kisa tunakariri kuwa Mungu ni mmoja katika kutafuta amani kijamii ecumenically.
✝Ni imani pekee yenye *kweli yote*(Yohana 16:13) Haina utata(innerate and infalliable faith)
*TUILINGANISHE NA IMANI ZINGINE*
Imani hii imeeleza vizuri kuhusu uumbaji wa Mungu(Genesis 1&2) lakini ktk Dharmic faiths kuna historia ya uumbaji (Babylonian Creation story) iitwayo *_Enuma Elish_*
Ambapo wanaaeleza kulikuwa na Two giants mmoja aliitwa Marduk(Merodaki mungu wa Babeli/ Yeremia 50:2) na mwingine aliitwa Tiamat ,na kwamba hawa waligombana ila huyo Marduk akamshinda Tiamat akamkata 🗡vipande viwili na kipande cha juu ndiyo mbingu/anga na kipande cha chini ardhi yaani dunia. Huu ni mfano mmoja tu wa namna Imani hii imetakasika sana kwa habari ya kuwa na Kweli yote.
✝Ni imani pekee yenye tumaini la kweli
>Hatujaachwa bila taarifa yakini,Mungu wetu ametujulishaa yote,Tunajua tutokako na tuendako
Imani nyingine hazina tumaini la kweli
Mfano imani nyingi ktk Dharmic faiths hazina fundisho la Mbinguni na Kuzimu. Mfano hai ni Hinduism wao wana fundisho lao la *_SAMSARA_* yaani rebirth/reincarnate .Wanaamini mtu akifa anazaliwa tena. Mara nyingi ule mwili wa kwanza wanauchoma moto,Ila wanafundisha kwamba ukiishiaisha mema,basi ukifa unazaliwa tena ukiwa ni mwanadamu mwenye viwango vya juu,kama ulikufa huna utajiri kabisa ila ulitenda mema,basi ukizaliwa tena unakuwa hata waziri mkuu etc,lakini kama uliishi maisha maovu ya ubakaji uuaji n.k basi unaweza zaliwa ukiwa paka🐈 nyau👉🏾😾 Au mdudu🐜 etc etc
Sasa sisi ktk Imani hii tumetanabaishwa vyema kwa habari ya yote baada ya maisha haya(Ukweli ambao kama maandishi ya Biblia hayatoshi,Basi Bwana anawaonesha watu hata kwa maono ya wazi)
✝Ni imani pekee yenye kuushinda ulimwengu,tamaa zake na maovu yote
*1John 5:4*
*_Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, HIYO IMANI YETI._*
✝Ni imani hii pekee ndiyo inayoufanya ulimwengu/dunia iendelee kuwa salama(it sustains the world)
Earth Science proves that the world is not static,its existence us uncertain,mambo kama natural catastrophes,global warming,nuclear threats etc etc yanatishia uwepo wa planet earth
MAMBO MATATU
*Kiapo cha Mungu kwa mtu mmoja aliyeishika imani hii (Mwanzo 8:21)
*Watu wa imani hii kwa kuwa bado wapo duniani (Mathayo 24:22,2Thes 2:6)
*Mungu ameiweka🌍akiba kwa moto,so inalindwa (2Petro 3:7)
*TUKIINGIA KTK IMANI TUNAPASWA KUFANYA NINI?*
✝Kujijenga na kuongezeka hata kufikia kwenye kimo cha cheo ch utimilifu wa Kristo (xv✝Kuendelea kumjua Bwana (Hosea 6:3,Ayu 22:21)
✝Kuishindania Imani hii(Yuda 1:3)
*FAIDA ZA KUWA KTK IMANI HII*
✝Ni watu wa imani hii pekee ndio wanaoingia mbinguni (Kondoo wa zizi lolote lingine sharti waletwe ktk zizi la imani hii👉🏾Yohana 10:16)
✝Ni watu wa imani hii pekee ambao mbingu zina *_full control_* juu ya yao. Ufalme wa giza hauwagusi ili kuwadhuru Mathayo 10:29-30,1Yohana 5:18-19
>Hawawezi kufa *_prematurely_* kwa mapenzi ya Shetani,kwani wako malaika(wakalimani) mmoja kati ya elfu wanazuia hatari zote juu yao (Ayub 33:23-25) Maana duniq yote hukaa kwa yule mwovu(1yoh 5:18-19) ,mara baada ya anguko,Shetani alitawala vyote juu ya mwanadamu, .Yesu aliitangua hiyo mamlaka kwa wamwaminio.
So to say,watu wa imani hii ndio wali salama kuliko yeyote ktk dunia hii mbovu(Gal 1:4)
Dini kuu zote 19 na matabaka ya kidini 270 yanagawanywa ktk makundi manne kimsingi yaani kulingana na namna wanavyoamini kuhusu Mungu/Uungu
1.DEISM;wanaamini Uungu/Mungu aliuumba ulimwengu,akaufanya uanze kazi zake(functioning),lakini haendelei kujishughulisha nao
2.PANENTHEISM; Huamini uungu ni sifa ya kiroho ya kila kitu duniani lakini pia ipo nje ya dunia
3.PANTHEISM;Huamini kila kitu ulimwenguni kina sifa ya kiroho ya uungu ila hiyo sifa haipo nje ya ulimwengu.
4.THEISM;Huamini Mungu aliumba ulimwengu na anaendelea kujihusisha na shughuli za dunia na wanadamu.
Hili kundi la nne(THEISM) lina matabaka matano pia yaani
1.DUOTHEISM; Wanaamini ktk miungu wawili wenye kukadiriwa kuwa na nguvu sawa.
2.HENOTHEISM; Wanaamini Mungu mmoja mwenye miungu wasaidizi wengi
3.MONOTHEISM; Wanaamini ktk Mungu mmoja ambaye ni Mungu mme/Male Deity
4.POLYTHEISM; Huamini miungu wengi wake/waume male and female deities
5.TRINITY; Huamini nafsi tatu ktk Mungu mmoja,hii ni aina ya ile Monotheism pia
NB:
YAKO MAKUNDI MATATU YALIYO KINYUME NA MISINGI YOTE YA IMANI TAJWA HAPO JUU
A.)AGNOTICISM;Hili ni kundi ambalo halijafanya maamuzi kuamini kwamba kuna uungu au la .
B.)ATHEISM; hawaamini chochote kuhusu Mungu
C.)STRONG ATHEISM; Hawa wako extremely and fanatic ktk kukataa kuhusu kuwepo kwa Mungu
*DINI MBALIMBALI NA MISINGI YA IMANI ZAO*
Pamoja na makundi tajwa hapo juu,kuna makundi mawili zaidi ambayo yanatokana na wapi imani hiyo iliasisiwa ikiwa na mshikamano(affiliation) na mzizi gani.Kwa hiyo tunazo
Abrahamic Faiths(Judaism,Islam and Christianity) na pia tunayo Dharmic Faiths.Ingawa asili yake ni India (Hinduism) lakini neno hilo linatumika kuzieleza dini zote za mashariki ya kati na mbali (Buddhism Hinduism,Jainism,Shinto,Taosm,Sikhism) Etc etc
TAKWIMU ZINAONESHA KATI YA DINI KUBWA 19 THE MOST POPULAR
NI HIZI, KATI YA WANADAMU WANAOKADIRIWA KUZIDI BILIONI 6.5 , BILIONI 2.1 NI WAKRISTO, BILIONI 1.6 NI WAISLAMU NA DINI YA TATU KWA WINGI WA WATU NI CTR (CHINESE TRADITIONAL RELIGIONS) YENYE WATU MILIONI 780
*TAOISM*☯
Hii ni dini most popular huko China,inaamini ktk mamia ya miungu (watu wasiokufa/immortal people) ,iliasisiwa na Deo De Jing(inatamkwa Tao Te Ching) Imani imejengwa juu ya kuamini nguvu/nishati isiyobadilika,inayojitosheleza,isiyo na muundo/kuumbwa ilikuwepo kabla ya ulimwengu na inaendelea kuwepo ktk kila kitu,imebezi ktk zoezi liitwalo Qi gong/Tai Chi-exercise na falsafa yao kuu ni hii *_"Kama unaamini kitu fulani basi ni halisi"_*
*SIKHISM🕎🕉*
Dini yenye asili yake yake India,inatokana na neno sikh (sanskrit/sisya-student/disciple)
Neno hilo sanskrit ni mtu yeyote anayeamini uwepo wa nafsi isiyokufa (🦁Lion-Sikh)
Falsafa yao ni _Ishi kwa namna ambayo Mungu angependa._
*Mungu hawezi kubainishwa jinsia yake,Ni wa milele,anajitegemea,naye amefunuluwa na Guru (Gurus ni walimu waliokuwa na asili ya kiroho na kibinadamu (walikuwepo miak 239 kati ya 1469 na 1708)
*Wanaamini Mungu mmija wa dini zote na kuwa hakuna dini moja inayoweza kudai Mungu ni wa kwao
*SHINTO*
Wanaamini katika kuwaabudu 'Kami' yaani roho,kuwa hizo roho zipo karibu na wanadamu na wanasikia dua zao,wanazo nguvu za kuathiri nguvuza aili na matukio ktk maisha ya mwanadamu ,wanawesa kutoa uzima na kuwaweka watu vizuri (Musubi) na mapenzi mema (Makoto),Sio kami wote ni wazuri wapi waovu
*BAHA'I*
Yatokana na neno Baha'ullah mwanzilishi wake i Abdu-Baha ilijitokeza toka ktk dhehebu la Shia karne ya 19 huko Iran.Wanaamini Mungu hawezi julikana (Unkowable God) ,Ni kweli yeye ni muumba mwenye sifa zote,Lakini haiwezekani mwanadamu amfahamu,yaani ufahamu wa kiumbe kinachoweza kufa hakiwezi kumfahamu Muumbaji. Pia husema kila tunachofikiri kuhusu Mungu sio Mungu halisi,yeye hajulikani,hafikiriki.
*JAINISM*
Hawa hawaamini kuhusu Mungu,wala miungu ,Ila wanaamini ktk ukiroho/uungu(au ukamilifu wa viumbe vinavyohitajiwa/stahili kuheshimiwa,wao wanaweza kueleza kwa wepesi swala la uovu kwa kuwa hawaamini kuhusu Mungu. Wanaamini kila kiumbe kinaweza kuwa mungu kwa sababu kinaweza kuwa *perfect*
Jainists hawana sala na maombi ya kuomba kwa Mungu (God-focused prayer),wao maombi yao ni kwa nja ya kujikumbusha matendo mema na sifa nzuri za tirthankaras,hawaamini uumbaji wa dunia.
*TUNAWEZA KUFANYA SURVEY KTK DINI ZOTE ZINA MAMBO YA KUFANANA, NA HIZO NDIZO DINI AMBAZO MATAIFA YALE YANAJISIFU NI DUNIA YA KWANZA WAMEYASHIKA NA KUYAAMINI, LAKINI SISI KUPITIA KWA YESU KRISTO TUMEKIRIMIWA KUMFAHAMU MUNGU PEKEE WA KWELI*
*Yohana 17*
*_Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma_*
*KAMA MPAKA SASA HUJAINGIA KTK NJIA HII (IMANI HII) YA MUNGU HUYU ALIYEJIFUNUA MWISHO WA SIKU HIZI KATIKA YESU KRISTO (HEBREWS 1:1-3) BASI HUU NI WAKATI SAHIHI, HAKUNA WOKOVU KWA MWINGINE AWAYE YEYOTE,HAKUNA JINA JINGINE,HAKUTA TUMAINI LINGINE, HAKUNA POPOTE KWENYE KWELI YOTE ILA KWA HUYU MUNGU MKUU NA MWOKOZI YESU KRISTO*
Mwl Proo
0762879363 (whatsapp)
0718922662(calls/texts)
alltruth5ministries@gmail.com

No comments:
Post a Comment