Wednesday, October 16, 2024

MAISHA YA VIJANA WA KILEO

*NACHELEWA KIDOGO KUELEWA, AU KUAMINI MAISHA YA VIJANA WENGI WAKRISTO WA KILEO* 🤔🤔🤔


_Anaandika Mwl Proo_ ✍️ 

Mwaka huu nimetimiza miaka 20 tangu nilipoamini Injili na kuokoka. Miaka ya hapa usoni, nimechunguza maisha na mienendo ya maisha ya vijana wakristo, ukiacha wachache, wengi wao (majority) maisha yao huoni tena ule ushindi, ile ladha, ule uchaji/kicho, ile bidii, ule ukiroho... Najiuliza hawa wanashindaje? wanaishije maisha ya utauwa katikati ya uchafu mwingi ulioletwa na utandawazi? Mbona hawazipigi mbio zile tulipiga? 🤔🤔🤔 

Wakati ule naamini na kuwa mwongofu, hakukuwa na maendeleo makubwa ya teknolojia, Shule ya Sekondari Ya Wavulana 1,400, wenye viswaswadu tulikuwa wachache mno. Nakumbuka kule kuomba kusikokoma, nakumbuka mifungo ya lazima na hiari, iliyofanya kuwa na siku mpaka 204 za kufunga kwa mwaka, mpaka ikawa desturi ya kuwa na wastani wa siku 3 au 4 za kufunga kila wiki. Nakumbuka kuhusu gatherings & fellowships siku 6 kila wiki, ukikosa siku moja, jiandae kupokea wapendwa kibao huko kwako wakija  kujua sababu ya kukosa ibada. Nakumbuka namna tulisumbuka kuomba ruhusa ili kuhudhuria semina zote za Mwakasege, mikutano ya injili kule Biafra na Jangwani. Nakumbuka namna ambayo hakuna Joint-Mass tuliwahi kuikosa weekends zote pale DIT, IFM, UDSM na penginepo, makongamano yote ya pasaka hakuna hata moja tuliwahi kukosa kwa sababu yoyote. Nakumbuka jinsi ambavyo tulishikamana na mafundisho ya fellowship yetu kuwa hakuna mahusiano (relationship)  kwa wanafunzi wa Sekondari kidato cha kwanza mpaka cha sita.. Uhusiano halali pekee ni  'Kaka' & 'Dada' (Na watu tukaishi maisha hayo hayo) kile kinachoitwa Boyfriend &. Girlfriend kuna sisi hapa hatukuwahi jua kama kipo... Na ndio maana haikuwa ajabu, si ajabu kwa sisi wa kizazi kile na maisha yale yenye nidhamu ya kiroho kuwa tuliishi bila zinaa, haikuwahi kutajwa kwetu kamwe, tulikuwa hata hatufananii mambo hayo... (Our walk with the Lord shaped our lifestyles)... Tunao ujasiri wa kusema tulishinda tamaa za dunia na mambo yake. Yale maisha ya utauwa yalifanya hata nikiona kapicha tu kwenye gazeti au Tv kenye viashiria nudity (uchi) tachukia hapo vya kuchanwa vitachanwa, vya kufutwa vitafutwa, vya kuondolewa vitaondolewa, na nitafanyia kazi fikra zangu kuhakikisha no memories za huo uchafu zitabaki hata kwa mbali 🧠. Sasa kwa nini naandika haya.... Nimeona miaka ya usoni yale mazoezi ya kiroho yaliyotupa kuishi maisha ya wokovu yenye   ushindi, yenye usafi kimwenendo, ni kama yanakwepwa sana na vijana... Hesabu idadi ya vijana kwenye mikesha ya maombi, kwenye makusanyiko ya mifungo, na huduma nyingine...... Vijana wengi utawapata kwenye programs & events (they live too ceremonial)... Ndio najiuliza kwa lifestyle hii ya kwao, wanaweza kuishi maisha ya utauwa hawa? Na uchafu wote wa kwenye TV wanaweza kuepuka hawa kujaza vitu vichafu  kwenye nafsi zao? Nguvu zao chache watashinda kweli na ushawishi wa mitandaoni, picha za uchi kila mahali, sio Facebook, sio Instagram, sio TikTok sio WhatsApp, hata kama huja-follow kurasa mbaya utakutana tu na watoto wa Belial ambao kutwa nzima wanatengeneza contents za utupu.... Vijana wa sasa wanashindaje? Wanaepukaje uasherati? Wanaepukaje usagaji na kujichua? Mnaepukaje kuwa na mazungumzo mabaya mkiwa mnawasiliana wa jinsi mbili tofauti? Mnawezaje?  Yale ambayo yalikuwa ni sababu ya kuwapa ushindi hamyafanyi, mmeyakimbia, mnawezaje kushinda? Ni vijana wangapi wa kileo wapo serious na ratiba za kusoma na kujifunza maandiko, na wakawa strict kuhakikisha wanazifuata? Nilihitaji miezi 8 tu kwa mwaka kumaliza vitabu 66 vyote vya Biblia (tena nasoma kwa parallel-system:- English Bible juu/Swahili Bible chini)... Kijana ambaye kinachomfurahisha ni matamasha ya muziki pekee, anavukaje kwa ushindi??

_mwlproo_
Ujumbe huu ufikishwe kwa vijana. Kwamba maisha safi ya Kikristo yanahitaji nidhamu, utauwa ni wa kujizoeza, mpaka ifikie mahali mambo yote yasiyofaa unayachukia, huwezi puuzia mambo ya muhimu ya kiroho na ukabaki salama tu, ukipuuza nidhamu na bidii kwenye kujifunza maandiko, nidhamu na bidii kwenye kuomba, nidhamu na bidii kwenye kufunga, nidhamu na bidii kwenye kufanya huduma, jiandae kuwa na maisha ya hovyo, kurudi nyuma, na kutawaliwa na matendo ya mwili... Zingatia sana hayo nisemayo, inawezekana kabisa kuwa na mienendo safi, maisha yasiyo na uchafu, uadilifu kama iwapasavyo watumishi wa Kristo Yesu... Katika zama za Teknolojia hizi unaweza kuchagua kubaki kijana wa mfano, kinara kwa mambo ya kiroho, mnyoofu kabisa kiuadilifu na maadili, si tu ukiwa kwa watu, bali ukiwa sirini sana, bado uwe mnyoofu!


Asante kwa kusoma... Tuwasaidie, tuwaombee vijana!

Mwl Proo
0762879363
Bado tunatoa ofa ya vyombo vya muziki kwa makanisa kwa bei ya sadaka. Piga simu uweke oda yako

1 comment:

  1. Ubarikiwe Mtumishi mbona hatuoni post mpya humu jamvini? sikuizi huposti mara kwa mara nini shida mtumishi?

    ReplyDelete