Friday, December 8, 2017

BASI SASA, NAFANYA NINI HAPA!

*B͟A͟S͟I͟ S͟A͟S͟A͟, N͟A͟F͟A͟N͟Y͟A͟ N͟I͟N͟I͟ H͟A͟P͟A...͟*🤷🏽‍♂

*_ʍաӀ Թɾօօ_*
~0762879363 (Whatsapp)~
_*(mjumbe wa matengenezo)*_

Haleluya, Haleluya!
Kuna watu wengi nyakati hizi wako chini ya miretemu 🌳, viroho vyao, huduma zao, uchumi wao, na kila jambo linaliwahusu lime-stuck/kwama kwa namna fulani, kunahitajika geuko thabiti *turnaround*, ili wakae sawa.

*UKIKAA CHINI YA MRETEMU KIROHO, UNAKUMBWA NA MAMBO MAWILI MAKUBWA*

*_💡KU-OPARETI CHINI YA VIWANGO_* (Your General Spiritual Performance inakuwa chini).
Nabii Eliya Mtishbi, mmoja kati ya manabii hodari sana, alipokaa chini ya mretemu aka-opareti chini ya viwango. Ni nabii huyuhuyu ndiye aliisimamisha mvua, ni nabii huyuhuyu aliyemnyima raha mfalme hadi mfalme akambatiza jina *mtaabishaji wa Israeli*, huyu aliomba moto ukashuka na kuzilamba sadaka na maji na kuni, ni huyu ndiye aliyeamuru the beheading ⚔ of 400+ ya manabii wa Baali, _what a hero!!_. Akiwa chini ya mretemu alioparet chini ya kiwango, na akaanza kumtetemekea malkia Yezebel, wakati hata boss mkubwa Ahab, hakumwogopa sikuzote.

Ndivyo ilivyo leo kuna watu wa Mungu wengi mpaka watumishi, ambao wanaopareti chini ya viwango (GSPA), kwa sababu ya kunasa chini ya miretemu. Ulimwengu wa kiroho una ma-super Giants ambao walishawahi fanya mambo makubwa, wakatunukiwa vyeo vya kiroho, then kuna mambo yaliwakwamisha (kama vitisho vya Jezebel), na wakabaki wamelala chini ya miretemu ya mashaka, wakiopareti chini ya viwango. Eliya alihitaji *Neno la Bwana*, limpe geuko *turnaround*, na alipotoka chini ya mretemu akapokea kitu kipya.

1 Wafalme 19 : 9
_*Akafika kunako pango, akalala ndani yake. Na tazama, neno la Bwana likamjia, naye akamwambia, Unafanya nini hapa, Eliya?*_

*_💡KUPITWA NA FURSA KATIKA ULIMWENGU ROHO_*
Wanaokuwa wamenaswa chini ya miretemu, mambo yao yakiwa-stuck, wanatawaliwa na *missed opportunities*, mamvo mazuri rohoni yaliyopasa kuwapata, yanawapita.

Yeremia 46 : 17b
_*.......muhula alioandikiwa ameuacha upite.*_

Andiko hili katika kingereza (NIV) linasomeka *"He has missed his opportunity"*. Kumbe kiroho kuna kumiss fursa, na hili linawakumba wengi zama hizi unknowingly.

*JE! UNAOTA NDOTO ZA NAMNA HII?*
🚀 Unaota ndoto za kuchelewa kwenye kituo cha mabasi, na basi limekwishaondoka? unashtuka ukiwa hujapata suluhu, umebaki unayongayonga kwenye bus terminal/stop, ukiumia?

🚀 Unaota ndoto za umeshuka kwenye basi mara moja, labda kwa ajili ya chakula au kuchimba dawa, then unaachwa?

🚀 Unaota unaenda kwenye chumba cha mtihani, ila umekawia sana?

🚀 Je! unaota upo kwenye foleni/queues za mgao wa chakula, au unasevu chakula ila haubahatiki kabisa kula, na unastuka usingizini moyoni mwako unahisi deni, why you didn't eat, na ulikuwa ukihisi njaa haswaa

🚀 Ndoto za kuona mtumishi mkubwa wa Mungu, au kiongozi wa kiserikali, na ukaona una shauku ya kumwambia kitu, but unakosa nafasi unaishia kumsalimu tu, huku unapanga moyoni namna ya kupangilia sentensi zako, na unastuka ukiwa hujapata nafasi ya kumwambia.

🚀 Ndoto za kuota umestuka usingizini umechelewa ibadani, au umeigia kanisani unakuta wamemaliza ibada, na inaonesha watu wamehudumiwa sana na Mungu, unajibidiisha kujiweka nao sawa, haifui dafu, unasimulia jinsi ulivyopitilizaza kwa usingizi haizai matunda, na unastuka you still feel ile hali ya ndotoni

🚀 Kuna mpango mkubwa wa pesa, biashara, scholarship n.k, lakini mpango ukiwa kule ndotoni haukamiliki, au ubaona kabla hujapata maelekezo sahihi ndoto imekatika...

🚀 Umepotea njia, na unaota umejitahidi mpaka ukafik karibu na njia unayoifahamu, ndoto ikakata (Mara nyingi hutumiwa mitaa uliyowahi kuishi siku za nyuma sana)

👆🏾👆🏾👆🏾👆🏾👆🏾👆🏾MIFANO HIYO MICHACHE YA NDOTO, YOTE INA MAANA MOJA YA KUWEPO KWA *MISSED OPPORTUNITIES*, KUNAKOTOKANA NA KUNASA CHINI YA MIRETEMU, YAANI YALE MEMA YA MUNGU YANAKUJIA, HAYAKUKUTI KATIKA NAFASI YA KUYAPOKEA, KUMBUKA HATA KAMA ULIANDIKIWA BARAKA NA USHINDI NA KUINULIWA, UKIWA NJE YA NAFASI, U CHINI YA MRETEMU, ULIYOANDIKIWA YANAWEZA KUKAWILISHWA AU KUAHIRISHWA *(DELAYED/POSTPONED OR RELENTED)*.

*INAKUWAJE MTU AKANASWA CHINI YA MRETEMU?*

🚦Mtu akiacha kudumu katika *huduma na maombi*, ni rahisi sana kunaswa chini ya mretemu. Haya mambo yanaenda pamoja, kila mwamini ni mtumishi, hapaswi kukoma katika haya mawili, jitahidi upate somo langu katika blog na page ya kihuduma ya facebook, liitwalo *HUDUMA NA MAOMBI; NI YA MUHIMU SANA*. ukiacha kimoja wapo slowly utaanza kupiga hatua kuelekea chini ya mretemu.

🚦Kupuuzia maonyo yanayoletwa kwako kwa njia ya neno (linalohubiriwa), na ndoto za kuonywa juu maanguko au hali yako ya kiroho kutoridhisha.. Upuuziaji huu hauwaachi watu salama, lazima baada ya muda fulani, utajikuta chini ya mretemu (Mithali 1:30, 29:1).

🚦Kuruhusu upuzi kukaa katika hema yako (Ayubu 11:14). Kuna mambo ambayo ni ya kipuuzi, ukiyaruhusu ktawala hema yako, amin nakuambia baada ya muda utajikuta tu chini ya mretemu. Mtumishi wa Mungu, sharti aishi kwa standards za kitumishi, wala hapaswi kujaribisha ujinga kidogo. Kuna wachungaji  una mke/familia, ukaruhusu mazoea na personal  secretary/mshirika binti, anaanza kukuita kwa petty names za mapenzi kama dear/baby/darling/sweetheart etc na ukayavumilia, ukayapa ushirikiano hayo majina, anayatumia akikutext au mkiwa peke yenu. Au wewe binti umeruhusu kutembelewa na kijana chumbani kwako, and it is often times, unaruhusu kuguswa au kushikwa hata maeneo ambayo siyo kabisa. Hapa Biblia inaita umeruhusu upuzi ndani ya hema yako, And I bet you, the *broom tree🌳* is coming your way.

🚦Dhambi zisizo tubiwa, kuendelea katika kutenda dhambi, bila kufanya toba halisi inayolenga kuacha kwa kugeuza direction kabisa na kuyatenda matendo ya kwanza. Ili kufahamu maana kamili ya toba/teshuvah (jipatie somo langu liitwalo *KUNA TUMAINI KATIKA TOBA, HATA KAMA KOSA NI KUBWA*, na ujue kuhusu toba kikamilifu)

*NAFANYA NINI, NIKIJIGUNDUA NIKO CHINI YA MRETEMU?*

Isaya 52 : 5b
_*Basi sasa, nafanya nini hapa, asema Bwana, ikiwa watu wangu wamechukuliwa bure?........*_

JAMBO LA MSINGI SANA, NI KUTENGENEZA *TURNING POINT* FORCEFULLY, HIYO SENTENSI HAPO JUU NI BWANA ALITAMKA, NAMI NIKAIAZIMA KWA AJILI YAKO. UKIJIONA CHINI YA MRETEMU, JIULIZE, JIHOJI KWA HASIRA NA NIA YA BADILIKO KUSEMA,  _*"BASI SASA (IMETOSHA), NAFANYA NINI HAPA (CHINI YA HUU MRETEMU"*_. NA CHUKUA HATUA MARA MOJA, MAANA WAKATI MTU AKIWA CHINI YA MRETEMU ANATAWALIWA NA ROHO YA MAUTI KATIKA KILA JAMBO, MAANA NAFSI HUPIGILIWA MISUMARI NA KUFUNGWA KWA KAMBA ILI USINASUKE KWA HARAKA. MKUMBUKE ELIYA, AKIWA CHINI YA MRETEMU AKAANZA KUSEMA BWANA YATOSHA, UNIUE TU, YEYE NI MWANADAMU AMBAYE MUNGU ALIMWEKEA RATIBA YA KUTOONJA MAUTI, LAKINI AKIWA CHINI YA MRETEMU NAFSI YAKE ILICHAGUA KUFA. CHUKUA HATUA JINASUE, ONDOKA CHINI YA MRETEMU NA UANZE MARA MOJA KUYAIMARISHA YALE YALIYOSALIA, YANAYOTAKA KUFA. MUNGU AKUSAIDIE SANA

JE! FURSA ULIZOPOTEZA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO ZINAWEZA KUKURUDIA?

Moja ya wakufunzi wa Udsm, tukiwa katika semina fulani, alitufundisha *Time is non retrievable*, muda hauurudishi ukipita na kupotea. Kukaa chini ya mretemu ni kupoteza muda (time/opportunity), ndio maana swali la kwanza linakuwa unafanya nini hapa? Ndivyo Bwana alivyomuuliza Eliya, nas tunalitumia swali hili kwa mtu tunayeona anapoteza muda kwa mambo hatuyaelewi.

*TUMAINI*
KWA MUNGU WETU, TIME IS RETRIEVABLE, YAANI MISSED OPPORTUNITIES ZAWEZA REJEZWA KWA UPYA, WASTED YEARS ILIYOLIWA NA TUNUTU, NA PARARE, NA MADUMADU, MUNGU ANAWEZA KUKUREJEZEA KABISA, UKITENGENEZA NA BWANA (Yoeli 1:4, 2:25)

Yoeli 2 : 25
_*Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu.*_

Mwl Proo
0718922662/0762879363

alltruth5ministries@gmail.com

3 comments:

  1. Aise umeipiga hili somo sawa sawa. Hakika nimepata sehemu yangu, Mungu wa mbinguni na akubariki Sana shujaa

    ReplyDelete