*USIPOSHUGHULIKIA UDHAIFU, WAWEZA ONDOLEWA KATIKA NAFASI(OFFICE/POSITION). MUNGU HUJITAFUTIA MTU KUICHUKUA NAFASI HIYO*
*_ʍϖʆ Թɾσσ_*
*+255762879363*
Shalom Shalom!
Siri za Bwana, ziko kwao wamchao (Zaburi 25:14), pokea siri hizi..
Wapendwa katika Kristo Yesu, naamini kila mtu ni wa kipekee kwa Mungu, naamini juu uvumilivu wa Mungu kwetu, na namna Yesu hutuchukulia udhaifu wetu kwa kipimo cha uvumilivu akijuacho yeye mwenyewe (Ufunuo 2:21). Pamoja na hayo, si kweli kwamba Mungu ataendelea tu kukuonya juu ya udhaifu unaokukwamisha daima, nawe haushughuliki nao ili kuutua huo unaosimama kukuzinga kwa upesi (Ebra 12:1). *_NI MUHIMU KUKUMBUKA, MUNGU HAWI RADHI NA WAPUMBAVU (Mhubiri 5:4b)_*. Yaani anakuonya juu ya udhaifu wako, ukaamua ku-mark time tuu, bila hatua yoyote
DHAMBI KUTOKUKEMEWA SANA, HAIIFANYI ISIWE NA ATHARI, INABAKI KUWA NA ATHARI VILEVILE. KWA HIYO UKIONA MAKALI YA YULE MCHUNGAJI WAKO KUKEMEA UZINZI (NA DHAMBI YOYOTE UIJUAYO) KAMA YAMEPUNGUA, NA UNAONA KAMA KUNA MWANYA MWEPESI ZAIDI TU, WA KUFANYA DHAMBI, HAIIFANYI HIYO DHAMBI KUWA ISIYO NA MADHARA. HATA WAKATI AMBAPO HAKUNA MAKEMEO MAKALI JUU YA DHAMBI, WEWE BAKI UNAYACHUNGA MAISHA YAKO, WALA USISEME MARA HII TU MOJA!.
Hatutarajii uliyeokoka kusikia unaendelea na maisha ya dhambi, lakini upo ukweli wa wazi kwamba ukiyachunguza na kujipima maisha yako (2Kor 13:5, Gal 6:4), unaweza kugundua kuna mahali pana shida.. Siungi mkono ule uhalalishaji haramu wa udhaifu kwa kusema *_"kila mtu na udhaifu wake bwana"_*, Lengo likiwa sio kuonya watu watafute kushinda madhaifu hayo, bali hutumika kama ngao/shield 🛡, muda akionywa mkosaji. Sasa Bwana alinifundisha jambo miaka karibu miaka 8 iliyopita, kwamba *_Waweza kubakiwa na udhaifu mmoja, lakini uushinde na huo, ili ukae na Bwana, maana Yeye hawi radhi na wapumbavu (watu ambao wana-ignore maonyo, na kuendeleza kutimiza dhambi zao)._*
MTU HAUSIFIWI MBELE ZA BWANA KWA KUSHINDA MENGI, KWAMBA OOH UMEJITAHIDI KUYASHINDA MENGI, BALI UNAHIMIZWA JUU YA HUU UDHAIFU AMBAO, WEWE MWENYEWE UKIHOJIWA JUU YA UNYOFU, MOYO WAKO UNAKUELEKEZA HAPO TU. WAKATI AMBAO NILIJIFUNZA HAYA, NILIKUWA KATIKA KUJIJARIBU NA KUJIPIMA MAISHA YANGU YA KIROHO. HIVYO NILITAMANI KUJUA HIVI HAPA NINADAIWA NINI KWA HABARI YA UNYOFU, YAANI KATIKA YALE NIYAJUAYO, NISIYOYAJUA KWAMBA NAKOSEA ATANIFUNDISHA MUNGU, NIKIJUA SITATENDA TENA HAYO (Ayubu 34:32). KAMA AMBAVYO KILA MMOJA DHAMIRI YAKE INAMSHUHUDIA, TENA NAFSI YA KILA MMOJA YAJUA SANA, NAMI NIKAONA KWAZO MOJA, KWAMBA PAMOJA NA KUISHI MAISHA YENYE KICHO, LAKINI NILIKUWA NAFANYA MAWASILIANO NA BINTI FULANI, HAYAKUWA MAZURI SANA, YALIGHARIMU MUDA MWINGINE KWENDA KUZUNGUMZA NA SIMU NJE 📱👦🏽👧🏻📲. SO KILA NIKIGEUKA, NIKABAKI NAELEKEZWA HILO NI LA KULIONDOA. ILI KULIELEWA HILO, NDIPO BWANA AKANIPITISHA KATIKA KITABU CHA WAFALME I&II, NAMNA TANGU ZAMA ZA SULEIMANI, ASA, YEHOSHAFATI, YOASHI, AMAZIA, AZARIAH, YOTHAMU NA HEZEKIA. KULIKUWA NA UDHAIFU MMOJA, AMBAO MUNGU HAKUU-IGNORE ETI KWA KUWA NI MMOJA TU, SOMA HAPA CHINI
1 Wafalme 15 : 5
*_kwa sababu Daudi alifanya yaliyo mema machoni pa Bwana, wala hakukosa katika yote aliyomwamuru, siku zote za maisha yake, isipokuwa katika habari ya Uria, Mhiti._*
Mungu ambaye hawi radhi na wapumbavu, hakukaa kusifia unyofu wa Daudi, bila kupin-point udhaifu, akayasifu yote with exception, kwenye ule udhaifu akaonesha kuna doa.
Katika hao wafalme wachache na wengine wote waliotajwa toka 1Falme 11 mpaka 2Falme 18, uko udhaifu mmoja uliokuwa ukiendekezwa, yaani kulijengwa mahali pa juu (high places), kwa ajili ya matoleo kwa miungu. Wafalme wengi walikuja, Biblia inataja kila mmoja hata kama alitenda mema, lakini *final remark* imeandikwa kwamba lakini mahali pa juu, hapakuondolewa, mpaka akaja aliyeuondoa na huo udhaifu mmoja.
*MOYO WA SOMO*
Jambo la kwanza ni hili, udhaifu usioshughulikiwa, wale kupelekwa kwa Bwana akushindie, ukaamua kuulea, waweza kukufanya uondolewe katika ofisi, au nafasi uliyoketishwa 💺.
Isaya 22:19
*_19 Nami nitakusukuma na kukutoa katika mahali pako, naye atakushusha utoke hapa usimamapo._*
MUNGU ANAWEZA KUKUPA MUDA MWINGI, ILI YAMKINI UWEKE VITU SAWA, NA KWA KUWA WEWE NI WA THAMANI NA WA KIPEKEE, TENA ALITUMIA GHARAMA KUKUANDAA, ATAENDELEA KUKUPA MUDA ANAOJUA YEYE. LAKINI KAMA HUTASIKIA KUTAKA KUGEUKA, NAKUPA UHAKIKA HUU, ATAFANYA *_REPLACEMENT_*, NA HIYO NAFASI ATAMWEKA MWINGINE ATAKAYESIMAMA MBELE ZAKE KWA UKAMILIFU, SOMA HAPA
Isaya 22:20-21a
*_20 Na itakuwa katika siku ile nitamwita mtumishi wangu Eliakimu, mwana wa Hilkia;_*
*_21 nami nitamvika vazi lako, nitamtia nguvu kwa mshipi wako, nami nitamkabidhi yeye mamlaka yako;_*
HUU NDIO UJUMBE AMBAO UMEKUWA UKINIWAKA KAMA MOTO 🔥🔥, KWAMBA MUNGU HAWI RADHI NA WAPUMBAVU, KUNA MAMBO AMBAYO UKIDUMU YA KUYATENDA (MADHAIFU), YANAKU-DISQUALIFY KUKAA KATIKA POSITION FULANI💺 KATIKA ROHO, UKIWEKA MAMBO SAWA, UNAREJEZWA KWA HIYO OFFICE/POSITION, LAKINI UKIAMUA KUYAENDEKEZA HAYO, BILA KUTAFUTA MSAADA WA BWANA AKUSHINDIE, MUNGU ANAZIBA ILE NAFASI, HATAVUMILIA KUWA NA JAMBO LISILOTENDEKA, KWA SABABU, MHUSIKA UMEKAA NA UDHAIFU, UKAKUONDOA KWA NAFASI.
NB:-
KUKIWA NA MWENENDO USIOFAA, LAZIMA MUNGU ATAKUONYA KWA NDOTO, MAONO, SAUTI YA WAZI HATA KUTUMA WATU PHYSICALLY. LAKINI USIPOYASIKIA HAYO MAONYO KWA MUDA MREFU, ANAWEZA KUACHA KUKUONYA, AKAKAA KIMYA, LAKINI JUA GHARAMA YA KUTENGENEZA BAADA YA MUNGU KUACHA KUKUONYA JUU YA KUENDEKEZA UDHAIFU, INAKUWA KUBWA. UNAPOFANYA HIMA KUTENGENEZA MARA BAADA YA KUONYWA NA BWANA, UNAPOKEA DEZO FULANI HIVI, MAANA MAONYO HAYO HUAMBATANA NA NEEMA FULANI YA KUKUSAIDIA KUTENGENEZA (2Nyakati 29:36).
Mungu akubariki na kikusaidia...
By Mwl Proo
0762879363
0718922662
alltruth5ministries@gmail.com
@2017 *🅜🅦🅐🅚🅐 🅦🅐 🅚🅤🅣🅔🅝🅓🅐 🅚🅐🅩🅘*
1Ƙσɾ 15:58, уσнαиα 9:4
No comments:
Post a Comment