Friday, December 1, 2017

NYIKA TUPU!

*NYIKA TUPU*

Mwl Proo
0762879363

Haleluya Haleluya!!
Kwa kuwa tunaye Mungu, hakuna mazingira magumu yoyote kwetu, hakuna hali zozote za kutufanya tushindwe, no need to despair (giving-up) and no need to give-in (kwamba basi tu, tutafanyaje unafikiri, tukubaliane na matokeo). Hakuna mahali patamu, kama  mahali ambapo akili za kawaida zimegoma, resources mlizo nazo zinapunguka kutimiza makusudi, kuna deficits na shortfalls, huo ni mtaji mzuri sana aisee. Nyumbani kwetu nilipolelewa, tangu kuzaliwa kwetu mpaka tunakuwa watu wazima, kulikuwa na kibao sitting room, kiliandikwa *GOD IS THE SOURCE OF MY TOTAL SUPPLY*, Nilipopata elimu ya kuweza kusoma kingereza, baba alinisomea hayo maneno, na kunielezea. Lakini sasa ndio nina yaelewa sana, nikiwa nimejaa imani katika Mungu. Ni wachache wanamwelewa Paulo....

2 Wakorintho 12 : 10 *_Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu._*

Ni nani mtu yule baada ya kugundua bajet ya harusi imegoma, atacheka moyoni, kwa sababu ya kumjua Mungu wa miujiza kwamba hizo ndizo anga zake sasa. Unapokuta upungufu, kuishiwa,  sio nafasi ya kulialia, wala usipange kupiga dili. Leo hii kuna vitu ambavyo ni kupiga madili in the name of upako. Kama umenunua katoni kadhaa, za dasani sijui maji ya uhai. Ukadai uliyahatamia kwa maombi, na chupa cha mia sita unauza elfu 10 as anointed water, you are just enjoying supernormal profit, ukiwa hata TIN number ya TRA huna, hilo ni dili, katika jitihada za kushindana na upungufu, utalitolea hesabu lakini (Sio hoja yangu ya leo, that is called *_Simony act_*).

Mungu tuliye naye ni wa kweli, anaweza ruhusu deficities na shortfalls akijua kwamba utayalekeza kwake hayo, yaliyo-fail. Yeye si lazima kuwe na vitu vya kusaidia au dalili ya muujiza, kutoka katika viashiria vya kutowezekana kabisa, ndio mazingira yanamuongezea ladha. Anaweza kuhitaji ulichonacho mkononi kama chanzo, lakini sio mara zote, maana hapo napo, walimu wa ujasiriamali wameongeza idea ambayo haibalansi kwenye injili, masomo ya ujasiriamali yame-replace Sunday-schools zote katika kutafuta kunasua wapendwa kiuchumi, watu Mungu wao hawajamwelewa vizuri, kwa hiyo wanapata vijipesa kwa mfumo ule wa kawaida tuu, without any supernatural increase (SUBSISTENCE INCOME), na hatuwapati tena kwenye mid-week services. Ila endeleeni sina ukorofi na mafunzo ya ujasiriamali... Ila I wish mwe na Mungu huko, ambaye supernaturally atafanya mazidisho. Mungu aliyashusha mabeberu ya kiroho ili ku-mate na mifugo ya Laban, alipopunja mshahara wa Yakobo mara 10. Yaani alipostahili kulipwa laki 7, akapewa elfu 70. Mungu ambaye alipindua formula ya mazao ya shamba (Mwanzo 26:12) akafanya muujiza wa kipimo kimoja kwa mia, anataka umjue ili kwenye Biashara zako, wakati umebanwa na mamlaka husika kama Sumatra, TRA, Ewura,Tbs, TFDA, Badala la kufanya dili la kuwaibia, Mungu ambaye ni Shujaa wa Yakobo, anataka katikati ya mfumo mbaya unaokukandamiza mpaka wakati mwingine unalaani mashine za EFD📠📟, Mungu wa miujiza tunayemwabudu anaweza kufanya muujiza uka-make profit bila kuchakachua. Hali za kiroho za wengi zimedorora, kwa sababu mfumo wa uchumi ni mgumu, unaolazimisha kufanya uchakachuaji, sasa katika kuchakachua processes wengi wanatengwa na Mungu. Hawako huru tena kumwendea Mungu, akikumbuka kodi aliyopora TRA, akikumbuka mizigo aliyocheza dili kuitorosha bandarini, yeye mwenyewe anapiga-pause kumwendea Mungu. Hawezi kutubu maana anajua dhambi hiyo hiyo anapaswa kuirudia mwisho wa mwezi. Kwa hiyo watu hawa hupendezwa sana na zile kauli za *"Kila mtu ana udhaifu wake, hakuna mkamilifu etc"*. Daaah😰

*HIVI HAMSHTUKI, KUWA YALE MABUBUJIKO YA KWELI IBADANI YANAPOTEA?, IBADA NYINGI NI MASHEREHESHO FULANI HIVI, NDIO MAANA TUNADIRIKI KUKODI WAPIGA VYOMBO VYA AKUDO IMPACT WAJE KANISANI🎹🎸🎤🎼*
*MOYO WA SOMO*

Mathayo 14 : 15
*_Hata kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea, wakasema, Mahali hapa ni nyika tupu, na saa imekwisha pita; uwaage makutano, waende zao vijijini, wakajinunulie vyakula._*

Mungu alipoumba, viko alivyoumba bila kuwa na kianzio. *Creatio ex Nihilo* (CREATING OUT NOTHING), Yaani hamna kitu, akakifanya kiwepo. Anao uwezo wa kuleta ambacho hakipo kabisa, sileti hypothesis hapa, huyu ndiye Mungu wa Biblia habari hizi ni za kweli, ndio maana sijawahi kupata sababu ya kuchakachua. Sina baraka maishani mwangu (baada ya kuokoka), ambayo ni matokeo ya kufanya uchakachuaji, hamna kabisa!!! Wengi leo hii wameokoka lakini wapo vyuoni, wanasolve leaked papers, wananunua Research Paper ili wamalize vyuo 🎓 na digrii za kubumba (UMEMFICHA WAPI MUNGU?). Wanafunzi walipoona wapo katika *NYIKA TUPU* , waliona namna pekee ni kumwambia Yesu awaage watu (state of despair). Kumbe wakiwa hapo katika nyika tupu, hata matunda pori hamna, huo ndio mtaji wa Mungu. Yesu anaagiza ketisheni watu katika safu, watu takribani elfu 20 (women/children inclusive) toka katika samaki wawili🐟🐟 na mikate mitano 🍞🍞🍞🍞🍞, walikula wote, vikakusanywa mabaki vikapu 12.

KATIKA MAISHA YAKO, KUNA MAENEO UNAYAONA YAKO NYIKA TUPU. USIYAPIGIE DILI, NYIKA TUPU INAMHITAJI YESU ASIYE BADILIKA. ATATOA MAHITAJI YOTE KATIKA HIYO NYIKA TUPU. WATU WA UCHUMI WANATUAMBIA RESOURCES ARE SCARCE, 😀😀 NIKIWA FORM SIX BWENINI ENEO NILILOKUWA NALALA NILIPABANDIKA KARATASI ZENYE MANENO HAYA *_TO GOD THERE IS CEASELESS SUPPLY, AND INEXHAUSTIBLE STOCK_*, MUNGU HAISHIWAGI UJUE, TUNAKOSEA KUMLETA KWENYE VIWANGO VYA WANADAMU. NAJARIBU KUFIKIRIA ILE JEURI YA KUWAAMBIA WAISRAEL WAKUSANYE KWARE, ILA WAKIROAST, WAKIPIKA MCHEMSHO, NYAMA IKILALA TUPA KULE🐓🐓🐓🐓👉🏾👉🏾👉🏾👉🏾👉🏾👉🏾 KWA SIKU 29 NYAMA KILA SIKU KWALE FRESH, HAKUNA VIPORO. HUYU MUNGU WAPENDWA HAJABADILIKA. WANADAMU WANA KITU KINAITWA FEAR OF THE FUTURE (KUHOFIA WAKATI UJAO). KWA SABABU MAISHA YAMEJAA UNCERTANITIES, BASI WATU WANA WASIWASI WA KUFILISIKA, KUPOTEZA KAZI, KUPATA HASARA YA BIASHARA/RISKS ETC. LAKINI MTU AMBAYE ATAMTAMBUA MUNGU AS THE SOURCE OF HIS/TOTAL SUPPLY, BADALA YA ILE HOFU YA WAKATI UJAO, YEYE ATAUCHEKA WAKATI UJAO..

Mithali 31 : 25
*_Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake; Anaucheka wakati ujao._*

Mungu akusaidie, nyika tupu katika maisha yako, sio nafasi ya kukosana na Mungu, ni nafasi ya shuhuda tuu...

Mwl Proo
*0762879363*

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment