Monday, December 4, 2017

KUOKOLEWA KATIKA KINYWA CHA SIMBA

🦁 *KUOKOLEWA KATIKA KINYWA CHA SIMBA!.* 🦁

*Mwl Proo*
*0762879363*

Bwana Yesu Kristo asifiwe!.
Ndugu mpendwa msomaji, uwapo katika maskani hii, unapaswa kupata neno hai la Mungu, ili upate kusimama siku ya uovu. Yako majira ya kujiliwa (Luka 19:44), na wakati huo kama haukuwa na msingi mzuri wa neno hai, utaishiwa silaha katika ya vita. Kabla sijaendelea na nilichopewa moyoni, nikuhamasishe sana, ukiwa katika shwari na amani kuu, huo ndio wakati wako wa kuomba kwa bidii, wakati ambapo store yako ya chakula imejaa vyakula vyote vizuri (choice food), huo ni wakati wako mzuri wa kuusaka uso wa Bwana kwa kufunga (Zaburi 32:6), zinaweza kukujia nyakati ambazo nguvu ya kufunga haipo, vita imeinuka kubwa, ile akiba ya maombi na kumtafuta Bwana (ile uliyoifanya wakati wa shwari kuu), kutakusaidia nyakati hizo, uvuke salama bila anguko!

Leo moyo wangu, ulijazwa Neno hili, kuokolewa katika kinywa cha simba🦁. Tusome 2Timotheo 4:17

*_17 Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu, ili kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, hata wasikie Mataifa yote; nami nikaokolewa katika kinywa cha simba._*

Sijui ni mara ngapi ulipita hapa, ukajiuliza.  Paulo mtume anasema, aliokolewa katika kinywa cha simba. Ingawa zama anayatamka hayo   kulikuwa hukumu za watu kuwekwa mbele ya wanyama wakali ili waliwe, lakini historia inaonesha, hakuwa akizungumza kuepushwa na kinywa cha simba, kwa hukumu ile, maana alikuwa na kinga fulani, hukumu haikutekelezwa kwa mwenye uraia wa Rumi kama Paulo (Ingawa yeye ni mzaliwa wa Tarsus, Turkey), na alikuja kukatwa kichwa baadaye 68 A.D. Sasa kuokolewa katika kinywa simba, alizungumzia jitihada zote za shetani, kuwinda uhai wake kwa matukio ambayo ni kama kuponea chupuchupu, lakini Paulo alijua yuko Mungu, aliyemnasua katika majanga na hatari zile alizoziita *kinywa cha simba*.

Mpendwa uko ambaye umewahi kupita katika hali ambayo, hujui ilikuwaje ukanasuka, uliumwa ugonjwa ambao huelewielewi ulinasukaje, mauti ikapishwa mbali. Na uko mwingine ambaye sharti uniaikilize kwa makini; Yuko Mungu awazae kukuokoa katika kinywa cha simba. Kuna vikao vya kuzimu, wameandaa yaani wakutakapo kunasa, wakutoeshe kabisa, kuna wachawi wanaokuotea na kuwaza ubaya mkuu mno, unaweza kutwa na ugonjwa ambao ukiwa wodini ndoto zote, unawaza utakavyo kufa, na namna watu watalia. Katika yale matukio ambayo ni almanusura kusalimika, hayo yanaitwa kinywa simba. Kwa wenye uzoefu wa kufuatilia mambo ya wanyapori (Wildlife), wanapata picha jinsi meno ya simba yalivyo, na yakiisha kukamata windo. Unaweza kuwindwa ukaepushwa na maadui wanaokuwinda, lakini pia unaweza kupatikana, na ukawa kimywani mwa simba tayari!.... Bwana hajaahidi tu kukulinda simba wasikuone, unaweza kukutwa na hilo janga, lakini Bwana hata ukiwa katika kinywa cha simba, Bwana aweza kabisa kukuokoa!.

NIMEKUWA NA JUHUDI SANA, YA KUFUATILIA MAMBO YAHUSUYO VITA ROHONI. ADUI SHETANI, FALME NA MAMLAKA ZA GIZA, WAKUU WA ANGA, MAJESHI YA PEPO WABAYA, NA MAAJENTI WAO WA KIMWILI KAMA WACHAWI, WAKO KATIKA KUSHINDANA DAIMA, KAMA ISINGEKUWA MUNGU NA ULINZI WAKE, TUNGELIMEZWA HAI HAKIKA. KUNA WAKATI ULIPAMBANA KATIKA MWILI NA UGONJWA ULIHISI NI KAWAIDA, KUMBE VITA VIKALI VILIPIGWA KATIKA ROHO, ADUI ALINUIA KWA HUO, AKUONDOSHE, BWANA AKAKUNASUA. VIKAO VYA KUZIMU VILIVYO KULENGA WEWE BINAFSI ULIYESIMAMA KWA BWANA NI VINGI MNO, YALIPITISHWA MAAZIMIO MENGI, YA KUKUANGUSHA KATIKA DHAMBI, MAAZIMIO MENGI TU YA AJALI MBAYA, ULITEGEWA MITEGO MINGI KATIKA ROHO NA MWILI, NA BWANA ALIKUNASUA. KUNA WAKATI ULITUMIWA MAADUI WENYE KUTISHA KATIKA ROHO, LAKINI MUNGU ALIAHIDI KUKUOKOA NA MKONO WAO....

Yeremia 15 : 21
*_Nami nitakuokoa na mkono wa watu wabaya, nami nitakukomboa katika mkono wao wenye kutisha._*

Ni muhimu kukumbuka, mtu akianza kuelewa vita katika ulimwengu wa roho, anaanza kuishi kwa umakini zaidi. Maana maisha yasiyozingatia vita ya kiroho, ni rahisi kufanya mambo yanayopunguza utetezi wa kimungu. Nilikuwa nikisoma stori ya kiyahudi (Jewish lore) kuhusu vita ile wakati Ibrahimu alipowafuatia akina Kedorlaoma kumkomboa Lutu (Mwanzo 14), katika Biblia haijaeleza haswa, aliwezaje kuwashinda wafalme wajuzi wa vita, yeye akiwa na kundi dogo, lakini katika historia hiyo, ilieleza na kumtaja malaika aliyehusika na kuwashindia ile vita. Shetani kajizoeza kupinga kila jema linalokujia, hata kama Mungu amekulidhia tayari na ameagiza upewe, bado adui atajibidiisha kuzuilia, au kukutoa wewe kwenye position ya kimungu, usistahili kuyapokea unayopewa. Katika kitabu kitabu kiitwacho Yalcut Reuben 43:3ff, Kinaeleza dakika ile ambayo Ibrahimu alitaka kumchinja Isaka, tayari Mungu alimruhusu Miakaeli amshushe kondoo mume 🐏, katika mlima Moria, lakini linaeleza ushindani mkubwa katika roho kati ya Mikaeli na Shetani. Yaani ingawa Mungu aliyempima Ibrahimu, akajiridhisha kuwa ananipenda, na akaagiza malaika ashushe Kondoo, lakini adui alikusudia acheleweshe mpaka Ibrahimu akamilishe kumchinja mwanae. ASHUKULIWE MUNGU ATUPAYE KUSHINDA (1Kor 15:57). PAMOJA NA MAPINGAMIZI YOTE KATIKA ROHO, BWANA ATAKUOKOA TU KATIKA KINYWA CHA SIMBA, NAWE UTAKUWA SALAMA. HAKIKISHA UNASIMAMA KATIKA ZAMU YAKO, USIPOTOSHE SAFU YAKO, NA UUONGEZE UWEZO WAKO KIROHO (Nahum 2:1). KUNA MABAYA YANAWEZA KUFANIKIWA KUKUANGUSHA, KAMA HUTAELEWA KABISA KINACHOENDELEA. TAMBUA ANGA ULIYOPO, NA KIASI CHA VITA UNAPASWA KUIFANYA. KAMA UTAWALA WA GIZA UKO MORE STRONG ENEO LAKO USIWE MWENYE KULALA USINGI KIROHO, KWANI UTAONEWA SANA!. SHETANI ANAWEZA RUHUSU MATESO KWA NAMNA YOYOTE TU, USIPOSHTUKA UTASEMA NI MAPENZI YA MUNGU, KUMBE PALIKUTAKA USIMAME, UVIPIGE VITA. UNAUGUZA MKE AU WATOTO MIEZI SITA WANAFULULIZA TUU, SHTUKA KWAMBA MMMH🤔 WHAT'S GOING ON HERE, INGIA VITANI, MKONO WA ADUI WA KUONEA KWA NJIA YA MAGONJWA UONDOLEWE. PAMOJA NA UKWELI WA MUNGU LAZIMA ATAKUOKOA KATIKA KINYWA CHA SIMBA, LAZIMA WEWE MSOMAJI UBAKI KWENYE NAFASI YA KIMUNGU KATIKA ROHO, LA SIVYO UTAHESABU VIFO KIZEMBE TUU KWA WATU WANAKUHUSU. ZAIDI SANA, HAKIKISHA UNAKAA KATIKA KUMTUMIKIA MUNGU DAIMA. USIWE NA UDHURU WA KAZI WALA MASOMO, FANYA KAZI, ENDELEA NA MASOMO HUKU, UKIMTUMIKIA MUNGU KWA BIDII. MAISHA YA KUDUMU KATIKA HUDUMA YANAONGEZA KIASI CHA VITA KINYUME CHAKO, AMBAYO HIYO NAYO INAVUTA KUONGEZEWA MAJESHI YA KIMUNGU KATIKA ROHO, UPANDE WAKO.

Mwl Proo
0762879363
0718922662

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment