Tuesday, December 5, 2017

KUZIDISHIWA NEEMA!

*KUZIDISHIWA NEEMA*
*wཽaཽtཽuཽmཽiཽsཽhཽiཽ  vཽeཽrཽsཽiཽoཽnཽ*

*_мωℓ prσσ_*
*0762879363*

Haleluya Haleluya!!
Kuna watu mtapokea jibu la swali ambalo liliwasumbua kwa kitambo, na wengine mtapata prayer-point ya kukutoa mahali ulipo. Kuna watu wanafanya mambo ya huduma, mpaka wanafikia kiasi cha kushindana kimwili (Filip 2:3), wengine wameingia katika mtego wa kutafuta kufunikana (Nani mwamba). Wako watumishi wanatumika kwa dimensions zilezile, ambazo walitumika nazo mwaka 2002. Wako ambao basi tuu kwa sababu ya upepo uvumao alikuwa anaitwa Mchungaji so and so, anakurupuka asubuhi moja hivi, anaamua kuandika naye ni mtume (hajawahi kufanya utume wowote popote), anakurupuka na kujitaja ni nabii (hata hakaribii dalili za kuwa kaitwa kwa hiyo ofisi). Sasa hakuna haja ya kujipachika huduma ambayo hujapewa, unaanzaje kuwa mtume na nabii wakati watu hatuoni muhuri wa hiyo huduma kwako?( 1Kor 9:2), Umejipachika mtume na nabii watu hatuoni hata zile karama sita za ufunuo na za nguvu and all those things that mark an apostle/prophet?. Kama unayaandika hayo kwa kuwa una shauku, basi kaa hapa leo ujifunze yakupasayo. Kila mtumishi unalo lako la kulibeba hapa.

JAMBO LA KWANZA KABISA, NI MUHIMU KUELEWA KWAMBA, WATU HUTENDA KAZI ZOTE KWA KADRI YA NEEMA YA MUNGU NDANI YAO. HUWEZI FANYA MAMBO ZAIDI YA KIASI CHA NEEMA. UNAPOONA BIDII YA MTUMISHI MMOJA KUJITAHIDI KUSEMA VIBAYA KUU YA MWINGINE, AMBAYE  TUNAONA HUYO ANAYESEMWA NEEMA YAKE NI KUBWA MNO KULIKO HUYU MKOSOAJI, NI ISHARA ZA MAJARIBIO YA KUTAKA KWENDA ZAIDI YA KIASI CHA NEEMA ILIOY JUU YAKO. TUSOME MAANDIKO HAYA HAPA, JIKAZE UYASOME YOTE....

1 Wakorintho 15 : 10 - *_Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si bure, bali nalizidi sana kufanya kazi kupita wao wote (mitume wengine wakubwa); wala si mimi, bali ni neema ya Mungu pamoja nami._*

1 Wakorintho 3 : 10
*_Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, naliuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake._*

Waefeso 3 : 7
*_Injili hiyo ambayo nalifanywa mhudumu wake, kwa kadiri ya kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa kadiri ya utendaji wa uweza wake._*

Warumi 12 : 6
*_Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani;_*

Warumi 12 : 3
*_Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani._*

Waefeso 4 : 7
*_Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo._*

*MTUME PAULO, HALI AKIJUA KWA HAKIKA KUHUSU KIASI CHA NEEMA YA MUNGU JUU YA MTU NDICHO KINACHO MWEZESHA KUOPARETI KWA KIWANGO FULANI, AKAYAANDIKA HAYO HAPO JUU. ALIJUA KILICHOFANYA APIGE KAZI MATAIFA MENGI ZAIDI KULIKO MITUME WALIOKAA NA BWANA KABISA, ILIKUWA NI KIASI CH NEEMA. MITUME WENGINE HAWAKUJISUMBUA KUMPIGA VIJEMBE NA KUMWEKEA MABANGO, WALIPOSOMA NYARAKA ZAKE, WAKAINUA MIKONO🙌🏽🙌🏽🙌🏽. NA KUAPPRECIATE KIASI CHA NEEMA YA MUNGU JUU YA PAULO. KAMA PETRO ANGEKITUTUMUA KUTAKA AONEKANE YEYE NDIYE BIG FIGURE KATIKA UKRISTO, ANGEJIUMIZA KICHWA, ALICHOFANYA AKAMU-ENDORSE PAULO,KUWA DUUUU!!!😨😨🙌🏽🙌🏽🙌🏽👍🏼👍🏼👍🏼 HUYU JAMAA NI BIASHARA INGINE KABISA SOMA (2Petro 3:15-16). NITAFAFANUA HAPA BAADAE.
*MOYO WA SOMO*

Kilichonisukuma kuandika ujumbe huu, ambao naamini Mungu aliuweka moyoni mwangu, ni ili kuwasaidia watumishi wajue siri hii moja. Kuwa wanaweza kuzidishiwa/kuongezewa Neema. Kuna mtumishi unayesoma hapa, kiango chako cha kuhubiri ni kilekile ulichokuwa nacho miaka mitano iliyopita, kiasi chako cha ufunuo ni kilekile hakijaongezeka, mpaka baadhi ya washirika washajua kila utakapokanyaga (your locus), na kuna muda wanajua kabisa lazima tuu usome mstari fulani, unakosa na amani ukiwaona washirika wakongwe, kwamba watajua umerudia ujumbe.  Ili kuona kazi hata ndogo tuu za udhihirisho wa kimungu ni mpaka siku unayohitimisha mfungo wa siku 40, au saba kavu. Mwimbaji umejitahidi kubandua albums kama nane hivi📀💿📀💽📀💿📀📀, kwa mwaka mmoja, ni kama watu hawakuelewielewi, wakati mwenzio alitoa  Single album miaka mitano iliyopita, mpaka sasa distributors wanadurufisha kwa wingi, ametoa single track anatajwa kila kona ya nchi kwa huo wimbo mmoja. Huo sio wakati wako wa kusononeka... Unapoona unaabudia kwenye temporary building full-suit (umepiga mabati kote juu chini), na wenzio wanazindua Big Churches, sio wakati wako wa kuguna na kuwasema ni free masonic members, katika missions yao hao free masonry, hakuna la ujenzi wa makanisa makubwa ya kikristo.

MUNGU ANASEMA NA WEWE MTUMISHI, UNAYETUMIKA KWA NAMNA YOYOTE, KUWA WAWEZA OMBA KUZIDISHIWA NEEMA, MAANA NEEMA YAWEZA ZIDISHWA/ONGEZWA. YAANI KUNA MCHUNGAJI HAUTENDI DHAMBI, UNAMTAFUTA MUNGU KWA BIDII, LAKINI HUONI KAZI KUBWA UNAZOZIONEA SHAUKU, HUONI KARAMA FULANI FULANI ZIKIFANYA KAZI KWAKO KWA NGUVU, HATA KAMA HAIKUWA SEHEMU YA NEEMA YAKO, UNAWEZA KUOMBA UZIDISHIWE NEEMA. MAANA UNAHUDUMIA WAGONJWA UNAOGOPA HATA KUWAULIZA MMEKUWA WAZIMA? UNAACHA WATAJIJUA WENYEWE HUKOHUKO, SASA KAMA KARAMA YA KUPONYA HAIKO, HAINA MAANA HUWEZI KUZIDISHIWA NEEMA ILI HIYO IFANYE KAZI KWA NGUVU. KUNA MTUMISHI FULANI TOKA TANZANIA VISIWANI, ALIWAHI KUMWOMBEA MTOTO AFUFUKE HAPO KAWE DAR, ALIPOJITAHIDI KUFANYA HIVYO KWA MASAA KARIBU MAWILI, AKAWAJIBU WENYE MTOTO NA WALE WALIOOUWEPO PALE, KUWA _*"Yesu anafufuaga, ila lei hajataka kumfufua mtoto wenu"*_, NA ALIPOPATA KAMPENYO, ALICHOROPOKA AKAWAHI BOAT FASTAAA⛴ KURUDI KWAKE. KUTAMANI SANA KARAMA ZILIZO KUU SIO KOSA NI SAHIHI KABISAAA. WALA UKIONA HAYAPO HAINA MAANA KWAMVA HUWEZI KUZIDISHIWA NEEMA UKAZITENDA NA KAZI HIZO PIA, HATA KUFUFUA.

TUSOME HAYA MAANDIKO, ILI TUELEWE NINI MUNGU ANATULETEA LEO...

2 Wakorintho 9 : 14
*_Nao wenyewe, wakiomba dua kwa ajili yenu, wawaonea shauku kwa sababu ya neema ya Mungu iliyozidi sana ndani yenu._*

2 Wakorintho 9 : 8
_*Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna siku zote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema;*_

Matendo ya Mitume 4 : 33 *_Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi, na neema nyingi ikawa juu yao wote._*

Warumi 5 : 20
*_Lakini sheria iliingia ili kosa lile liwe kubwa sana; na dhambi ilipozidi, neema ilikuwa nyingi zaidi;_*

2 Wakorintho 4 : 15
*_Kwa maana mambo yote ni kwa ajili yenu, ili neema hiyo ikiongezwa sana, kwa hao walio wengi shukrani izidishwe, na Mungu atukuzwe._*

1 Timotheo 1 : 14
*_Na neema ya Bwana wetu ilizidi sana, pamoja na imani na pendo lililo katika Kristo Yesu._*

Yakobo 4 : 6
*_Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu._*

KATIKA MAANDIKO HAYO HAPO JUU, NIMEKUONESHA TABIA YA NEEMA, NI KUZIDI AU KUONGEZEKA. HUNA SABABU YA KUOPARETI KATIKA VIWANGO VILEVILE HAFIFU, HATA KAMA NI KWELI MUNGU ALIKUGAWIA KIASI HICHO, USIWAHI KUSEMA NEA YA MUNGU YANITOSHA, HUKU UNAZITAMANI KAZI ZINGIME NA HUZIONI, NEEMA YA MUNGU YAWEZA KUZIDISHWA KWAKO. TENA WAWEZA OMBA MUNGU NIZIDISHIE NEEMA.

*MAZINGIRA SAHIHI YA KUOMBA KUZIDISHIWA NEEMA*

1.)Mtu huyu anayeomba kuzidishiwa neema, ni muhimu awe na unyofu, yale anayoyaona kuwa ni udhaifu ajitahidi ayashinde hayo kwanza, yasisimame kama kwazo, pata somo langu la *_KUUSHUGHULIKIA UDHAIFU!_* ( Lipo kwenye mitandao).
Yaani ifike point wewe mwenyewe huoni kwazo, ibakie kazi kwa Mungu, kwamba kama kuna jambo haliko sawa, akuambie Yeye, na akikuambia weka sawa....sawa na (Ayubu 34:32)

2.Uwe na nia ya Kristo (Filip 2:3-5). Huyu anayromba kuzidishiwa Neema, kama ndani yake anasaka awe *_Baab kubwa_*, Anapoteza muda. Nia ya Kristo ndani ya mtu italeta tuu kuzidishiwa neema. Kama bado unafurahia maanguko ya walioinuliwa, basi itakuchukua muda sana. Kwa mfano kuna watumishi waliposikia jina la Gwajima kwenye list ya Makonda mioyo yao ilifurahi💙👉🏾😂😂, maana kwa kitambo wakisikia anaenda kwenye ziara zake kwa chopa thing🚁au hammer🚘, mioyo yao inabetuka kwa hasira😒 (Huyu kajiunga freemason) (SILENGI KUMTETEA GWAJIMA HAPA, NIMECHAGUA CASESTUDY ILIYOKO MJINI NOW. So nia isiyo ya Kristo inashangilia maanguko ya waliomzidi, kumbe wenzake wanakaa na washirika elfu 70 ibada moja, kwa Kadri ya Neema waliyopewa hao watu. Hauongezewi neema kuwa na kinyongo juu ya wengine..

*UMUHIMU WA NEEMA YA KUTENDA KAZI*

Jambo la muhimu ni kwamba ukipewa neema, hautashindana, utafanya kwa kadiri ya hiyo neema, neema nyingi/kubwa, kazi kubwa, utukufu mkubwa zaidi.

1 Petro 4 : 10
*_kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu._*

TAFUTA KUZIDISHIWA NEEMA, ONDOKA KWENYE KUSHINDANA, KUWAWEKEA WENZIO MABANGO, MAANA NEEMA ITAKUONDOLEA KUTUMIA JASHO JINGI. KAZI AMBAZO MWINGINE ANAZITENDA TU KWA KUWA KAFUNGA SIKU 21 BILA KUGUSA HATA MAJI, KAMA UMEPEWA NEEMA KAZI HIZOHIZO WEWE UTAZITENDA HATA WIKI AMBAYO UMEKULA SUPU ASUBUHI MCHANA JIONI, 😋😋🍹☕🎂🍗🍖🧀🍞🍕🌮🍲🍜🌯
. HAPA SITETEI KUTOFUNGA, LA HASHA!, ILA NATAMANI UELEWE UTENDAJI WA KAZI NA UHUSIANO WAKE NA KIASI CHA NEEMA.

Mungu akubariki, tukutane kwenye somo lijalo.

Mwl Proo
0762879363
0718922662

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment