🇦 🇱 🇱 🇹 🇷 🇺 🇹 🇭
*HALI YENU YA KWANZA*
*_Na Mwl Proo_*
0762879363
0718922662
BWANA YESU ASIFIWE SANA.
Somo hili halilengi kuwarudisha watu nyuma, Infact ni mimi ndiye nimefundisha somo lisemalo, *_Kwenda mbele moja kwa moja_* siku chache zilizopita. Lakini nilipata pia ufunuo juu ya hali za watu za mwanzo na za sasa ktk kupokea imani.
*Ufunuo 3:3*
Ufunuo wa Yohana 3 : 3 - *_"Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu......"_*
Kuna hali ulikuwa nayo ulipoamini ndiyo hiyo Bwana anataka kusema nasi na anaidai.
Bila shaka kila mmoja wenu akijiangalia hali yake ya sasa, "in the first pace" atatoa hitimisho kuwa *"nimeongezeka sana ktk maarifa ya kiroho na kumjua Mungu"* sasa Bwana analo neno kwako,kuwa maarifa hayo mengi kama yangeambatana na ile hali yako ya kwanza ulipoamini "ungekuwa/utakuwa heri/bora sana".
*Ezekieli 36 : 11*
_Nami nitaongeza juu yenu mwanadamu na mnyama, nao watazidi na kuzaa; nami nitawakalisha watu ndani yenu, kwa kadiri ya *HALI YENU YA KWANZA*, nami nitawatendea mema kuliko mema ya mianzo yenu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana._
*KITU KTK HALI YAKE YA KWANZA(UPYA)*
Wapenzi hivi mnakumbuka namna kitu kikiwa ktk hali yake ya kwanza(upya)?
Kuna wakati nakumbuka nilinunua viatu fulani vipya vizuri sanaaa,na kwa sababu ya hali yake ya kwanza,nakumbuka niliviweka kabatini juu ya nguo zilizonyooshwa/pigwa pasi.Sasa ni viatu hivyo hivyo ambavyo muda ulifika hata mvunguni mwa kitanda havikustahili,kuna wakati nilikuwa navivulia kwenye ua wa nje na kuvificha kwenye maua kuepusha _bad smell_ ndani.
Je! unakumbuka upekee uliokuwa kwenye vazi jipya au suti yako ambayo ktk upya wake(hali ya kwanza) uliipeleke kwenye special laundry company ili ifanyiwe dry cleaning,na hata ukiisafisha nyumbani hauichanganyi na mavazi mengine. Je! unakumbuka gari jipya la hapo kwenu mlipolipa heshima ya kuliosha kila siku kwa maji safi,likiwa ktk hali yake ya kwanza,Je baada ya kuwa limechoka limepondeka kwa kugongwa mara nyingi,vipi ratiba ya kuliosha huko parking. Kumbuka vitu vyote ktk hali yake ya kwanza(upya).
INGAWA NI KWELI MTU ANALOENDELEA KUDUMU KTK WOKOVU ANAENDELEA KUTAKASWA NA KUFANYWA BORA,LAKINI IKO HALI YA KWANZA AMBAYO BWANA ACHUNGUZAYE MIOYO ANAIJUA NA ANAIDAI.
KIBIBLIA UPENDO WA KWANZA(UPENDO WA WAKATI WA UPOSO) NI MKUBWA ZAIDI YA ULE WA BADAE,LAKINI MUNGU ANAUTAKA ULE UPENDO WA KWANZA WA WAKATI WA UPOSO NDIO UWE WA "LIFETIME"
*Yeremia 2 : 2*
Enenda ukalie masikioni mwa Yerusalemu, ukisema, *_Bwana asema hivi, Nakukumbuka, hisani ya ujana wako, upendo wa wakati wa uposo wako;_* Jinsi ulivyonifuata huko jangwani, katika nchi isiyopandwa mbegu.
*Ufunuo 2*
4 Lakini nina neno juu yako, *ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza.*
5 Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye *matendo ya kwanza.* Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu.
MUNGU ULE UPENDO WA KWANZA ANAUITA UPENDO WA WAKATI WA UPOSO,BILA SHAKA WANANDOA NA WALIOWAHI KUWA KTK UHUSIANO WA UCHUMBA BAADA YA UPOSO,UPENDO UNAFIKIA JUU KABISA,NDIPO WATU WANAKUWA KAMA WAMERUKWA NA AKILI HAWASIKII TENA,MNAKUMBUKA NYAKATI HIZO NA NAMNA AMBAVYO HATA MESEJI KUTOKA KWA PARTINER WAKO 📱💌📲UNAIONA YA MAANA SANA, UNAWEZA KUIONA MESEJI,UKAIWEKELEZA ILI UKATAFUTE POZI LA KUISOMA VIZURI UKIWA CHUMBANI🙈, ILA HUO UPENDO KUNA MUDA UNASHUKA,NA HALI YA KWANZA IKIISHA UNAWEZA JIBU MESEJI HATA HUJAISOMA MPAKA MWISHO NA UNAJIBU SHORTCUT TENA KWA HATA KWA KUTUMIA EMOJI (🙅🏽=NO) (😏=RACCA)
SASA MUNGU NAYE ANAUKUMBUKA UPENDO ULE ULIKUWA NAO ULIPOAMINI,KILE KICHO CHA BWANA,KULE KUUTIMIZA WOKOVU WAKO KWA HOFU NA KUTETEMEKA.
NILIKAA NA MCHUNGAJI FULANI WA EAGT(PSTR CHISSORO) AKATUSHUHUDIA KUHUSU MIKESHA WALIYOIFANYA MIAKA YA EARLY 1970's ,ALISEMA KWA WAKATI HUO MIKESHA KTK MAKANISA YA PENTEKOSTE ILIKUWA SIKU YA JUMAMOSI SIO IJUMAA KAMA NYAKATI HIZI,LAKINI WALIKESHA TOKA SAA MBILI USIKU MPAKA SAA MOJA ASUBUHI MWISHO,PIA WALIRUDI MAKWAO NA KUJA TENA IBADANI BAADA YA SAA CHACHE. TENA IKUMBUKWE CONTENT YA MKESHA WAO ULIKUWA NI MAOMBI YALE YA KIPENTEKOSTE YENYE UVUVIO MZITO WA ROHO 😪🙌🏽 ACHA HIZI *"DRY LANDS"* ZETU ZA UNAOMBA HUKU UNACHUNGULIA MESEJI ZA WHATSAPP KIDOGO. SASA NAJARIBU KUIFIKIRIA HALI HII YA KWANZA,JINSI WALIVYOPOKEA,MAANA MIAKA MICHACHE IMEPITA NILIHUDHURIA MKESHA KANISA FULANI LA KISASA,NILIKUTA CONTENTS ZA MKESHA NI STAREHE FULANI,KULIKUWA NA MUDA MWINGI WA PERFORMANCES KAMA YOUTH DANCE TEAM,GUEST SINGERS WENGI MNO,PAMOJA NA KWAMBA MKESHA ULIANZA SAA NNE LAKINI SAA SABA NI BREAK TIME YA KUPATA ☕🍹🌮🌭🍞,MAOMBI NI YA KUBIPU "BEEP" ,NA KUNA MAHALI PENGINE NILIKUTA ILIKUWA TOO MUCH. MAANA HAPO KULIKUWA NA RATIBA NDANI YA MKESHA,KUANZIA SAA TISA NI MUDA WA KUANGALIA NIGERIAN MOVIE 📺📼,MAANA NGUVU NI CHACHE ZA KUOMBA (MITHALI 24:10) KWA NINI NIMETOA SHUHUDA HII??
*Yeremia 6 : 16*
*Bwana asema hivi, Simameni katika njia kuu, mkaone, mkaulize habari za MAPITO YA ZAMANI, I wapi njia iliyo njema? Mkaende katika njia hiyo, nanyi mtajipatia raha katika nafsi zenu. Lakini walisema, Hatutaki kwenda katika njia hiyo.*
*Ayubu 8 : 8*
Basi, uwaulize, tafadhali, vizazi vya zamani, Ujitie kuyaangalia yale baba zao waliyoyatafuta;
YAKO MAPITO YA ZAMANI AMBAYO BWANA ANAKUTAKA UYATAZAME,UNAJUA KUNA WAKATI ILIKUWA HATA WACHUMBA WAKITAKA KUONANA WANAENDA KUKUTANIA KANISANI,NA ZAMA HIZO MTU AKITAJWA AMEANGUKA KWENYE ZINAA,ILIKUWA KILIO NA KUSAGA MENO,NA WATU WALIJISALIMISHA WENYEWE,SASA ZAMA HIZI NI NYAKATI ZA HATARI,WACHUMBA WAKISHATANGAZA TUU,WAKO "OUTING" KILA WIKIENDI,WANAJIANGUSHA KWENYE UASHERATINI/UZINZI WEE KWA KIGEZO CHA "SHETANI ALIJIINUA"
SO WENGI WANAKAUSHA😷 MNAKUJA KUJUA BADAE,BAADA YA WEDDING💍💍MIEZI MITANO SITA BINTI KAJIFUNGUA WALA SIO "PREMATURE BIRTH"
NI MUHIMU UKUE HATA UFIKIE KIMO CHA CHEO CHA UTIMILIFU KRISTO,LAKINI HUPASWI KUIACHA HALI YA KWANZA,ILE HALI AMBAYO MUDA WOTE ULIJIKUMBUSHA MOYONI KUWA "YESU ANARUDI TENA,SAA NISIYODHANI" IKAKUPA BIDII YA KUMZALIA BWANA MATUNDA. ILE HALI YA KWANZA YA MSIMAMO WA "NITENDEJE UOVU HUU NIMKOSE MUNGU"(Mwanzo 39:9) ILE HALI YA MWANZO YA KUTEGA ALARM CLOCK ⏰KUAMKA KUOMBA, ILE HALI YA KWANZA AMBAPO ULIKUWA UKIKAA WIKI NZIMA BILA KUFUNGA UNAJIHISI MDHAMBI 😰🙏🏾UNATUBU KWA KUGAAGAA CHINI CHUMBANI,YALE MAOMBI YA KUJIMIMINA MOYO KWA BWANA,SIO UCHANGA (1SAM 1:15) SAIV SI UNAFANYA MAOMBI YA KISOMI👔🎓👠,UNAOMBA HUKU UNAREKEBISHA TIE AU GAUNI LIKAE FRESH😀,NILIHUDHURIA IBADA FULANI HUKO KAWE,MUDA WORSHIP INAENDELEA NILIMUONA DADA MMOJA KAKAA 💺ALIFUNGUA POCHI NA KUTOA KITU KAMA KOPO LA LOTION AKAJIONGEZEA USONI,NILISHTUKA KIDOGO KUONA HILO(NDIO MAANA KUFUMBA MACHO KUNA FAIDA YAKE),TATIZO NI KWAMBA HALI YA KWANZA IKIONDOKA UNASAHAU MAMBO YA KUWA UPO MBELE ZA MUNGU (2SAM 6:21)
VIPI MPENDWA DO YOU STILL FEEL HIM(GOD) MOVING YOUR HEART KAMA MWANZO?
TUYAPITIE MAANDIKO YAFUATAYO
*Ezekieli 16 : 55*
Na maumbu yako, Sodoma na binti zake, watairudia hali yao ya kwanza, na Samaria na binti zake watairudia *hali yao ya kwanza,* na wewe na binti zako mtairudia *hali yenu ya kwanza.*
*Ezekieli 38 : 8*
Na baada ya siku nyingi utajiliwa; katika miaka ya mwisho, utaingia nchi iliyorudishiwa *hali yake ya kwanza,* baada ya kupigwa kwa upanga, iliyokusanywa toka kabila nyingi za watu, juu ya milima ya Israeli, iliyokuwa ukiwa wa daima; lakini imetolewa katika kabila za watu, nao watakaa salama salimini wote pia.
UNAPOGUNDUA HALI YA ZAMANI ILIKUWA NJEMA BASI KATA SHAURI NA AMUA KUYATENDA AU KUYAFUATA MATENDO YA KWANZA
Hosea 2 : 7 - Naye atawafuata wapenzi wake, lakini hatawapata; atawatafuta, lakini hatawaona; ndipo atakaposema, Nitakwenda nikamrudie mume wangu wa kwanza; kwa maana *hali yangu ya zamani ilikuwa njema kuliko hali yangu ya sasa.*
*Yeremia 33 : 11*
itasikilikana tena sauti ya furaha na sauti ya shangwe, sauti ya bwana arusi na sauti ya bibi arusi, sauti yao wasemao Mshukuruni Bwana wa majeshi, maana Bwana ni mwema, rehema zake ni za milele; na sauti zao waletao sadaka za shukrani nyumbani kwa Bwana. Kwa kuwa nitawarudisha wafungwa wa nchi hii *kama kwanza,* asema Bwana
*Yeremia 33 : 7*
Nami nitawarudisha wafungwa wa Yuda, na wafungwa wa Israeli, na kuwajenga *kama kwanza.*
*BWANA YUKO RADHI AKUFANYE TENA KWA KADRI YA HALI YAKO YA KWANZAA NA KUKUREJEZEA UPENDO WAKO WA WAKATI WA UPOSO(ULIPOAMINI)*
OMBI
Maombolezo 5 : 21 - Ee Bwana, utugeuze kwako, nasi tutageuka; *Zifanye mpya siku zetu kama siku za kale.*
Asante kwa kufuatilia, na Mungu wa mbinguni akuwezeshe ktk nia ya moyo wako, ya kumkaribia zaidi.
Mwl Proo
0762879363(whatsapp only)
alltruth5ministries@gmail.com
ubarikiwe
ReplyDelete