MFULULIZO WA SOMO LA KUIJENGA NAFSI
*_Mwl Proo_*
0762879363
*UTANGULIZI*
"Adui anafurahia kuona tuna-retreat (rejea nyuma)
Retreat
"The act of pulling back or withdrawing as from something dangerous,or unpleasant".
"The act of reversing direction and receding from a forward position".
>Adui Nahashi Mwamoni(1Sam 11:1-11)
>Adui Senakeribu wa Ashuru (2Nyak 32:1-23)
Ndivyo wanavyofanya maadui hata sasa,watakuogofya ili uwezr kuretreat.
•Shetani,mapepo/majini,wachawi,mizimu e.t.c watafanya yote ili uache kufanya kizuri unachofanya(retreating),Ujifunze siri ya kuto-retreat kamwe,kwani ufalme tulioupokea hautetemeshwi (Hebrews 12:28)
•Unaweza kufanyiwa maombi ya shida fulani,ikazidi,adui akatafuta mwanya ili uweze ku-retreat
•Unaweza kuwa muombaji na unaomba usiku wa manane,ukakuta,adui anaweka vitisho ili uli-retreat,na wengine hufanya maamuzi yasiyo sahihi kusitisha kuomba
•Wachawi wakiwepo kanisani nao hufanya kila kitu ki-retreat kwa mapenzi yap
>Ushuhuda wa Msiba ni ambapo kulikuwa na mchungaji alihubiri ujumbe wa ku-retreat(retreatant preaching) kwamba msikubali kuambiwa ndugu yako kukuloga kwa nini huyo mganga asikuambie kuwa aliyewaloga yuko Marekani(Alitoa mahubiri hayo kwa kuhofia kuwachokoza wachawi
•Pia wakiona vitu fulani hawavitaki huviwekea barrier ili kanisa li-retreat,kwa hiyo watu wataogopa kuwatajataja maana watakuwa ktk hofu ya kupata madhara.
*"BUT AS FOR US, WE ARE NOT GOING TO RETREAT"*
*_SOMO KAMILI_*
*NI NAFSI ILIYOJENGWA PEKEE, NDIYO ITAKAYOSHINDA NA KUZIRITHI AHADI*
Sehemu za somo
1.)Ifahamu nafsi
2.)Sifa/Tabia za nafsi
3.)Maadui wenye kuiharibu nafsi na namna wanavyoiharibu
4.)Namna ya kuijenga nafsi
5.)Namna ambayo nafsi iliyojengwa inashinda yote
6.)Tunarithi vipi ahadi
7.)Namna ya kuikomboa nafsi iliyo haribiwa na kutekwa
*1.)IFAHAMU NAFSI*
©Neno nafsi ktk Biblia,kuna wakati limetumika "interchangiably" na moyo au roho,lakini iko tofauti ya msingi sana.
Mfano:- Ezek 18:20
(Roho/Nafsi)>>Lakini kitu halisi kilichotajwa hapo ni "Nafsi"
(Vulgate>Anima
Jewish Bible>Nefesh(mwili wenye nafsi hai
©Nafsi/Soul ndiyo inayosimama katikati ya mwili na roho
Kwa lugha za asili za Biblia (Hebrew/Greek)
*Nafsi(Nefesh,Psuche)
*Mwili(Basar,Soma)
*Roho(Ruach,Pneuma)
Mahali ambapo maneno haya yanetajwa kwa pamoja ndiyo yanatusaidia kujua tofauti yake
1Thes 5:23,2Kor 7:1
*Nafsi ndio uhai(breath of life) ndicho kilichoifanya ile sanamu ya udongo iitwayo mtu=adama=adamu=udongo iwe hai
Mwanzo 2:7(Akawa nafsi hai-Nefesh)
*Nafsi ambayo inaitwa Psuche(matamshi -Psookay) ina maana ya mind,ikumbukwe neno hili Psuche ni Psych kwa kingereza na ndilo linaloleta neno "Pyschology" na watu wanaosoma Cognitive theories,Hushughulika sana na human mind. Wanasaikolojia wanapofanya _Guidance and Counselling_ wanashughulikia ~MIND~wanaponya nafsi na magonjwa kama stress(Sonona) msongo wa mawazo. Walichokosa wao ni ufahamu wa kiroho kuhusu NAFSI hivyo wanatumia njia za kimwili kuponya kitu kinachohitaji zaidi uponyaji wa kiroho
*Kiroho nafsi ni zaid ya akili (mind) nafsi ni pumzi ya uhai,inasimama kati ya roho na mwili,na ndio iliyobeba akili,utashi na nia/dhamiri/maamuzi yote,ina-provide _LINKAGE_ kwa vyote na ndiyo "driving force" ya maisha inayoamua "Personality" iweje pia,na imebeba consciousness/conscience
*Nafsi inasimama kama referee kuamua juu ya roho na mwili
*Mungu ameyaacha yote ktk "Freewill" yaani freedom of choice (uhuru wa kuchagua)
>Roho iko radhi na matendo mema yote,lakini haiwezi kuiburuta/kuuburura mwili
Math 26:41
>Mwili na roho ni adui,wanaoshindana,maana kimoja(roho) asili yake ni mbinuni na kingine(mwili) ni cha duniani
Galatia 5:16-17
_Hamwezi kufanya mnayotaka_
(Roho inafurahia maagizo ya Mungu/mema)
Rumi 7:22
Lakini upinzani wa mwili unaosaidiwa na nafsi isiyojengwa, unakufanya ushindwe kutenda mazuri ya kiroho.
*Warumi 7:15-20*
*Kwenye vita ya roho na mwili,kinachonishinda ni roho kama nafsi imejengwa,na mwili lazima uishinde roho,kama nafsi haijajengwa,kama nafsi imetekwa,kama nafsi imechoka,imefungwa,kama ipo tupu..Roho itashindwa
*Mwanadamu ameumbwa kwa namna ya ajabu
>Roho sio nafsi,zinayofauti kubwa.Roho ni mtu halisi wa ndani,asiyeonekana,na mwanadamu anaweza akawa hai,hata kama roho ikitoka(Swali mwanadamu alianza kuwa hai lini,roho ilitoka wapi,je roho inakuwa ndogo na inakuwa kubwa?
>Roho ina thiolojia pana sana,Lakini kwa mafundisho ya kiyaudi(Yuko malaika aitwaye Lailah anayehusika na kuiweka roho muda wa mimba kutunga "conception",roho ni za milele,hazifi kwa jinsi ya kufa,hata ile mauti ya pili,ya roho kutupwa hazitakufa zitateseka zikiwa hai ika inaitwa mauti ya pili.
*Nafsi ya mwanadamu inaweza kumilikiwa na roho yoyote,na iliyojengwa atakaa Roho Mtakatifu pekeake,isiyojengwa roho yoyote inaweza kuivaa nafsi na kuimiliki. Mapepo yanaimiliki nafsi ndio maana huitwa (demon-possessed) anaimiliki nafsi. Ziko levels nyingi za mtu mwenye pepo.
>Wako wanaume wengi wenye pepo ila pepo huwajia kuwatumikish kwa matendo ya giza na kuwatoka
>Mtu akipandisha pepo nafsi yake inakuwa ktk "Trance" ndio maana wengi wakirudiwa na fahamu,hawaelewi kiliendelea nini,ingawa yule pepo aliutumia mwili wake kuleta fujo n hata ulimi wake kunena. Ni kama ambavyo Roho Mtakatifu anaweza kunena kwa kinywa cha mwamini.
>Mapepo yakikaa kwenye nafsi ya mtu yanamwambukiza tabia zao.Ni hatari sana kama wanandoa mmoja wenu atamilikiwa n mapepo nafsini mwake,atskutendea mabaya mengi ambayo sio kwa mapenzi ya nafsi yake ,ikitokea amefunguliwa nafsi anaweza akalia sana akijua aliyokutendea.
*2.)SIFA/TABIA ZA NAFSI*
*Nafsi inaweza kujengwa (1kor 14:4) kwenye mafunzo ya "Human Development" wanajua kuhusu ukuaji huu. Kama nafsi ingekuwa ipo kama ilivyo na ukubwa wa ufahamu na utashi toka tumboni,tungeweza kukumbuka maisha yetu ya tunboni pia. Inajengwa na kukua.
*Nafsi ina thamani kubwa (Mithali 6:26,16:26,Zab 49:8
*Nafsi inaweza kuuzwa
(Kumbu 28:68,1Falme 21:20,2Falme 17:17
>Shetani ananunua nafsi (Form za kujiunga na jumuiya ya siri kama Illuminati/Freemasonry zimeandikwa _SELL YOUR MORTAL SOUL TO THE SATAN_
>Kuna mtoto aliletwa kanisani,na nikashuhudiwa shida ni wazazi,walimuuza nafsi yake(ikumbujwe nafsi ina thamani mtu akiwa ktk uzima wake wa mwili huu,akifa basi tena hana faida na walionunua watadai fidia nyingine.
>Kuna family spirits(mizimu/mapepo) zilinunua nafsi za ukoo au familia,kwa hiyo wotr wanazaliwa wanamilikiwa (Ila wako ambao hawakuuzwa nafsi zao hivyo zinataka kuwamiliki watahitaji ridhaa yao
*Nafsi huharibika/wa
Kutoka 32:7
Ziko nafsi zinaweza kuharibiwa kwa kiasi cha kutofaa tena kwa kazi za ufalme(Waliowahi kuwekwa/kuchukuliwa misukule)
_wako ambao huwa wamefanywa ndondocha nafsi zao_
*Nafsi zaweza kuwa kifungoni
Zabur 142:7,Isaya 42:22
-nafsi inayokuwa kifungoni inatumikishwa inaoteshwa ndoto n.k
*Nafsi yaweza kuwa tupu
Isaya 29:8,ikumbukwe nafsi ni chumba kikubwa cha kuvutia sana,yaweza kuwa tupu kama haijawa _fed_ na mambo mengine
*Nafsi huchoka
Yer 2:24,Zek 11:8,Ayu 10:1 Mungu anyo nafsi (Yohana 5:26) na hivyo anazosifa zingine za nafsi kwafano nafsi yake pia huchoka(akasema ktk maandiko nimechoka kughahiri,mmenichokesha kwa maovu yenu,Ingawq Mungu hazimii wala hachoki (Isaya 40:28-29)
*Nafsi huumia
Yer 12:13
*Nafsi hujichukia au kuchukia
Ezek 6:9,Isay 1:14
Wengi wanaifikia uamuzi wa kujinyonga au kujiua ni matunda ya either "Spirit of suicide" au nafsi imejichukia
*Nafsi inaweza kushiba
Zab 123:4,Kut 15:9,Mhu 6:3,7
*Nafsi huugua
Rumi 8:23
*Nafsi inaweza fanya shauri/inasema
Neh 5:7,Luka 12:9
*Nafsi inaweza pata uchungu
Ayu 7:11,Isay 38:15
*Nafsi husononeka/stress
Ayub 30:25
*Nafsi hufadhaika(fadhaa/mzigo/lemewa) Zaburi 6:3
*Nafsi huona kiu (Zabur 42:2,63:1) Njaa na kiu ya haki
*Nafsi huinama (Zaburi 42:5)
-Ikiinama mtu anakosa changamko hadi nafsi iinuliwe tena.
*Nafsi hukinai (Zabur 63:5)
*Nafsi hua hai(Zaburi 119:175,Wimbo 5:2)
*Uhai wa nafsi una umuhimu mkuvqa kwa mtu aliyeokoka(itakusaidia ku-sense vitu vya kiroho)*
*Nafsi huzimia (Wimbo 5:6)
NB:
Nafsi ina sifa na tabia nyingi mbali na hizi chache nilizotaja kukupa nuru tuu ila jifunze ktk maandiko utafahamu zaidi
*3.)MAADUI WANAOIHARIBU NAFSI NA NAMNA/JINSI WANAVYOIHARIBU*
*Katika sifa za nafsi tuliona ya kuwa nafsi inaweza kuhribiwa (Kutok 32:27) na kwa kuwa somo linasema "Nafsi iliyojengwa" ni dhahiri kuwa inaweza kuharibiwa
*Maadui wanaoiharibu nafsi wengi wao wanajua umuhimu wa nafsi
*A.)SHETANI*
Shetani akipata nafasi(Efes 4:27) anaweza kuiharibu nafsi kwa kiwango ambacho tiba yake inaweza kuwa na gharama kubwa au ngumu sana .
>Watumishi wake(mawakala/wachawi) Nafsi zao zimehribiwa na shetani,dhamiri zao zimekufa ili waweza kufaa kwa utumishi wa ufalme wa giza
>Hata wakristo ambao wanadumu na viroho vilivyoharibika muda mrefu,Shetani anaziharibu nafsi zao(Ufunuo 2:21)
>Na wale ambao adui akitqk kuwapoteza milele,awe nao Jehanamu,basi hufanya shambulio kubwa la kabisa la Nafsi
*B.)WAKUU WA GIZA/MAJINI(MAPEPO)*
*Kumbuka tunafanya vita na hili kundi (Efes 6:12) ,Wakuu wa giza/majini(mapepo) Wanatabia ya kujenga ngome kwenye fikra(nafsi),hizi ngome (vifungo) hziwi nyepesi kuangushwa mpaka upate maarifa .Ziko tabia chafu zinajengewa ngome(Addiction) -- 2Kor 10:4-7
Tabia zote mbaya zinajengewa ngome na hawa maadui ili kuharibu nafsi
•Uvutaji sigara🚬
•Unywaji pombe🍺
•Ugomvi/Hasira
•Kusagana/Kujisaga/Kujichua(Masturbation) utazamaji wa pornography etc etc Hizi haziitaji mtu aadhibiwe ili kuacha,wala sii mahali pa kutoa ushauri *NI SWALA LA KUANGUSHA NGOME/KUVUNJA/KUBOMOA NGOME*
*C.)WACHAWI/MAWAKALA WA SHETANI*
Hawa pia wanao uwezo wa kuteka nafsi,kuzitia vifungoni na wanaziharibu ili kuyaharibu maisha ya mtu
*Wanaweza kuitumikisha nafsi na asipopata msaada wa kiroho atapotea kabisa huyo mtu
*Wachawi ni wabaya sana wanakuwa na roho ya Shetani kwa level ya juu,wanaweza kuutenda ubaya kwenye nafsi hata bila sababu,mtoto anaweza kuwa na akili nyingi nafsini mwake,wanamfunga ili ashindwe(Kutok 22:18--- Msimwache mwanamke mchawi kuishi
*D.)MITUME NA MANABII(WA UONGO)*
Manabii/mitume wa uongo wanaweza kuharibu nafsi za watu kwa kuwalisha watu chachu(Mafundisho potofu)
Chachu--Luka 12:1/Yer 5:31
Nabii wa uongo anaweza kukuharibu nafsi jwa kukueleA mambo yanayopingana na kweli ya Mungu
>Mtu wa Mungu toka Yuda na yule nabii Mzee(1Falme 13:14-32)
>Nabii wa uongo Hanania (Yer 28:1-17)
>Nabii wa uongo (Bar-Yesu) Elima mchawi Mdo 13:8ff
*Yesu alipotoa tahadhali ya manabii wa uongo alijua namna wanavyoharibu nafsi (Math 7:15)
*Binafsi niliwahi msikia mtume fulani Dar akiwaruhusu washirika wafanye makosa fulani kwa kigezo kwamba atawatetea mbinguni
*Habari ya mtume mmoja huko Kenya aliyewaambia waumini wa kike wasivae underwears/pants ili Kristo awaingie👙🙊
*E.)HALI YA MAISHA(NZURI AU MBAYA),MAKUZI/MALEZI*
Hali ya maisha ina mchango mkubwa ktk kuiharibu nafsi,nafsi ikajikinai au kuchoka n.k (Kumb 8:2-18/ Mithal 30:8--.*usinipe zaidi*)
*Yeshuruni alifanikiwa nafsi ikaharibika (Kumb 32:15
mifano ya watu kama Jack Pemba+Baba Juniour
MALI IKIONGEZEKA MSIIANGALIE SANA MOYONI zaburi 62:10
*F.) MAMBO UNAYOYARUHUSU KUINGIA NAFSINI KWA KUPITIA MILANGO YA FAHAMU*
*Milango ya fahamu macho,pua,ulimi,msikio na ngozi(Macho na masikio hasaa) ni milango mikubwa ya nafsi inayoingiza vitu,na uwe makini sana jinsi unavyosikiliza
Luk 8:18 Jiangalieni jinsi msikiavyo
Rumi 10:17 Basi imani chanzo chake ni kusikia.........)
Linda sana moyo(nafsi) --- Mithali 4:23,Kumbu 28:34(must read verse)
Zab 119:37,Mhub 10:6,1Yoh 5:17
>Ukipendelea kuona/kusoma/kusikia vitu vichafu,vitaharibu nafsi
•Magazeti ya Udaku
•Vipindi vya Tv visivyo na maadili unavyoviruhusu vinaenda nafsi n kujenga kitu kisicho cha kimungu
•Ukifuatilia riwaya na tamthilia za mapeni,nafsi yako utaundiwa kiu ya hayo mambo.
*Kwa hiyo ni lazima uweze kufanya filtering(mchujo),uweze ku-refrain (kujizuia) baadhi ya mambo ili nafsi isiharibiwe
*Ziko movie-series za kisasa za Zombies👺👺,movies za kichawi😈👿,Vimpires zimelenga kuharibu nafsi,hivyo lazima ujiponye nafsi.
*G.) WANAWAKE*
Wanawake ni miongoni wenye uwezo wa kuziharibu nafsi. Mithali 31:3,
*Yezebel alimharibu nafsi Ahabu mfalme(soma habari za Naboth)
*Zereshi mke wa Haman alikuwa chanzo cha nafsi iliyojikinai ya Mmewe
>Usirefushe bila sababu mazungumzo na mwanamke (Mithal 7:21)
>Wanawake wanazo nguvu za kuiteka nafsi (Mithali 6:24-29
>Hata yeye.......(Nehemia 13:26)
>Usijione eti una nguvu sana (Mithali 7:10ff)
#Lakini pia unaweza kuwa na viwango ambavyo watu hata wakuone na wasichana hawawazi baya kabisa (Yohana 4:27)
NB:
*WATAWALA WANAWEZA KUZIHARIBU NAFSI*
1Falme 3:2(Mahali pa juu)
>Yeroboam mwana wa Nebati aliwakosesha wana wa Israel
>Watawala wanaweza kuwaingoza watu kinyume na Mungu na kuziharibu nafsi
Yer 5:31
>WafalmE wanaweza kushauriwa na wasaidizi ili kuziharibu nafsi za watu Mithali 29:12
*ATHARI ZA NAFSI KUHARIBIWA*
*Kuteswa mwili
*Hutaweza kumwabudu Mungu
*Hutaweza kurithi ahadi ambazo ulipaswa kuzirithi ktk haya maisha ya sasa na ya badae
*Hutaweza kuyashinda mashindano ya rohoni
*Maisha yako kijamii yatakuwa na shida (Zab 119:165)
*4.)NAMNA YA KUIJENGA NAFSI*
Kumbuka kichwa cha ujumbe wetu
(1Korintho 14:4,Yuda 1:20,Ayubu 22:23 ,Yer 31:4
Neno "Jenga" ---- Edify (build/construct/instruct,improve morally/intellectually)
*Kama ilivyo sifa/tabia ya nafsi,inajengwa na zipo njia kadhaa za kuijenga
i.)Kukaa na BWANA (Awe rafikiako Isaya 41:8,Mithali 22:11Yoh 15:15)
Isaya 57:15,33:14-24
Zabur 15:1-5,24:3-6
ii.) Kunena kwa lugha/kuomba ktk Roho
>Kunena kwa lugha kuna upinzani mkubwa juu yake ,lakini hii ni _sponsored version_ ya kuijenga nafsi bila gharama (1Kor 14:4)
>Kuomba ktk Roho sio lazima useme kwa lugha za rohoni,unaweza omba kwa lugha za wanadamu ila utagundua kuwa frequencies zimebadilika,mpangilio wa maneno umebadilika,uvuvio upo sio wa kawaida
Verse 39............ *Wala msizuie kunena kwa lugha*
Verse 18
*Namshukuru Mungu nanena kwa lugha zaidi ya ninyi nyote*
*AINA 3 ZA KUNENA KWA LUGHA*
A.Kunena kwa lugha mpya ambapo mtu unasema tu na Mungu,yaani roho peke yake inaomba (1Kor 14:14,2)
B.)Kunena kw lugha ambapo kuna ujumbe wa watu ila umekuja kwa lugha za rohoni,inahitaji karama ya kufasiri
1Kor 14:5,13,27
1Kor 12:10,30
C.Kuna kunena kwa lugha ambapo,Mungu anataka kukutumia kusema na watu wa lugha usizozijua,kwa uwezo wa Roho Mtakatifu,unaingea lugha ya hao watu na unaweza kuwa wewe muongeaji/mnenaji huelewi,ila wao watasikia kwa lugha zao na kupata ujumbe wa Mungu
Mdo 2:7-13
NB
Nashawishika ktk siku ya Pentekoste walijaliwa aina hizi zote ikiwa ni introduction of the New Era "New season of the Spirit" na hii haijakoma hata sasa.
iii.)Mahubiri ya Neno la Mungu kwa wingi
>Sio aina zote za mahubiri zinajenga nafsi,ila yako aina ya mahubri/jumbe ambayo ni edification-based,yako mengine ni knowledge-based n.k
>Ni muhimu kuyasaka kwa bidii mahubiri yenye kujenga nafsi hadi ufike kiwango kizuri cha nafsi kujengwa.
>Ukiwa na neema ya kusoma vitabu vya watumishi wa Mungu,basi fanya hivyo ili ujengeke nafsini mwako
iv.)Kusoma neno la Mungu,kwa wingi (Intensive Bible Reading/Bible study)
Kol 3:16,Yoshua 1:8,Zabur 119:1-176,20,16,14,54,72,77,97,103,111,140,165
v.)Maombi yanayofanywa ktk hali ya kufunga(Fasting&Prayer)
2Kor 4:16,2Nyak 20:3,Ezra 8:21,Zabur 35:13,69:10,109,24.Yer 36:9,Dan 9:3,Yoel 2:12,Yona 3:5.Math 17:21,Luka 2:37,Mdo 13:2,Mdo 14:23,2Kor 6:5,11:27
vi.)Kutumia muda mwingi kwa BWANA, kwa mambo ya Mungu
Neh 9:3,Walitumia masaa 12 mbele za Bwana
Zabur 27:4,122:1,84:10,2,Mhubir 8:3a,1Yohana 3:19
NB
*Watu ambao wametoka kufunguliwa vifungo kama mapepo/majini,magonjwa sugu,hasa ya kurithi au wametoka kwenye vifungo vikubwa vya dhambi na uovu,wanapaswa kuwa mstari wa mbele ktk kujijenga nafsi*
*5.) NAMNA AMBAYO NAFSI ILIYOJENGWA INASHINDA YOTE*
Mithal 22:3----- ......huyaona mabaya akajificha
*Watu tuliookoka tumeitwa tuishi ktk ulimwengu wa mwili na wa roho,kwa wakati mmoja,tunaishi ktk dunia mbili kwa wakati mmoja.
*Pia tunakabiliwa na vita toka ktk kila ulimwengu, unaweza shindwa ktk ulimwengu wa roho ikawa chanzo cha kushindwa ktk ulimwengu wa mwili
*Nafsi ikijengwa waweza shina bila shaka (Hesabu 13:30)
*Ahadi kuu za Mungu ni kwa ajili ya walioshinda,kama tunavyosoma
Ufunuo 2:12,26,7,11,17,3:21,12,5,21:6ff
*Mtu ambaye nafsi yakr imejengwa,anaxhipushiwa mti wa uzima ndani,utakaompa tuna la Roho. Hili tunda lina kazi ya kumshindia vita ya mwilini inyotaka kumkosesha (Mathayo 18:7-8,Luka 17:1-2,Gal 5:22)
*Muda wote mambo ya kukisesha yatajaa mlangoni,na inapasa uyashinde mabaya,ukapaswa kushinda kwakutenda mema utaweza? Rumi 12:21
>Yusufu na kakaze(Mwanzo 50:15-20)
>Daudi kukata upindo wa vazi ila hakumuua adui(1Sam 24:1-12)
>Daudi kutwaa fumo na gudilia la maji na kukataa wazo la Abishai kumwua Sauli🗡 (1Samwel 26:7-22)
*Unaweza kufikia wakati inapotakiwa ufanye hujuma(embezzlement/forgery) kwenye mambo fulani,Je utakwepa au utafanya haki??
Unapaswa kugushi sahihi,au hti feki,au kukwepa kulipa deni
Yer 32:11ff ,17:10,Mithali 11:1,Ayubu 31:6,
>Unafanya biashara ya maziwa utajaza maji?
***Unaweza kukutana na upinzani kwa jamaa zako wa mwili(wazazi),Unalenga kukukosesha,sasa sharti ushibde bila kuharibu chochot.
*mtu mwenye nafsi iliyojengwa atashinda tuu*
*UKOMBOZI KWA DAMU YA YESU*
Neno "komboa" linaleta maana tamu zaidi tukiliangalia kwa upana toka kwa lugha zingine (Hebrew:-Pedut) (English:-Redeem)
Maana yake ni hii.....
*To recover ownership of something by buying it back
*Liberate by payment or a ransom
*To set free by force
*To clear,release from debt/blame
*To restore the reputation or honour
Kwa habari ya ukombozi wa nafsi tujifunze mambo manne ya msingi kuhusu ukombozi
*A.KWA NINI UKOMBOZI*
*Dhambi,uovu na makosa yalitupa kuuzwa,tusiwe mali yake Mungu,nafsi zetu ziliuzwa
Isaya 50:1,52:3
*Tangu Adamu wanadamu wote waliokufa baada yake walienda kuzimu,maana dhambi ilibadilisha ownership...Watu walitofautiana tu wapo eneo lipi la kuzimu either Sheol,Gehenna au penginepo maeneo mengine ya kuzimu ni kama Abussos,Chasm,Tartarus (Luka 16:19-26,Zabur 16:10,Ufun 9:1,
Na ndio maana kufufuka kwa Yesu kulihusisha transmigration ya wale waliokuwa huko Sheol watoke kwenda mbinguni(Math 27:51-53)
*B.)MUNGU ANAWEZA NA ANATAKA KUTUKOMBOA*
Zaburi 72:14,34:22,Yer 32:11,Ayu 33:28,Hoses 13:14,Omb 3:58
*C.)KWA KUWA TULIUZWA ILIKUWA LAZIMA TUNUNULIWE,YAANI LAZIMA ITOLEWE FIDIA(RANSOM)*
Ufunup 5:9-10,14:4,Mdo 20:28,1Kor 7:23,6:20
*D.)UKOMBOZI HUU NI KWA NJIA YA YESU,DAMU YAKE NA MSALABA*
Ebra 9:15,9:12(Once for all),Gal 3:13,Luk 24:21,1:64,1Tim 2:6.Kol 1:14,Efes 1:7
Mwl Proo
0762879363(whatsapp)
0718922662(texts/calls)
alltruth5ministries@gmail.com
No comments:
Post a Comment