Saturday, December 9, 2017

MSINGI MBOVU WA NDOA

*MSINGI MBOVU WA NDOA*
_*SALAMU KWA WATU WOTE, NA KWA WADADA WENYE WATOTO ILA HAWAKO KWENYE NDOA*_

*Mwl Proo*
*+255762879363*

*Nawasalimu kwa jina la Bwana (Yesu). Sijaleta kama somo kamili, ila nawaamsha kwa kuwakumbusha. Msingi ni wa muhimu, ukiharibika mwenye haki atafanya nini? (Zaburi 11:3)*
*Katika siku hizi za mwisho kunatokea mengi sana yanayouvuruga mwili wa Kristo, miongoni mwa taasisi nyeti, ambazo shetani anajibidiisha kuzivuruga ni "NDOA". Maana ndoa zenye amani na takatifu zinazaa kanisa takatifu na lenye amani, na ndoa zikiwa za machafuko na kanisa linakuwa la machafuko.*

*Msingi hutangulia yote, Je! mlioana kwa sababu zipi?, nyakati hizi tunazo ndoa za kuchemshwa, yaani sababu iliyofanya mwoane ni uovu/dhambi, hapo ndipo msingi wa kwanza mbaya. Yaani mlianguka kwa uasherati, mkaamua ku-process harusi fastafasta ili ule ujauzito uonekane uliwakuta ndani ya ndoa. Hapa mmeunda dhambi itakayokuwa hai daima, mpaka kwa gharama kubwa ya toba. Niliwahi kuwa katika kanisa fulani, walihamia watu ambao huko walipotoka walikataliwa kufungishwa ndoa, kwa sababu waliripotiwa kuwa na mienendo ambayo sio katika uchumba wao (Mkiisha propoziana haiwapi ruhusa ya kuendelea na tendo la ndoa). _"LET ME BE LITTLE BIT HARSH HAPO, SEX NI KWA AJILI YA WANANDOA HALALI TU, MOYONI MWA MUNGU HAKUWAI WAZA KUWAUMBIA TENDO LA NDOA WATU WASIO WANANDOA, LABDA WANYAMA"._ Sasa watu hawa wakaja na kuomba mchungaji awafungishe ndoa, na kwamba watabaki kama washirika waaminifu hapo. Mchungaji kwa shauku ya kuongeza kondoo wahamiaji, akatangaza tarehe ya kufunga hiyo ndoa. Mzee mmoja wa kanisa akatumiwa kwa karama ya unabii, kufunua siri kwamba watu hawa wametenda dhambi, na bado maneno hayo yalipuuzwa. Miezi haikutimia hata sita yule mama akajifungua, na wala sio "premature birth", Ila mambo yalifunikwafunikwa wakaendelea. Hapo ndoa imejengwa kwenye msingi mbovu wa dhambi, hawa watu wataandamwa sana kupungukiwa na utukufu wa Mungu, na baraka zake (Kumbuka "UTUKUFU UNAWEZA KUONDOKA", jitahidi upate somo hilo la utuufu kuondoka, lipo kwenye mtandao). Hawa watu waliutweza unabii, wakamfanya aliyetumiwa aonekane mwongo, kumbe wao katika uchumba walikuwa wakitembeleana kubanjua amri ya saba kama kawaida yaani kula keki ambayo sio halali kwao kwa wakati huo. Kwa jinsi walivyojitahidi kula dili hilo, kumzuzua na mchungaji, watakuwa na gharama kubwa ya roba (Jitahidi upate somo langu liitwalo, "KUNA TUMAINI KATIKA TOBA HATA KAMA KOSA NI KUBWA")*

*AINA NYINGINE SITA ZA NDOA ZENYE MSINGI MBOVU*

💍Ndoa ambazo ziko kwa sababu ya watoto

💍Ndoa ambazo ziko kwa sababu ya kukosa pa kwenda

💍Ndoa zilizopo kwa sababu ya kushauriwa mara kwa mara

💍Ndoa zilizopo kwa sababu ya shinikizo la wazazi

💍Ndoa zilizopo kwa sababu ya vitu

💍Ndoa zilizopo kwa sababu ya kulinda huduma

*👆👆👆👆👆👆YAANI NDOA ZLIZOSHIKILIWA NA HAYO, ZINAKUWA FEKI KIMSINGI, NDOA ZINAPASWA KUWA NI ZILE ZILIZOTOKANA NA UPENDO WA MKE NA MME*

NB:-
*NAWAONYA MBELE, MSITHUBUTU KUJENGA NDOA KWENYE MSINGI WA UOVU/DHAMBI, MTAKUWA NA MDORORO WA KIROHO AMBAO UTALETA ATHARI MPAKA MAISHA YA KIMWILI, MNAWEZA KUWA WOTE MNA KAZI NZURI ZA KULIPWA MAMILIONI, LAKINI KITENDO CHA UTUKUFU ULE WA MUNGU KUFARAKANA NANYI (Isaya 59:1-2), MNAWEZA KUTA MNAONEKANA DUNI, NYUSO ZIMEPAUKA WAKATI DRESSING TABLE MMEJAZA VIPODOZI VYA KILA AINA, NA HAMTAPA NAFASI KATIKA MAISHA YENU KUU-ACCESS UWEPO WA MUNGU, MPAKA MRUDI PALE MLIPOJIKWAA MTENGENEZE (Ufunuo 2:5).*

*WADADA WENYE WATOTO, NA HAWANA NDOA*
*Roho aliniwekea kitu ndani niwahimize. Wengi wenu mnakabiriwa na kuharibikiwa mahusiano au kutopata watu wa kuwaoa. Wanaume nao ni waharibifu, wamewapa mimba wadada kadhaa, wamewabikiri wasichana kadhaa, na muda wa kuoa anasaka tena wale clean, unakuta kakataa mimba, au amekataa kukuoa ila amesema tu atalea mtoto (gharama). Sasa unakutwa na wakati mgumu wewe mdada unapohitaji ndoa halali. Hapa kuna mtego na tanzi, wadada wengi wanaamua kuwa-dump watoto wao kwa bibi zao huko vijijini, yeye anabaki mjini kuji-dadaisha zaidi, kurahisisha kupata mume. Kitendo cha kutoweka wazi kwamba una mtoto, ni MSINGI MBOVU wa ndoa*
*JAMBO LA KWANZA, NI MUHIMU UFAHAMU WEWE KUWA NA MTOTO HAINA MAANA NDIO MDHAMBI SANA KULIKO WADADA WENGINE, HUENDA ULIFANYA UASHERATI MARA MOJA TU, NA HAPOHAPO MIMBA IKASHIKA, WENGINE WALISEX TANGU SEKONDARI MPAKA CHUO MARA ZISIZO IDADI, ILA HAWAKUPATA MIMBA, SO THEY ARE NO BETTER THAN YOU, NI KWAMBA TU WEWE UMEBAKI NA UTHIBITISHO*

NB:-
*_DARE NOT (USIDIRIKI) KUMFICHA MTOTO, AU KUTAKA AWE MBALI, ULIPOOKOKA ULISAMEHEWA DHAMBI ZOTE PAMOJA NA HIYO, SASA HATA ATHARI ZINAZOSABABISHWA NA MAKOSA YA KALE, UNAWEZA KWA UAMINIFU KUMWAMBIA YESU AFANYE KITU. YEYE ANAWEZA KUMLETA MUME SAHIHI, AMBAYE ATAKUPENDA KWA DHATI PAMOJA NA HUYO MTOTO. USITUMIE HICHO KIKWAZO CHA KUPATA MUME KUOLEWA NA YEYOTE. NA WENGI NILIOKUTANA NAO WANAJARIBIWA KUWAZA KUOLEWA NA WATU WASIO NA IMANI MOJA NAO (IMANI KATIKA YESU), DARE NOT(USIDIRIKI) KUOLEWA SIJUI NA MWISLAMU BAADA YA KUONA KAKA WATUMISHI WANAKUKWEPA KWA AJILI YA MTOTO. NI BORA UISHI MSEJA/BACHELA/SINGLE MPAKA YESU ARUDI, UKICHEPUKA KIIMANI UMEENDA MBALI SANA KATIKA KUUJERUHI MOYO WA YESU. HATA UKIACHIKA HUKO KWA TALAKA TATU, UKAONA URUDI KUNDINI, UNAWEZA SAMEHEWA, LAKINI MOYO WA MUNGU HAUTAKUAMINI_*

*NDOA HALALI NA TAKATIFU*

_*Kama nilivyoeleza kwa uchache, katika somo langu la "Talaka katika Ukristo", Jitahidi ulipate! Ndoa ya Kikristo sharti iwe halali na takatifu. Ndoa halali ni ile ambayo imefuata taratibu zote zinazokubaliwa na jamii, za kidini au kiserikali, kuwa kwa taratibu hizi hawa ni wanandoa halali. Sasa ndoa kuwa halali sio kuwa takatifu, maana hata kama watu mtaanza kuishi mkafanya uasherati, na mkaenda bomani mkafunga ndoa kiserikali, bado mtatambulika ni wanandoa halali, lakini hiyo sio ndoa takatifu. Na hatutarajii waamini (Mliookoka) mwe na ndoa halali tu bali takatifu, ndoa takatifu inajumuisha msingi mzuri wa ndoa, sio mmeanza kukaa (cohabitation) halafu mnaenda kuchemsha ndoa, mahusiano tunayoweza kuyatambua kwa watu wa Mungu ni kaka&dada (urafiki), uchumba na ndoa. Na hapo kwenye urafiki sio kwa tafsiri ile ya "boyfriend na girlfriend", yaani mpo kwa urafiki ila kuna wakati mnatimiziana na haja za kimwili za tamaa zenu, HUO HAUPO!*_

*HAYA MAMBO YA KUBARIKI NDOA KUNA WAKATI YANACHUKULIWA VIBAYA MAANA NI MAFUNDISHO YA KIMAKANISA KATIKA KUTAFUTA KUWASAIDIA EITHER WATU WALIOKOKA WAKIWA HAWANA NDOA HALALI, ILA WALIKUWA WAKIISHI TU. SASA BAADAE IKAJA KUWA SHIDA, HATA WALIOAMINI WAKIFANYA DHAMBI YA UASHERATI, WAKAPEANA MIMBA, WANACHUKUANA, KWAMBA TUTAKUJA KUBARIKI NDOA. WELL AND GOOD, KWA AMBAO MPO KWA HUO MTEGO WEKENI SAWA MAMBO YA NYUMBA ZENU (Isaya 38:1b). LAKINI KWA WENGINE NI MUHIMU MHAKIKISHE MNASIMAMA, MUNGU HAWI RADHI NA WAPUMBAVU (Mhubiri 5:4b), HAWEZI KUPOTEZEA UOVU/DHAMBI AKA-ASSUME KAMA HAONI (Matendo 17:30, Kutoka 34:7b). KWA NINI MFANYE MAMBO YA KUUNGAUNGA, KWA NINI MCHEMSHE. NDOA TAKATIFU NDIZO TUNAZITARAJIA KANISANI, NA NDOA TAKATIFU INAWAHUSU WAAMINI(WALIOOKOKA), KWA MAANA INAKUWA HAINA MSINGI WA DHAMBI, NI HALALI (MAANA IMEFUATA TARATIBU ZINAZOKUBALIKA KWA NDOA HALALI, LAKINI NI TAKATIFU MAANA WANANDOA NI WATAKATIFU).*

NB:-
*INGAWA NIMESEMA NDOA HALALI NI ILE ILIYOPITIA TARATIBU ZOTE ZINAZOKUBALIWA NA JAMII, DINI AU SERIKALI KUWA KWA TARATIBU HIZO, HIYO NI NDOA HALALI, LAKINI KWA WATU WA MUNGU HATA HIYO NDOA HALALI WATAIZINGATIA TOFAUTI NA WATU WA JINSI YA MWILINI. KWA MFANO TUKIONA MWAMINI, UNAFUNGA NDOA YA KIMILA, UTATUACHIA MASWALI FULANI, TUKIKUONA ULIYEOKOKA UMEENDA KUFUNGIA BOMANI PIA TUTABAKI NA ❓❓❓❓, UMEKIMBIA NINI MADHABAHUNI PA MUNGU, HATA KAMA BADO VYETI NI VYA KISERIKALI.*

*POSSIBLE QUESTION/SWALI LINALOWEZA KUZUSHWA*

_*Mtu ata-challenge, hasa ambao kuna namna walivuruga mienendo, kanisa likawatilia shaka kuwafungisha ndoa, kwamba andiko gani linalonitaka nikafungie ndoa madhabahuni kanisani?. Ikumbukwe mambo mengi kuhusu harusi na ufungishwaji wa ndoa, iko culturally-based kuliko kuwa kibiblia, hata yale utakayoyaazima kwenye Biblia sio yote ni maelekezo ya Mungu kwa ulimwengu, mengi kuhusi harusi na ufungishwaji wake ni ya utamaduni tu (Graeco-Roman&Jewish culture), lakini kama watu wa jamii ya waaminio, na hujavurunda njia zako, huoni kuwa ni bora zaidi kwa mwamini kuanzia safari ya ndoa madhabahuni?*_

NITARUDI TENA, TUKUTANE KWA NEXT POST
*_Mwl Proo_*
*0762879363*

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment