Thursday, December 14, 2017

MAMBO YA KIROHO YAKIHARIBIKA; TENGENEZA!

KWELI YOTE SERIES

Na Mwl Proo
0762879363
0718922662

*MAMBO YA KIROHO YAKIHARIBIKA; TENGENEZA.*

Somo lina sehemu saba
I. Maana ya kila neno ktk kichwa habari
II. Viashiria vya mambo ya kiroho kuwa mazuri
III. Viashiria vya mambo ya kiroho kuharibika(Bwana kukuacha)

IV.
A.)Vitu/Mambo yaharibuyo kiroho
B. )Vitu/Mambo yawezayo kuinua/kutengeneza kiroh9 kilichoharibuka
V.) Hatari ya kukaa na kiroho kirichoharibika
VI.) Bwana anatazamia nini,kwa mtu ambaye mambo yake ya kiroho yameharibika?
VII.) Hitimisho

*I.) MAANA YA MANENO YA KICHWA CHA UJUMBE*

A.) Mambo ya kiroho
Include/indicate/imply
-Hali ya kiroho
-Mahusiano na Mungu
-Sensitivity kwa mambo ya Mungu
-Activiteness
-Inclination of spiritual graph ktk
*Prayers(of all types)
*Fear of the Lord(Kicho)
*Huduma(zote)
*Holiness
*Kiu ya mambo ya Mungu
-Uhusiano wako  na watumishi wengine/watu ambao hawajaamini bado(Ndugu wa kiroho/kimwili)

B.) Yakiharibika
Maana yake
*Kuna uwezekano wa mambo ya kiroho kuharibika
*Kuna jambo  mtu anapaswa kufanya,mara anapogundua huo uharibifu (Zabur 11:3)
Luka 14:34 Chumvi ikiharibika.....
*Unawajibika kulinda kiroho kisiharibike/kuna uwezekano wa kuwa na kiroho kisichoharibika

C.Tengeneza
-Tengeneza mambo ya nyumba yako (Isaya 38:1b)
-Tengeneza njia na matendo (Yer 7:3b)
*Mwenye jukumu la kutengeneza ni wewe(1Sam 7:3 Mtengenezee Mungu moyo wako......)
*Yanatengenezeka

MATUKIO YA PEKEE (EXCEPTIONAL CASES)
Kuna namna mambo ya kiroho, yanaweza kuharibika yasitengenezeke...wala Mungu hawi radhi tena
Yeremia 15:1-2,14:11
Katika maandiko haya, ni mahali ambako Mungu hayupo radhi hata kusikia sala za kuhitaji arehemu..na anazuia usiombe kabisa
Pitia haya vizuri
Ezek 14:14,20
Yer 7:16
1Samwel 16:1

MAZINGIRA HAYA YANAFAFANULIWA ZAIDI KAMA KUMKUFURU ROHO MTAKATIFU
Kuna namna mbili kuu za kulielewa jambo hili, la kumkufuru Roho Mtakatifu.

A.) Deliberately, Unakana kweli kuhusu Roho Mtakatifu na kumfedhehi
Marko 3:29-30; Ebran 10:25, 6:4-6

*USHUHUDA:*
Kuna binti mmoja alihamia Shule ya wasichana fulani, mikoa ya kusini.. ujio wake ulibadili hali ya kiroho yote pale shuleni kwa kutokea kwenye fellowship ambayo aliiletea uamsho..wote waliamini kuhusu wokovu kupitia yeye akiwa form II
Alipofika form II aliwaomba viongozi wa michezo na burudani waandae disco ya wikiend anataka acheze mbele ya wote ili wajue ameacha ulokole.. kwa kawaida disco hizo huandaliwa mwisho wa mwezi lakini wakaandaa ili wamshuhudie mlokole akicheza disco ikiwa ni ishara ya kuacha wokovu mchana kweupe.. baada ya tukio hilo hata walioamini mambo ya utakatifu wote wakarudi nyuma.
Alipo maliza masomo na kurudi kwao.. mama yake(mzee wa kanisa) akagundua sura ya Mungu haipo kwa bintiye na alipomuuliza alithibitisha. Yeye na wamama wengine wakaingia kufunga na kuomba masaa 72 ili Bwana arejeze rehema zake... wakiwa siku ya pili na usiku wa manane wanaendelea kuomboleza..Mungu akasema na mmoja wao.."ACHENI KUMWOMBEA NIMEMKATAA" nitafafanua hili vizuri

Ikumbukwe kumkana kwa kusudi ni kama haya anayoyafanya Nabii Tito   anavyohimiza watu wazini na mabinti wa kazi kwa kutumia Biblia .Pia ana hamasisha ulevi kwa kutumia Biblia.Anafanya haya kwa Bidii akiwa anajua kweli ya Mungu

B.)Kumkufuru Roho Mtakatifu kunakotokea kwa stages
Ziko stages 4 za msingi
*1 Dhambi nyingi zisizotubiwa
Isaya 1:4;Ufu 1:21
*2 Kumhuzunisha Roho Mtakatifu
Efes 4:30;Isaya 63:10
*3 Kuwa na moyo mgumu/mbovu
Ebran 3:12,3:8
*4 Kumpinga Roho Mtakatifu
Mdo 7:51

Mtu akipitia hatua hizi 4 anakuwa amefikia kumkufuru Roho Mtakatifu

KINACHOFANYA HUYU MTU AITWE AMEMKUFURU ROHO MTAKATIFU NI KWA SABABU HAWEZI KUTUBU TENA;SIO HAWEZI KUSAMEHEWA ILI HAWEZI KUWAZA TOBA..IKUMBUKWE ROHO MTAKATIFU NDIYE ANAYEUSHUHUDIA ULIMWENGU KWA HABARI YA DHAMBI HAKI NA HUKUMU..ANAYELETA CONVICTION OF SIN MTU AKIJIHISI GUILTY NI ROHO MTAKATIFU AMBAYE HAYUKO TENA

NB:
Mambo ya rohoni  yanategemeana...ukiharibu jambo moja you are likely kuharibu mengine.. huenda umejikwaa ktk utoaji unakuta linakunyima uhuru kwenye maombi etc etc.

*THE IDEA OF PREDESTINATION(Ukweli kuhusu hatma zilizopangwa tayari)*

Katika uislamu yuko malaika aitwea Khatibun, anayehusika na kuyapima matendo mema na mabaya. Ikionekana matendo mema yanayazidi mabaya basi unaingia peponi..lakini yale ya kushoto yani mabaya yaki-outweigh yale mema basi unatupwa Jahanam..lakini wanaamini kuwa bado unaweza kutenda mema lakini Mwenyezi Mungu anaweza tu akapendelea kukuona Jahamam hivyo Khatibun atakuambia kuwa Sorry matendo yako ni mema lakini Mwenyezi Mungu anapenda tuu kukuona motoni

Katika Ukristo fundisho la Predestination lipo ila lina utata fulani.
Yako maandiko kadhaa yanayoonesha Mungu ana watu wake aliwachagua kabla ya kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu (Rumi 8:29-30; 2timothy 2:19) pia yako yanayoonesha kuwa wako walioandikiwa hukumu tangu zamani (Yuda 1:4). Na Yesu alisema kuwa mtu hawezi kwenda kwake asipovutwa na Baba yake. Wapo watu kadhaa ambao wameitwa kwenye deliverance ministry wameshuhudia yako maeneo wanashuhudiwa wasiwahudumie watu fulani..yaani Mungu hayuko radhi nao..Mungu hana upendeleo (Mdo 10:34-35; Rumi  2:11) lakini Mungu Baba ktk nafsi yake anayo maamuzi ambayo hayahukumiwi ingawa kibinadamu ni upendeleo wa kimungu (Kutoka 33:19) anasema anamhurumia amhurumiaye na kumrehemu amrehemuye... hayo anafanya kama CHOICE yake ilivyo...Kwa mfano kabla Esau na Yakobo kuzaliwa Mungu alisema mkubwa atamtumiaka mdogo (Mwanz  25:27-41) na kabla watoto hawajajua kuita  baba au mama.. Mungu akasema Nimempenda Yakobo bali Esau nimemchukia (Malaki 1:2ff)..Mungu alitumia vigezo vipi kwa hawa mapacha kumchukia au kumpenda mmoja wapo wakiwa bado wachanga????

WARUMI 9

11 (kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto, wala hawajatenda neno jema wala baya, ili lisimame kusudi la Mungu la kuchagua, si kwa sababu ya matendo, bali kwa sababu ya nia yake aitaye),

12 aliambiwa hivi, Mkubwa atamtumikia mdogo.

13 Kama ilivyoandikwa, Nimempenda Yakobo, bali Esau nimemchukia.

14 Tuseme nini basi? Kuna udhalimu kwa Mungu? Hasha!

15 Maana amwambia Musa, Nitamrehemu yeye nimrehemuye, nitamhurumia yeye nimhurumiaye.

Lakini pamoja na kusudi la Mungu ktk kuchagua(Upendeleo) bado inabaki kweli kuwa "NEEMA YA MUNGU IWAOKOAYO WANADAMU WOTE IMEFUNULIWA....."ila yeye anaijua miisho yetu yote (Isaya 42:9,46:10)
Mungu aliwahi kunionesha kuwa kuna mtu atakufa bila kutubu.. nilifanya kuomba akumbuke rehema lakini ikawa vilevile exactly kama nilivyoona

*III. VIASHIRIA VYA MAMBO YA KIROHO KUWA MAZURI*

*Kujaa na kufurika kiroho
Zabur 23:5(Kikombe changu kinafurika). Nilikuwa na kiongozi wangu mmoja wa fellowship (Frank Martin) akiwa amejitahidi kuishi kikamilifu alitamani aijue hali yake kiroho..akamuuliza Mungu ktk maombi ajulishwe yupoje kiroho (Akaona malaika/mtu mbele yake ameshika kikombe kimejaa maji safi mpaka juu karibu ya mwagike) mtu huyu aliyefurika rohoni mtamjua tuu hata ktk Mazungumzo

*Kumsikia Mungu kwa njia zote anazozitumia kusema (Verbal Voice,Visions,dreams etc) Hesabu 12:6

*Hataridhika kukaa na uovu/kosa hata kama dogo.Na hivyi Roho Mtakatifu ataenda nawe kwa viwango hivyo..(Yupo rafikiangu aitwaye Eliya..alichukua peni ya mtu akakawia kuirudisha na mwenye yake akawa akilaumu sana..Tukiwa darasani akasinzia sekunde chache akaona kucha zina uchafu.. kushtuka hivi anaona kucha zake alizaka na hakuna uchafu..Roho akamjulisha ni hiyo peni ya mtu inayoleta kwazo akairudisha fasta.Kumbuka kama ukichukua mali ya mtu na unakawia kuirudisha hadu ufuatiliwe sana umekosa kitu kinaitwa INTEGRITY.sasa unaweza ona jinsi ambavyo kitu kidogo sana anadili nacho yaani peni tu ya kuazima.

*Uaminifu kwenye mambo ya Mungu
Ebrania 2:17

*Mwepesi kwenye mambo ya Mungu
Yesu ni shahidi mwepesi (Mal 3:5)Ahadi ya Mungu ni kukuvika vazi la sifa badala ya roho nzito(Isa 61:3)
-Yesu ni mwepesi kutenda haki Isay 16:5

*Utakuwa unasikia raha yakumshirikisha Mungu mambo yako (Isaya 29:15)

*Kutumia muda mwingi kwa Mungu
Zaburi 27:4;Neh 9:3 Hawa watu wa zama za Nehemia walitumia masaa 12 mbele za Mungu

*Unakuwa huru mbele za Bwana (Amuz 6:18)

*Hata kama mpo watumishi wengi ni rahisi wewe kuona mambo katika ulimwengu wa roho (Ezekiel 1:1;Dan 10:7;Mark 1:9-10)

*Hutamwogopa adui(Shetani)
-1Yoh 5:18

*Kila huduma utakayoifanya,kutakuwa na udhihirisho wa kimungu
Yoh 14:21b;Mdo 19:11;Isay 58:9

*Unapendezwa na Neno (Yer 15:16;Zab 119:1-176)

*Utakuwa na neema ya kunusurika katika hatara/janga/msiba/shida ambayo imewapitia wengi (Ayu 33:23-24)

*Utatafuta amani na watu wote,kwa kuwa vertical relations are built up  on the holizontal relations. So utakuwa tayari kujishusha hata kama ni wewe umekosewa (Heb 12:14;Math 17:27)

*Unakuwa na moyo wa toba (Rumi 2:5)

IV. VIASHIRIA VYA MAMBO YA KIROHO KUHARIBIKA (Bwana kukuacha/kukukataa)

*Neno la Bwana kuwa adimu/kukosa mafunuo dhahiri (1Sam 3:1)-Rhema+Logos

*Unapoteza ujasiri mbele za Bwana (Yeremia 21:2b)

*Kuyajenga uliyoyabomoa (Gal 2:18;1Sam 28:3b,7)

*Mungu anaacha kusema na wewe (1sam 28:15)

*Hutapenda suluhu (2Tim 3:3)

*Hata ukirudiwa(ukiwa punished) hurekebishi
(Amos 4:6-11,2Nyakat 16:12B,28:22)

*Kumwepuka Bwana (Yona 1:3,Amos 7:12-13)

*Hutafurahia neno  (Yeremia 6:10,20:1-2,Isa 30:9-10 )

*Hutataka kumuuliza BWANA
Yer 10:2;Ezek 20:31;Isa 30:1;2Falme 1:1-3;2Nyak 18:4-7

*Kujihesabia haki (moyo usio na toba)
Ufunuo 3:17;Rumi 2:5

*Tunda la Roho(mti wa uzima uliopandww ndani yako) linafifia,unakosasome qualities upole<>Mkali😠 etc (Galatia 5:22;2Pet 1:5-8)

*Ushindi juu ya nguvu za giza unapungua .(Kwani kiroho kilichoharibika  kinafanya usifike mbali kwenye uwepo wa Mungu(Beeping),You pray,but prayer becomes only a click

*Kukosoa kila jitihada za watumishi wengine katika nyumba ya Mungu;badala ya kuwatia moyo na kutafuta yaliyopunguka uyafanye wewe.

*Kuwa na maisha yasiyo na utaratibu (Disorderly living) (2Thes 3:6,11;1Thes 5:14)

*So excusive (udhuru)kwa kigezo cha ubize..but the same responsibilities/duties ulipokuwa na kirohovkizuri ulufanya hata. Unaposongwa(Yakob 4:17;Rumi 1:20)
-Unapotoa udhuru kwa Bwana,ili uwe exempted from your duty ;Bwana anahesabu umeuacha   upendo wako wa kwanza (Ufun 2:4,Yer 2:2)

*Kusitasita (naye akisitasita .......Ebran 10:38)
The one who hasitates,is not sure or has not made decision where to be,where to stand,where to go,probably what he/she is supposed to do (Yakob 1:8)

*Ndoto na maono yanayokuja yamejaa maonyo tuu(Ayub 7:13-14)

*Unaogopa watumishi wa Mungu ,hasa ambao mambo yao ya kiroho yako okey (1Falme 21:20,18:17;Marko 6:20)

*Kumtaka Mungu katika shida tuu
(Yer 2:27)

V. VITU/MAMBO YAHARIBUYO KIROHO

*Kuacha kulifuata neno la Mungu,lote bila kulipunguza wala kuliongeza (Kumb 12:32,Zaburi 119:160,Mith 30:5-6,Ufun 22:18

*Kuwa na neno lisilofaa moyoni
(Kumb 15:9;Mwanz 27:41)

*Kutazama visivyofaa (Zabur 119:37) including pornographic contents in this modern world

*Bad companions (1Kor 15:33) and advisers (2Sam 13:5-14;Zab 1:1)

*Prolonged time in prayerlessness life
1Thes 5:17,Luka 18:1;Kol 4:2

*Kufuatisha namna ya dunia hii
(RUMI 12:2)

*Kuchoka kutenda mema (Galatia 6:9)

*Kuwa na desturi ya kutotii (Yer 22:21)

*Kufungiwa nira na wasioamini,isivyo sawasawa (2Kor 6:14ff;Zab 1:1)

*Unauthorized intimacy- relationship (1Kor 7:34a;Math 1:18b)

*Kuacha huduma (2Nyak 28:22-24/ff)
-Huduma inakupa sababu ya
>Kulinda utakatifu
>Kuomba/Kutafuta uso wa Bwana

*Kuacha kuambatana na watumishi wenza
Dema alim-desert Paulo(2Timo 4:10);Mdo 15:37-41 Barnaba

*Kufanya dhambi kwa makusudu,ambako kunaiua dhamiri (Conscience/inner conscious Ebran 10:26)

*Kwenda mahali ambapo unajua utatenda dhambi..Kwenda Bar,Disco,Nude Beaches 👙🏊🏻etc (Amos 4:4)

SEHEMU YA 5 B YA SOMO INASEMA.. MAMBO YANAYOWEZA KUINUA KIROHO KILICHOHARIBIKA/KULINDA KIROHO KISIHARIBIKE

👆🏼I'M SKIPPING THAT PART KWA KUWA NI VICE VERSA OF THE FORMERLY EXPLAINED SECTION

NITARUKIA SEHEMU YA 6 YA SOMO

VI) HATARI YA KUKAA NA KIROHO KILICHOHARIBIKA
*Aibu (Mithali 14:34;Rumi 6:23)unawaza ukajikaza na kiroho kilichoharibika ipo siku utapata aibu.. mnakumbuka ushuhuda wa dada aliyetuma  picha zake za uchi kwenye grupu la whatsapp la wanakwaya...kumbe alikuwa anafanya sexchat na mpenzi wake ikatokea bahati mbaya akakosea kutuma na alijinyonga..aliishi na kiroho kimeharibika bila kutengeneza (Wewe ambaye umasoma hii kama umeharibikiwa kiroho tengeneza maana Mungu kakulia pozi for so long..Ufunuo 2:21

*Anguko la kiroho
Mmewahi ona mtu anaanguka kwenye uzinzi au anaficha mimba au ukimwi unamuumbua? Ni kwamba kiroho kiliharibika akaendelea zake tu

*Kuikosa mbingu. Hakuna mwenye kiroho kilichoharibika atakaeingia mbinguni

*Baraka za Mungu zitaondolewa juu ya maisha yako..

*Kuondolewa kinara chako mahali pake (Ufunuo 2:5b) ile sifa yako kiroho na mipango ya Mungu kukufanya mkuu na mtawala popote inayeyushwa hiyo nyote na utakosa mng'ao wa utukufu

*Kukosa kibali kwa Mungu na kwa wanadamu ..unapoteza mvuto.. hutakuwa na ushawishi wa kufanya watu wakufuate au kukuiga wewe..hasa watu wa rohoni.. unaweza toa hoja ukakuta husikilizwi

*Kukosa furaha na amani ya kweli . Utajitutumua tuu lakini ndani mwako hutakuwa na furaha na amani  ya kweli...maana hauko sawa na anayetoa hivyo vitu

*Utakosa future( bright future)
Kila mtu mwenye Mungu anao mwisho hatma/destiny yenye baraka Zaburi 37:37
Lakini ambaye unawayawaya kiroho kama machela lazima utakosa bright future maana hukishiki Kichwa...(Kolosai 2: 19)
*Kwenye hatari zako Mungu anajificha .
Mithali 1:26-33

VII) BWANA ANATAZAMIA NINI, KWA MTU ALIYEHARIBIKIWA KIROHO?

Mara anapokufikishia ujumbe, UTENGENEZE!!!

Matengenezo:
*Toba (2Sam 12:13;Ezra 9:6;Dan 9:3ff

*Kulipa gharama ya toba (Ezra 10:2b,3
-Gharama ya toba ni pamoja na kutenda matendo ya mwanzo kwa bidii zaidi(yale yanayofanya kiroho kisiharibike mkumbuke Zakayo (Luk 19:1-11)

MATENGENEZO NI KWA WATU WOTE:
Kwa nini hapa hachomoki mtu?

Waweza bakiwa na udhaifu mmoja;yapasa uuache/uushinde,ili UKAE NA BWANA

Uko udhaifu ambao ulidumu muda mrefu..na wafalme wengi waliingia hawakutengeneza.. walijatahidi kutengeneza machache

Kulikuwa na mahali pa juu (High places) pa kutolea dhabihu kwa miungu ya kigeni

1Falme 11:7;12:31
*Sulemani 1Falme 3:3

*Asa (alishinda baadhi ya dhambi
1Falme 15:11-14

*Yehoshaphat alishinda baadhi tuu
1Falme 22:43,46

*Yoash (he prevailed many) lakini ule udhaifu wa kushindwa kupaondoa mahali pa juu hakuushinda
2Falme 12:2-3

*Amazia
2Falme 14:3-4 hakuushinda ule udhaifu

*Azariah
2Falme 15:3-4
Hakushinda udhaifu wote

*Yotham
2Falme 15:34-35

***HEZIKIAH (He overcame)
2Falme 18:3-4;5 huyu ni mfano wa kuigwa

VIII.HITIMISHO

A) Kwa nini tutengeneze??
Tunatengeneza kwa kuwa tunataka kukaa na Bwana!!!
Isaya 57:15;33:14-24
Zabur 15:1-5;24:3-6

B) Tunapotengeneza tunafanyiwa nini na  BWANA?( 5R's)

>Reposition (Zabur 18:19
>Re-establishment
>Restoration (Ayub 22:23)
>Revival (Hosea 6:2)
>Rectification

UTAKAPOREJEA UTAJENGWA.... KWA NINI KUTANGA MBALI? AYUBU 22:23

NB:
UKIWEZA PANGA RATIBA HATA YA KUFUNGA NA KUOMBA ILI KUTENGENEZA

Mwl Proo

0718922662/0762879363

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment