*NINI UKWELI KUHUSU FUNDISHO LA ZAKA/FUNGU LA KUMI*
©2015
Na
_Mwl Proo_
0762879363
0718922662
Nina wasalimu katika Jina la BWANA(Yesu) . Karibu tujifunze ili utoaji wetu uwe na maana sawa na kweli ya Injili.
SOMO LINA SEHEMU 12
I.)UTANGULIZI
II.)ETIMOLOJIA
III.)HISTORIA YAKE
IV.)ABRAMU NA YAKOBO
V.)ZAKA YA KILAWI(LEVITICAL TITHE)
VI.)TAFSIRI ISIYO SAHIHI KTK MALAKI 3
VII.)ZAKA KTK AGANO JIPYA
VIII.)LINI FUNDISHO HILI LILIINGIZWA?
IX.)NINI MSINGI WA UTOAJI KTK AGANO JIPYA(POST-CALVARY COVENANT)
X.)SHUHUDA ZA WALIOBARIKIWA
XI.)POSSIBLE GROUNDS TO JUSTIFY TITHING IN CHRISTIANITY
XII.)HITIMISHO
*I.) UTANGULIZI*
Kumekuwa na pande mbili zinazokinzana whether fundisho hili ni sahihi au sio sahihi ktk UKRISTO. Na tatizo kubwa lipo ktk msingi wa fundisho(Zab 11:3). Niseme kwamba UKRISTO SIO UYAHUDI INGAWA ULIANZA KAMA DHEHEBU NDANI YA DINI YA KIYAHUDI. Sasa ktk kuyachukua yale yaliyokuwa ktk dini ya KIYAHUDI(JUDAISM) kuyaleta ktk Ukristo inahitaji ufahamu mzuri wa kiroho wa kuweza kuchanganua ni nini ktk yale ya dini ya kiyahudi ambapo kuna (Maagizo ya Mungu+Utamaduni wa kiyahudi/traditions) Sasa lazima tujue kipi ni utamaduni na kipi ni agizo la Mungu endelevu(eternal moral principle).Utata umezuka ktk mambo mengi tu hasa inapofika kwenye kuyavusha mambo ya AGANO LA KALE KUYALETA KTK UKRISTO (Post-Calvary Covenant) Je tuyaache yote au tuyabebe yote? Kwa hiyo unakuta kila mtu anafundisha cha kwake maana mwingine akijaribu kuliset fundisho la MALIMBUKO kwa namna ileile ya Taurat anaona inakuwa ngumu au fundisho jingine lolote na hivyo kila watu ktk dhehebu lao hufundisha wanavyoona inafaa wao. Tunawezaje kupatata pure Christian Doctrine ktk maswala haya yote. Hatuwezi kama hatutarudi kwenye msingi ili kupata maarifa
*II.)ETIMOLOJIA*
Ktk historia ya neno zaka/tithe haikuwa na tafsiri ya sehemu ya kumi moja kwa moja. Kama ambavyo tutaona ktk sehemu ya tatu ya somo kuwa kiwango kiwango kilifanyiwa makaribisho ya chini(Rounded down) lakini sehemu ndogo yoyote ile ya ongezeka la pato (produce/income) na ndiyo maana ktk Kumbukumbu la torati 14:22-26 tunakutana na usemi wa ZAKA YA FUNGU LA KUMI
22 Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka.
Lakini tafsiri baadae ikawa ukizungumza TITHE/ZAKA UNAZUNGUMZIA SEHEMU YA KUMI(TENTH) ingawa tutaona ktk sehemu ya 5 ya somo kuwa jumla ya zaka ilikuwa ni <23% ktk Biblia. Sasa kietimolojia Neno la kiebrania Ma'aser linamaanisha zaka yaani sehemu ndogo(ya kumi) inayotolewa toka ktk increase ya produces na neno lilitumika ktk Septuagint(LXX) ni "Dekate" linalomaanisha moja kwa moja sehemu ya kumi. Neno hili Tithe/Tenth limetokea kwenye Old English "Teogopa" au Teopa(Western Saxon) na kijerumani "Teguntha" utoaji wa sehemu ktk mapato ilikuwa ni namna ambayo mataifa mengi yaliitumia hata kabla ya Sheria ya Musa(Mosaic Law) haya tutayaona ktk sehemu inayofuata lakini hata Yusufu akiwa Misri aliasisi sheria ya kutoa sehemu ya 5 ya mazao kwa Farao na sehemu ya 4 ilikuwa watu waitumie wenyewe(Mwanzo 41:34,47:24,26)
*III.)HISTORIA YA ZAKA(TITHING IN HISTORY)*
Utoaji wa zaka haukuanzia kwa Ibrahimu kama ambavyo wengi wanaotumia single source wanafundisha. Ktk Assyriological&Ancient Babylonian Literature tunaona kuwa hata mataifa ya kipagani ya vile vizazi baada ya Nuhu wote walikuwa wakitoa ZAKA kwa miungu(Waashuru walitoa zaka kwa mungu aitwaye *Anzu* na wale wababeli ya kale kwa mungu aitwaye *Merodaki*(Marduk)Wafalme walikuwa na local priests waliopokea Zaka ambazo ni sehemu ya kumi iliyo karibishwa chini. Kwa mfano Sheria iliwataka ktk nyara za vitani ktk kila mavazi 85 watoe zaka mavazi 8 na kwa kwa sababu hiyo ni kwamba ilikaribishwa chini maana mavazi hayo hayagawiki kwa kumi bila sehemu.Sasa kwa wale wenye haki sana walitoa mavazi 9 Sheria hii ilikuwa na limitation kulingana na nyara.Lakini ikumbukwe pua Sheria ya Musa ilizingatia hilo wale waliokuwa na vitu pungufu hawakutoa zaka ya fungu la kumu.Mfano mtu mwenye ng'ombe chini ya 10 kiidadi hakutoa zaka (Lawi 27:32). Kwa hiyo tayari mataifa yenye kuabudu miungu yalikuwa yana utaratibu wa kutoa zaka kabla ya Abramu na kabla ya Sheria ya Musa
*IV.)ABRAMU NA YAKOBO*
Katika Mwanzo sura mbili 14&18 zinazungumza watu wawili kutoa sehemu ya kumi ya walivyopata(Abramu alitoa sehemu ya kumi ya kila nyara na Yakobo anaweka nadhiri kutoa fungu la kumi kama Mungu akimfanikisha ktk njia yake)
_a.)KUHUSU ABRAMU_
Maswali la matatu ya msingi kuhusu Abramu...i. Kwa nini alitoa sehemu ya kumi ii.Nani alimwagiza iii.alijifunza wapi
Maswali haya wahubiri wengi husema alifanya kwa hiari yake(Okey nice) inapofikia kuhoji alijifunza wapi hatuwezi kukwepa ukweli kuwa Abramu(maana alikuwa bado hajatahiriwa wala hajapokea yale maagano yaliyopelekea kubadilishwa jina kuwa Ibrahimu swala la Mwanzo 12 Abram's call limezingatiwa) Lakini huyu Abram alilelewa ktk familia ya kipagani yenye kuabudu miungu kwa mzee Terah na ilikuwa kule Mesapotamia(Ancient Babylon) huko ndipo tulipoona hizo desturi za kutoa zaka zilikotokea nitaeleza haya sehemu ya 12 ya somo.
Katika Encyclopedia of Religion imeeleza kile alichofanya Abramu kinaitwa "Arab Custom of War" ndio maana alitoa sehemu ya kumi na vilivyobaki vyote hakuchukua hata uzi wala sindano wala gidamu vyote akampa mfalme wa Sodoma(Inaitwa Law of the Land) (NA HAKUNA NUKUU YOYOTE KUWA ALIWAHI KUFANYA HIVYO AU KUTOA TENA KWA OCCASION YOYOTE(one time recorded event)
_b.YAKOBO_
Kwa habari ya Yakobo ni ishu tofauti maswali yale ya kwanza yanaweza kujibika sema huyu alifanya _"VOWED TITHING"_ alijinadhirisha mwenyewe kuwa Mungu nikienda huko nikafanikiwa nitakutolea sehemu ya kumi.
*V.)ZAKA YA KILAWI(LEVITICAL TITHE)*
Sasa tumeingia kwenye moyo wa somo. Katika Hesabu 18 ndipo tunapoona swala la zaka kwa upana likielezwa. Sasa zaka hii ya kilawi na taratibu zake zitatula kuona kuwa haziwezi kuwa applied ktk UKRISTO AU KANISA kabisaa. Tutayaona hayo ktk sehemu ya saba ya somo. Zaka ya kilawi ilitokana na ukweli kwamba WALAWI HAWAKUPASWA KUMILIKI MALI(Should not own properties) na pia hawakupaswa kuwa na urithi kama makabila mengine. Na hivyo tuelewe kuwa ZAKA haikupelekwa kwa Makuhani toka waisrael bali zilikuwa zikipelekwa kwwnye miji ya walawi (Levitical cities) Hes 18:21 Kwa hiyo Wana wa Israel walipeleka Zaka kwenye miji ya walawi (10%) na wao Walawi walichukua 10%ya kile kilicho bora ktk Zaka ndicho walipeleka kwa makuhani kwa maana zaidi ya 80% hawakuwa makuhani ingawa kabila lao ndilo lililotengwa kwa utumishi huo. Kwa maneno mengine ni 1% ya maongeo ya watu ndiyo yaliyofika kwa kuhani. Ikumbukwe zaka ilikuwa ni kwa vile ambavyo vimezalishwa(produces) ndani ya ardhi takatifu ya Waisrael . Hakukuwa na zaka ya pesa ingawa pesa zimetajwa mara 44 toka Mwanzo mpaka mpaka wakati wa agizo la Musa lakini hakukuwahi kutolewa zaka ya pesa (Luka 11:42). Ile zaka ambayo walipewa kibali kuibadili iwe fedha nitatoa ufafanuzi na pia kuna mjadala mzuri unaojadili kwa nini yule Farisayo (Luk 18:12) alisema anatoa zaka ktk mapato yote. Jambo jingine la muhimu ni hili Zaka zilikuwa za aina 3. zinazofanya jumla ya Zaka ni 23% na sio 10%.Wanaofundisha kuhusu Zaka leo hii wanaangalia juujuu tuu bila kutanabaisha na kubainisha ktl zile aina tatu ipi wao hasa wanaifundisha kwa sababu zipi
Zaka aina ya kwanza ni ile ya 10% inayopelekwa ktk miji ya walawi (Lawi 27:30,Hesabu 18:21)
Zaka aina ya pili ndiyo ile ambayo walipaswa kuitunza kwa ajili Sikukuu ya Bwana kila mwaka wa tatu na walipeleka Yerusalem Kumbukumbu 26:12 12:6,14:22-27 Zaka hii nayo ni asilimia 10 ila wapokeaji walikuwa ni Walawi,Wageni,Wajane na Yatima
Na ipo ambayo ilipaswa kuhifadhiwa ndani kwa ajili ya maskini na makundi mengine ya marginalized hii ilikuwa Around 3% it makes a sum of around 23%{Deut 14:28-29} Wengi wanaofundisha zaka hawafafanui hizi zaka zinazoliwa na raia mpaka mtoaji
*VI) TAFSIRI YENYE MAKOSA KTK MALAKI 3:8-10*
Wahubiri wa Zaka ya fungu la kumi au wakristo wengi ukitaja tuu zaka wanapachika Malaki 3:8-10
Hiki ni kifungu kinachofanyishwa kazi isiyo yake
Zipo kanuni za kutafasiri maandiko (HERMENEUTIC PRINCIPLES) Zinatutaka tuulize vitu vya msingi nani aliandika na alimwandikia nani?Kulikuwa na nini hasa(Background&History) kulikuwa na muktadha upi(Context) Nabii huyu Malaki hakuwaandikia Israel wote ila uko ujumbe wa taifa lote pia..Aliwaandikia Makuhani (Mal 1:6ff,13-14) historia inaonesha hekaluni kulikuwa na chumba kikubwa(storeroom) kinatajwa ktk Nehemia 10:37,13:5) makuhani walikuwa wakiiba ktk vile vilivyopo kwenye storeroom na hata kuwasaidia wananchk wengine kuiba kwa kutoleta.Ikumbukwe raia walipeleka zaka kwa walawi nao walipeleka sehemu ya kumi bora ya ile sehemu ya kumi(1%) Makuhani pato lao kuu ualikuwa zaka bali ktk sadaka za hiari.Nao hawakutoa zaka tena kutoka ktk zile zaka bali walitoa kwa hiari kutoka ktk sadaka za hiari. Kwa hiyo nabii Malaki aliufunua uovu huo na akaagiza iletwe zaka kamili. Agizo la kuleta Zaka ktk kile chumba chenye ukubwa wa 10x20feet au 3x6metres halikuwa la Waisrael wote kwa kuwa zaka zao hazikupelekwa hekaluni na pia kwa kuwa zaka ilihusisha mazao ya ardhi na mifugo isingetosha kamwe kwenye ghala ya ukubwa huo kama Sitting room yetu .Hivyo ni muhimu kujifunza tafsiri sahihi ya maandiko ili mahubiri ya sahihi..
*VII)ZAKA KTK AGANO JIPYA*
Agano jipya halikatazi kutoa zaka ya fungu la kumi kama ambavyo pia haliagizi watu watoe(And the New Testament does not condemn Tithing). Kimsingi agano jipya limetaja zaka maeneo matatu kimsingi yaani
1.Mathayo 23:23/Luka 11:42
2.Luka 18:12
3.Ebrania 7:1-10,12
Maeneo mawili ya kwanza Yesu aliitaja akiwashutumu Mafarisayo kwa unafiki wao kisha e mfano wa Farisayo
Na baada ya hapo ipo ktk Ebrania 7 ikifanya mrejeo wa utoaji wa Sehemu ya kumi kwa Melkizedek na mstari wa 12&18 inaweka turning point na kwa msingi huo inaonesha kama ukuhani ukibadilika na sheria inabadilika..Haya tutayachambua ktk sehemu ya tisa ya somo. Kimsingi hakuna mtu anaweza akafundisha utoaji wa sehemu ya kumi kwa namna yoyote kwa kufuata Agano Jipya. Ninaposema Agano Jipya ni Post-Calvary Covenant... wengi wanatumia Mathayo 23:23b
*".....hayo imewapasa kuyafanya wala msiache yale mengine*
JE ANDIKO HI LITAWEZA KUHALALISHA FUNDISHO LA ZAKA. La hasha,Yesu ktk zama zake alikuwa ktk Jewish Religion&Tradition 100% Ingawa alileta tafsiri sahihi(Math 5:17) Sasa Post-Calvary Covenant sio Ndilo Agano Jipya... Wengi tukisema Agano Jipya wanawaza kitabu na zile nyaraka...Kumbe baada ya Yesu kuondoka Kanisa la kwanza lilikaa miaka karibu 30 hakukuwa na Injili wala nyaraka za mitume...Lakini Practically walikuwa ktk AGANO JIPYA ambalo Mungu alisema halitakuwa kama lile alilogana na mababa zao(Yer 31:31-40) sehemu ya tisa nitaeleza kwa kina haya yote.
*VIII.) LINI FUNDISHO HILI LA ZAKA LILIINGIZWA KTK UKRISTO?*
Wanahistoria wa kanisa wameeleza kwa kina kuhusu fundisho hili. Viongozi wa kwanza wa kwanza wa kanisa baada ya mitume(c95 hadi c200)AD hawakuwahi kukubali kuingiza fundisho hili maana waliliona kuwa 100% ni Jewish tradition. Hii haina maana kuwa hakuagiza Mungu.. Bali ktk yale maagizo yako ambayo hayawezi kuwa eternal moral principles maana yalikuwepo kwa muktadha fulani(Certainty of Context) So wazee wetu walijitahidi kujua kipi ni FUNDISHO LA UKRISTO kipi ni completely Jewish Tradition which not necessary to be incorporated in Christian Doctrine .Watu hawa Clement of Rome,Justin Martyr,Irenaeus na Tertullian hawakuruhusj fundisho hilo pamoja na kukubalina sana na swala la *UTOAJI* ila sio zaka ya kilawi.
Cyprian wa Cathage alijitahidi kwa bidii sana 250 A.D kuingiza swala la zaka bila mafanikio..Hata Karne ya nne ambapo UKRISTO ulipotambulika kisheria kama DINI bado hakukuwa na fundisho hilo. Mwaka 585 wakati wa baraza la Macon huko Ufaransa walijaribu tena bila mafanikio kuingiza zaka. ZAKA HAIKUWAHI KUWA FUNDISHO MPAKA MWAKA 777 AD Ambapo Emporer Charlemagne alipoipitisha kisheria kanisa kukusanya zaka (IKUMBUKWE WAKATI HUO KANISA LILIKUWA NI TAASISI YA SERIKALI) kwa sababu hiyo Catholic Church ikawa ina fundisho hilo mpaka wakati wa kuinuka kwa Uprotestanti Karne ya 15 ambapo wengi wa wale fathers of protestantism hawakukubaliana nalo pia,ingawa hawakuweza kuchuja mafndisho yote..mengi yaliendelea ktk uprotestant.Hata wahubiri wa kipentekoste ambao nawaita ni 4th Generation wakiwa ni zao toka kwenye uprotestanti lakini Karne ya 20 hawakuweza kuchuja sana kwa habari ya mafundisho ila kuwa na mkazo maeneo mihimu kama ujazo wa Roho Mtakatifu,karama za rohoni etc etc Hivyo hakuna muhibiri hata wa kipentekoste ambaye anaweza kutueleza nini msingi wake kufundisha hilo ktk Agano Jipya. Jibu walilo nalo nitalijadili sehemu ya 11
*IX.)NINI MSINGI WA UTOAJI KTK AGANO JIPYA(POST-CALVARY COVENANT)*
Msingi mkuu wa mambo mengi ktk Agano Jipya ni Imani na Upendo wa kumpenda Mungu ndio ulete msukumo wa matendo ya haki. Hakupaswi kuwa na shuruti ili ufanye kitu au vitisho kama baadhi ya wahubiri wanavyo tumia Malaki 3:8-10 kuwatishia *LAANA* watu waliokombolewa toka kwenye laana(Gal 3:13)
UTOAJI KTK AGANO JIPYA NI HIARI(inayotokana na kuenda Mungu na kufahamu kuwa unapaswa kutoa)
2Kor 9:7
7 Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.
SWALA LA KIASI GANI mtu anapaswa kuamua moyoni mwake kwa ukunjufu sio kutaja sadaka na viwango ambavyo wengine unakuwa umewalalia hasa.Na hata ile 10% sio kipimo cha kumpenda Mungu na tena hakuna usawa
2Kor 8
11 Lakini sasa timizeni kule kutenda nako, ili kama vile mlivyokuwa tayari kutaka, vivyo hivyo mkawe tayari na kutimiza, kwa kadiri ya mlivyo navyo.
12 Maana, kama nia ipo, hukubaliwa kwa kadiri ya alivyo navyo mtu, si kwa kadiri ya asivyo navyo.
13 Maana sisemi hayo, ili wengine wapate raha nanyi mpate dhiki;
14 bali mambo yawe sawasawa; wakati huu wa sasa wingi wenu uwafae upungufu wao, ili na wingi wao uwafae ninyi mtakapopungukiwa; ili mambo yawe sawasawa.
MISTARI HII INAJADILI EQUALITY
Mtu mwingine anafanya biashara ha kuingiza magari ya kifahari anapata milion 400 sasa wengi kwa fundisho la zaka..akitoa milion 40 ananihesabu kuwa na haki huku kabakiwa na milion 360 na kuna uhitaji zaidi ktk ufalme..na hivyo anaendelea kutoa sadaka shiling elfu1 akiamini ametimiza ile sheria ya zaka.Huu haupaswi kuwa msingi wa utoaji. Wengine imebidi wabuni sadaka mbali mbali kumbe ni matokeo ya kutotambua nini msingi hasa wa utoaji ktk Agano jipya.Wiki hii nimeongea na mshirika mmoja wa kanisa la Assemblies of God. Amesema kwao imeongezwa sadaka inaitwa *SADAKA YA MWANAKONDOO* ambapo mtu anapaswa kuahidi kiwango kikubwa at abnormal rate🤔💵💰 Sasa haya ni matunda tu ya kuoelewa msingi. Sadaka inapaswa kuwa hiari,ya binafsi na kwa nia ya kutaka kutoa kwa imani na kumpenda Mungu
Kutoka 35:5,21,2Nyak 29:31,Ezra 2:68,7:5,Zab 54:6
SACRIFICAL "FREEWILL" GIVING NDIO HASWAA MSINGI WA UTOAJI
*X.)SHUHUDA ZA WALIOBARIKIWA*
Shuhuda za waliobarikiwa walipotoa Zaka ya Fungu la kumi...halitoi mwanya wa kutengeneza fundisho. Maana GIVING AND RECEIVING ITSELF IS A PRINCIPLE (Mdo 20:35,Filip 4:15)
15 Nanyi pia, ninyi wenyewe mnajua, enyi Wafilipi, ya kuwa katika mwanzo wa Injili, nilipotoka Makedonia, hakuna kanisa lingine lililoshirikiana nami katika habari hii ya kutoa na kupokea, ila ninyi peke yenu.
NITAYELEZA HAYO KWA KINA KTK HITIMISHO
*XI.) GROUNDS ON WHICH I JUSTIFY TITHE*
Jambo la kwanza nieleze kuwa mimi natoa mafungu ya kumi ktk mapato yangu. Natoa kwa utaratibu wa kanisa letu tuliorithishwa ila sio kama fundisho au agizo kwa wakristo maana moyo wa kupenda Mungu sihesabu kile kuwa ni kitu kama ninavyojitoa nafsi yangu yote kwa Bwana na pia utoaji wa zaka ktk dhehebu ninaloabudu hautunyimi sisi wanafunzi wa Biblia kujifunza.
A.)Jambo la kwanza kuhusu kujaribu kueleza kwa namna gani naweza kui-justify tithe ni hii. Ingawa asili yake inatoka kwa mataifa ya kipagani hata kabla ya Abramu wala Sheria ya Musa..bado yale mataifa ya kipagani yaliyoishi baada ya Gharika ni muendelezo wa Uzao wa Nuhu.Sasa inasemekana watoto wa Nuhu walikuwa na maelekezo hayo toka Baba yao kuhus tabia ya kumtolea Mungu na pia sources nyingine zinaonesha Ile miungu iliyodai kupewa TITHE iliiga tabia/kanuni ya Mungu.Imumbukwe ibada za sanamu enzi za Nimrodi ni kitu ambacho wanadamu walifundishwa na wale malaika wasioilinda enzi na kuyaacha makao yanayowahusu(Yuda 1:6,2Petro 2:4) Sasa kama umesoma kwenye kitabu cha Henoko...ingawa wahubiri wengi wanapinga bila kufahamu, ila ni source of knowledge na waandishi wa Biblia walikisoma na kuuamini unabii wake(Yuda 1:14) Utagundua kuna mambo ambayo wale malaika 200 waliwafundisha wanadamu kimakosa.Ila vingine ni principles halisi za Mungu
B.) Namna ya pili ni hii kwa kuwa msingi tayari uliharibika(Zabur 11:3) at least basi njia hiyo inasaidia wakristo kujiepusha na choyo(Luk 12:15) maana wengi wakiachwa huru wanachagua vibaya *KUTOTOA KABISA* ingawa kutoa kwa sababu umeletewa mwinjilisti maalum wa muhimiza *UTOAJI* Akaweka na vitisho vingi vya kulaaniwa.Huo ni msingi usio sahihi
*XII.)HITIMISHO*
Somo hili kamwe halilengi kupinga UTOAJI bali kufundisha msingi sahihi
*KUTOA/GIVING IS A MUST*
WATU WANAPASWA KUFUNDISHWA KUWA LAZIMA WATOE
WHY?
1.NI AGIZO(Luka 6:38)
2.ILI KAZI YA MUNGU ISONGE MBELE (1Kor 16:1-3)
3.ILI KUJIWEKEA HAZINA MBINGUNI(Math 6:19-21)
4.ILI KUPATA BARAKA ZA MWILINI HAPA DUNIANI(Filip 4:12-19)
ASANTE KWA KUFUATILIA NAAMINI UMEJIFUNZA MENGI
Mwl Proo
0762879363
alltruth5ministries@gmail.com
Amin, zidi kubarikiwa sana mtumwa wa Bwana Yesu.
ReplyDelete