TAFSIRI RAHISI YA
UFUNUO 12
A.)ISHARA YA MBINGUNI (mstari 1-6)
Tunamuona mwanamke aliyevikwa jua,mwezi na nyota chini ya miguu yake.Tafsiri rahisi ya ishara hii ni kama ifuatavyo
●Mwanamke ni taifa la Israel (Mwanz 37:9-11)
●Jua ni Yakobo (Mwanzo Mwanz 37:9-10)
●Mwezi ni Raheli ambaye anawakilisha wanawake wa Kiyahudi
●Mtoto anawakilisha Wayahudi 144,000 . Ijapokuwa wapo wanaoamini kuwa mtoto anamwakilisha Yesu Kristo
Mwanamke ni taifa la Israel na si Mariamu mama yake Yesu kama wengine wanavyoamini kwa sababu ni lazima mwanamke huyu awe ameteseka wakati wa dhiki kuu,kitu ambacho ambacho Mariam hajapitia. Pia mtoto huenda akawa ni wayahudi 144,000 ambao watanyakuliwa ktk kipindi cha dhiki kuu,na si Yesu kama wengi wanavyoamini maana Yesu hatanyakuliwa wakati wa dhiki kuu. Ila Yesu atatazamiwa aje awaokoe wanaoteseka wakati wa dhiki kuu. Upande wa pili wa hoja hii unapaswa iangaliwe vizuri,kwani mtoto atachunga mataifa kwa fimbo ya chuma (Sifa ambayo ni ya Yesu) .
Hata hivyo tunaweza tukajumlisha kwa kusema ni 144,000, kwani tunamuona Yesu akiwapa walioshinda kutawala kwa fimbo ya chuma (Ufunuo 2:26-27). Pia joka anayetaka kummeza mama pamoja na mtoto,mama anafichwa na mtoto ananyakuliwa mbinguni. Hii inaonesha kuwa wale Wayahudi watalindwa na Mungu,wakati wale 1440,000 wakinyakuliwa mbinguni . Joka anayetamkwa hapa ni Shetani ambaye atampa uwezo wote Mpinga Kristo ambaye habari zake zipo sura ya 13
B.) VITA MBINGUNI (mstari wa 7-18)
Mstari wa 7 tunaona vinatokea vita mbinguni kati ya Joka(Shetani) na malaika wake na Mikael,malaika mkuu pamoja na malaika zake. Lakini hapa tunaona Mikael akimshinda Shetani na kumtupa chini.
Mstari wa 8 kunaonekana kushindwa kwa Shetani kama ambavyo alishindwa kwanza pale msalabani,wakati wa dhiki kuu atajaribu tena kufanya vita na majeshi ya Mungu na atashindwa.
Mstari wa (9-11) tunaona baada ya Shetani kushindwa watakatifu nao wanashindana kwa Neno la Mungu na damu ya Mwanakondoo (Warumi 8:36-37)
Katika mstari wa 12 tunaona shangwe ikifanyika mbinguni ikiambatana na ole maana ya Shetani anajua amebakiwa na muda mchache ambao si zaidi ya miaka mitatu na nusu.
Ndio maana andiko hili ni unabii utakaotimia na si unabii uliopita. Unabii uliopita Shetani alikuwa na muda mrefu (kama inavyoaminika alipotupwa mara ya kwanza) kabla ya kunjaribu Adamu
Mstari wa 13 tunamuona Shetani akiwakamia Wayahudi kuwaangamiza japo mpango wake huu hautafanikiwa, kwa maana Bwana Yesu atakuja kuwaokoka.
Mstari wa 14 tunaona Wayahudi wakiwa ktk dhiki Yerusalem na malaika wakiwa tayari kuwalinda . Huenda watakimbilia nchi ya Moab, Edom na Amon (Dan 11:41)
Mstari wa 16 maji kama gharika yanawakikisha mateso yakijiandaa kwa ajili ya kufanya vita na Wayahudi . Neno hili limetumika pia ktk kitabu cha Daniel 9:26 akielezea uvamizi wa Warumi kwa Israel uliotimia mwaka 70 AD,mateso yalikuwa kama gharika.
Mstari wa 16,inaelezea juu ya maangamizi yatakayotokana na tetemeko la nchi Mungu atawaokoa wwnye haki kutoka kwa wanadamu waovu kupitia tetemeko hili.
Mstari wa 17,watu watakaoshambuliwa moja kwa moja na Shetani ni pamoja na Wayahudi, watu watakaompinga Mpinga Kristo.
Mstari wa 18,Yohana anasema anasimama juu ya mchanga wa bahari,mchanga wa bahari unawakilisha utawala wa Mpinga Kristo. Utawala wa Mpinga Kristo utatumiwa na Shetani kufanikisha mambo yake ambayo ni kinyume na mapenzi ya Mungu
Asante kwa kufuatilia
Credits to
Rev Aulerian Ngonyani
Mwl Proo
0762879363
No comments:
Post a Comment