Tuesday, December 12, 2017

TALAKA KATIKA UKRISTO

*NDOA SERIES BY MWL PROO 0762879363*

*1.)TANGU MWANZO HAIKUWA HIVI*

*2.) JE YESU ALITOA SABABU YOYOTE YA KUACHANA/DIVORCE?.*

*3.)KATIKA UKRISTO KUNA KUTALIKIANA/KUACHANA KIBIBLIA?.*

Bwana Yesu asifiwe,Leo tujifunze kweli hii ili tuache kutembea ktk yale ambayo sio yetu.

MAFARISAYO WALIMUULIZA YESU JAMBO AMBALO LILIKUWA NA JIBU JEPESI LA *NDIO* KTK MAFUNDISHO YA KIYAHUDI,LAKINI YEYE ALIKUJA NA TAFSIRI SAHIHI ~*ekprilo*~BEYOND MAFUNDISHO YAO.

Mathayo 19 : 3

*_Basi Mafarisayo wakamwendea, wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu?_*

MAJIBU YA YESU KTK MSTARI WA 4-6 YALIASHIRIA MTU HAPASWI KUMWACHA MKEWE,AKIMWACHA ABAKI HIVYOHIVYO MAANA MUNGU ALIUMBA MTU MKE NA MME(MMOJA TUU) .WAKAMHOJI KWA JINSI GANI MUSA ALIRUHUSU NDIPO AKAWAJIBU

Mathayo 19 : 8

*_Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi._*

KISHA AKAWAMBIA WALE WATU HIVI

πŸ‘‡πŸ½πŸ‘‡πŸ½πŸ‘‡πŸ½πŸ‘‡πŸ½πŸ‘‡πŸ½

Mathayo 19 : 9

*_Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini._*

πŸ‘†πŸΌπŸ‘†πŸΌπŸ‘†πŸΌWAKRISTO WAJANJA WAMETAFUTA KUJIFICHA HAPO ILI WABADILISHE WAKE KILA WENZA WAO WAANGUKAPO.

SASA TWENDENI SHULE YA ROHO MTAKATIFU NA YA DUNIANI.

>Dini ya kiyahudi(Judaism) hususani Wayahudi wa Kiashkenazi(Wayiddish)  inaamini kwa habari ya swala wenza kimili wa nafsi(perfect soulmate) inayoitwa *_Bashert_*  Taurat imetoa vidokezo vichache sana kuhusu muongozo wa hatua za ndoa. Ila mambo yote  na hatua zote za kutafuta mwenza,kufanya sherehe ya harusi na namna ya kuhusiana ktk ndoa yameelezwa kwa kina ktk *_TALMUD_* (Ambayo ni fasihi simulizi ya mapokeo ya namna ya kuifasili Taurat/Torah. Dhumuni la msingi la ndoa ni ~PENZI~, ~USHIRIKA~ na ~KUZAA~, ,Na kuna kunakuwa na mkataba uitwao *_KETUBAH_* Huu ni mkataba wa ndoa unaoeleza vigezo na masharti ya ndoa na maswala ya kutalikiana,na wajibu wa mume kwa mke. Rabi Yehuda  alifundisha kwa habari ya Bashert kwamba  siku 40 kabla mtoto wa kiume kuzaliwa,Sauti hutoka mbinguni kutangaza huyo mtoto atamuoa binti wa nani,kirahisi inasemwa muunganiko huo hufanywa mbinguni. Lakini mtu akimpata Bashert wake(Perfect match)  haina maana ndio atakuwa na ndoa tambarare isiyo na mabonde ndio maana Talmudi ikaruhusu  TALAKA tena kijamii hunenwa mtu anaweza kupata mwenza mwingine akafurahia ndoa kuliko alipokuwa na yule Bashert wake,

*NAMNA YA KUPATA MWENZA*

Katika mkusanyiko wa awali wa mapokeo ya fasihi simulizi za kiyahudi uitwao *_MISHNAH_* umeeleza hatua mbili za muhimu,ingawa mwandishi wa Mishnah aitwaye Rambam alijadili uhusiano unaokuwepo kabla lakini sisi tuangalia hatua mbili za uhusiano yaani *KIDDUSHIN* hatua ya kwanza na ndoa kamili yaani *NISUIN*

1.KIDDUSHIN
Hatua ya kwanza ya kutafuta mwanamke na kumpropose kama mke mtarajiwa,ambapo njia tatu hutumika

i.)Pesa
ii.)Mkataba(Ketubah)
iii.)tendo la ngono
Haya matatu kila moja lilijtosheleza,ila liko moja wapo la lazima ili kuweza kukiathiri chanya kile kifungo cha ndoa.

➡Kutoa pesa kuliko ambatana na wedding ring,hakukumaanisha kamwe kumnunua mke au kama mtumwa anavyonunuliwa,na ndio maana Talmud ikaweka wazi kuwa lazima aolewe kwa matakwa yake (bride's consent) na si vinginevyo

Mwanzo 24 : 58

*_Wakamwita Rebeka wakamwuliza, Je! Utakwenda na mtu huyu? Akasema, Nitakwenda._*

Hatua hii ya Kiddishun ni ile itwayo *Betrothal* hatuwezi kusema ni uchumba ni steji ya uposo iliyoendelea sana ni nusu ndoa maana inakuwa imeruhusu mambo muhimu ya ndoa,ila bado hawakai pamoja,na iliweza kuchukua hata mwaka mzima ktk hatua mume anaandaa makao ya familia mpya kabla hajamleta mkewe..Hii ndiyo hatua ambayo Yusufu baba kivuli wa Yesu alikuwa nayo kwa Mariamu,Neno hilo Kiddushin limetokana na maneno *_Qof-Dalet-Shin-* yaani kutengwa au kutakasika kwa mahusiano ya kindoa(Na kumfanya mwanamke awe wa mwanamme mmoja tu) Level ambayo ni zaidi ya uchumba tunaoujua sasa uliweza kuvunjwa kwa *Kifo au Talaka*

Na hatua ya Mwisho ni *NISUIN* humu ndani ndiko kuna taratibu zote za wedding ceremony ambazo baada ya hizo hawa soulmates huanza kuishi pamoja.Lakini hizo sitaeleza maana sio mlengwa wa somo.

KATIKA TALMUD ILIWEKA WAZI KUWA MUME ANAWEZA KUMWACHA MKE KWA SABABU YOYOTE,AWE AMEUNGUZA CHAKULA JIKONI,AU MUME AKIMWONA MWANAMKE MREMBO ZAIDI YA MKE WAKE ILA AMWANDIKIE TALAKA,LAKINI *```UTAMADUNI WA KIYAHUDI ULISEMA IKIWA NI KWA HABARI YA MTU KAMKUTA MKE AMEZINI BASI HAPO HATA KAMA UNA ITAYARI WA KUMSAMEHE SHARTI UMWACHE!!!```*

Kumbukumbu la Torati 24 : 1

*_Mtu akiisha kutwaa mke kwa kumwoa, asipopata kibali machoni mwake, kwa kuwa ameona neno ovu kwake, na amwandikie hati ya kumwacha, akamtilie mkononi mwake, na kumtoa katika nyumba yake._*

KWA HIYO SWALI LA MAFARISAYO,WALIMUULIZA YESU WAKIWA WANAJUA JIBU LAKE NI NDIYO MTU ANARUHUSIWA KUMWACHA MKE KWA SABABU YOYOTE,NA YESU AMBAYE ALIZALIWA CHINI YA SHERIA AKAANZA TARATIBU KUWANYOOSHA,ILA ALIPOWAAMBIA KUWA *_isipokuwa kwa habari ya uasherati_* hakuwa anatoa fundisho kwa ajili ya ukristo,alinukuu fundisho la Talmud lililowataka Wayahudi wenye mioyo migumu kusamehe wawaache wake zao hata kama wako tayari kusamehe..Yusufu alipotaka kumwacha Mariam alifanya kwa siri ili kuepusha majanga,maana ilikuwa Mariamu either apigwe kwa mawe kwa dhambi ya kushiriki ngono na mtu mwingine akiwa kwa level ya uposo.

SASA NATAKA KUWEKA SAWA.....

*CHISTIANIATY IS NOT THE JEWISH RELIGION(JUDAISM) THOUGH IT BEGAN AS A SECT IN JEWISH RELIGION...* YAANI UKRISTO SIO DINI YA KIYAHUDI HATA NA SISI TUFUATE TALMUD MAFUNDISHO YA MAPOKEO YAO,INGAWA ULIANZA KAMA DHEHEBU NDANI YA YA DINI YA KIYAHUDI

AND THE NEW TESTAMENT IS NOT THE RESTATEMENT OF THE OLD ONE,IT IS COMPLETELY THE NEW ONE,AKASEMA HALITAKUWA KAMA AGANO NILILOAGANA NA BABA ZAO ......Yeremia 31:31-42

UKRISTO UNAZO STANDARD ZAKE TOFAUTI. KWA MFANO WEWE MWANAUME UKITOKA SAFARI,KUINGIA GHAFLA  BEDROOM,UKAMKUTA MKEO YUPO NA MTU WANA-DUUπŸ™Š USIKURUPUKE KUSEMA YESU ALISEMA ISIPOKUWA KWA HABARI YA UASHERATI NARUHUSIWA KUKUTALIKI TENA KWA TAARIFA YAKO WANANDOA HAUITWI UASHERATI BALI UZINZI,KWA HIYO UKITAKA KUTAFSIRI KWA USAHIHI KAMA NI KUVUNJA UNARUHUSIWA KUVUNJA UCHUMBA. LAKINI KWA VIWANGO VYA UKRISTO,BADO UNAYO NAFASI YA KUMSAMEHE MKEO AU MMEO BAADA YA FUMANIZI,AKIOMBA UMSAMEHE MSAMEHE,AU AKIWA NA URADHI WA KUTAKA KUAAMEHEWA,USIMKOMALIE KWAMBA HAPA BEBA KILICHO CHAKO UENDE...KUMBE KUNA MWANAMKE ULIKUWA UNAMTAMANI SASA UNAONA MWANYA,HAPO HAUTENDI UKRISTO UMEAMUA KUWA MYAHUDI KWA JINSI YA MWILI. UKRISTO UNA STANDARDS ZAKE

KUNA MITUME WAMEZUKA WANAACHANISHA NDOA ZA WATU KWA SABABU YOYOTE,HUO SIO UKRISTO.

WATU HATA KAMA WALIOANA WAKIWA WABUDHA,WAKAOKOKA WOTE BADO NDOA YAO NI HALALI .

1Kor 7

10 Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe;

KAMA AKIOKOKA MWANANDOA MMOJA,MWINGINE AKABAKI KUWA MPAGANI,HIYO NDOA NI HALALI ISIVUNJWE,TENA WEWE ULIYEOKOKA UMENYANG'ANYWA RUNGU ILI ISIJE UKATUMIA WOKOVU KUMWACHA AU KUTAKA KUACHIKA. ALIYEPEWA HUO UHURU NI YULE ASIYEAMINI,AKIONA AAAH MIMI MAMBO YAKO YA ULOKOLELOKOLE SITAKI AKAONDOKA NA KUKUACHA HAPP WEWE MWANAMKE AU MWANAUME UNAWEZA KUOA/KUOLEWA. ILA YULE MKE AU MUME MPAGANI AKISEMA INGAWA UMEOKOKA,MIMI SIOKOKI ILA NAKUPENDA MKE/MUME WANGU HUPASWI KUCHAKACHUA BIBLIA INASEMA KAA NAYE WALA USIMWACHE HIYO NI STANDARD YA UKRISTO,MSITUCHANGANYIE MISHNAH MAHALI PENYE KWELI YA YOTE YA MUNGU.  UKIONA KUKAA NA MPAGANI HUTAKI WAKATI ANAKUPENDA,BASI UKI-DIVORCE KAA HIVYO ULIVYO PURE SINGOLO(SINGLE) MPAKA KUFA

*_10 Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe;_*
*_11 lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe._*

*_12 Lakini watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana, ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache._*
*_13 Na mwanamke, ambaye ana mume asiyeamini, na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache mumewe._*
*_14 Kwa maana yule mume asiyeamini hutakaswa katika mkewe; na yule mke asiyeamini hutakaswa katika mumewe; kama isingekuwa hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi; bali sasa ni watakatifu._*
*_15 Lakini yule asiyeamini akiondoka, na aondoke. Hapo huyo ndugu mume au ndugu mke hafungiki. Lakini Mungu ametuita katika amani._*
*_16 Kwa maana wajuaje, wewe mwanamke, kama utamwokoa mumeo? Au wajuaje, wewe mwanamume, kama utamwokoa mkeo?Maisha ambayo Bwana Ameagiza_*

KWA HIYO KTK UKRISTO UKIWA NA SABABU YA KUMWACHA MKEO NI MAHALI PA KUPRACTICE UKRISTO WAKO KWA KUSAMEHE,HATA KAMA KUNA JAMBO GANI,LILE LA UASHERATI TULIFUTE TULIBUGI STEPU,MWINGINE ANASEMA,SASA KAMA MKEO AMEKUWEKEA SUMU KWENYE  CHAKULA NA UKAMSHTUKIA JE UTAENDELEA KUISHI NAYE,AU MWANAMKE KAPATA MAGONJWA KAMA HIV/AIDS HUKO NJE JE UNAENDELEA NAYE AU UNA M-DIVORCE✍🏽?? NA NDIYO MAANA UNAPASWA KUKUA KIROHO UJUE NAMNA YA KUFANYA CONSULTATION TO THE HIGHER AUTHORITY LAKINI CHRISTIAN CODE OF CONDUCT INATUAMBIA *FORGIVE!!!!* MIZIGO MINGINE YUPO WA KUMTWIKA,YUPO ATUCHUKULIAYE,NA KAMA UKIMHUSISHA  TANGU MWANZO HUTAFIKA HUKO. MAANA FASIHI ZA KIYAHUDI ZINASEMA MUNGU BAADA YA KUMALIZA KUUMBA KAZI YAKE KUBWA KWA SASA NI *_ARRANGING MARRIAGES_* MPE NAFASI ATAKACHOKUPA YEYE HUTAJUTIA(RUMI 11:29)

NB:
*MTU ALIYEAMINI, ANAOLEWA AU KUOA MTU ALIYEAMINI TUU. HAKUNA KUOKOKESHANA ILI KUOANA, HUWEZI KUMSHAWISHI MTU AOKOKE ILI MFUNGE NDOA (HUO NI USANII JUU YA MSALABA WA KRISTO).*

MUNGU AWABARIKI

Mwl Proo
0762879363
0718922662

Credits to Christopher Kalolo

alltruth5ministries@gmail.com

1 comment:

  1. Mwalimu umeeleza vizuri sana.... Yani kwa ulivyodadavua inatosha kabisa kusema unaweza kumuacha isipokuwa wewe unakuwa na uhuru wa kuchagua kuendelea naye au kumuacha...

    Kama ukisema hivyo aliokuwa anasema uasherati alikuwa akizungumzia kitu gani??? Na ni kwann ahusishe wasiooana kwenye swali la waliooana???

    ReplyDelete