Sunday, December 17, 2017

WALA HAKISHIKI KICHWA!

🇦 🇱 🇱     🇹 🇷 🇺 🇹 🇭

*WALA HAKISHIKI KICHWA*

*_Na Mwl Proo_*
0762879363

©2015

Shalom Aleichem!🙋🏽
Wapendwa ktk Bwana(Yesu Kristo) naomba niwashirikishe Neno la Uzima.

*Wakolosai 2 : 19 -*

*_wala hakishiki KICHWA, ambacho kwa yeye mwili wote ukiruzukiwa na kuungamanishwa kwa viungo na mishipa, hukua kwa maongeo yatokayo kwa Mungu._*

Yesu Kristo anatajwa pahala pengi ktk maandiko kama/kuwa ni  *KICHWA*

Angalia haya maandiko

*Waefeso 1 : 22 -*

*_akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe KICHWA juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo.._*

*Wakolosai 2 : 10*

*_Na ninyi mmetimilika katika yeye aliye KICHWA cha enzi yote na mamlaka._*

*Waefeso 4 : 15*

*_Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye KICHWA, Kristo._*

*Wakolosai 1 : 18*

*_Naye ndiye KICHWA cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote._*

*Waefeso 5 : 23*

*_Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni KICHWA cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili._*

NGOJA NIANDIKE KWA HERUFI KUBWA(Galatia 6:11)

MAANDIKO YAMETUTAJA SISI KUWA NI VIUNGO,SASA KWA SAYANSI YA KIMBINGU SHARTI KILA KIUNGO KIKISHIKE KICHWA,KIWE KIMEUNGAMANISHWA NA KICHWA ILI KIENDELEE KURUZUKIWA, KUUNGAMANISHWA NA VIUNGO ILI KIENDELEE KUKUA KWA MAONGEO YATOKAYO KWA MUNGU.

*Waefeso 2 : 21*

*_Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana._*

*Waefeso 4 : 16*

*_Katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadiri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo._*

*TURUDI KTK SAYANSI YA VIUMBE  YA DUNIANI*

Wale ambao mnakumbuka Biology kwa sehemu kuhusu *"BODY COORDINATION"* mtakumbuka vizuri swala Central Nervous System. Viungo vyote vinaweza kufanya vinavyofanya kama tu vimeungamanishwa na *KICHWA* . Ikitokea umemchoma mtu kwa sindano💉au kitu chochote chenye ncha kali,iwe umemchoma mguuni au mkononi au mtu akigusishwa moto ✋🏼🔥,Atashtuka na kutoa mkono au mguu kwa haraka sana. Sasa ukweli ni kwamba mkono hautaweza kutambua maumivu ya sindano wala muunguzo wa moto kama hakutakuwa na kushikama na *_KICHWA_* ,kisayansi ukimchoma mtu na kitu kama sindano,uko ujumbe/taarifa(Nerve impulse/message) inayotumwa very fast kwenda kwenye *KICHWA*(ubongo) ambapo huku KUTATAFSIRI HILO TUKIO NA HAYO MAUMIVU THE UJUMBE UNARUDISHWA KUWA UMECHOMWA NA SINDANO. NDIPO MTU ANAHISI CHA KUHISI NA ANAWEZA AKAUVUTA MKONO KWA HARAKA SANA. INGAWA UNAONA KINACHOTANGULIA KUONDOLEWA NI MKONO LAKINI TAARIFA YA KUCHOMWA💉NA AGIZO LA KUUONDOA MKONO LILITOKA KWENYE *KICHWA*

BAADHI YA TECHNIQUES ZA KITABIBU KTK UPASUAJI,NAMNA YA KUMFANYA HUYU   ANAYEFANYIWA UPASUAJI ASISIKIE MAUMIVU NI KU-DISTURB ILE NERVOUS SYSTEM ILI KICHWA(UBONGO) KISITAFSIRI MATUKIO YANAYOENDELEA,IWE NI SINDANO ZA KUTIA GANZI AU DAWA ZA UZINGIZI OR ANY ALCOHOLIC RECIPE ITAKAYOFANYA MUDA WA TUKIO MTU ASIWEZE KU-SENSE,LA SIVYO THEATRE KUNGEKUWA NA VILIO VYENYE KELELE KUU *(KAMA KUNA MAPUNGUFU KTK MAELEZO YANGU BASI WALE WENYE TAALUMA ZAO WATAWEKA SAWA,MAANA MIMI NI MTAALUMA WA TAALUMA TOFAUTI KABISA NA SAYANSI)*
LAKINI TUJIFUNZE,WATU WASIPOSHIKAMANA NA KICHWA YESU KRISTO WANAPATA GANZI KTK MIOYO/ROHO,NAFSI NA MIILI YAO NDIPO WANAPOWEZA FANYA KILA UBAYA NA MACHUKIZO YA UOVU

*Efeso 4:19*

*_19 ambao wakiisha kufa ganzi wanajitia katika mambo ya ufisadi wapate kufanyiza kila namna ya uchafu kwa kutamani._*

MTAFUTE MTU ALIYEPOOZA MKONO AU MGUU(PARALYSIS)  AMBAYE AMEPOOZA HASA,MWAMBIE  INUA MKONO HUU ULIPOOZA,ANA KUTA MAAMUZI ANAYAFANYA KICHWANI KWAMBA AUINUE LAKINI MKONO HAUJAUNGAMANISHWA,MPAKA ANAWEZA AKATUMIE MKONO MWINGINE KUUSAIDIE HUU *_USIO KISHIKA KICHWA_* UWEZE KUINUKA

NDUGU MPENDWA NENO LA BWANA NI HILI

UNAPASWA UBAKI UMEUNGANA NA KRISTO *_"(FULL CONNECTED)"_* NA YEYE ALIYE KICHWA,UPOOZA WA KIROHO UNAOFANYA UNA MEZWA NA DUNIA,NA KUUONA WOKOVU NI MZITO,NI KIASHIRIA CHA WAZI KUWA *"HUKISHIKI KICHWA"* TAWI LIKIKATWA TOKA SHINANI, HALIWEZI KUJIHUDUMIA LENYEWE HATA LIKAZAA🍊🍒🍎🍓, UWEZO WA KUPANGA MCHAKATO NA BINTI HADI AKAJA GHETO MKA-DUU 🙊🙊 UNADHANI ULIKUWA MCHAKATO MWEPESI?? AMINI NAKUAMBIA NI KAZI NGUMU KULIKO KUMTUMBUA RAISI WA NCHI MWENYE KINGA ZA KISHERIA,ILA ULIWEZA KUSIMAMIA STEP BY STEP HILO DILI BILA KUSIKIA KALE KAONYO KA NDANI YA DHAMIRI NA KILE KIDOLE CHA ROHO 👉🏾😾KILICHOKUWA KINAKU PIN-POINT NAFSINI,NI KWAMBA ULIKUFA GANZI(EFESO 4:19)  AMBALO NI TOKEO LA KUACHA KUKISHIKA KICHWA. JE WEWE AMBAE HAPO MWANZO, WEWE KINYWA CHAKO KILIJAA MANENO YA NEEMA KILA SAA HALELUYA,AMEN,UBARIKIWE LEO HII MISEMO YOTE YA KIDUNIA NDIYO IMEKUJAZA MOYO(LUKA 6:45),WEWE AMBAYE ULIPOKUWA UKIONA PICHA ZINAZOONESHA MAPAJA YA WADADA KWENYE GOSSIP MAGAZINES🗞📰ULITAMANI KUFUMBA MACHO🙈 LEO HII SMART PHONE YAKO📱📲 UMEIJAZA PORN VIDEOS NA NUDE PHOTOS KIBAO👙,WEWE AMBAYE ULIPOPIGA GOTI KUOMBA🛐🚼 TU ULISIKIA ATMOSPHERE NA NAFSI YAKO IMEKUWA *_INUNDATED_* NA UMANDE WA ROHO MTAKATIFU,SASA UNAISHI KWA SALA ZA KUOMBEA CHAKULA,WEWE ULIYEKUWA MFUATILIAJI WA VIPINDI TBN NA SASA UNAHISI VIPINDI VYA KWENYE TV ZA KIKRISTO VINABOA FULANI HIVI,WEWE AMBAE ULIJIKINGA NA MAMBO MACHAFU LAKINI KWA SASA UNA-LIKE KILA UKURASA WA FB WENYE MAMBO MACHAFU,UME-SUBSCRIBE KWENYE WEBSITES KADHAA ZENYE MAMBO YASIYOFAA,ULIOWA-FOLLOW INSTAGRAM NI CELEBRITES WENYE KUPOST PICHA ZA UTUPU WAO NA UDAKU UDAKU,KALE KAUWEPO KALIKUWA KAKIKUSHUKIA MUDA UNAOMBA KALISHAGA POTEAGA 5YEARS AGO,ILA UMEPOTEZEA TUU,UMEAMUA KUISHI BILA HAKIKA YA KUWA NA MUNGU,WEWE AMBAYE DHAMBI NA UDHAIFU MWINGINE ULISHA USHINDAGA ZAMANI,UMEUFUFUA TENA YAANI UMEYAJENGA ULIYOYABOMOA (GALATIA 2:18),ETI ULIPOOKOKA MKAKA ULISHAACHAGA KUJICHUA(MASTURBATION) HALAFU SAIV UMEIZINDUA HIYO TABIA HUKU UNAFANYA *"RECONSIDETATION"* NI DHAMBI AU SIO DHAMBI,UNACONCLUDE MWENYEWE, *"ITAKUWA SIO DHAMBI"* 😂😂,NI KWELI ULIANGUKA KWENYE UZINZI,ILA HAUPO TAYARI KUTUBU MAANA UNA-ORGANIZE DILI JINGINE LA KUDUU TENA,SO UNAPANGA RATIBA KUWA UTATUBU BAADA YA HIYO *_one more shot_*AS IF MUNGU NI ADMIN WA GRUPU LA WHATSAPP,KWAMBA AKIKULEFTISHA ATAKUADD TENA🌍

SASA SWALI NI HILI

*_"JE! BADO UNAKISHIKA KICHWA???_*

JE UNAWEZA KUJIJARIBU NA KUJITHIBITISHA KAMA BADO UMEKISHIKA KICHWA???? *2Korintho 13:5*

HEY BRETHREN,IT IS NEITHER TOO LATE NOR IMPOSSIBLE TO RECONNECT YOURSELF WITH THE HEAD,THERE IS ACCEPTANCE FOR YOU AT THE TABLE OF THE LORD,HIS MERCY IS GREATER THAN YOUR SIN.

*BAMBELELA KUJESU UZOTHOLA UTHANDO*
*UYABIZWA SONDELA UZOSINDISWA*😰 nimeongea kizulu kuonesha msisitizo, come back bhana

Mwl Proo
0762879363(whatsapp number)

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment