Friday, December 8, 2017

BWANA HATAMTUPA MTU

*_B͙W͙A͙N͙A͙ H͙A͙T͙A͙M͙T͙U͙P͙A͙ M͙T͙U͙; L͙A͙K͙I͙N͙I͙ S͙H͙A͙R͙T͙I͙ M͙A͙D͙H͙A͙B͙A͙H͙U͙ I͙W͙E͙ J͙U͙U͙ Y͙A͙ M͙S͙I͙N͙G͙I͙ W͙A͙K͙E͙_*

*M͟w͟l͟ P͟r͟o͟o͟*
*0762879363*
*0718822662*

Bwana Yesu asifiwe sana! Kuna jambo moja naam mambo mawili yanayonishangaza nyakati hizi. Kuwa na mahubiri yasiyowiana na kweli, yako _*Unbalanced*_, ambapo hata waovu wanatumainishwa baraka za Mungu, utetezi wa kimungu, na mema yote yatokayo kwa Mungu, Baba wa mianga, bila kukemewa juu ya kukosea kwao na kuziacha njia za mbaya. Na jambo la pili ni baadhi ya watu kujaribu kumshtaki Mungu, kwa watumishi wake, kwamba anawaonea, anapotosha hukumu zao na kuwanyima wanayostahili. Kivipi hapo? Kuna watu utasikia yaani mtumishi, nimejitahidi kutoa sadaka na zaka mpaka senti ya mwisho, lakini mambo yanazidi kuwa mabaya, au mwingine utasikia najitahidi kufunga siku 4 kila wiki na kuomba masaa matatu kwa siku, lakini sioni mpenyo, mambo yangu yanazidi kudidimia tuu 😔. Kauli hizi ni majaribio feki, ya kumshtaki Mungu kwa watumishi wake, as if watumishi wake wanatenda haki kumzidi Mungu.

Ayubu wakati hali imekuwa tete, naye aliingiwa na ukengeufu wa fikra, hata kumshutumu Mungu kuwa amemwonea na kumpotoshea hukumu ya haki yake.

Ayubu 19 : 6
*_Jueni basi kuwa Mungu amenipotosha, Na kunizingira kwa wavu wake._*

Ayubu 16 : 9
*_Amenirarua katika ghadhabu zake, na kunionea; Amesaga-saga meno juu yangu; Mtesi wangu hunikazia macho makali._*

Lakini yule rafikiye aitwaye Bildadi Mshuhi, akamkosoa kwa hiyo hoja, tunasoma hapa

Ayubu 8 : 3
*_Je! Mungu hupotosha hukumu? Au, huyo Mwenyezi hupotosha yaliyo ya haki?_*

HAKUNA WAKATI MUNGU ANAWEZA KUKUONEA, KUKUPOTOSHA, KUIPOTOSHA HAKI YAKO, AU UKATENDA MAAGIZO YAKE, HALAFU AAMUE TU KUKU-IGNORE, SI KWELI KABISA. DAUDI ANASEMA ALIKUWA KIJANA, AKAWA MZEE, HAKUONA MWENYE HAKI AKIACHWA, KUMBUKA MUNGU HUYU ANAPENDEZWA NA HALI NZURI (WELL-BEING) YA WATU WAKE (Zaburi 37:25, 35:27). KWA HIYO MADAI YOTE, YA KWAMBA NAJITAHIDI KUTOA SANAAAA, LAKINI NAZIDI KUDIDIMIA, NAOMBA SANA LAKINI NAHISI MUNGU ANAZIDI KUNITENGA, HAYA YOTE IKO KASORO, MUNGU HAWEZI KUKUTUPA KAMWE BAADA YA WEWE KUTENDA HAYO YOTE, UKIMTAFUTA SHARTI AONEKANE KWAKO, UKITOA KWA UAMINIFU FORMULAR INADAI MILANGO YA BARAKA IFUNGUKE TUU, SHIDA ITAKUJA KAMA UTAFANYA HAYO, NA MADHABAHU YAKO HAIKO JUU YA MSINGI WAKE. NA NI JAMBO HILO PEKEE LINAKUFANYA USIWE MWENYE HAKI WA KUZIRITHI AHADI, KAMA SI MWENYE HAKI NI HALALI KWA MUNGU KUIPOTOSHA HAKI YAKO, YAANI UNAOMBA KIMYAAAAAA😷🤐, UNATOA MALI ZAKO, NI KAMA UNAZITUPA, MAANA IMEANDIKWA

Zaburi 146 : 9
*_Bwana huwahifadhi wageni; Huwategemeza yatima na mjane; Bali njia ya wasio haki huipotosha._*

*MOYO WA SOMO*

Maombolezo 3

*_31 Kwa kuwa Bwana hatamtupa mtuHata milele._*

*_32 Maana ajapomhuzunisha atamrehemu,Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake._*

*_33 Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu.Wala kuwahuzunisha._*

*_34 Kuwaseta chini kwa miguu, Wafungwa wote wa duniani,_*

*_35 Kuipotosha hukumu ya mtu, Mbele zake Aliye juu,_*

*_36 Na kumnyima mtu haki yake, Hayo Bwana hayaridhii kabisa._*

👆🏼👆🏼👆🏼MATESO YANAYOKUKUTA, KUSETWA CHINI UKAKANDAMIZWA KABISA, KUPOTOSHEWA HUKUMU YAKO, KUNYIMWA HAKI YAKO, KUOMBA MAOMBI YASIJIBIWE, KUTOA KWA AJILI YA UFALME NA UKABAKI KUFILISIKA, NA MENGINE YOTE, YOU NAME THEM! BIBLIA INASEMA MAMBO HAYO YOTE MUNGU HAYARIDHII, HAYUKO RADHI NAYO, HAWEZI KUYAKUBALI. HIVYO ACHA KABISA KUMSEMEA MUNGU KWA WATUMISHI WAKE KWAMBA NIMEOMBA SANA, NIMETOA SANA HAKUNA KITU, RUDI KWENYE MSINGI.

Ayubu 34 : 12
*_Naam, hakika, Mungu hatatenda mabaya, Wala Mwenyezi hatapotosha hukumu._*

MUNGU HAZIDIWI WALA HAPITIWI, BARABARA ZILE PANA ZENYE NJIA MBILIMBILI (Two-way Traffic), NAZO HUPATWA NA JAM, ZIKAWA HAZIPITIKI NA MAGARI HAYASOGEI. MUNGU KICHWA CHAKE HAKINA JAM, KUSEMA KAZIDIWA AU KAPITIWA AKAKUSAHAU. NI KWELI YAKO BAADHI YA MAMBO MUNGU ANAWEZA AKAKUTAKA KUSUBIRI (Ebrania 6:15), LAKINI SIO KUYAKAWILISHA KWA KUKUACHA UTESEKE, BWANA ALICHOKISEMA KWA KWAKO HAKITAKAWILISHWA (Ezekiel 12:21-28).
SWALA LA MSINGI NI HILI, MADHABAHU YAKO, IKO JUU YA MSINGI WAKE?. WENGI WANAIFAHAMU ILE MADHABAHU ILIYOJENGWA KWA MBAO, KIOO, SIMENTI NA MATOFALI LAKINI IKO MADHABAHU YA KIROHO YA MOYO WAKO, NA KWA HILI SOMO NAZUNGUMZIA MADHABAHU KAMA KIUNGANISHI CHAKO NA MUNGU KWA MAMBO YOTE, UNAPOKUWA NA FULL CONNECTION NA MUNGU, MAISHA YAKO HAYANA LAUMU (BLAMELESSNESS) MBELE ZA MUNGU, UNAO UWEZO WA KUSIMAMA MBELE ZA MUNGU KWA UJASIRI, HICHO NI KIASHIRIA CHA MADHABAHU IKO JUU YA MSINGI WAKE, LAKINI KAMA UNAJUA UNA KONA KONA (MEANDERS), YANAYOONDOA UJASIRI WA 100% KWA MUNGU BASI HAPO MADHABAHU  YAKO HAIKO JUU YA MSINGI WAKE, NA HILO NI JAMBO LA KUANZA NALO KABLA YA KUANZA KUMSHTAKI MUNGU KWA WATUMISHI WAKE.
Tusome hapa......

Ezra 3 : 3
_*Wakaiweka madhabahu juu ya msingi wake; maana hofu imewashika kwa sababu ya watu wa nchi; wakamtolea Bwana sadaka za kuteketezwa juu yake, sadaka za kuteketezwa za asubuhi na jioni.*_

Haya ni mambo ambayo chini wa usimamizi wa akina Ezra, yalifanywa mara baada ya kutoka uhamishoni Babeli. Kuwa nje na Yerusalem kulihusishwa na madhabahu pia kutokuwa juu ya msingi wake. Mambo yanayokuta wengi mpaka wanamshtaki Mungu, kumbe wapo uhamishoni, ukiwa uhamishoni ndipo unapoona unatenda juhudi lakini response ya Mungu ndooooogo 👌🏽. Kutoa, kuomba, kufanya huduma na mambo mengine ya kimungu, huku madhabahu haiko juu ya msingi wake, maana yake unajitahidi kuimba nyimbo za Bwana ukiwa katika nchi ya ugenini (Upo kando ya mito ya Babeli) *Zaburi 137:1-4)*, na kama hauko kando ya mito ya Babel, basi umerejea Yerusalem, lakini hujaisimamisha madhabahu juu ya msingi wake.

Leo sina haja ya kusema mambo ambayo yanaweza isogeza madhbahu pembeni, rejea katika somo langu la *_Acha mtungi, acha nyavu zako!!_* utapata kujua namna ya kutoendelea kufanya juhudi bila maarifa, kumbe una scandals nyingi zisizo tubiwa, ila mwenyewe unasema mimi nina amani tu😌, swali ni amani ipi hiyo inayopatana na kukosa unyofu, kumbe dhamiri imeanza kuwa butu _(dull)_, haina sensitivity tena. Unabaki kujifariji tuu. Tena nikuweke wazi mwenzangu, Mungu yuko so specific, I said it katika moja ya masomo yangu, Mungu hawezi kusema nawe maneno ya faraja, kukuonesha ndoto za ushindi, ukiwa umefanya meandering⚡, kwa hiyo mara nyingi huamua kutulia🤐, au kukupa ndoto zilizo jaa maonyo, ukiona baada ya wewe kuvuruga mambo ya kiroho na bado unaota ndoto njema tuu, za ushindi za unyakuo unanyakuliwa, unabarikiwa, iko shida hapo, yuko anayepotosha ili usiifikirie toba. Ukiona unaota ndoto kama hizi hapa chini, ni kiashiria kuna vitu vya kushughulikia ili kuirudisha madhabahu juu ya msingi wake.
1.) Kuota unaachwa na basi 🚌
2.) Kuota unakwenda miguu pekupeku (bare footed)
3.) Kuota upo toilet 🚽, lakini maji ya kujisafishia yameisha au hayatoshi, nawe ulimaliza shughuli
4.) Kuota upo kwenye mazingira machafu
5.) Kuota umevaa shati, lakini huna nguo ya chini, au kinyume chake.
6.) Kuota kuna nyoka kwenye mazingira yako.
7.) Kuota upo kwenye mapambano, lakini umeshindwa kule ndotoni.
8.) Kuota kuna kitu cha thamani umepoteza, ukiwa bado unatafuta na haujakiona ukawa umeshtuka usingizini
9.) Kuota upo mbele za watu, ila hauna kibali, upo ndotoni lakini umahisi utafute namna ujifiche, au unayofanya hakuna anaye-appreciate
10. Kuona mashambulizi ya kiroho, ambayo kwa kawaida ulipaswa kukemea, lakini ukajiona ndotoni unafanya kitu tofauti, mpaka ukiamka unajihoji kwa nini hukukemea kile ulichoona kule ndotoni

HIYO HAPO JUU NI MIFANO MICHACHE YA NDOTO ZINAZOASHIRIA MAANGUKO MEPESI YANAYOREKEBISHIKA KWA GHARAMA NDOGO.

Lakini ukiona ndoto kama
1.Kuumwa na nyoka
2.Kukimbizwa na wanyama
3.Kutumbukia shimoni
4.Kupata ajali ndotoni
5.Kufariki
6.Kuona unazini/fanya uasherati
7.Kuota unaikana imani
8. Kuota umepanga mpango wa kufanya uasherati, au kuisaliti ndoa yako, lakini kabla hujatelekeleza, ukashtuka usingizini
9.Kuota ndoto za kuona wafu

Na nyingine za namna hiyo, zinakiashiria kibaya zaidi juu ya madhabahu yako. Mungu anaowapenda anawaonya na kuwarudi.
MADHABAHU ISIPOKUWA JUU YA MSINGI WAKE, LAZIMA UTAONA NDOTO ZENYE VIASHIRIA VYA MAANGUKO, LAKINI NI HATARI ZAIDI UKIWA UNAJUA KUWA VITU VYAKO HAVIKO SAWA, NA BADO UNAONA TU NDOTO NZURI NZURI, MPAKA UNAAMUA KUYA-OVERLOOK YALE MABAYA KWA KUTOYATUBIA, MAANA ZIKO NDOTO ZINAZODANGANYA KAMA NILIVYOELEZA KATIKA SOMO LANGU LA _*Ufahamu Ulimwengu wa roho*_, KWA HIYO ZINAWEZA KUJA ZA KUKUPITOSHA NJIA, ILI UKAE UNAJIPA MOYO, BADALA YA KUMLINGANA MUNGU.

*HITIMISHO*
*MUNGU WETU HUYU JEHOVAH-BWANA NI MZURI MNO, PENDO LAKE KWETU KWA KRISTO YESU MWANA WAKE NI KUU MNO, AMETUPENDA UPEO KWA HUYO MPENDWA, HE LOVES US IMMEASURABLY, BEYOND EXPRESSION, UNAPOYAGUNDUA MAISHA YAKO YAMEKOSA LADHA, RUN TO HIM, CLING TI HIM, HE IS ABLE TO RENEW HALI YAKO, AKAKUFANYA KUWA MPYA KABISA, UKAIREJEA HALI YAKO YA KWANZA (Jitahidi ulipate somo langu liitwalo  _HALI YENU YA KWANZA_)*

Mungu awabariki sana!

Prosper Kadewele (Mwl Proo)
0762879363

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment