*NAMNA NYEPESI YA KUZIELEWA NDOTO UNAZOOTA, NA JINSI YA KUSHUGHULIKA NAZO*
~*_Mwl Proo_*~
0762879363 (WhatsApp)
Bwana Yesu apewe sifa sana sana! Niliwekewa hili moyoni, nami nimeona vyema kuwaandikia. Ndoto utaziota tu, uwe na kiroho kizuri, kilichoharibika au hutaki kufuatilia mambo ya kiroho, bado utaota tu. Ziwe za kutoka kwa Mungu, Shetani, za kutokana nafsi/roho yako au madhabahu ya mahali ulipo, utaota tu. Na kuna watu ambao wanapinga kuamini juu ya ndoto, lakini nao pia wanaota tu, na kuna mengine yanatukia wanayashangaa kwamba imekuaje niliona kitu cha jinsi hii kabla, kwa kukosa maarifa uangamivu na majanga huwajia kwa maana hawakujua liwapasalo walitende.
Ufahamu huu kuhusu ndoto ni wa muhimu na lazima, maana hauna namna ya kuikimbia hii njia nyepesi ya kupata habari na taarifa kwa haraka na wepesi, ndio maana tunaota mara kwa mara kama sio kila siku.
Kukosekana kwa maarifa ni jambo baya, nimeshuhudia watu wakishirikisha ndoto zao kwenye mitandao ya kijamii ili wapate msaada, sasa nakusihi fuatana nami, ujipatie ujuzi ili ndoto zisiwe mzigo.
*MUHIMU:*
NDOTO NI KITU HALISI SANA, NAMNA NYEPESI YA KUUSHIRIKI ULIMWENGU WA ROHO NI KWA NJIA YA NDOTO. NDIO MAANA VIFUNGO VYA KICHAWI VINGI VINANZIA NDOTONI, YAANI MTU ANAOTA AMEKUWA *ATTACKED* NA SNAKE'S BITE🐍, NA HIKI ALICHOKIONA NI KITU HALISI KABISA. NA WENGINE NIMEWASHUHUDIA ANAAMKA ANAHISI MAUMIVU ENEO LILE LILE ALILOUMWA NA NYOKA, NA BAADA YA HAPO ANAANZA KUWA NA EXPERIENCE YA MATESO YA KICHAWI. NA NIMEWASIKIA WAJUMBE WA KAMBI YA PILI, KWA VINYWA VYAO WAKIELEZA WANAVYOWEZA KUTUMIA MTU NYOKA KIROHO/KICHAWI ILI KUFANYA SHAMBULIO LA KICHAWI. SASA NAOMBA NIELEZE KITU SENSITIVE HAPA, ROHO YA MWANADAMU NI HALISI, INAWEZA KUYASHUHUDIA MAMBO YA KIROHO MAANA YENYEWE NI YA KIROHO TAYARI, HIVYO HAIJALISHI HALI YA KIROHO YA MTU BADO MWANADAMU YEYOTE KWA ROHO YAKE ANAWEZA KUYA-EXPERIENCE MAMBO YANAOENDELEA ROHONI. MTU ANAWEZA KUWA NI MPAGANI KABISA, AMEJAA UCHAFU WA KILA AINA, LAKINI ANAWEZA AKAONA NDOTONI KITU AMBACHO NI KWELI KIMEFANYIKA. ANAWEZA KUOTA KUNA MFANYAKAZI MWENZAKE ANAMLOGA, NA HATA AKIJA KWA WATU WA MUNGU WANAFUNULIWA HILOHILO. MTU ANAWEZA ONA WACHAWI WANAMLISHA VITU VYA AJABU, NA KAMA UMEBAHATIKA KUMNASA MCHAWI KWENYE MAOMBEZI AKIDAKWA AKAANZA KUELEZA ALIYOWAFANYIWA WATU, UNAKUTA MTU NAYE HATA KAMA NI MTU WA TABIA YA ASILI, BADO ANAWEZA KUWA NA KUMBUKUMBU KABISA KWAMBA KUNA SIKU ALIOTA ANALISHWA KITU HICHOHICHO KINACHOTAJWA NA MCHAWI. NINACHOMAANISHA NI NINI, HAYA UNAYAONA KWA SABABU *THE HUMAN SPIRIT IN YOU, TRIES TO TELL YOU, WHAT'S GOING ON IN THE INVISIBLE REALM OF THE SPIRIT*, KWA HIYO UNAWEZA KUTA MTU AMBAYE HAENENDI KIROHO AKAOTA NDOTO KAMA YA KIMUNGU/KIROHO KABISA, NI KWA SABABU ROHO YAKE NI YA KIROHO TAYARI, KITENDO/HALI CHA YEYE KUTOKUWA WA ROHONI KUTAMFANYA TU ASHINDWE KUYAPOKEA MAMBO YA ROHONI (1Korintho 2:14-15), HAPA MAANA YAKE ATASHINDWA KUYAELEWA NA ATAKOSA KUJUA NAMNA YA KUSHUGHULIKA NAYO.
*I. AINA ZA NDOTO KWA KIGEZO CHA MUDA NA WAKATI*
A.) NDOTO ZA PAPO KWA PAPO (INSTANT DREAMS WHICH NEED IMMEDIATE RESPONSE)
Kuna ndoto ambazo, hazina hata haja ya kuandikwa popote, maana ni taarifa inayokujulisha jambo la wakati huo, linalohitaji hatua muda huohuo. Wiki mbili zilizopita niliota ndoto za namna hii mbili, zote zililenga kunijulisha kinachoendelea rohoni wakati huo. Nilota ndoto moja ambayo nilishangaa namuona nyoka mdogo kama wa nusu mita kwa urefu, kitandani kwenye shuka langu, na katika jitihada za kutaka kukwepesha mguu asiuume na nimfunue maana shuka lilimfunika nikaamka ghafula tu, na nikasikia kijana aliyelala decor ya chini akihangaika kama mtu alikabwa na jinamizi, nilielewa kwa haraka maana nilipostuka nikagundua muda huo kuna uvamizi wa nguvu za giza unaonitaka nifanye vita. Pia niliota ndoto kuna mtoto amenijia kwa nguvu za kichawi, ila nilikuwa namzidi nguvu maana nilikuwa namgeuzia mgongo huku nikitamka unaona huo moto🔥🔥🔥🔥🔥, mimi nilitamka kwa imani, ila yeye alikuwa akiuona kweli na kukimbia, na nilihisi kabisa kuwa moto upikuwa unanitoka mgongoni kumfukuza, huyu alikuwa mtoto, ila alikuja mwingine mkubwa wake mwenye nguvu zaidi na niliona mpaka kanyosha mkono kanishika ubavu, muda huu sasa nilimuona halisi pembeni mwa kitanda, na niliponyosha mkono wangu kumkamata nikayafungua mpaka macho haya ya mwilini, ila nayo nilipostuka nilijua juu ya kile kilichokuwa kikiendelea katika ulimwengu wa roho, ni muhimu ndoto za namna uwe umeshinda huko rohoni, yaani usiamke ukiwa umeshindwa. Na wale ambao wameshindana kiroho na nguvu za giza, wakaona bora tu walale wanakosea sana. Kama uliwahi kukutwa na hali ambayo umebanwa usingizini ukashindwa kuomba na kukemea kwa jina la Yesu, bali zile nguvu zile zikakukandamizia ulale kabisa, basi hakikisha unashinda wewe, adui akuachie akimbie (USIKOSE SOMO LIJALO LIITWALO *UNDERSTANDING THE WARFARE IN THE SPIRIT THAT AFFECTS OUR DAILY LIVING*), So ndoto za namna hii zinaweza kuja kukujulisha kitu cha wakati huo, ukishughulikie papo hapo.
B.) NDOTO ZINAZOKUJULISHA HALI ILIVYO ROHONI KWA WAKATI HUO.
Ndoto hizi nazo si lazima hata kuandika, maana unajulishwa hali ya kiroho, na uhitaji wa kufanya intervention kimaombi, sio ya papo kwa papo bali unaweza hata kupanga ratiba maalum ya maombi hata wiki nyingine, ingawa nia ya badiliko au response ya moyo wako inapaswa kuwa *YES* tangu muda umeona. Kwa mfano unaweza kuota ndoto unaoneshwa mazingira yako machafu, unaona shuka za kitanda chako chafu, au uko bafuni umepaka sabauni maji hayatoshi, au yamekata kabisa, au ukaota unahitaji maji ya kujisafisha uchafu ila maji yameisha au hayatoshi, au unakazana kupanda mlima unashindwa. Hii ni mifano tu, hizi sio ndoto za kuamka na kukemea haraka haraka, it took time kwa wewe kuingia katika hali hiyo, hivyo unapaswa kuwa tena na muda wa kutosha kupaponya palipobomoka. Ndoto za namna hii *evaluational dreams*, umepimwa kwenye mizani weeeee (Ayubu 31:6), na sasa unajulishwa kilichopo rohoni. Hizi ndoto zinatokana na Mungu, anayekuotesha ndoto za hizi ni Roho Mtakatifu maana anakutamani (Yakobo 4:5), na Mungu anatamani kukitembelea kituo chako ila kina shida (Kumbukumbu 14:23), Sasa unajuzwa ilivyo ili uweke sawa, ndoto za hivi huwa hazijagi alfajiri mara nyingi huja midnights/usiku wa manane.
C. NDOTO ZINAZOKUJA KUKUJULISHA MATUKIO AMBAYO YATATUKIA PUNDE KIDOGO TU (NEAR FUTURE)
Ndoto hizi huja alfajiri, dakika chache kabla hujaamka. Hizi nazo ni muhimu kuwa na progressive prayer/maombi endelevu kuanzia muda unaamka, na kila unapopata nafasi, mpaka uhisi rohoni kuwa, umevushwa, au likishatokea ila madhara yake yameondolewa. Mwaka 2015 mwanzoni niliamshwa na mama mzazi ili kumsindikiza baba hospitali, aliniamsha saa kumi na moja alfajiri, na ni muda huohuo tu, nilikuwa nimeota ndege✈, imeangukia nyumba za watu maeneo ya Tangi bovu, Mbezi Beach, sio mbali na nyumbani. Baada ya hiyo ndege kuanguka, niliona nimesimama na mama pembeni mwa barabara tujiladili tukio hilo. Niliomba tu Mungu aingilie kati maana ndoto za namna hiyo ni za *near future*. Mchana saa saba mama akatufuata hsapitali na gari toka ofisini, akatuchukua kuturudisha nyumbani. Akiwa anaendesha ghafula akagundua brakes zimekata, tulikuwa njia ya panda ya Kawe, akaona aipeleke taratibu mpaka Tangi Bovu, lakini muda anakata kona kukawa na binti mbele ambaye hakusikia hata horn ya gari. Basi katika kumkwepa gari ikashika uelekeo kwenye makazi ya watu, na ni kama kwa bahati mbaya alikanyaga accelerator, maana ilipaa juu ikaongeza mwendo tukagonga myumba ya watu na fensi ya mabati mpaka ndani. Wote tulitoka hatujapata hata mkwaruzo, nikakumbuka ndoto ya alfajiri, niliona ndege ila ilijadili hili gari kwa fumbo, na hiyo ndio lugha ya ndoto, lugha ya unabii n.k inakuwa na fumbo/riddles na symbols zaidi, hilo ni somo jingine.
D.) NDOTO ZINAZOKUJA ZIMEBEBA UFAFANUZI NA TAARIFA ZA MAMBO YAJAYO YAWEZA KUWA MIEZI AU MIAKA MINGI IJAYO.
Ndoto hizi kwa kawaida huwa ndefu, zinaweza beba ujumbe mrefu kama unaangalia movie📼📺 fulani huko usingizini. Ndoto hizi, zina haja ya kuandikwa (Habakuki 2:2-4) huwa zinabeba mambo mengi, na mengine ni ya kukusaidia njiani kuelekea katika ukamilifu wa kile kilele cha ndoto hiyo. Hivyo andika, na unaweza pata tafsiri ya kwanza mara unapoamka, ukakaa wiki au miezi kadhaa ukapata tafsiri nyingine au nyongeza ya tafsiri ya kwanza n.k
E.) NDOTO INAYOJIRUDIA KWA MUDA MFUPI
Ndoto itakayojirudia kwa muda mfupi, inakuwa ni ndoto ambayo utimilifu wake haupo mbali, na nguvu ya maombi uliyoiruhusu iishughulikie haijatosha kulisawazisha. Bado ushindani wa rohoni unaonesha upande wako kuzidiwa, kama imejirudia na ni ndoto mbaya, kama ni nzuri basi inafanyiwa tu *Echoing* kama mkazo zaidi. Mwaka jana November, nilikuwa naugua kichwa, na nilikuwa nimetoka kumaliza maombi ya mwezi mzima. Niliamka asubuhi nimeota kwamba nimedondoka barabarani, nikaomba kidogo lakini nilikuwa dhaifu wa mwili. Mchana nimerudi toka kazini, nimejiegesha kitandani, ikarudia tena, nimeona nataka kuvuka barabara, ila nimeanguka tena katikati ya barabara kwa kuumwa kichwa usiku wake nilipolala tena, nikaona kama kuna ujenzi wa barabara, then nikaanguka chini na wakati huu nikaona na nguzo za umeme zimeanguka ilikuwa kidogo ziniguse kuniunguza, nikagundua issue iko serious sanaaa... Nikaamua kuongezea nguvu kwa kuwajulisha na makamanda wengine wa kiroho. Na Bwana akanionesha kwa ilikuwa ni shida kubwa kama ya mauti, lakini aliniomesha nimeogelea katika kina kikubwa nikatokea upande wa pili na ku-escape, nikawa nimesalimika.
Zile zinazojirudia kwa time intervals kubwa, unakumbushwa tu, kwamba kuna suspended issue huko rohoni, haukuishughulikia ipasavyo, ila bado inadai, na haijafikia expiry yake. Zipo ndoto ambazo zinakuwa zimefikia expiry, so hazina kazi tena, hata kama ukiandika, yani muda wake umepita huko rohoni.
*NB*
*_SIO NDOTO ZOTE ZINAHITAJI KUANDIKWA, TOO MUCH DREAMING IS ALSO NOT TO BE ENTERTAINED (Mhubiri 5:7), KUMBUKA ZIKO NDOTO ZA KUDANGANYA, ZIPO NDOTO KATIKA ULIMWENGU WA ROHO ZINALENGA KUKUPOTOSHA PIA. THE ONLY WAY YOU CAN BALANCE NI WEWE UJAWE NA KWELI YA NENO LA MUNGU NA SIO MANDOTO TU KIBAO HUKU HUNA KWELI YA MUNGU WALA MAARIFA YA KUTOSHA KIROHO MAANA HATUONGOZWI NA NDOTO._*
*II. NAMNA NYEPESI YA KUIELEWA NDOTO UNAYOIOTA NA HATUA YA KUCHUKUA*
Ndoto ni mlango mwepesi sana kutumiwa hata na Shetani, ili kuleta ukengeufu/uharibifu ndio maana unapaswa kuwa makini. Kuna watumishi wametengeneza mpaka dictionaries za ndoto, ili ukiota unaenda ku-refer fasta. Sio mbaya sana, hiyo ni secondary source ambayo kimsingi inaweza tu kukupa ufahamu, ili uweze kwa siku za badae kujua namna ya kuelewa lugha za rohoni hata kama utaota ambayo kwenye glossaries za vitabu vya watumishi hawajataja jambo lako. Kwa nini nimesema ni secondary source na wala sio ya msingi, ni kwa sababu kitu kimoja anaweza kukiona huyu ndotoni kikaa na maana tofauti na mtu mwingine akikiona kitu kilekile, kwa nini, endelea kufuatilia.
🇲 🇦 🇷🇦 🇺 🇦 🇲 🇰🇦🇵🇴
🛌 JARIBU KUKUMBUKA (MEMORIZE) NDOTO YAKO ILIHUSU NINI, FANYA KAMA KUJISIMULIA FULANI
🛌UKIWEZA IFANYIE CATEGORIZATION, IPO KATIKA KUNDI LIPI LA NDOTO, KWA UFAHAMU ULIOUPATA, ILI UJUE HATUA YA KUCHUKUA KIMAOMBI. KUMBUKA MAOMBI NDIO KIFUNIKO CHA YOTE, HATA NDOTO USIPOIELEWA KABISA, WA NJIA YA MAOMBI ITASHIGHULIKIWA TU (HAKIKISHA UNAPATA KUSOMA SOMO LANGU LIITWALO _*WHY PRAYING?*_
🛌 HATAKA KAMA NDOTO INATISHA SANA, HUPASWI KUANZA KU-PANIC, MAANA LUGHA ZA ROHONI UNAWEZA KUONESHWA KIFO, KUMBE HATA HAIHUSU KIFO, AND AS THE MATTER OF FACT NDOTO ZA KIFO MARA NYINGI UNAWEZA ONA KITU TOFAUTI, KWA MFANO TAA INAZIMA💡, MTI UNAANGUKA, MTU ANAPACK MABEGI ANAONDOKA KAMA KUSAFIRI ETC, INGAWA ZIKO PIA UNAONESHWA KABISA KIFO, JENEZA, MAKABURI ETC. HIVYO HATUCHUKUI HATUA KWA KUANGALIA ILIVYOTISHA BALI HALI YA MOYO, YAANI UNAJISIKIAJE MOYONI ULIPOAMKA UKAIKUMBUKA NDOTO? FARAO ALIOTA NDOTA ALIPOAMKA MOYO WAKE ULIFADHAIKA (Mwanzo 41:8) VIVYO HIVYO NEBUKADREZA (Daniel 2:1). HALI UNAYOJISIKIA MOYONI UNAPOSTUKA UKAIKUMBUKA NDOTO, NDIYO INAYOKUPA KWANZA UJUE NDOTO IMELENGA NIN, UNAWEZA KUONA MAMBO FULANI MABAYA UKAAMKA MOYO AMANI YAKE HAIJAGUSWA KABISA, UJUE HAPO NI ISHU NYINGINE TU, KWA UTULIVU UNAWEZA MUULIZA ROHO MTAKATIFU HAPA ULIKUWA UNASEMAJE?
🛌 KAMA NDOTO UNAONA INAKUPA UJUMBE WA KUKUVURUGA, ANGALIA HALI YAKO NA MUNGU KIMAHUSIANO IKOJE KWA WAKATI HUO, YANI HALI YAKO YA KIROHO INAENDANA NA AINA YA NDOTO ZINZOKUJA. KUNA NDOTO ZINAKUJA ILI KUKUVUNJA MOYO ILI UONE JITIHADA ZAKO NI BURE (ZINAZOTOKA KAMBI YA ADUI), KWA HIYO UNAWEZA PIMA NA KUJUA HUO NI WAKATI UPO NA UHUSIANO *INCLINED* NA MUNGU HALAFU UNAOTESHWA NDOTO UNAZINI AU UNAKUNYWA POMBE ETC UTAJUA NAMNA YA KUISHUGHULIKIA, NA ZIPO NDOTO NYINGINE ZINAPASWA KUWA *IGNORED*, UNAZIPUUZA ILI UWE SALAMA, KAMA UTATAKA KUCHUKUA HATUA ZA MAOMBI NA KUFUNGA KWA KILA NDOTO, THEN YOU WILL SOON GO MAD.
🛌 HATUA YA TANO, NI KUIWEKA HIYO NDOTO KWENYE MAISHA YAKO NA MAZINGIRA YAKO, HATA KAMA IMEKUJA KWA FUMBO, UKIISHA MALIZA HATUA NNE HAPO JUU, HATUA YA TANO IWEKE KWENYE MAZINGIRA YA MAISHA YAKO, UTAIONA KWA HARAKA INAZUNGUMZIA SWALA LIPI KATIKA MAMBO YAKO YANAYOENDELEA.
*NAMNA NYEPESI YA KUELEWA NDOTO, NI KWA NJIA YA NENO (BIBLIA) NA KUULIZA KWA ROHO MTAKATIFU DIRECTLY*
Kwa zaidi ya 75% ya lugha zinazotumiwa na Mungu/Roho Mtakatifu katika ndoto unazipata katika Neno lilioandikwa ndani ya Biblia. Na kwa wanaofuatilia vitabu vya manabii (major and minor prophets), Zimebeba lugha ya kinabii na alama(symbols), zinazotumika zaidi rohoni infawani kwa vitabu vyote tu vya Biblia .. Unaweza kuona miti, milima, nyumba, wanyama, wadudu, mapambo, silaha za jadi au za kisasa, vyombo vya ndani, vyombo vya usafiri, vitabu, mito, bahari, matukio na vitu vingine vingi na kwa zaidi ya 75% ya yale tuyaotayo yametajwa kwa lugha za kinabii yanawakilisha nini, ukiyaota ukayajua maana yake ndipo utakapoyashughulikia kwa usahihi.
Katika sehemu nyingine ya somo la ndoto, nitajitahidi kuweka mifano ya vitu common ambavyo watu wanaota mara kwa mara na tafsiri zake kwa kutumia lugha za kinabii katika Biblia. Ingawa mpaka sasa naamini umepata mwanga wa namna unaweza ukafanya.
Kwa mfano miongoni mwa ndoto mbaya ni kama za kuona wafu/watu waliokufa. Lakini ubaya wake zaidi utatokana na hali ya kiroho ya huyu anayeota, na je ni mara ngapi. Na je kama ni nadra unajua hatua za kuchukua? Ziko ndoto unapaswa kufanya *REVERSING & REFUTING*, yaani unazigeuza na kuzibadilisha kwa kuzifuta. Kwa mfano najua kabisa ndoto za wafu ni mbaya, nyingi zinaonesha wewe muotaji unawindwa na roho za mauti, au unafuatiliwa na mizimu, au kuna vitu vya urithi mbaya unavipokea kiroho toka marehemu, au unafanyishwa agano la kuzimu kwa namna fulani (hasa kama utaota unapewa chakula au unakula pamoja na marehemu) na kadhalika na kadhalika. Lakini mimi nimeota usiku wa jana ndoto, niko na ndugu yangu aliyefariki, nililala saa sita na robo nikastuka saa saba kasoro dakika nne, lakini kwa dakika hizo niliota niko na mtu huyo, na ingawa ndoto haikuwa mbaya, ila kuna muda nilimkumbatia na nilimpa ujumbe fulani wa kweli.... Nilipstuka tu hali ya ndani ya moyo wangu ilinielekeza kuwa kuna kitu cha kushughulikia instantly, nilipata (Isaya 25:8) kwamba Mungu ameimeza mauti hata milele, na ingawa yule mtu nilimpa ujumbe fulani wa kweli, lakini neno la Mungu ni mzani mzuri (Isaya 38:18), inasema washukuao shimoni/kaburini hawataitarajia kweli yako, ni muhimu kujua there should be no connection between the dead and the living (Isaya 8:19). Hivyo niliposimama kitandani kushughulikia niliyoyaona niliingia rohoni nikiwa na kila nikitakacho, ikiwemo kauli ya Mungu kuhusu ndoto hiyo. Na niseme tena hali ya kiroho ndiyo imayoweza fanya tupate tafsiri sahihi ya ndoto, na mtu huyu awezaye kuielewa zaidi ndoto, kwa zama hizi za Roho Mtakatifu kiutendaji, ni mtu mwenyewe aliyeota.
Mwl Proo (Prosper Kadewele)
0718922662
0762879363
alltruth5ministries@gmail.com
No comments:
Post a Comment