Sunday, December 3, 2017

GHARAMA YA UANAFUNZI

*GHARAMA YA UANAFUNZI*
🔥💰🗡💵🔥
*(The Cost of Being a Disciple)*

🅜🅦🅛  🅟🅡🅞🅞
*0762879363*

Haleluya Haleluya!
Nambariki Bwana, kwa wokovu aliofanya. Nakukaribisha katika somo hili, ambalo ni chujio/filter pia ni pepeto/winnowing fork.  Ujumbe umeniunguza ndani yangu kama kwa moto. Wengi tumezoea nukuu ile ya Mathayo 13:29, Kwamba tuyaache magugu na ngano yakue pamoja, wakati wa mavuno ndipo tutajua magugu na ngano (weeds/wheat). Leo nilichopewa nikuyasaidia magugu yanapoendelea kukaa katika shamba la ngano yajijue yenyewe ni magugu. Lakini pia ngano ijue yenyewe, na hata magugu yanayotokea kufanana sana na ngano, yawe dhahiri.

Wapenzi katika zama hizi kumekuwa na hatari, nina shuhuda za wengi walioangushwa katika wokovu, kwa sababu kuna magugu yalijiingiza kwa siri (Yuda 1:4). Zama hizi ambapo kila mtu anajinadi *NIMEOKOKA, NAMPENDA YESU*, ili kunogesha salamu ya utambulisho popote. Tunao mabinti walioangushwa kwenye uzinzi, tunao ambao ndoa zao zinachoma kwa maumivu kuliko 🏹 mshale na zina uchungu kuliko pakanga/wormwood. Kisa na mkasa, kijana wa kiume au binti alijitambulisha kanisani, nimeokoka nampenda Yesu, Haleluya wapendwa! Then ukarukwa na akili kuprocess uchumba fastafasta... kama ungekuwa na Mungu ungenasuka, lakini ukaharakisha na sasa waenjoi uchungu wa pakanga😣😤 (Mithali 22:3, Mhubiri 7:26).

Wokovu sio dhehebu, dhehebu ni kama chama tu na ndio maana denominations zile za kwenye Biblia zilitajwa kama sects/parties. Wokovu unahusisha watu kukutana na Mungu, naam kumpata Yesu mioyoni. Kwa hiyo hata wapentekoste, wasiubinafsishe wokovu kana kwamba ni wa kwao tuu, hapana!. Mimi sina shida na vikundi vya uhamsho vyote (Charismatic movements), wakigundua kwamba kwa kweli iko njia ya wokovu mbali na mifumo yetu ya dini, ni vyema na heri. Mkazo wangu leo upo juu ya viwango/standards.... Mtu anayetamka *NIMEOKOKA*, ajue hiyo sio salamu ya kupamba maamkizi, Hold on!✋🏾haipo hivyo... Mtu anayetaja sema ameokoka, lazima ajue gharama ya kuwa mwanafunzi...Njia ya wokovu ni nyembamba na imesonga mno, kwa nini nyembamba??? *You cannot go through it, along with your past stuffs.* Hii popularity ambayo imepunguza quality/ubora hapana kabisa. Watu wanaotuambia wameokoka kwenye salamu zao, tukiyaangalia maisha yao hatumwoni Kristo, wala hawatembei kama alivyonenda Kristo (1Yoh 2:6). They better stop grabbing that claim (Bora waachane na kauli ya nimeokoka). Hakuna faida yoyote kwenye ufalme, kuwa na sentensi ya kukariri kusema, *"NIMEOKOKA, NAMPENDA YESU"*, wakati wajijua wazi kabisa, hujakutana na Yesu, au ulikutana naye na hujaitaka gharama ya kuwa mwanafunzi wake.

TULIOAMUA KUWA WANAFUNZI WA YESU, TULITOA YOTE KWA YESU (We gave it all). Na tukajidhabihu kwa BWANA, ili maisha yetu yaoneshe sura ya Kristo. Waliojiingiza kwa siri, tunawakuta mtaani wamejazwa na scandals/tuhuma mbaya kila kona. Na ukiwahoji kidogo, wanasema kila mmoja na udhaifu wake Bwana ☹. Kwa nini umeamua  kujitutumua kwamba umeokoka, wakati dhambi inakugalagaza vya hatari?? Imani yetu katika Bwana Yesu, aliye Kristo, inahusisha kushinda dhambi, kuushinda ulimwengu, soma hapa;
1 Yohana 5 : 4
*_Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu._*

👆🏽👆🏽MNAIONA SHUGHULI HIYO?, WALE WANAOSEMA HAKUNA KUOKOKA DUNIANI LEO SINA UGOMVI NAO, MAANA HAO WALISHAONA MSALABA✝ WA YESU HAUNA NGUVU YA KUWASHINDIA DHAMBI, LEO NASHUGHULIKIA MAGUGU AMBAYO HAYAJAAMUA KWA DHATI, KUMWAMINI YESU NA KULIPA GHARAMA YA UANAFUNZI. IMANI YETU IMEJENGWA JUU YA KUMWAMINI YESU NA KUUSHINDA ULIMWENGU. WEWE MWENYE WOKOVU WA KIFAFA, ULIAMINI KWA BWANA YUPI?? YESU ALILIPA GHARAMA, AKABEBA MSALABA TUUPATE WOKOVU, LAKINI WEWE UNAYETUSALIMIA KWA JUHUDI ZOTE NA KUJITAMBULISHA KWAMBA UMEOKOKA, SHARTI UUBEBE MSALABA WAKO (GHARAMA YA UANAFUNZI), UMFUATE YESU. MNATUPUNGUZIA TASTE MAANA TUKISEMA TUMEOKOKA HAINA UTISHO KAMA WA HAPO MWANZO, MAANA WATU WAPO KWENYE VILABU VYA POMBE😞😞🍺🍻, NI WANAFELLOSHIP YA UAMSHO, NA WANAGONGA MAJI YA ILALA (TBL) MDOGOMDOGO, NA WAKIWA WAMESHIKILIA CHUPA CHA SERENGETI🍾, WANAJITAJA SISI TUMEOKOKA, UNAJUA UNAWEZA KUNYWA, SEMA USILEWE! 👈🏽👈🏽MAGUGU YANAKUNYWA POMBE, NA KUENDELEA KUMKIRI YESU TU. KIJANA MWANA-FELLOWSHIP UNATEMBEA NA MABINTI KWA KUFANYA NGONO, LAKINI UNAJITAMBULISHA NIMEOKOKA, MACHO YAKO YAMEJAA UZINZI (2Petro 2:14), LAKINI BADALA YA KUMTAFUTA YESU AKUSHINDIE, UNATIA BIDII KUTUVUNGA SISI TUSIOKUONA KWAMBA UMEOKOKA. NAZUNGUMZA NA WEWE MWANAMKE AMBAYE BOSI WA KAMPUNI AMEKUFANYA UWE SEX-MACHINE, KWA MATUMIZI YA TAMAA ZA MWILI WAKE, NAWE HUTAKI KUIKIMBIA OFISI, MAANA KAKUPANDISHA MSHAHARA MARA DUFU, NAYE ANAJUA WEWE NI MLOKOLE, LAKINI ANAJISIFIE HUKO NJE, KWAMBA WALIOKOKA SIO KITU, UKIWA NA HELA KAMA KAWA TU UNAMGUTUSHA🙊. WEWE KIJANA USITUHARIBIE DILI, HATA KUOA HUJAOA, UPO BIZE NA VIJARIDA VYA JIFUNZE TENDO LA NDOA, JINSI YA KUMFIKISHA MWANAMKE KILELENI NA MATERIALS ZINGINE ZA WANANDOA, AT THE SAME TIME HUKUMBUKI NI LINI ULIKISOMA KITABU KIMOJA CHA BIBLIA UKAKIMALIZA, GUGU WEE!🙁 MATOKEO YAKE NDIO HAYO YA KUKAGUA MAKALIO YA WANAWAKE KILA WAKIKATISHA MBELE YAKO, SASA NI LINI HIVI UTAWASHUHUDIA HABARI ZA YESU?? MAANA MIONGONI MWA VIASHIRIA VYA KWAMBA UMEKAA NDANI YA YESU, NI PAMOJA NA KUWALETA WENGINE KWA YESU. MIMI NINAYEANDIKA, NIKIKUTANA NA WADADA WANAOVAA NUSU UCHI 👙WAZO LA KWANZA NIKIWAONA, NI KUTAFUTA GIA KUWAULIZA, VIPI MNAAMINI HABARI ZA YESU?? SASA WEWE UNAJITIHADA ZA KUOMBA NAMBA ZA SIMU TU, BALOZI GANI WEWE??? MTU AKIKUTANA NA WEWE ULIYEOKOKA, EXCLUSIVELY AYAPATE MAMBO AMBAYO ANGEYAPATA, KAMA ANGEKUTANA NA YESU. SASA WEWE UNASHINDWA NA KILA DHAMBI, MTU AKILIPUKA KAPEPO NAWE UNATOROKA, MAPEPO YAMEKUSHIKILIA, UKIAMBIWA MWAMINI YESU UOKOKE, HUTAMILIKIWA NA MAPEPO, KAZI KUTAJA FELLOWSHIP YENU, NANI ALIKUAMBIA WOKOVU NI DHEHEBU AU FELLOWSHIP YA KIUAMSHO???  WOKOVU NI KUKUTANA NA YESU, AWE BWANA NA MWOKOZI (AKIWA NI BWANA KWAKO UTAMTII YEYE YESU) UKIMWAMINI KWA KUAMUA KABISA KABISA, ATAKUOKOA NASI SOTE TUTAJUA.

Yesu Kristo alipojitoa kwa ajili yetu, na kufa kifo cha aibu, alikuwa anaugharamia wokovu ili unukie harufu ya manukato (Efeso 5:2). Sasa leo hii kwa kuwa watu, wamegundua njia pekee ya kuepuka sauti za mahubiri ya kuchomwa mioyo, ni kujitaja nimeokoka, matokeo yake wametuingizia mainzi mafu,

Mhubiri 10 : 1
*_Mainzi mafu huvundisha marhamu ya mwuza marashi; Kadhalika upumbavu haba ni mzito kuliko hekima na heshima._*

MAINZI MAFU HAYATAKIWI KABISA, USIKUBALI KUWA MAINZI MAFU, USIKUBALI KUWA GUGU. TAMBUA WOKOVU SIO MAIGIZO NI KITU HALISI KABISA, USIJE UKADHANI WOTE TUNABABAISHA, KWA KUWA WEWE UNABABAISHA... HAKIKISHA UMEKUTANA NA YESU.

*MOYO WA SOMO*

Luka 14

*_26 Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu._*
*_27 Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu._*

👆🏽👆🏽👆🏽KUNA WATU NIMEWAHI KUSIKIA WANASEMA, JESUS IS MY NUMBER ONE! SWALI LA MSINGI YESU NI NAMBA MOJA KATIKA CATEGORY IPI?? KAMA UKISEMA YESU NI NAMBA MOJA, HALAFU KATIKA CATEGORY HIYO HIYO MKEO NI NAMBA MBILIA AU WAZAZI, AU BIASHARA ZAKO, NI WAZI IPO SIKU HAO NAMBA MBILI WATAMPIKU TUU HUYO YESU.. YESU AKIWA NAMBA MOJA SIO KATIKA CATEGORY MOJA NA HIVYO VITU VINGINE, MAANDIKO YANASEMA, *_IN YOUR HEARTS, SET CHRIST APART (1Pet 3:14)_* YESU ATENGWE KIPEKEE KABISA. MAANDIKO HAYO HAPO JUU, INAITWA GHARAMA YA KUWA MWANAFUNZI WA YESU. ANASEMA MTU AJAYE KWANGU, HAMCHUKII BABA, MAMA, MKE WAKE ETC HUYO HANIFAI... SASA SIO TU UNAWACHUKIA, LAKINI KUSIWE NA MWENYE AMRI KWAKO, KULIKO YESU BWANA. ENYI WATOTO WATIINI WAZAZI WENU *KATIKA BWANA* (Efes 6:1)/ MZAZI AKITOA AMRI ZA KUMPINGA YESU WAKO HAPO NDIPO PA KULIPA GHARAMA YA UANAFUNZI, UKIANZA KUTUAMBIA WAZAZI WAMESEMA NISIBADILI DINI SIJUI DHEHEBU, WAKATI UNAJUA KABISA HABARI ZA WOKOVU NIMEZISIKIA HUKU, MAFUNDISHO YASIYOGHOSHIWA NIMEYAPATA HUKU, KISHA UKAAMUA KUTII, HAPO UMETII WAZAZI SIO KATIKA BWANA, NI BORA UNGEAMBIWA KAMA HAUACHI WOKOVU, TAFUTA PA KWENDA, BWANA ANGEKUKARIBISHA KWAKE (Zaburi 27:10). TUNALO WINFU LA MASHAHIDI, MKEO ANAKUSHAURI MAMBO KINYUME NA YESU, JIFUNZE KWA AYUBU, AKAMJIBU MKE WAKE, WEWE WANENA KAMA MMOJA WA HAO  WANAWAKE WAPUMBAVU (Ayubu 2:10). WOKOVU UKIISHA KUUPOKEA LAZIMA UUBEBE MSALABA, UWE RADHI KU-SACRIFICE MARAFIKI WA OVYO, KUACHA MAMBO YA KWANZA YASIPOTANA NA UTAUWA, HAKUNA WOKOVU WA KUENDELEA KUHUDHURIA NIGHT CLUBS, HAKUNA WOKOVU WA KUENDELEA KUWA NA BOYFRIEND, AU KUMSHAWISHI AOKOKE ILI MUENDELEE, AKIOKOKA AOKOKE KWA SABABU BABA AMEMVUTA KWA YESU HUYO BOYFRIEND, SIO UMUOKOKESHE, ILI MUENDELEZE UHUSIANO HIYO HAIPOGO, HAPO MNAFANYA DA'WAH YA KIISLAMU SIO INJILI YA YESU. TUMEUBEBA MSALABA KWA KUACHA MAISHA YA DHAMBI KABISA, WALE WAJANJA WANAONUKUU (1Yoh 2:7), KWAMBA TUKISEMA HATUNA DHAMBI TWAJIDANGANYA, WANASAHAU KUSOMA (1Yoh 2:1ff, 3:9-10). UKIENDELEA KUSEMA UNAMJUA YESU NA UMEOKOKA TEMBEA KAMA YESU, TUKUSHUHUDIE NA MWENENDO WAKO WA WOKOVU, KAMA IWASTAHILIVYO WALIOOKOLEWA. LIPA GHARAMA YA KUUTAFUTA USO WA MUNGU, KAMA NI KWA KUFUNGA NA KWA KUOMBA, NA KUMTUMIKIA MUNGU KWA UAMINIFU. USANII,MAIGIZO NA UBABAISHAJI WOTE UUACHE, ILI USIINAJISI KAZI YA MSALABA, MATAIFA WAKAONA MAMBO YA KUOKOKA NI MZAHA FULANI.

Mwl Proo
0762878363 (Whatsapp)

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment