*NINI CHANZO CHA ELIMU YA NYOTA,INAHUSIKAJE NA MAISHA YA WANADAMU,NA JE WAKRISTO WALIOOKOLEWA WANAHAJA YA KUIFUTILIA KWA NAMNA YOYOTE?*
Ufafanuzi by Mwl Proo
0762879363
0718922662
NDUGU WAPENDWA UHURU WA KWELI UNAUPATA KWA KUIFAHAMU KWELI. ELIMU YA NYOTA (UNAJIMU/UMAMAJUSI/ASTROLOGY) NI ELIMU AMBAYO HAIKUWA MPANGO WA MUNGU WANADAMU WAIPATE ILA KIMAKOSA WAKO MALAIKA WALIOWAFUNDISHA WANADAMU. KATIKA KITABU CHA HENOKO 7:1-6 TUNASOMA KISA CHA MALAIKA WALIOJIVIKA MIILI YA KIBINADAMU WAKASHUKA KTK MLIMA HERMON YAPATA 200 KWA IDADI ZAMA ZA YAREDI BABA MZAZI WA HENOKO.HAWA 200 WALIKUWA NA VIONGOZI 19 KATI YAO YUPO AITWAYE BARAQIJAL HUYU NDIYE HASA ALIIWASILISHA ELIMU YA UNAJIMU,YUPO AITWAYE KOKABEL NDIYE ALIYEFUNDISHA WANADAMU MPANGILIO WA NYOTA NA SAYARI NA VITU VYA ANGA(GALAXIES/ CONSTELLATION) YUPO AITWAYE SHAMSIEL ALIFUNDISHA ISHARA ZA JUA NA SERIEL ALITOA ELIMU YA MWEZI. HAYO YOTE HAYAKUWA MPANGO WA MUNGU NDIO MANA IKO ADHABU ILIYOWEKWA JUU YAO KWA KOSA HILO.
KATIKA BIBLIA MWANZO 10:8ff TUNASOMA KWA KIFUPI KUHUSU NIMRODI MTU HODARI KTK NCHI HASA KTK HUNTING HUYU ANATAJWA KAMA MUASISI WA IDOLATRY(IBADA YA SANAMU) ZAMA ZAKE WALIYASHIKA MAARIFA YALE YA NYOTA YALIYOFUNDISHWA KINYUME NA MPANGO. KATIKA MWANZO 11:1-9 ;TUNAONA HABARI ZA KUJENGWA KWA MNARA WA BABELI SASA HIYO STORI IMEFICHA MENGI NYUMA YAKE. TUUANGALIE MSTARI WA 6
6 Bwana akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya.
SASA SWALI LA MSINGI HII KAULI YA MUNGU INA UTATA,ATI HAWATAZUILIWA NENO WALILOKUSUDIA KULIFANYA...KWANI WANGEWEZA KUJENGA WAKAIFIKIA MBINGU?AMBAYO NI SEHEMU YA KIROHO ZAIDI KULIKO KUIWAZA AS A GEOGRAPHICALLY LOCATED AREA. UKWELI NI KWAMBA HAWA WATU WALIKUWA NA ELIMU YA ANGA KWA HALI YA JUU WALIFAHAMU WAKIFIKA SEHEMU FULANI WAFANYE NINI KUWEZA KU-ACCESS WANACHOTAKA NI MALAIKA WALIVUJISHA SIRI HIZO. NA ELIMU HII ILIENDELEA KUSHIKWA SANA..KULE MESAPOTAMIA (ARAM NAHARAIM) ILIKUBUU ZAIDI,MKIKUMBUKA HABARI ZA MNAJIMU BALAAM BIN BEORI (HESABU SURA YA 22 HADI SURA YA 24) MTAELEWA ZAIDI. HUYU MNAJIMU KWA ELIMU YA NYOTA ALIMTABIRI MPAKA YESU (HESABU 24:17)
17 Namwona, lakini si sasa; Namtazama, lakini si karibu; Nyota itatokea katika Yakobo Na fimbo ya enzi itainuka katika Israeli; Nayo itazipiga-piga pembe za Moabu, Na kuwavunja-vunja wana wote wa ghasia.
UKWELI NI KWAMBA KULEKULE ALIKOTOKEA MNAJIMU BINGWA BALAAMU NDIPO WALIPOTOKEA WALE WANAJIMU/MAMAJUSI WA MASHARIKI (MATH 2:1-2) HUKO MESAPOTAMIA
SASA TUNAO WANAJIMU LEO AMBAO UKIWAULIZA UNAJIMU NI NINI WATAJIBU NI SAYANSI INAYOHUSU VITU VYA ANGANI(JUA,MWEZI,NYOTA NA SAYARI ZINGINE) NA UHUSIANO WAKE NA MAISHA YA VIUMBE. WANAJIMU HUSEMA "CELESTRIAL PHENOMENA ARE CONNECTED TO ALL LIVING ORGANISMS... NAFASI YA VITU VYA ANGANI(CELESTRIAL BODIES)VINAWEZA KUANGALIWA KWA KUTOKEA DUNIANI AU MAHALI ALIPOZALIWA MTU ILI KUJUA TAARIFA ZOTE ZA KIUMBE.. ILE POINT YA KIUMBE CHOCHOTE DUNIANI UKIINGALIA KWA USAWA (VERTICALLY) KUELEKEA ANGANI KULE JUU KUTAITWA "ZENITH" NA KTK JEDWALI LA WANAJIMU LINAZINGATIA MUDA NA MAHALI PA KUZALIWA NA WANAPROCESS HIZO TAARIFA KUPATA VIASHIRIA VYA MAMBO YA KILA KIUMBE(SIO LAZIMA IWE KIUMBE HAI HATA KIWANDA NA BIASHARA) WANASEMA KWA KUZINGATIA ILE NAFASI NA MUDA UKISOMA MAMBO YA VITU VYA ANGANI KUNA UHUSIANO WA MOJA KWA MOJA KATI YA SPECIFIC CELESTRIAL OBJECT NA KITU KILICHOPO CHINI YAKE IF WE DRAW A VERTICAL LINE DIRECTLY NA HII IMEFANYIKA KWA KARNE NYINGI OBSERVATION OF CELESTRIAL OBJECTS IKAONESHA KUWA YANAYOSOMEKA KULE ANGANI YANA UHUSIANO NA VITU VYA DUNIANI. UKIMFUATA LEO HII MNAJIBU ANA-TRACE TUU ULIZALIWA MAJIRA GANI NA ENEO GANI BASI..HII HAPA CHINI NI SAMPULI YAKE
Sun 15°37' Pisces
Moon 1°19' Aquarius
Mercury 0°34' Pisces
Venus 21°46' Aquarius
Mars 29°53' Scorpio
Jupiter 18°39' Я Virgo
Saturn 16°05' Sagittarius
Uranus 18°32' Aries
Neptune 9°43' Pisces
Pluto 17°01' Capricorn
Chiron 20°42' Pisces
True Node 21°48' Я Virgo
True Lilith 17°57' Я Libra
KATIKA JEDWALI LAKE LIMEGAWA VIPINDI VYOTE VYA MWAKA KUANZIA MARCHI 21. WAWEZA FUATILIA HIVYO VIPINDI/ISHARA ZA KINAJIMU KUHUSU ANGA VINAVYOITWA "ZODIACAL SIGNS"
www.astrotheme.com/astrology_signs.php
TAIFA LA ISRAEL AMBALO NI PICHA HALISI YA WATU WA MUNGU LEO...MUNGU ALIWAZUIA KUFUATILIA ELIMU YA NYOTA KUJUA ISHARA ZA ANGA (YEREMIA 10:1-2)
Bwana asema hivi, Msijifunze njia ya mataifa, wala msishangae kwa sababu ya ishara za mbinguni; maana mataifa hushangaa kwa sababu ya ishara hizo.
Thus saith the LORD, Learn not the way of the heathen, and be not dismayed at the signs of heaven; for the heathen are dismayed at them.
SASA WAKRISTO WANAOISHI ZAMA HIZI ZA ROHO MTAKATIFU HAWAPASWI KABISA KUWEKA TUMAINI LAO LA KUPATA TAARIFA TOKA KWENYE ELIMU YA KIJINI, SIO TUU WATAMUUZINISHA ROHO WA NEEMA LAKINI NI AIBU MAANA TUMELETEWA ELIMU NA MAARIFA YOTE KWA NJIA YA ROHO MTAKATIFU. MUNGU HATAPENDEZWA KAMA TUTATUMAINIA CHOCHOTE KINGINE MAANA PAMOJA HUKO KUHUSIKA KWA MIENENDO YA ANGA NA MAISHA YA VIUMBE...NGUVU YA UKOMBOZI TULIOUPATA KWA YESU INASHINDA NGUVU ZOTE NATURAL AND SUPERNATURAL POWERS/FORCES.. NI HATARI KUJITIA KATIKA ELIMU AMBAYO MUNGU HAKUTUKUSUDIA ILI MWANADAMU ASIUWAZE MSAADA MWINGINE ZAIDI YA ULE ULIO KTK MPANGO WA UKOMBOZI WA MUNGU WETU KWA NJIA YA YESU KRISTO... KAMA MUNGU ATAKUPA UFUNUO UOMBE JUU YA NYOTA BASI HIYO PERSONAL REVELATION,ISITUMIKE KAMWE KUUNDA FUNDISHO LA MWILI WA KRISTO YAANI KANISA..PIA UJIZOEZE KUTOFUNDISHA VITU AMBAVYO KRISTO WALA MITUME WAKE HAWAKUTENDA WALA KUFUNDISHA (RUMI 15:18) NA PAULO MTUME ALIONYA KUSEMA USITENDE, USIZIDI YALE YALIYOANDIKA (DON'T GO BEYOND WHAT WAS WRITTEN)
1Kor 4:6
Basi ndugu, mambo hayo nimeyafanya kuwa mfano wa mimi na Apolo kwa ajili yenu, ili kwamba kwa mfano wetu mpate kujifunza kutokupita yale yaliyoandikwa; ili mmoja wenu asijivune kwa ajili ya huyu, kinyume cha mwenziwe.
And these things, brethren, I have in a figure transferred to myself and to Apollos for your sakes; that ye might learn in us not to think of men above that which is written, that no one of you be puffed up for one against another.
MWANA AKIWAWEKA HURU MTAKUWA HURU KWELI KWELI. INATOSHA NA MBARIKIWE MNAPOENDELEA KUSHIKAMANA NA KWELI NA KUACHA KUSIKILIZA ROHO ZIDANGANYAZO NA MAFUNDISHO YA MASHETANI.
Mwl Proo
0762879263(whatsapp only)
alltruth5ministries@gmail.com
No comments:
Post a Comment