Saturday, December 9, 2017

MSIHUKUMU!

*MSIHUKUMU; MSIWE WA KIROHO KUPITA KIASI!*
_*Don't judge; don't be extremely spiritual*_

*_Mwl Proo_*
*+255762879363*

Shalom Aleichem!✋🏽
Kuna moto unawaka huku moyoni mwangu (Zaburi 39:3), nataka kuutua 🔥🔥.

*BILA SHAKA, UMEWAHI YASIKIA HAYA MANENO AU KUYATUMIA WEWE MWENYEWE. KWA ZAIDI YA 90% MATUMIZI YA KAULI HIZI ZIMEKUWA NA NIA ISIYO SAHIHI, NA HATA KAMA LABDA WANAKUSUDIA KUNUKUU ANDIKO LA KIBIBLIA, BASI WANALIPOTOSHA KAMA WANAVYOPOTOSHA NA MENGINE PIA (2PETRO 3:16b).*

*WAKRISTO WANAOKATAA MAONYO, HUTAFUTA NA MSTARI WASIOULEWA KAMA HUU WA _"MATHAYO 7:1"_, ILI KUJIWEKEA KINGA WASIPOKEE MAONYO YA BWANA KUPITIA WATUMISHI.*
*Ni rahisi zama hizi watu wanaomchanganya Mungu na vitu vingine (Syncretism) wakihojiwa au kuonywa, wanawahi kusema _USIHUKUMU_, Yaani inachekesha sana; Eti mtu akisahihishwa kwa upendo tu, kwamba mpendwa mbona unakaa na mwanaume hamjafunga hata ndoa? (Usihukumu!). Mpendwa si vyema kwa wewe unayepiga vyombo vya muziki katika madhabahu ya Mungu, kuonekana upo Club unapiga muziki 🎸🎹🎷🥁 wa dunia (zenye maudhuhi ya kifuska); USIHUKUMU! Mpendwa si vyema kwako kufanya collabo ya wimbo wa injili na mtu ambaye hajaamini, USIHUKUMU!  Ndivyo ilivyo sasa, kila mtu akifanya jambo linalostahili kuonywa au kusahihishwa anawahi kunukuu usihukumu. Na nimeona katika ukurasa wa mpendwa fulani ameandika, "Mtu anayekuhukumu, hakikisha anayo mbingu ya kukupeleka".*

*NINI MAANA YA KUHUKUMU?*

*Neno hili hukumu (krínō/κρίνω-Greek  "shofeṭ /תשפוט -Hebrew) kama lilivyotumiwa katika lugha za asili na vyanzo vingine vyote vya kiyunani na kiebrania (including Rabbinical Talmud) zinakubaliana maana moja ya kimuktadha kuhusu Mathayo 7:1, yaani (an act of condemning/decreeing-inflicting penalty to wrongdoers). Hapa mtu alikuwa akihukumiwa kwa mujibu wa maelekezo ya torati. Kuhukumiwa huku sio maonyo, kuna kitu kitaitwa kiebrania "mitath ben din yaani execution by the rabbinic court" ambako hukumu zilikuwa nyingi kufuatana na kosa, miongoni mwa hukumu hizo zilihusisha SEKILA (stoning/piga kwa mawe), HEREG   (decapitation/kukata kichwa), SEREFAH (burning/kuunguza), CHENEK (strangulation/kabwa njia za hewa mpaka kufa). Sasa hizi ndizo zinaitwa hukumu. Yaani Sheria na amri ziliwekewa na hukumu zake, kwamba usifanye hivi, ukifanya utahukumiwa, na hukumu ni hizo adhabu sasa (Deutoronomistic view of history).*

_Soma haya maandiko hapa chini._
Malaki 4 : 4
*_Ikumbukeni torati (sheria) ya Musa, mtumishi wangu, niliyomwamuru huko Horebu kwa ajili ya Israeli wote, naam, amri na hukumu._*

Kumbukumbu la Torati 5 : 31
_*Lakini wewe, simama hapa karibu nami, nami nitanena nawe sheria zote, na amri na hukumu, utakazowafunza, wapate kuzifanya katika nchi niwapayo kuimiliki.*_

*_SASA KUMBE TUNAKOSEA SANA KUDHANI KUONYWA, KUSAHIHISHWA AU KUHOJIWA JUU YA MISCONDUCT FULANI NI KUHUKUMIWA, SI KWELI! MAANA SHERIA NA AMRI 613 ZILIZOPO KWENYE TORATI YA MUSA, ZILIWEKEWA HUKUMU. NA YESU ALIPOSEMA USIHUKUMU CONTEXTUALLY WASIKIAJI WAKE WALIELEWA NI KUTEKELEZA ADHABU KWA MKOSAJI (CORPORAL&CAPITAL PUNISHMENTS)_*

Yohana 8 : 11
*_Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena._*

👆🏾👆🏾YESU ANAMWAMBIA YULE NWANAMKE ALIYEKUTWA AKIZINI, KUWA HATA MIMI SIKUHUKUMU. HIYO HAIMNYIMI YESU NAFASI YA KUMWONYA HAPO b YAKE, KWAMBA USITENDE DHAMBI TENA.

Ingawa literal meaning ya kuhukumu, inaweza kuwa to decide wrong or right. yaani hata kule kusema sahihi au sio sahihi, bado haikatazwi kufanya hukumu ya haki

Yohana 7 : 24
*_Basi msihukumu hukumu ya macho tu, bali ifanyeni hukumu iliyo ya haki._*

*BIBLIA IMETUTAKA TUONYANE, TENA KWA UVUMILIVU, KWA UPENDO*

Tumekuwa na wahalifu wa kiimani (fraudsters), wanaoanzisha liberism ndani ya ukristo, yaani uhuru usioingiliwa, kwamba wameitwa wapate kuwa huru (Galatia 5:13), na hawa watu watakuwa na *"COMPROMISES (kuchukulia poa)"* nyingi sana!. Wanapoendelea kuachiwa wanapelekea kumomonyoka kwa maadili ya kikristo, tunakosa *STANDARDS*, Na hasa katika huu ulimwengu wa sasa ambao hakuna *UMOJA WA IMANI*, ni tatizo zaidi. Siku ya jana nimeshuhudia ambavyo hata wachungaji wana kauli tofauti, Baada ya mwanamuziki wa kidunia *Diamond Platinum* kutoa video ya wimbo wa kidunia uitwao *HALELUYA*, wako waliosema hiyo haina madhara mwacheni afanye biashara zake, aongeze fan base, na wako waliotaka BASATA iufungie. Najua na leo mjadala utakuwa huo. Lakini kwa nini imekuwa shida haya yote, wazamiaji kwenye wokovu walishakuwa wengi. Wokovu haumilikiwi na mtu fulani, wala sio wa kugawiwa kanisani, KUOKOKA KUNA MAANA YA MTU AMEAMINI KATIKA KRISTO YESU KABISAKABISA, AKAKUTANA NA HUYO BWANA KIBINAFSI, AKAPATA KUZALIWA KWA PILI KWA KUFANYWA UPYA NA ROHO MTAKATIFU (TITO 3:5), THEN KAMA KUSANYIKO LA WALIOOKOKA LINGEKUWA NI LA WATU WA JAMII HII, SHIDA INGEKUWA NDOGO, SASA TUNA WANAOJIITA WAMEAMINI HUKU NI FANS WA KARIBU WA KAZI ZA MUZIKI ZA WATU KAMA HUYO MTUNZI WA WIMBO WA HALELUYA, LAZIMA UWE NA UHAKIKA ATAWACHONGANISHA TU NINYI WAAMINI MSIO FANS WAKE NA WALE FANS/FOLLOWERS WA DAMU.
ATHARI ZAKE MTAKUJA KUZIONA SIKU SI NYINGI. NIMEMWONA BINTI MASHUHURI WA KUPOST PICHA ZAKE ZA UCHI KATIKA FACEBOOK *Ritha Rahmanino*, NAYE JANA KAPOST PICHA YAKE YA UCHI AMEWEKA CAPTION YA *Haleluya!*

*WATU WAZIMA KIROHO, AMBAO AKILI ZAO ZIMEZOEZWA KUPAMBANUA MEMA NA MABAYA, HAWAPASWI KUACHA, KUONYA, KUKARIPIA, KUKOSOA, KUSAHIHISHA, ILI KUTUNZA STANDARDS ZA MAISHA YA UKRISTO, KWA KIZAZI CHA SASA NA KILE KIJACHO*

2 Timotheo 4 : 2
*_lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho._*

Tito 2 : 15
*_Nena maneno hayo, onya na kukaripia kwa mamlaka yote; asikudharau mtu awaye yote._*

TUSIACHE HIZI KAULI ZA MSIHUKUMU, NA ZILE ZA MSIWE WA KIROHO SANA ZIKA-PREVAIL, MATOKEO YAKE NI KUKOSA STANDARDS KATIKA CHRISTIAN ETHICS

NITARUDI TENA BAADAE KIDOGO KWA POST YA PILI

Cc/Nakala: KWA WAKRISTO WOTE WENYE MAISHA YENYE MAKANDOKANDO, NA UDAMBUDAMBU, ILA HAWATAKI KUONYWA WATENGENEZE NJIA ZAO, KAZI KUNUKUU TU MATHAYO 7:1, USIHUKUMU!

Mwl Proo
0762879363
alltruth5ministries@gmail.com

Tembelea liki hapa chini upate somo pacha lenye kusaidia

http://alltruthjohn1613.blogspot.com/2016/09/mungu-wako-hakukupa-ruhusa-kutenda-hayo.html

No comments:

Post a Comment