Friday, December 15, 2017

KUHUSU PASAKA

*KWELI KUHUSU PASAKA!*

By Mwl Proo
0718922662/0762879363

HALELUYA WAPENDWA...!!!!! NATAMANI KWA POSTI HII, TUUFUHAMU UKWELI. HULAZIMISHWI KUAMINI, LAKINI UKIELEWA INATOSHA. NENO PASAKA LIMETOOLEWA TOKA KATIKA MATAMSHI YA KIEBRANIA PESACH/PASAKH AU PASSOVER KWA KIINGEREZA; LIKIWA NA MAANA YA *"PITA JUU YA"*. LINATAJWA KWA MARA YA KWANZA KATIKA KUTOKA 12:11; WAYAHUDI WALIELEKEZWA KUPAKA DAMU YA KONDOO AU MBUZI (KUTOKA 12:5) KATIKA MIIMO YA MILANGO, ILI YULE MALAIKA MHARABU (DESTROYER) ATAKAPOPITA JUU YA MISRI, AKIIONA DAMU KATIKA "DOOR POSTS" AWE ANAPASAKA (PITA JUU),  ASIPOIONA DAMU ANAUA WAZALIWA WA KWANZA. MUNGU AKATOA MAELEKEZO HIYO SIKU WAISHEREKEE KAMA AMRI YA MILELE (KUTOKA 12:14). SASA NAMNA YOTE YA KUIADHIMISHA PASAKA KWA KIYAHUDI, TARATIBU ZIPO KATIKA SURA HIYO YOTE
YA 12 (NA MAELEZO MENGINE YOTE YAPO KATIKA MISHNA NA GEMARA). MTUME PAULO KWA UFUNUO ANAMFANANISHA YESU NA YULE MWANAKONDOO WA PASAKA, NAYE AMECHINJWA KWA UKOMBOZI WETU, NAAM YEYE NDIYE PASAKA WETU (1KOR 5:7-8).

*MUHIMU:*
UKRISTO SIO DINI YA KIYAHUDI (JUDAISM)
INGAWA ULIANZA KAMA SECT(DHEHEBU) NDANI JUDAISM.

*_JE! PASAKA NI EASTER?_*
KOSA KUBWA SANA NI WATU KOKOSA MAARIFA, NA KUSEMA TUNASHEREHEKEA EASTER. EASTER SIO PASAKA NENO EASTER NI LA KIINGEREZA LIMETOKANA NA JINA "ISTHAR", THE BABYLONIAN GOD OF FERTILITY, MUNGU WA UZAZI WA BABELI. NDIO MAANA MAPAMBO YA EASTER HUKO ULAYA NI MAYAI NA SUNGURA,  EITHER PICHA AU VITU VILIVYOTENGENEZWA KWA PLASTICS AU RUBBER.

JARIBU KWENDA GOOGLE-IMAGES TAFUTA
"EASTER ORNAMENTS" UTALETEWA MAPAMBO YA EASTER NI MAYAI NA SUNGURA. SASA MAYAI AU SUNGURA HAYANA UHUSIANO NA IMANI YA UKRISTO. MAYAI YAMETAJWA KTK BIBLIA, LAKINI OCCASIONS CHACHE TUU ZA MAANA NA SIO KWAMBA YAMEHUSIANISHWA NA IMANI. BISHOPS WA KARNE YA TATU WALIPOONA KUNA SHEREHE ZA KIPAGANI WAKAONA NI HERI HIZO TAREHE WAACHANE NA ULE UPAGANI WAAZIMISHE MATUKIO MUHIMU YA UKRISTO (KWA KUWA MTAWALA KOSTANTITO ALIKUW AKIJARIBU KU-SYCHRONIZE MAMBO YA DINI ZA KIPAGANI YA RUMI NA UKRISTO AMBAO AMEAMUA KUUKUBALI, ANATAFUTA HARMONY KWA KUTAKA KUUNGANISHA VYOTE. IKUMBUKWE THE GREGORIAN CALENDER REPLACED THE JULIAN CALENDAR, NA NDIYO ITUMIKAYO DUNIANI KOTE KWA NAMNA NYINGI, HATA WALE AMBAO WANAZO KALENDA ZAO ZA KIDINI, BADO WANAITUMIA (Ilitengenezwa under Catholic Priest, Father Greogory, Lakini haijaifanya kuwa ya Kikristo). NB:- UFAFANUZI WA KINA KUHUSU MAMBO YOTE YA KALENDA, UPO KATIKA SOMO LANGU LA KRISMASI, JITAHIDI ULISOME. NITAFAFANUA CHINI KIDOGO INASHEREHEKEWAJE SASA?
PASAKA YA WAYAHUDI NI TAREHE 14 MWEZI
NISANI, IKUMBUKWE KALENDA YA WAYAHUDI MUNGU ALIIFANYIA AMENDMENT WAKATI ANAWATOA MISRI (KUTOKA 12:2), ALIWAAMBIA HUU UTAKUWA MWANZO WA MIEZI KWENU. KUMEKUWA NA HOJA AMBAZO NI MATOKEO YA KUTOELEWA MAMBO. JEWISH CALENDAR NA GREGORIAN CALENDAR HAZIFANANI KWA LOLOTE!
THE TIME WATU WATACHANGANYIKIWA NI PALE MNAPOTAKA KUITAJA UKIWA UNATUMIA HII GREGORIAN CALENDAR!. ANAYETAKA KUELEWA ASOME HAPA, WIKI ILIYOISHA TAREHE 25 (INGAWA JUMAPILI NI SIKU YA KWANZA YA JUMA NAIWEKA HIVI NISICHANGANYE WAZO JINGINE), ILIANZA TAREHE 19, YAANI 19 MARCH 2018. TAREHE HIYO KWENYE CALENDAR YA KIYAHUDI ILIKUWA TAREHE 27
ADAR 5777, KALENDA YAO INA SIKU 30 MIEZI YOTE. SASA HUO MWEZI WAO ADAR NI WA MWISHO KTK KUHESABU TOKA MWEZI NISANI. MWEZI NISANI/ABIB WA KIYAHUDI NI WA KWANZA, LAKINI KWENYE GREGORIAN
CALENDAR,TOFAUTI YA MIEZI MITATU ILITOKANA NA MUNGU KUWAAMBIA WAISRAEL "HUU UTAKUWA MWANZO WA MIEZI KWENU" WAKATI ILIKUWA MWEZI WA TISA/KUMI (SEPTEMBER/OCTOBER--KISLEV/TEVET). SASA WANAOTAJA 14 NISANI KUWA NI PASAKA, HAPO SIO JANUARY, MNAPASWA KUONGEZA MIEZI MITATU ILI KU-MATCH NA CALENDAR ZENU MLIZOBANDIKA SITTING ROOMS.


NB:- WAKATI HUO HAKUKUWEPO NA HIZI CALENDAR ZINGINE (JULIAN CALENDAR WALA GREGORIAN CALENDAR).

Pitia hapa

_*1st of Abib and the beginning of the Biblical calendar made by our Heavenly Father. The month of Abib/Aviv does not coincide with a month in the standard western calendar in any way. This means that the 1st day of the Biblical Year could fall on any day in the season of March/April. The biblical calendar is not one which is set in paper, but which is set in the heavens. When our Creator made the Sun, Moon & Stars, He proclaimed “let them be for signs and for seasons, and for days and years”.*_

WALE BISHOPS WALIO ''SWAP'' ILI KUONDOA SIKUKUU ZA KIPAGANI, WALIZINGATIA HILO. NDICHO WALICHOFANYA MWAKA 368 A.D KUHUSU 25 DESEMBA YAANI KRISMASI, MAADHIMISHO YA ISTHAR FELL IN THE MID APRIL, INGAWA INATOFAUTIANI NA HATA KUANGUKIA MARCH MWISHONI. KILICHOLENGWA NI YALE MAJIRA. MNAWEZA KUCHANGANYIKIWA
MTAKAPOKUTA CALENDAR YA KIYAHUDI
WAMEIMECHISHA NA SECULAR LAKINI YAO
SIKU ZA MIEZI INAKUWA TOFAUTI NA HII YA KAWAIDA.KUIDOWNLOAD TU GOOGLE STORE..

*JE NI UPAGANI KUSHEREHEKEA KUADHIMISHA PASAKA?*

NDUGU WAPENDWA WAPO WANAONA SI VYEMA, NA WAPO WANAONA NI VYEMA ULIMWENGU UKUMBUSHWE KILA MWAKA, KUWA YESU ALIZALIWA, ALIKUFA KWA MAUTI YA MSALABA NA KUFUFUKA. HAKUNA HAJA YA UGOMVI WALA KUHUKUMIANA. ANAYEONA HAIFAI AACHE, NA
WANAOONA VYEMA, WAADHIMISHE. HAKUNA UPAGANI MAANA KATIKA SECULAR KALENDA EASTER NI SEASONS NA SIO KUMWABUDU MUNGU WA UZAZI WA BABELI, NDIO MAANA WAKRISTO KWA MAJIRA HAYO HATUPAMBI MAYAI NA SUNGURA, WALA HATUFANYI LOLOTE LILILOKUWA LIKIFANYWA NA WALE WAPAGANI. BALI TUNAITANGAZA KWA WAZI MAUTI NA KUFUFUKA KWA YESU, TUKIJIDHILI KWA KUFUNGA NA KUOMBA MAJIRA HAYA YA PASAKA. KUNA WANAOSEMA PASAKA NI MEZA YA BWANA, HIZI NI DOCTRINES TOFAUTI ZA MADHEHEBU HATUWEZI FANYA WABADILISHE. MFANO MEZA YA BWANA MITUME NA WAKRISTO WA KWANZA WALIIFANYA REGULARLY KILA WALIPOKUTANA, NA JE NDIVYO INAVYOFANYWA KATIKA MADHEHEBU YOTE?KILA MKIKUTANA MNASHIRIKI MEZA YA BWANA? NA KAMA NDIVYO MBONA INATOFAUTIANA NA MAANA ILE YA PASAKA YA TAREHE 14NISANI, AMBAYO INAANGUKIA TAREHE FULANI ZA MWEZI WA TATU/NNE?. NA HAYA MAANDIKO MATH 26:1-2, MARKO 14:1, LUKA 2:41-41, YANAONESHA MAJIRA YA PASAKA YA KIYAHUDI NDIYO MAJIRA YA PASAKA YA KIKRISTO. YESU ALIPOKUJA ALISHIRIKI YOTE KWA TARATIBU ZA KIYAHUDI SIO ZA KIKRISTO. AMBAPO UKRISTO ULIKUJA KUWA DINI KAMILI HUKO MBELE YESU AKIWA AMEONDOKA KITAMBO. WAFUASI WA YESU WALIITWA WANAFUNZI WA YESU, BADAE WAKRISTO (MDO 11:26).

*IKUMBUKWE:*
CHRISTIANITY IS NOT THE JEWISH RELIGION, THOUGH IT BEGAN AS THE SECT WITHIN JUDAISM. WANAOTAJA TAREHE 14 NISANI, HIYO NI TAREHE NGAPI KWA KALENDA TUNAYOITUMIA?... TOFAUTI YA MIAKA TANGU AZALIWE YESU MWAKA (4BC) LEO NI MWAKA 2018, LAKINI HUU NI MWAKA WA 5777 WANAUINGIA MWAKA 5778  KWENYE KALENDA YA WAYAHUDI, NA NI MWAKA WA 1437 KWA WAISLAMU.
IT IS THE CONTENT THAT COUNTS!

Mwl Proo 0762879363/718922662

alltruth5ministries@gmail.com

Originally ©2015, it has been edited to fit current usage

No comments:

Post a Comment