Saturday, December 9, 2017

KUNENA KWA LUGHA MPYA

*KUNENA KWA LUGHA*

Ufafanuzi by Mwl Proo

Kunena kwa lugha/kuomba ktk Roho
>Kunena kwa lugha kuna upinzani mkubwa juu yake, lakini hii ni ​sponsored version​ ya kuijenga nafsi bila gharama (1Kor 14:4)
>Kuomba ktk Roho sio lazima useme kwa lugha za rohoni, unaweza omba kwa lugha za wanadamu ila utagundua kuwa frequencies zimebadilika,mpangilio wa maneno umebadilika, uvuvio upo sio wa kawaida

Verse 39............  ​Wala msizuie kunena kwa lugha​

Verse 18
​Namshukuru Mungu nanena kwa lugha zaidi ya ninyi nyote​

​AINA 3 ZA KUNENA KWA LUGHA​

A.Kunena kwa lugha mpya ambapo mtu unasema tu na Mungu,yaani roho peke yake inaomba (1Kor 14:14,2)
Hii haihitaji hata kutafsiriwa, hata mwenye karama ya kutafsiri huwa hatafsiri hii

B.) Kunena kwa lugha ambapo kuna ujumbe wa watu ila umekuja kwa lugha za rohoni, inahitaji karama ya kufasiri
1Kor 14:5,13,27
1Kor 12:10,30

C. Kuna kunena kwa lugha ambapo, Mungu anataka kukutumia kusema  na watu wa lugha usizozijua, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, unaiongea lugha ya hao watu na unaweza kuwa wewe muongeaji/mnenaji huelewi, ila wao watasikia kwa lugha zao na kupata ujumbe wa Mungu
Mdo 2:7-13

Hili kwangu limetokea mwaka juzi, niliamka kuomba usiku saa nane, binti mmoja kutoka South Africa, alikuwa macho chumbani kwake, akasikoa naomba kifaransa, na akawa anaelewa yote ninayotamka. Lakini mimi sifahamu kifaransa zaidi ya salamu tu

NB:-
Nashawishika ktk siku ya Pentekoste walijaliwa aina hizi zote ikiwa ni introduction of the New Era "New season of the Spirit" na hii haijakoma hata sasa.

ANGALIZO

EPUKA WABABAISHAJI, WANAOINUKA KUCHALENJI MAMBO YA KIROHO, AMBAYO WAO KWAO HAYAJAWATOKEA (DUE TO UNBELIEF), WANAKOSOA ILA WAO, HAWAONESHI HIYO HALISI IKO WAPI?, HAWA NDIO NIMEWAITA WATAABISHAJI KATIKA LILE SOMO LANGU LA  "MWILI NI WA KRISTO" (JITAHIDI ULIPATE, ILI UWANASE, HAWA WATU WASIO NA ELIMU WASIO IMARA WANAOPOTOSHA MAANDIKO (2PETRO 3:15-16)

0762879363

No comments:

Post a Comment