Sunday, December 17, 2017

KIROHO(UKIROHO); TABIA MUHIMU (KWA MWAMINI)

*SPIRITUALITY, AN IMPORTANT VIRTUE*
_Na Mwl Proo_
0762879363
0718922662

_KIROHO(UKIROHO); TABIA MUHIMU (KWA MWAMINI)_

*Ni mtu wa rohoni (aenendaye kiroho) ndiye mwenye kiroho
Gal 5:16,25
*Huwezi kuwa mtu wa rohoni kama hujajazwa Roho Mtakatifu
Rumi 8:9,14

AINA MBILI ZA WATU WANAOONEKANA KTK ULIMWENGU WA ROHO
*Katika ulimwengu wa roho wanaonekana watu wa aina mbili
i.)Watu wa rohoni
ii.)Watu wa mwilini/dini (Carnal people)
*1Korintho 2:10-16*

10 Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.
11 Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu.
12 Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu.
13 Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni.
14 Basi *mwanadamu wa tabia ya asili* hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.
15 Lakini *mtu wa rohoni* huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu.
16 Maana, Ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo.

*MTU WA ROHONI*
>Amejaa Roho
>Amezaliwa kwa Roho
>Anaishi kwa Roho
>Anayaangalia mambo kwa mtazamo wa kiroho

*MTU WA MWILINI/DINI*
>Anaufuata mwili/dunia(Yuda 1:19)
>Hajabadilishwa(The Unregenerate-mind/spirit)

*NB:-*
*NI MUHIMU KUKUMBUKA HILI,MATENDO YA IBADA/DINI ,HAYAMFANYI MTU KUWA WA KIROHO*
Luka 18:10-12

*ANAKUAJE MTU WA KIROHO*
>Yako mambo ya msingi yanayoweza kumfanya mtu wa kiroho,na mengine yote yatajengwa juu ya haya,iwe yale matendo ya ibada/dini yatafaa kama mtu amepitia hapa

*A.) MTU AKUTANE NA MUNGU BINAFSI (PERSONAL ENCOUNTER WITH THE LORD)*
Watu tunaowasoma ktk maandiko kama Henoko(Mwanzo 5:22),Ibrahim(Mwanzo 12:1ff),Yakobo(Mwanzo 28:12-25),Yusufu(Mwanzo 37:5ff),Musa(Kutoka 3:1-15),Samwel(1Samwel 3:1-10),Daudi(Zaburi 73:17),Eliya,Elisha,Isaya(Isaya 6:1-6),Ezekiel,Daniel

Hawa watu wana historia nzuri ya kuwa watu wa rohoni,of which haikutokea automatically,KUNA WAKATI WALIKUTANA NA MUNGU KIBINAFSI NA HIYO *_ENCOUNTER_* IKAFANYA WAWE WA ROHONI

*B.) MTU AWE AMEFANYA MAAMUZI THABITI YA KUWA WA KIROHO
*_Chagueni hivi leo........_* (Yoshua 24:15)

I WAS ONCE A RELIGIOUS PERSON,BEFORE THAT PERSONAL ENCOUNTER  WITH GOD,ILIYOFANYA NISIWE TENA MTU WA TABIA YA ASILI BALI MTU WA ROHONI

*SIFA ZA MTU WA KIROHO(Life experience of a spiritual person)*

>Mtu wa rohoni anajua njia za Mungu,siri za Mungu na anaelewa mambo ya kiroho *Zaburi 25:14,103:7*

>Hawezi ondoa alama za mipaka ana maintain standards kama mtu wa kiroho,kuna mambo hawezi fanya,kuna mahali hawezi kwenda,kuna maneno hawezi kutamka etc ni kwa ajili ya ule ukiroho wake, *Mithali 22:28*

>Anazingatia mambo ya kiroho(including matendo ya ibada/dini)

>Lazima atakuwa na misimamo (kama kuacha mambo ambayo wengine wanayashika) ili kuwa na maisha *distinctive* maana yeye yuko sensitive kujua kitu gani kinamtoa kwenye ukiroho wake kwa haraka

>Mambo matukufu,yanayoleta uwepo,ndiyo shauku yake kuuya wakati wote (Zaburi 1:2)

>Kwake utakatifu ni wito,na hivyo utakatifu sio *seasonal behaviour*,kwamba akiwa mazingira mageni,watu hawamfahamu then aanze ku-misbehave,No👐🏽

>Anadumu daima kwenye huduma

*FAIDA/HASARA ZA KUWA MTU WA ROHONI/DINI*

>Ni mtu wa kiroho pekee ndiye aliyefika kwenye kiwango cha juu kabisa cha kuwa *_salama_*
(Hata kama kuna mambo ya maisha haya amemiss
,yeye sio mtu wa kawaida) hawezi kuguswa (1Yoh 5:18) and its vice versa is true

>Ni watu wa kiroho ndio watakaoenda mbinguni wakati wa unyakuo

>Hatapitwa na baraka za kimungu,kila Mungu akitembelea watu wake,yeye lazima aguswe (Mithal 10:6.2Kor 6:17)

>Analindwa na maanguko ya dhambi
Hata kama kuna shambulio la anguko kwa njia ya dhambi,ambalo adui ameliandaa,Mungu atainua watu wa kukuombea,na kutuma mjumbe wa kukujulisha uchukue tahadhari

>Mambo ya Mungu huwa halisi kwake,hivyo *hatachoka* kiroho. Na hata wakati akishindwa,au ahadi ya Mungu ikaonekana kukawia,anapewa ustahimilivu.

MUNGU AKUPE NEEMA YA KUWA MTU WA ROHONI,AMUA SASA,UKIONA BADO UNABABAISHA KIROHO BASI BADO HUJAWA WA KIROHO,LAKINI UNAYO NAFASI YA KUCHAGUA KUWA MTU WA ROHONI.

*_#team kukaa ndani Yesu#(Yohana 15:1-7)#_*

alltruth5ministries@gmail.com

for inquiries/spiritual help (whatsapp only 0762879363)

No comments:

Post a Comment