Saturday, December 9, 2017

SYNOPTIC GOSPELS

*MSIGISHANO KATIKA INJILI ZINAZOFANANA*
_*Controversialities in Synoptic Gospels*_

*MWL PROO*
*0762879363*
*0718922662*

Shalom Aleichem
Bwana akubariki unayefuatilia masomo haya, karibu tujifunze zaidi. Ni heri uyapate maarifa haya mapema kabla changamoto haijakukuta, na uweze kuwa tayari wakati wote kujibu wale wakuulizao juu ya tumaini lako (1Petro 3:15)

*BILA SHAKA KATIKA USOMAJI WAKO WA AGANO JIPYA, HUSUSANI INJILI, ULIKUTANA NA TAARIFA ZINAZOSIGANA (DIFFERENT REPORTING) KWA VISA VINAVYOFANANA, HIVYO FUATILIA KUJUA SABABU, UFAFANUZI NA  SULUHU YA JAMBO HILO*

Injili tatu za mwanzo yaani Mathayo, Marko na Luka zinatambulika kwa jina la *Synoptic Gospel/Injili za kufanana*, neno hilo *Synoptic/  Συνοπτικός limeungwa na maneno mawili ya kiyunani yaani σύν/syn na  ὄψις/opsis-optic, ikiwa na maana ya "Seen together", yaani zikiwekwa kwa pamoja zinaonekana kufanana na kuonekana sawa, ambapo injili iliyoandikwa na Yohana imeondolewa hapo, maana haifanani na hizi nyingine, kuna tofauti kubwa ya matukio, nyakati (chronological discrepancy), muundo, maeneo yanayotajwa na kadhalika.*

*_KUNA BAADHI YA MAENEO, KUMEFANANA KAMA YAMEHAMISHWA TU (COPY AND PASTE). FUATILIA MAFUNGU HAYA MATATU......_*

📣FUNGU "A"
Mathayo 19:13-15
Marko 10:13-16
Luka 18:15-17

📣FUNGU "B"
Mathayo 22:23-33,
Marko 12:18-27
Luka 20:27-40

📣FUNGU "C"
Mathayo 24:4-8
Marko 13:5-8
Luka 21:8-11

_*UFANANO WA MPANGILIO/ORDER, FUATILIA HAYA MAFUNGU MAWILI.......*_

📣FUNGU "D"
Mathayo 16:13-20:34
Marko 8:27-10:52
Luka 9:18-51

📣FUNGU "E"
Mathayo 12:47-13:58
Marko 3:31-6:6a
Luka 9:19-56

Kwa chapisho hili, haitatosha kueleza yote kama ule ufano wa taarifa za ziada (Paranthetic material/ extra information) kama zile za kwenye mabano *"Asomaye na afahamu..... etc"* na ule ufanano wa mwandishi kufafanunua kwa kunukuu Agano la Kale (O.T quotations)

*BAADHI YA KUSIGISHANA KWA MAELEZO YA VISA SAWA*

🔭KISA CHA NCHI YA WAGERASI
Mwandishi  Mathayo, anaeleza kisa ambacho ni wazi ndicho kimeelezwa na Marko na Luka, ila wamepishana maelezo.
Mathayo 8:28ff, Marko 5:1ff na Luka 8:26ff, Mathayo anasema kulikuwa na wagerasi wawili wenye pepo, ambako Marko na Luka wote wanasema alikuwa mmoja, hatuwezi kabisa kuwaza kuwa ni visa tofauti, maana maelezo mengine ya tukio yote yako sawa kwa wote.

🔭KUNYAUSHWA KWA MTINI
Marko ameeleza kisa cha Yesu kuulaani mtini, na kwamba kesho yake asubuhi ndipo walipopita wakagundua umenyauka, lakini Mathayo anasema alipoulaani on the spot ulinyauka, na wanafunzi wakastaajabu ulivyonyauka mara (Marko 11:12-21, Mathayo 20:19-20).

🔭KISA CHA WANA WAWILI WA ZEBEDAYO
Mathayo 20:21/Marko 10:35, Wakati mwandishi Mathayo anaeleza kuwa ombi la Yakobo na Yohana waliombewa na mama yao mzazi, Marko anaeleza waliomba wao wenye, kwamba mmoja aketishwe mkono wa kuume na mwingine kushoto katika zama zijazo za ufalme ule.

🔭KISA CHA KUVIKWA VAZI WAKATI WA DHIHAKA KABLA KUCHUKULIWA KWENDA KUSULIBIWA
Waandishi wamepishana maelezo juu ya rangi ya vazi, Mathayo ambaye ni mmoja wa Thenashara kasema alivikwa vazi *JEKUNDU* (Mathayo 27:28), lakini Marko kaandika *ZAMBARAU*, rangi ambayo Mtume Yohana pia aliitaja (Marko 15:17,20, Yohana 19:2). Lakini tunajua kuwa Scarlet na Purple 🔯💗 hazilingani.

🔭KISA CHA KILIO CHA MSALABANI

Mathayo na Marko, wamepatana juu ya kilio cha Yesu, Cha *"Mungu wangu, Mungu wangu mbona umeniacha?"*, Kitu ambacho Luka sio kwamba amekiacha bali amekibadilisha (Mathayo 27:45ff, Marko 15:34ff, Luka 23:46.

🔭KISA CHA SAUTI WAKATI WA UBATIZO
Wakati Luka na Marko wakiripoti kuwa sauti ilimwambia Yesu mwenyewe kuwa, "Wewe ndiwe mwanangu mpendwa, nimependezwa nawe" (Marko 1:11, Luka 3:22), Mathayo anatueleza kuwa sauti iliwajuza wale watu wa halaiki, kuwa, "Huyu ndiye mwanangu mpendwa, ninayependezwa naye" (Mathayo 3:17)

HII NI MIFANO MICHACHE KATI YA MINGI INAYOONESHA KUSIGANA KWA TAARIFA, JE WOTE WAKO SAHIHI AU YUKO ALIYEDANGANYA? KUMBUKA THE TRUTH IS INDIVISIBLE, UKWELI HAUGAWANYIKI, KWA HIYO YUPO ALIYEELEZA KILICHOTOKEA, NA KINGINE SICHO. NILIWAHI KUULIZA SWALI HILI NIKIWA MDOGO KABISA, NILIJIBIWA KILA MTU ALIANDIKA KAMA ALIVYOONGOZWA, KITU AMBACHO SIO SAHIHI PIA.

*KWA NINI WALIFANANA, NA KWA NINI WALISIGANA KATIKA KURIPOTI MATUKIO?*
Biblia ni matokeo ya vyanzo vingine vya taarifa. Ni makosa makubwa kulazimisha kuamini kwamba uandishi wake ulitokana na watu kufurika rohoni huku wakibubujika ndipo wakaandika *(Kurohoisha kila kitu)*. Na kuna wakati hili andiko (2Petro 1:19-22 hutumiwa vibaya, wengine wakihisi huenda hawa watu walikuwa wanamsikia Roho Mtakatifu akiongea ndipo wakaandika, La Hasha! Kwa mfano Agano la Kale, ni matokeo ya kazi nyingine za uandishi wa kiyahudi (Jewish writings), yako mambo katika Agano la kwanza, ambayo yalitolewa katika vitabu kama Yashari, Kitabu cha tarehe za wafalme na kadhalika. Na kuna vyanzo mbalimbali ambavyo vilihifadhi habari za kwenye Biblia kabla hazijakusanywa, na vyanzo hivyo vilipelekea baadhi ya taarifa kuwa tofauti au kutajwa kwa majina tofauti. Vyanzo Sources) za Agano la Kale vilikuwa vinne vilivyopewa jina *JEPD*, Chanzo cha kwanza herufi J ni *YAHWIST/YAHWEH SOURCE* HIYO HERUFI "J" ILITOKANA NA TRANSLITERATION YA KIJERUMANI YA JINA YHWH. Chanzo cha pili ni *ELOHIST SOURCE*, Chanzo cha tatu ni *PRIESTLY SOURCES* na Chanzo cha nne *DEUTORONOMIST SOURCE*

Vyanzo vilileta tofauti ya taarifa hata katika Agano la Kale. Kwa mfano Baba mkwe wa Musa katika Yahwist Source ametajwa kama *Reueli*  (Kutoka 2:18), lakini katika Elohist source Bamkwe wa Musa ametajwa kama *Yethro* (Kutoka 3:1ff). Katika Yahwist source Mlima waitwa *Sinai* ndio ambao katika Elohist source unaitwa *Horeb*, Watu watokeao Palestina (Palestinians) wanaitwa *Wakaanani* katika Yahwist Source na wanaitwa *Waamori* katika Elohist source. Ndivyo ambavyo taarifa zilizohifadhiwa katika Injili zilipatikana zaidi kwa 1.Familia ya Yesu ya kimwili, 2.Watu wengine walioishuhudia huduma ya Yesu mwanzo mpaka mwisho. Katika uchambua kwa kina Injili hizi tatu za kufanana ilionekana ni mistari 55 tu ya Marko, ambayo haikutumiwa Mathayo, na Mathayo katumia 51% ya maneno halisi ya Marko. Luka ametumia 53% ya maneno ya Marko kama yalivyo, na katika mistari 55 ya Marko ambayoathayo hakuitumia, Luka alitumia mistari 24 katika hiyo. Kwa hiyo kati ya mistari 66 ya Marko ni mistari 31 tu ndiyo ambayo haijaonekana kwa Mathayo wala Luka. Na hivyo hukubaliwa kuwa *Marko* ndicho chanzo cha kwanza (Original source). Hii inathibitishwa na ukweli kwamba andiko lake Marko lilipatikana mapema 58 A.D, na Luka not earlier than 60 A.D, na Mathayo not earlier than 80 A.D yako madai mengine ya kupatikana mapema kwa injili ya Mathayo, lakini ni empty claims ambazo hazina uthibitisho wa vyanzo.

🎙 *DHANA YA VYANZO VIWILI*
(Two documents hypothesis)
Hapa inanenwa kuwa, kulikuwa na chanzo cha kwanza yaani Marko, na chanzo kingine kiitwacho *Q* imefupishwa kutoka kwenye neno *Quelle* la kijerumani ikiwa na maana ya source. Hivyo Luka aliandika akiwa na chanzo cha kwanza *Marko* ambako alipata mistari 606, na kutoka kwenye chanzo chake kingine *Q* alipata maneno 250, Mathayo aliandika akiwa na chanzo cha Marko na alitumia mistari     380 toka kwenye chanzo cha Marko na alipata Mistari 250 toka kwenye chanzo chake kingine *Q*

🎙 *DHANA YA VYANZO VINNE*
(Four document hypothesis)
Dhana hii inadai kulikuwa na vyanzo vinne, yaani Luka, Marko, Quelle "Q" na Mathayo. Hivyo Luka aliandika mistari 300 toka kwenye chanzo chake (L), mistari 606 toka kwa Marko (M), Mistari 250 toka kwenye chanzo Quelle "Q". Na Mathayo naye alikuwa ana chanzo chake Mathayo "M" alichotumia mistari 520, alitumia mistari 250 katika chanzo Quelle "Q"  na mistari 380 katika chanzo "M" Marko. Hivyo vyanzo binafsi ni vile ambavyo mtu either kwa kushuhudia au kuuliza kwa mashuhuda, mfano Injili ya Yesu kama ilivyoandikwa na Luka, sura ya 1&2 zinaitwa ni Injili ya Mariamu, maana inasimuliwa katika vyanzo vya kiyahudi kwamba Luka alikaa usiku kucha akimhoji Mariam maswali, ili apate taarifa hizo (Luka 1:1-3). Ili kufupisha stori leo sitazungumzia vyanzo fulani binafsi vinavyotupa dhana ya Mathayo pekee na Luka pekee (Proto-Matthew Hypothesis &Proto-Luke Hypothesis). Kwa hiyo kama tulivyoona hata Agano la Kale kuna baadhi ya mambo yameripotiwa tofauti kulingana na Sources husika, yako mambo ambayo waandishi hawa, waliyaeleza tofauti, *LAKINI MAANA HAIJABADILIKA*, Najua wako watakaosema Neno la Bwana ni fedha limejaribiwa kalibuni juu ya nchi, na kwamba limehakikishwa (Zaburi 12:6, Mithali 30:5-6). Sasa hapa napo tusijichange, haya niliyoeleza hayayafanyi maandiko haya kuwa sio ya Mungu, ila tunapaswa kuelewa tu huo uvuvio uko wapi, kivipi. Na ile kusema usiongeze wala kupunguza ilizungumzia nini?, maana kabla ya wale waliofunga (preclude) kuzuilia watu kuongeza (additions) tayari maandiko yalikuwa yamepitia kuongezwa na kupunguzwa, hayo nitayajadili wakati mwingine kuhusu kuiamua Biblia yaani *BIBLICAL CRITICISM* ambako ndani yake kuna kitu kinaitwa *REDACTION CRITICISM* inayohusisha *Add+Reduce*, Sio wengi wanaojua kwamba Mistari kwenye Agano jipya iliwekwa zaidi ya karne 11 badae tangu lilipokuwa *compiled*, na hata wengine watashangaa nikiwajuza kuwa Marko aliandika mwisho Marko 16:8, ila kuanzia Marko 16:9-20 ilikuja kuongezewa maana hakuwa ameimalizia vizuri Injili aliyoiandika, ila iliongezewa kwa utaratibu maalum kuwahusisha mashuhuda wa macho (eyewitness). Sasa kama nilivyosema, kile kolichokusudiwa na Mungu kuhusu neno lake lililoandikwa hakijabadilika, Mungu aliwatumia walioandika na waliokusanya maandishi hayo ili aunde chombo cha kibinadamu *Human tool*, ambacho kitamfunua Mungu jinsi alivyo, ambacho kitafunua mapenzi ya moyo wake, kitakachokuwa sauti yake ya wakati wote (Zaburi 103:20),  chombo kitakacho set standards, mwongozo wa kupambanua vyote, chombo hicho ni hili neno lililoandikwa katika Biblia, zile tofauti haziondoi ile sifa kuu ya kuwa Neno lilioandikwa katika Biblia liko *innerate and infallible*, lilionekana kuwa na sifa nne ambazo 1.Authentic, 2.Inspired, 3.Of divine authority 4.Genuine, kama nilivyozieleza katika somo lile liitwalo, *"JINSI YA KUITHIBITISHA BIBLIA KUWA NI NENO LA MUNGU" Jitahidi ulipate ulisome)*, Yako mambo mengine ambayo hayana utata, ila yakijadiliwa na watu wasio na ujuzi, huiwekea Biblia kwazo bure tu. Mfano nilikyta mjadala, uliohusiha injili iliyoandikwa na Marko na Yohana, jinsi walivyopishana muda wa Yesu kusulibiwa, Marko 15:25 inasema ni saa tatu, lakini Yohana 19:14 inaonesha ni saa sita. Hapo hakuna uongo bali watu walipaswa kupata uhesabuji wa masaa kwa mfumo wa kiyahudi na ule wa kirumi, ili kuelewa hayo. Kwa mfano katika agano jipya kuna maeneo 23 yaliyo-refer saa na muda kamili wa tukio, utakuta maeneo hayo, yametaja saa tatu, saa sita na saa tisa zaidi. Hiyo ilihusisha mifumo ya kuhesabu masaa kwa zamu nne. Sasa huenda tukio la Pilato kutoa hukumu na kusulibishwa kwa Bwana kulifanyika around 10:30am, So hatutarajii itajwe saa nne na nusu asabuhi, bali imeanguka kati ya saa tatu ma sita, hivyo kutaja saa tatu ni sawa na kutaja saa sita ni sawa kwa utaratibu ule wa kuhesabu muda uliotumika. Hivyo ndivyo ilivyo katika mambo mengi, BIBLIA HAINA UTATA (IT'S CLEAR ), ila inahitaji tu ujuzi kama huo, ili isipakaziwe makosa ambayo hainayo. Mungu akubariki kwa kufuatilia.

Kwa maswali,
Mwl Proo
0762879363
0718922662

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment