Monday, December 4, 2017

MAKAHABA WANATANGULIA MBELE YENU!

*_MAKAHABA WANATANGULIA MBELE YENU......_*

*ʍաӀ Թɾօօ*
*0762879363*

Bwana Yesu asifiwe sana! 😅

Leo sijafika kufundisha kwa kweli. Lakini kuna hoja inahitaji kupanguliwa, ili isiendelee kuvuma kama  mafundisho ya Hemenayo na Fileto, yenye tabia za kuenea kama donda ndugu (2Tim 2:17). Nasikia mara nyingi kauli za uongo, zisemazo, makahaba watatutangulia tuliookoka. *Wanatutangulia wapi??????*, What a lie!

*HILI NI MOJA YA MATATIZO MAKUBWA, YA KUHUBIRI VITU NJE YA MUKTADHA (OUT OF CONTEXT), KWA JINA LA UFUNUO (IN THE NAME OF REVELATION.* NAUNGA MKONO HOJA YA KUHUBIRI KWA UFUNUO HATA USIEGEMEA KATIKA ANDIKO PEKEE, MAANA PAMOJA NA BIBLIA KUKATAZA KUONGEZA (Ufunuo 22:18-19, Mithali 30:5-6), LAKINI INARUHUSU KUFAFANUSHA (Zaburi 119:130). LAKINI UNAPOFAFANUSHA, ISIWE KINYUME NA KWELI BALI SAWA NA KWELI, NA KWA AJILI YA KWELI.

Kuna watu, wakiona watu wana juhudi katika Bwana, wanawavunja moyo kwa kauli za uongo kusema, "Makahaba na walevi watatutangulia katika ufalme wa Mungu". Aku🤔, mnatumia Biblia gani labda??? Mlisoma wapi?? Nahisi mnatumia kimakosa hii hapa chini

Mathayo 21:31b

*_Basi Yesu akawaambia, Amin nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu._*

MAELEZO YANAYOTOLEWA NA WAHUBIRI HAPO, NI NJE KABISA YA MUKTADHA KIASI CHA KUPOTOSHA MAANA YA YESU. KATIKA KANUNI MOJA WAPO MUHIMU KATIKA KUFASIRI MAANDIKO (Hermeneutical principle), INATUTAKA TUFANYE JAMBO HILI, KUJUA HISTORICAL BACKGROUND, AMBAKO KANUNI HII, IMEMEGWA KATIKA VIPENGELE VIWILI, *_1.) History of the text, kisha 2.) History in the text._* KATIKA HAYA MAWILI, LA KWANZA NI GUMU KULIPATA MPAKA UFANYE *BIBLE STUDIES*, LAKINI LA PILI, LINAKUHITAJI TU KUANGALIA HIYO SENTENSI HAPO KULIKUWA NA KISA GANI, NANI ALISEMA, ALIMWAMBIA NANI NA KADHALIKA. SASA KAULI HII, YESU HAKUWAAMBIA WANAFUNZI WAKE, WALA WAYAHUDI WALIOMWAMINI. BALI HILI NI JIBU LA USHINDANI, KUWASHUSHUA WAKUU WA MAKUHANI NA WAZEE WA WATU. MAANA WALIONA KAZI ZA YESU, WAKAZIPINGA. WAKAJA KUMHOJI KUSEMA, "UNAFANYA HAYA KWA AMRI IPI?". SASA, YESU ALIWAHOJI SWALI, WAKAKOSA JIBU, MAANA YOHANA AMBATIZAJI ALIKUJA KUHUBIRI TOBA YA KWELI, WAKAMGOMEA. YESU AKATOA MFANO WA WANA WAWILI, WALIOPOKEA AGIZO KWA BABA, MTOTO WA KWANZA ALIWAKILISHA MAKUHANI WALIOONEKANA KUMTII MUNGU, HUKU HAWAMFUATI, NA MTOTO WA PILI ALIWAKILISHA (MAKAHABA NA WATOZA USHURU), AMBAO WALIPOSIKIA TOBA, WALIKIMBILIA YORDANI KUBATIZWA ILI WAONDOLEWE DHAMBI. KWA HIYO YESU ALIWAAMBIA HAWA WENYE VIBURI KUWA MAKAHABA NA WATOZA USHURU, WANAWATANGULIA MAKUHANI WALIOSHUPAZA SHINGO ZAO, MAANA WALIKIMBILIA TOBA ILE ILIYO HUBIRIWA NA JOHN THE BAPTIST. TUSOME;

MATHAYO 21:31b-32

*_Basi Yesu akawaambia, Amin nawaambia, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu._*
*_Kwa sababu Yohana alikuja kwenu kwa njia ya haki, ninyi msimwamini; lakini watoza ushuru na makahaba walimwamini, nanyi hata mlipoona, hamkutubu baadaye, ili kumwamini._*

*HOJA KAMILI*

Ni utoto, na ni ujinga, kuamini kuwa watu waliokwisha kuamini hawana thamani. Kusema Yesu alikuja kwa ajili ya hao, na sio wenye haki. Mmesahau kwamba sisi wenyewe tumetoka huko?. Sasa vipi,ni kwamba Yesu watu anaowatafuta kwa gharama, akiisha kuwaleta zizini wanakuwa hawana thamani (disvalued)? Ile mifano ya Yesu, ya kuacha 99, kumtafuta mmoja aliyepotea, haina maana kwamba 99 have lesser value than 1, Absolutely Not!. Lakini ile ni lugha ya kichungaji, kwamba hapendi hata mmoja apotee. (2Petro 3:9).

Sasa mwana mpotevu (prodigal son) akifanyiwa favour na karamu, haina maana kawazidi wale waliokaa daima na Mungu (Always with God), hapana!!! Tusome;

Luka 15 : 27
*_Akamwambia, Ndugu yako amekuja, na baba yako amemchinja ndama aliyenona, kwa sababu amempata tena, yu mzima._*

☝🏽☝🏽☝🏽HAO NDIO WALE WATOZA USHURU NA MAKAHABA

Luka 15 : 29-30
*_Akamjibu baba yake, akasema, Tazama, mimi nimekutumikia miaka mingapi hii, wala sijakosa amri yako wakati wo wote, lakini hujanipa mimi mwana-mbuzi, nifanye furaha na rafiki zangu;_*
*_lakini, alipokuja huyu mwana wako aliyekula vitu vyako pamoja na makahaba, umemchinjia yeye ndama aliyenona._*

☝🏽☝🏽HUYU NDIYE YULE, MLOKOLE MWENYE JUHUDI NYINGI KWA MUNGU, AMBAYE ANATISHIWA MAKAHABA WATAMTANGULIA. JIBU LA BABA (MUNGU), NDILO LINATUPA KUJUA *VALUE* YA ALIYEKAA NA BWANA DAIMA, NA YULE MWANA-MPOTEVU. THAMANI HATUIPIMI KWA KUCHINJIWA NDAMA ALIYENONA 🐄.

Luka 15 : 31
*_Akamwambia, Mwanangu, wewe u pamoja nami sikuzote, na vyote nilivyo navyo ni vyako._*

Tafuta nafasi umalizie na mstari wa 32. Huyu aliyeokoka thamani yake sio kuchinjiwa ndama, na kuvishwa pete, bali vyote vilivyo vya Mungu ni vyake. Tunapowatia moyo makahaba kwamba Bwana ana haja nao, sio kwamba Mungu anapendezwa na udhalimu wao la hasha.. Ni kwamba kuna ustahimili na uvumilivu wa Mungu bado unawavuta wapate kutubu, wasipofanya hivyo mpaka wakafa au kukatokea unyakuo, hawatakuwa na fungu tena katika ufalme wa Mungu... Wala hakuna kahaba atakayeamua sasa kutubu wakati wa dhiki kuu, wala injili ya Mizeituni miwili haitakuwa na kazi kwao kabisa...

1 Petro 3 : 20
*_watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji._*

Warumi 2 : 4
*_Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu?_*

HIVI NIWAHOJI WALE WANAOWAHUBIRI WATAKATIFU KUWA, MAKAHABA (WALE WANAOJIUZA SINZA KILA SIKU USIKU) WATAWATANGULIA KUINGIA MBINGUNI, LINI NA MBINGU IPI? SUPPOSE MCHANA WA KESHO KUKATOKEA UNYAKUO, WAO WATANYAKULIWA KWANZA????? AU NI VIPI SIWAELEWI!!! TUSOME HILI ANDIKO, HALAFU NIGONGE NYUNDO YA MWISHO 🔨🔨🔨🔨🔨.

1 Petro 4 : 18
*_Na mwenye haki akiokoka kwa shida, yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi ataonekana wapi?_*

*_SASA NADHANI HAPA IPO SAWA, WALE MAKAHABA KWAO KUNA UVUMILIVU TU WA MUNGU, ILI WATUBU, NASI TUMEPEWA NENO LA UPATANISHO (2Kor 5:18-19), ILI TUWAHUBIRI WAIJIE KWELI. HAKUNA KAHABA ATAKAYE HUSIKA KATIKA UNYAKUO, AKIWA NA UKAHABA WAKE, HAWEZI KUTUNGULIA, TULIOYAFUA MAVAZI YETU KWA TOBA YA KWELI, NA KUMTUMIKIA MUNGU KWA KICHO, DAIMA. HALAFU KAMA TULIOOKOKA, TUPO BIZE KUYACHUNGA MAISHA YETU, PAMOJA NA WOKOVU, PAMOJA NA KUACHA DHAMBI, TUNAANGALIA SANA JINSI TUENENDAVYO ILI TUUTIMIZE WOKOVU WETU. LAKINI BIBLIA INASEMA BADO TUTAOKOKA KWA SHIDA, SASA YULE ANAYEBWIA MADAWA YA KULEVYA, NA MBAKAJI, NA MKABAJI, NA MUUAJI ASIYETUBIA UUAJI WAKE, ATAONEKANA WAPI?_*

Sasa niwaombe wahubiri, hiyo kauli ya kutanguliwa na makahaba msiwahubirie watu waliojikana na kubeba misalaba yao kumfuata Kristo. Tafuteni vingozi wa dini wanaokana wokovu duniani, na wanadini ambao wanakiri ni wakristo, lakini wanakunywa pombe, wanazini, wanavunja ndoa,  wana michepuko, na bado wanakiri kuwa ni wanadini wafuasi wa Kristo. Hilo ndilo kundi sahihi litakalo reflect ile audiance/hadhira, ambayo Yesu aliwapa kauli hiyo, msiwatamikie wana wa Mungu hata kuwakatisha tamaa.

Asanteni, nimemaliza....

Mwl Proo... 0762879363

No comments:

Post a Comment