*ROHO MTAKATIFU*
_*Ruach Hakodesh*_
With
_*Mwl Proo*_
*0762879363*
YALIYOMO
I. Utangulizi
II. Mfahamu Roho Mtakatifu
III. Kazi zake kuu
IV. Roho Mtakatifu na roho saba za Mungu
V. Karama za Roho
*I. UTANGULIZI*
💎Tunaweza (wahudumu wa madhabahu) tukatengenza kundi la watoto (kiroho), au la watu wazima, kwa kile tunachotoa.
💎Kusanyiko la kanisa, sio la watu waliojiunga, bali *WAAMINI*
👉🏽Kuamini ndicho kinachokupa kuwa mmoja wa lile kusanyiko takatifu (Hatujiungi)
Mdo 8:37, 19:2, Marko 9:24
👉🏽MADARAKA/KIMO CHA CHEO, katika ulimwengu wa roho ni zao la mambo mawili, yaani
*KIWANGO CHA MAARIFA NA UFAHAMU WA ROHONI, NDICHO KINAAMUA UWE NA MADARAKA AU KIMO KIPI CHA CHEO ROHONI*
@Ukiwa mtoto (kiroho), huna tofauti na mtumwa {Galatia 4:4, 1Korintho 13:11}
💎Tukifundisha maarifa ya viwango (vya juu), sio kwamba tunapata wasiwasi, kwamba tutakuwa sawa, La hasha!
Bali tutatoa nafasi ya Mungu, kutupa ufunuo mkubwa zaidi unaolingana na kundi tunalolihudumia.
👉🏽Yesu ni mmoja (Yeye yule yule) Ebrania 13:8, lakini kiasi cha ufunuo wa Yesu, kiasi cha Yesu kujifunua au kujidhihirisha kwa mtu (Yoh 14:21b) hakiko sawa. Watu walioamini wanapaswa kuongezeka katika kumfahamu sana mwana wa Mungu (Efeso 4:13).
💎Kuna watu walipata ufunuo kidogo kuhusu Yesu, wakaishia palepale, hivyo wanatembea na ufunuo mdogo tu wa Yesu, mwana wa Mungu!
💎Wako watu ambao, Yesu alijifunua kwao kwa ufunuo mkubwa mno, Yesu ni yuleyule, ila kutenda kwao ni kwa viwango vya juu sana.
🇳🇧:-
*_Mungu alikusudia kusanyiko liitwalo kanisa, liwe "The most superior assembly", kwa njia ya Roho Mtakatifu, asiwepo mtu, watu, nguvu, falme, wala chochote (Luka 10:19, Efeso 3:10) kitakachoweza kuli-challenge (Mathayo 16:18-19)_*
💎Yako maarifa ambayo, huyapati tuu (you don't just get them), Ni mpaka cabinet/baraza la mbinguni lifanye shauri, na iruhusiwe kusema, *_"MFAHAMISHE MTU HUYU!"_* (Daniel 8:16, Yeremia 23:18, 22
👉🏽Kwa hiyo kuna ufunuo, unaweza kusikia kwa mtumishi fulani, ili nawe uende mbali kupitia alivyopokea.
MIFANO:-
👉🏽Sio wote ambao Mungu anaweza kuruhusu, wamwone mchawi "LIVE" ambaye yupo kiroho, maana maarifa machache, hayakupi kujua ufanye nini. Kwa hiyo Mungu anakusaidia kwa kukuficha, ingawa atakulinda usidhurike.
👉🏽Namna ya kushughulika na maadui kiroho, inahitaji ujuzi wa kiroho, na nafsi iliyojengwa haswa (Jitahidi usome somo langu, liitwalo *KUIJENGA NAFSI* ). Kuna siku ambayo nilitoka mkeshani (Mimi Mwl Proo), nilipojilaza tu nikaona mtu katika roho ananipuliza usoni. Na niliuhisi ule upepo mwilini, nami nilimpuliza mpaka nguvu zilipobalansi, akaacha.... Nikaona anabadili namna ya kushambulia, nikaamua kujiamsha (nilijikwatua miguu ili kuuamsha mwili wangu)
*TEKNOLOJIA YA ROHO MTAKATIFU IKO JUU SANA, INAPASWA HATA WACHAWI WAPIGWE BUMBUAZI, WAJE WASHANGAE, SIO KIWANGO CHAO, HAIPATIKANI KATIKA UFALME WANAOUTUMIKIA* (Matendo 8:9-25)
*Mwisho wa utangulizi*
💎Tusipowafundisha watu kwa kina, kuhusu Roho Mtakatifu, hatuwatendei haki*, Na kuwafanya wasipae katika viwango. Maana kwa Roho Mtakatifu sio kwamba wanapaswa waishie kiwango cha mhubiri, bali watu watapaa kwenye viwango walivyoandikiwa.
*SEHEMU YA PILI*
_*MFAHAMU ROHO MTAKATIFU*_
🕊Katika Yohana 14:16, Yesu anasema nami nitamwomba Baba, naye atawapa msaidizi mwingine.... ambayo katika kingereza tafsiri nyingi zimeandika *Another Comforter*, jina hilo linasomeka *ἄλλος παράκλητος yaani allos paraklétos* katika Agano Jipya la Kiyunani, likiwa na maana ya *Another of the same kind* yaani mwingine kama mimi. Na neno hilo *paraklétos* hutafsiriwa kama *one who is called to walk with you*, aliyeitwa kutembea nanyi.
🕊Katika Agano jipya majina haya yametumika yakimtaja Roho Mtakatifu kama separate entity, yaani kama nafsi ya Mungu, utakutana na Roho Mtakatifu, Roho wa Yesu, Roho wa Kristo, Roho wa Bwana, tofauti na ilivyo tafsiriwa katika Agano la kale kama roho ya Bwana, roho yako mtakatifu etc, sijaleta mjadala wa zile nadharia za Trinitarian na Anti trinitarian, nafundisha kuhusu Roho Mtakatifu kama nilivyoupokea ufunuo na ujuzi wa neno la kweli, nadharia pamoja na shule za mawazo hazifai kitu. wala hazikusogezi kwa Mungu wala kukuongezea kile kimo cha cheo rohoni.
🕊Kusanyiko la watakatifu baada ya ukombozi wa Kalvari, unatofautishwa tuu kwa njia ya Roho Mtakatifu (1Kor 6:17).
🕊Mungu aliahidi juu ya kusanyiko la wacha Mungu, kuwapa Roho yake (wake)
Yoel 2:28, Mdo 2:17
👉🏽Wala huyu Roho haji na kuondoka
Yohana 14:17
Huyu Roho anaweza kuwa
@With (Pamoja na)
@Upon (Juu)
@In (ndani)
🕊Huyu Roho, ambaye ni ahadi ya Baba (Luka 24:49, Mdo 1:4), ndiye mwenye jukumu la kuundaa mwili wa Kristo, kwa zama zijazo, ni huyu pekee, ndiye anayeweza kumfanya mwamini awe wa kumfaa Mungu kwa yote.
*SEHEMU YA TATU*
_*KAZI ZAKE KUU*_
⚙Kuushuhudia ulimwengu kwa habari ya dhambi, haki na hukumu (Yohana 16:8-9)
⚙Kuzaa kwa pili+kufanya upya (Rebirth and Renewal), Tito 3:5, Efeso 4:23-24, 1Petro 1:13-16, 1Yohana 3;9-10, 5:4, Yohana 3:3-7
⚙Anatufundisha kuomba, na anatuombea sawasawa na mapenzi ya Mungu
Warumi 8:26
👉🏽Yesu anatuombea (1Yohana 2:1), hata wakati hatuombi, Roho Mtakatifu anatuombea tunapoomba kwa Roho
⚙Anatufundisha na kutuwezesha kumwabudu sawasawa.
Yohana 4:22-24, 16:13-15, Zaburi 106:2
👉🏽Ibada sharti iwe na mtembeo wa kimungu, kama Roho Mtakatifu akihusika.
2Kor 6:17
👉🏽Akipewa nafasi atatembea, na wote mtajua nguvu zake zilikuwepo kwa dhahiri sio kwa hisia (Na atasema) *Jitahidi usome somo langu liitwalo "DALILI ZA ROHO NA ZA NGUVU"*
1Kor 2:4, 4:20, Mdo 4:31, 13:2
👉🏽Watu wanapaswa kuja kwa Mungu, wakiwa na shauku, sijui leo Mungu atatufanyia nini............?
NB:-
Mkibuni taratibu za kumkandamiza Roho Mtakatifu, anawaachia mwendelee, hana utaratibu wa ku-force, ila mkiwa na haja naye sana, anawajaza bila kipimo. (Yesu hamtoi Roho kwa kipimo) Yohana 3:34
⚙Anatupa kuwa na kiu ya kimungu, ambayo kwa asili ya mwili haipatikani.
👉🏽Mtu akiisha kujazwa Roho Mtakatifu anakuwa na kiu, shauku kuu ya kumtaka Mungu
@Petro aliyeshindwa kumpa Yesu sapoti ya kuomba nga lisaa limoja, akaanza kukaa mpaka siku tatu juu dari akiomba.
⚙Roho Mtakatifu anatupa nguvu na uwezo
Luka 24:49, Mdo 1:8
👉🏽Huwezi kutenda kazi kama Roho hayuko
👉🏽Huwezi kumshuhudia Kristo kwa nguvu kama hayuko Roho
Mdo 9:17-23
⚙Anatupa kujua hakika sisi ni wana wa Mungu. Pasipo kujazwa Roho Mtakatifu, na kuendelea kujifubza kuishi naye, mtu anacheza pata-potea "trial&error game".
Rumi 8:16, 14
⚙Roho Mtakatifu akijaa na kufurika, atamfanya mtu kuwa mwanana
2Timotheo 2:24
👉🏽Watu wote wataona una ladha, wanajisikia uhuru na amani kwa uwepo wako, kwa sababu, kuzama katika Roho Mtakatifu kunaondoa tabia za asili (matendo ya mwili) Galatia 5:19ff, Yule mtu wa tabia ya asili (man of unregenerate nature) anashughulikiwa
⚙Kwa njia ya Roho Mtakatifu, mambo ya rohoni yanakuwa halisi zaidi
Yoel 2:28, Yohana 16:13
Hakikisha unapata wasaa wa kusoma masomo haya hapa chini, yaliyoandaliwa na Mwl Proo
🍞 *Ufahamu Ulimwengu wa roho*
🍞 *Namna nyepesi ya kuzielewa ndoto*
*SEHEMU YA NNE*
*_ROHO MTAKATIFU NA ROHO SABA ZA MUNGU_*
Ufunuo 3:1, 4:5, 5:6
Isaya 11:2, Yeremia 10:12, 51:15
1⃣Roho ya Bwana
2⃣Roho ya Hekima
3⃣Roho ya Ufahamu
4⃣Roho ya Shauri
5⃣Roho ya Uweza
6⃣Roho ya Maarifa
7⃣Roho ya Kumcha Bwana
I. ROHO YA BWANA/SPIRIT OF THE LORD
Amu 3:10, 6:34, 11:29, Miak 3:8, Ezek 37:1, 11:5, Isaya 63:14
Hii inahusika zaidi na mambo kama
👉🏽Maongozi (Isaya 63:14)
👉🏽Nguvu (Amuz 15:14, 14:19, 14:6)
👉🏽Kutumiwa/Kutumwa
👉🏽Kusemeshwa (1Falme 22:24, 2Samwel 23:2)
👉🏽Inakujaza kuzuia roho zingine zisikuingie (1Samwel 16:14
II. ROHO YA HEKIMA/ SPIRIT OF WISDOM
(sio hekima ya mwilini 1Kor 1:26)
Kutoka 28:3, Kumbu 34:9, Efeso 1:17
👉🏽Mungu akiweka roho ya hekima ndani yako, ni uwezo maalum wa kuyatumia maarifa, ili kutenda mambo yote sawasawa.
Maarifa⏭Knowledge (Body of information )
👉🏽Uwezo wa kutumia maarifa, kwa nidhamu, kwa manufaa na kutatua mambo magumu yanayosimama kama kikwazo hiyo ni hekima.
III. ROHO YA UFAHAMU/UNDERSTANDING
Kutoka 35:30-35
Sofari Mnaamathi (Ayubu 20:3)
👉🏽Mtu aliyezaliwa upya, akajazwa Roho Mtakatifu, anapewa akili yenye kuelewa. Anaweza kuwa hakupata elimu ya kidunia/darasani, lakini ufahamu wake unakuwa juu (Dan 5:14, 12, 1:20, 9:22, Kolosai 1:9, 3:10, Filip 1:9
👉🏽Wayahudi wasomi waliushangaa ufahamu wa mitume maana wengi walikuwa ni *No school* Mdo 4:13/Mith 14:6, 2:1-6
IV. ROHO YA SHAURI/COUNSEL
Wana wa Isakari (1Nyakati 12:32)
Mdo 27:22, 1Kor 7:25, Ufunuo 3:18
Hii inahusisha *"The know-how, the know-what ability"*, pia kuna mashauri yasiyofaa kitu (Nahum 1:11)
V. ROHO YA UWEZA
👉🏽Tukiamini, tukajazwa Roho, tunakuwa na uweza (Efeso 1;19)
Roho ya uweza, inahusika na kutenda mambo/kazu ambazo haziwezekani kpaka kwa nguvu za kimungu (Supernatural power). Na karama nyingi za nguvu, zinahitaji roho ya uweza
Mdo 8:10, 11:28, 21:4, Luka 5:17
VI. ROHO YA MAARIFA
1Samwel 2:3
Maarifa kazi yake ni kukufumbua macho (Hesabu 24:16)
Kolosai 1:10, 2:3
👉🏽Ukimpokea Roho Mtakatifu, unaanza kupikea maarifa ya kimungu yaitwayo *"Gnosko"* kwa kiyunani, ambayo ni maarifa yatokanayo na ufunuo wa Roho Mtakatifu.
👉🏽 Huwezi kuwa mtumishi wa Mungu kama huna maarifa ya kimungu, kwa maana utashindwa kumwakilisha.
👉🏽Aina moja wapi muhimu katika maarifa haya ya kimungu ni aina ya *"Epignosis"* kwa lugha ya kiyunani, na maana yake ni utambuzi wa hali ya juu sana, na ujuzi halisi wa mambo ya kiroho.
Haya ni maarifa kamili na yaliyokamilika, hupatikana kwa kufanya tafakari na utafiti wa muda mrefu saba wa neno la Mungu katika anga la kiroho. Wenye maarifa ya Epignosis, huyajua mambo bila kukisia na kubahatisha, bali kweli wanayokywa nayo huwa ni halisi kabisa. Na wanakuwa na uhusiano mzuri na Roho Mtakatifu.
VII. ROHO YA KUMCHA BWANA
Fear of the LORD/Hofu ya Mungu
👉🏽Wanaozaliwa upya, na kupokea kipawa cha Roho, wao watakuwa na roho ya uchaji Mungu/Watamhofu Mungu
👉🏽Kumcha kwao Mungu, kunawafanya kuwa watu bora kila mahali, na katika kila jambo, Iwe kazini, shuleni, kwenye ndoa etc.
*SEHEMU YA TANO*
_*KARAMA ZA ROHO MTAKATIFU*_
👆🏽Credits to my Friend-Pastor Gaston Thadeo, huu mpangilio nitauweka kama alivyowahi kuufundisha yeye
1Korintho 12:7-11
Roho Mtakatifu anatoa vitendea kazi, kwenye offices ambazo Yesu amezigawa, na mwenye kazi yake ni Mungu Baba.
*MAKUNDI MATATU*
Karama za rohoni ziko tisa, ambazo huwekwa katika makundi haya matatu ili kuzielewa kwa wepesi
1⃣KARAMA ZA UFUNUO
i.)Karama ya neno la hekima
ii.)Karama ya kupambanua roho
iii.) Karama ya neno la maarifa
2⃣KARAMA ZA UWEZA/NGUVU
iv.) Karama ya imani
v.) Karama za kuponya
vi.) Karama ya matendo ya miujiza
3⃣KARAMA ZA USEMI/KUNENA/KUTAMKA
vii.) Karama ya unabii
viii.)Aina za lugha
ix.) Kufasiri lugha
I. KUPAMBANUA ROHO
1Yohana 4:1, 1Kor 14:29, Math 7:15, 24:24, Mdo 16:16-18
👉🏽Ufunuo wa moja kwa moja
👉🏽Kupambanua kupitia neno la Mungu
👆🏽JITAHIDI USOME SOMO LA MWL PROO, LIITWALO *ROHO ZIDANGANYAZO*
II. NENO LA MAARIFA
Hii ni karama ya ufunuo, inatoa taarifa ambazo ni siri (concealed), haziko wazi.
Luka 20:20-26
Yohana 1:47-50
*Utendaji wake*
👉🏽Kuletewa swala au tatizo kiuhalisia kwa kuliona👁🔭🔬au kubebeshwa hilo jambo husika.
📡UNAWEZA KUTAMBUA HATA MAWAZO YA MOYONI MWA MTU (Luka 3:15-16).
👉🏽Neno la maarifa (notification), inaweza kuja kama wazo, linalopachikwa ghafla likiwa limeingilia mtiririko wako
📡Inakuwa active zaidi unapoizoelea, hivyo uraelewa notifications za neno la maaeifa, ukizitofautisha na hisia zako.
📡Kuna umuhimu mkubwa wa kutofautisha hisia binafsi na notification ya kiroho (kwa sababu ya ya zile njia zinazotumika ujumba.
Mifano:-
Kuna siku nilikuwa napiga keyboard 🎹 muda wa maombezi. Dada mmoja hakufikiwa na waombezi ingawa alipita mbele. Ghafla nikasikia uchungu moyoni na mapigo ya moyo yameongezeka kwa kazi, nilipoinua uso, macho yangu yakamwelekea yule dada. Ila nilijua directly kuwa ninachohisi ndani, nimebebeshwa hali ya yule dada. Nilitoka kwenye kinanda, nikamfuata, kabla ya kumwombea nilimwuliza anajisikiaje, na alichonijibu ni kilekile nilichokihisi mimi.
III. NENO LA HEKIMA
Hii ni karama pacha ya karama ya neno la maarifa. Wakati neno la maarifa linafunua tatizo/swala lililofichika, neno la hekima linatoa solution, yaani inatatua tatizo.
Luka 3:15-17
1Falme 3:16ff
👉🏽Neno la hekima, linakuelekeza suluhu na hii haikaririwi, bali kila wakari katika kila tukio utajua cha kufanya
✍🏽Yesu alipotema mate chini kutengeneza tope
✍🏽Kumwelekeza Naaman akajichovye Yordan
✍🏽Nilipopata wazo la kumwelekeza mgonjwa aizunguke madhabahu, na akapokea uponyaji kamili
✍🏽Kumwaga chumvi kwenye chanzo cha maji ya nchi inayozaa mapooza
✍🏽Kutupa kijiti kwenye maji ili shoka ⛏ lipande juu kuelea
✍🏽Mauti sufuriani, jinsi Elisha Bin Shafat alipomwagia unga kwenye sufuria, kuiua sumu ya matango mwitu
Na mifano mingine mingi ya neno la hekima..., ambapo unaweza hata kutoa wazo litakalopelekea kutatu shida nzito
NB:-
*_LIKIKOSEKANA NENO LA HEKIMA, AU KUKARIRIWA, NDIPO TUNAPOANZA KYWA NA EXCESSIVE USE OF CULTIC OBJECTS, INABAKI KILA SIKU MAFUTA, KILA SIKU VITAMBAA, KILA SIKU KUOMBEA SABUNI, CHUMVI, MAJI, WAKATI HUO NI UFUNUO WA MARA MOJA UKITOKA UPATE UFUNUO MWINGINE KWA NENO LA HEKIMA_*
*KUNDI LA PILI NI KARAMA ZA NGUVU/UWEZA*
IV.) MATENDO YA MIUJIZA
V.) KARAMA YA IMANI
VI.)KARAMA ZA KUPONYA
✍🏽Ni ngumu sana kutofautisha karama hizi, kwani zinashirikiana na kuhusiana kwa karibu
✍🏽Mfano mtu anaweza kuponywa akasema Bwana amenitendea muujiza, hivyo tukashindwa kujua ni lini karama ya matendo ya miujiza imefanya kazi, na ni lini karama za kuponya, zimefanya kazi.
✍🏽Lakini kuna uwezekano wa kuzitenganisha; Mfano:- Yohana 12 (Lazaro kufufuliwa), karama ya imani, ya matendo ya miujiza ndizo zilizofanya kazi. Lakini karama za kuponya haziuhusika, maana Lazaro hakuwa mgonjwa.
✍🏽Lakini pia viwete, vipofu, vilema na wengine wasio na maumivu (magonjwa), tukisema kwamba karama za kuponya zimehusika, tunachanganya kiswahili. Watu wenye kansa, ukimwi n.k, wakipona ni karama za kuponya, na wale wengine viwete kutembea ni karama ya matendo ya miujiza.
✍🏽 Mara nyingi kama sio zote, karama ya imani haikosi, yaani kama ni karama ya matendo ya miujiza au karama za kuponya basi zitaambatana na hiyo ya imani, au zote tatu
NB:-
Na kuna wakati karama za mafunuo, huhusika moja kwa moja kukuwezesha huduma hii.
*KUNDI LA TATU, KARAMA ZA USEMI/KUTAMKA*
VII.) AINA ZA LUGHA
VIII.) TAFSIRI ZA LUGHA
👅Kuna kunena kwa lugha, ambako ni mwamini yeyote anaweza kunena (Marko 16:16-17), Lakini kuna karama ya kunena kwa lugha (aina za lugha), hii ni tofauti, hii ni karama anayoitoa Roho. kama apendavyo Yeye (1Korintho 12:29-30)
👅 Mtu akinena kwa lugha kama karama yake, kavuka viwango vya kawaida vya kunena. Anakuwa anafukua vitu/kitu katika ulimwengu wa roho, na Mungu anakywa anataka kusema na kanisa au mtu hali fulani. Na akiwepo mwenye kufasiri ile lugha basi kanisa. linafurahia hizo karama za rohoni na kujengwa.
👅 Na inaweza kutokea, mwenye karama ya kunena kwa lugha (aina za lugha), na yule mwenye kufasiri, wakabaki wameendelea kuomba, mmoja akanena na mwingine akafasiri.
IX. KARAMA YA UNABII
👅 Ni kosa kubwa kuchanganya nabii na unabii. Nabii ni ofisi/huduma, inayotolewa na Bwana (Efeso 4:11), lakini unabii ni karama tena ya kutamka inayotolewa na Roho.
👅Sio kila mwenye karama ya unabii ni nabii, ijapokuwa nabii akitabiri, pia huitwa unabii. Lakini mtu yeyote anaweza kutumiwa kwa karama ya unabii, akavuviwa hata temporarily, na kutoa unabii. Hii ni tofauti na ofisi ya nabii, ambayo mtu huwa hapo permanent na utendaji wake ni tofauti, na kwa uzoefu manabii wengi wanafanya kazi na zile karama sita za mwanzo, yaani za ufunuo na za nguvu, kuliko hizi za usemi/kunena.
Mbarikiwe kwa kufuatilia.
Mwl Proo
0762879363
0718922662
alltruth5ministries@gmail.com
Barikiwa sana Mwl kwa kazi njema ya Kuifundisha kweli ya Mungu
ReplyDelete