*FAHAMU USHINDANI ULIOPO ROHONI, UNAOATHIRI MAMBO YA HUKU MWILINI*
*_(Understand the wrestling in the spirit, with its effects in our corporeal world)_*
*Mwl Proo*
*0762879363*
Bwana Yesu apewe sifa zote! Mbarikiwe kwa jina la Bwana, mnapoendelea kumjua Mungu kupitia kweli hii. Katika somo la *VITA VYA ROHONI* (linapatikana mtandaoni), nilijadili kwa kina mambo ya vita katika ulimwengu wa roho, lakini bandiko (post) hili limeenda upande mwingine ambao sijawahi kuuzungumzia popote.
Katika utangulizi, nitatumia vyanzo vingi vingine hasa simulizi ya kiyahudi (Jewish literature lores/sages and some from pseudepigrapha). Nitatumia hivyo vyanzo kufundisha jambo ambalo liko katika Biblia (Ukiwa na swali kwa nini nimetumia, wasiliana nami nikueleweshe kabla hujayatupa haya, wala sio kwamba Biblia haijitoshelezi, ila kama nilivyofafanua katika somo langu la *WANEFILI*, ndivyo pia nimenukuu baadhi ya taarifa huko.
Post hii imejadili vitu vya kimalaika zaidi (it's more angelic), lakini imebeba mambo ya msingi kukusaidia. Matukio mengi yanayotokea kwenye maisha ya watu leo, mengi yameanzia rohoni, naam katika ushindani uliopo rohoni. Kuna baadhi ya vifo, ajali, kushindwa, maanguko ya kiroho, magonjwa n.k, vilitokea baada ya upande wa huyu mhusika kulemewa na kushindwa kule rohoni. Mungu hajawahi kushindwa, ila malaika wanahusika na mtu fulani wanaweza kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kiutetezi dhidi ya washtaki/maadui.
Kwa mfano mtu aliyeamini kabla hajaanguka kwenye uzinzi, kutakuwa na ushindani mkubwa unaojaribu kumtetea rohoni, na yeye atakuwa anahisi kutaabika, nafsini mwake atahangaika. Wakati wa huo ushindani, iko kambi ya adui, inayosukumiza anguko, na kutakuwa na upande wa malaika (roho wema wa Mungu), wakimshindania huyu mtu. Kama naye akitii maonyo ya Roho, akaomba wakati huo kwa juhudi, basi anautia nguvu ule upande wake, na malaika walioingia kumshindania watashinda na huyu mtu atavuka salama bila anguko. Kuna wakati unaweza usiombe wewe mwenyewe, Mungu anaweza akatia mzigo ndani ya mtu mwingine (muombaji), ili akuombee kuutia nguvu upande wako kama upande wako utazidiwa nguvu, ukashindwa basi hapo anguko halitaepukika, hutaamini kama ni wewe utauendea uzinzi kwa kasi mno, utajikuta unajiruhusu mwenyewe huku ukisema *_"Mungu samehe tu nitatubu, na utaendelea na tendo hilo huku ukiendelea kujihoji kwamba ni mimi kweli ndiye nafanya hili!!??"_* Shida ni kwamba upande wako ulishindwa kule rohoni (Hii najadili kwa mtu mwamini ambaye hakuzoelea uzinzi, kwa mzinzi mzoefu hakuna kushindaniwa bali anafigiwa tu) ....Yuko rafiki yangu alinisimulia, akiwa amelala usiku wa manane akaoneshwa binti fulani amelala kitandani, na aliona roho ya mauti imemfunikiza kwa juu. Akaamka muda huo na kukemea kwa bidii kuitoa ile roho. Asubuhi yake alipompatafuta akajuzwa juu ya hali ya kufa iliyomjia usiku, ilikuwa ni kifo kabisa, hakuwa anaumwa lakini mwili ulibadilika na alikuwa anakufa kabisa kwa kile alichojishuhudia mwenyewe. Tunalindwa na nguvu ya Mungu kwa njia ya imani. Iko mitego inakuwa imesetiwa rohoni, ila tunasuliwa na kuwa salama, na hasa tunaposimama kwenye zamu zetu bila kupotosha safu zetu. Kushindwa, kuanguka kunatokana mara nyingi na kushindwa katika ushindani wa kule rohoni.
USIJARIBU KUPUUZIA USHINDANI ULIOPO ROHONI KATI YA KAMBI YA MALAIKA WA MUNGU NA WA MSHTAKI MKUU (SHETANI)
Mambo yaliyokuwa yakitokea juu ya taifa la Israel mengi yalitokana na ushindani katika ulimwengu wa roho, kila unaposoma mabaya juu ya taifa la Israeli basi upande wao katika roho, ulishindwa, na sio kwamba walishindwa kwamba Mungu hana nguvu, lakini malaika husika hakuweza kutimiza majukumu ya kiutetezi, nitaeleza badae kidogo.
Wayahudi walitoka Babel na majina mengi ya malaika, lakini pia katika maandiko ya kiyahudi ya kale, yanataja malaika wakuu saba, kumbuka katika Daniel 10:13, Gabriel anamwambia Daniel kwamba akaja Mikael mmoja wa wakuu wasimamao mbele, kunisaidia. Hao wakuu tangu mwanzo ni hawa Anael, Gabriel, Mikaeli,, Raphael, Zakariel, Samael na Orifiel.
KATIKA DANIEL TUNAMWONA MKUU (PRINCE) WA WANA WA ISRAEL, AKISHINDANA NA MKUU WA ANGA YA UAJEMI, AKIWA AMEENDA KUMSAIDIA GABRIEL MAANA ALIKWAMISHWA KWA SIKU 21, AKISHINDWA KUVUKA.
Daniel 10 : 21
Lakini nitakuambia yaliyoandikwa katika maandiko ya kweli; wala hapana anisaidiaye juu ya hao ila huyo Mikaeli, mkuu wenu.
👆🏾MKUU WENU
Daniel 12 : 1a
Wakati huo Mikaeli atasimama, jemadari mkuu, asimamaye upande wa wana wa watu wako;.....
Shetani katika ufalme wake aliseti juu ya kila taifa malaika wake kama mkuu wa anga husika. Kwa mfano visa vingi vilivyotokea rohoni kuhusu Misri na Israel, ilikuwq ni ushindani kati ya malaika mpinzani aliyetawala anga ya Misri aitwaye Uzzah na Mikael. Mikael alikuwa ni prince of Israel na alikuwa in charge juu yao, akiwatetea wayahudi dhidi ya mshtaki wao (accuser) ambaye ni Samael, aliyeanguka toka kwenye utukufu wa Mungu, ambapo inaelezwa aliyashikilia mabawa ya mikael ili washuke wote; hili ndilo linakubalika na Rabbis (walimu wote wa kiyahudi), na majukumu hayo Mikael aliyaanza nyakati za mababa (Patriarchal era), uadui wa Mikaeli na Samael ulianza wakati ambapo barua ilianguka toka mbinguni, kama inavyoelezwa katika kitabu cha Henoko. Rabbi Eliezer B. Jacob anaeleza kwamba ni Mikael ndiye alimwokoa Ibrahimu alipotupwa na Nimrod kwenye tanuru la moto. Katika kisa cha Ibrahimu kumtoa Isaka, Biblia imeandika yale yaliyotokea pale katika ulimwengu wa mwili, lakini katika vyanzo vingine vya kiyahudi vimejadili mchuano mzito juu ya Mikael na Shetani (Samael), kwa wakati ule, ambapo Mikael alielekezwa kumpelekea Ibrahim mwanakondoo 🐑, lakini Shetani alimzuia kwa kumchelewesha ili Ibrahimu amwue mwanae (Haya yameelezwa katika kitabu mashuhuri kiitwacho Yalcut Reuben, Wayera session). Ni wiki mbili zimepita nilikuwa nikisoma kitabu kilichotajwa kwenye Biblia kiitwacho Yashari (Jasher), katika sura ya 23, kimeeleza kisa sawasawa na Mwanzo 22, ila kimeeleza kwa upana sana hatua kwa hatua, toka nyumbani kwa Ibrahim mpaka kufukia kule Mlima Moria. Njia nzima kulikuwa na vita ya waziwazi. Sitaeleza mambo mengi zaidi lakini kuna matukio mengi kwenye Biblia yalitokea yakiwa ni matokeo ya ushindani katika ulimwengu wa roho. Na hali ya dhambi pekee ndiyo inayoufifisha upande wako kuufanya ushindwe na upande wa adui/mshtaki. Awamu kadhaa malaika mtetezi aliwatetea waisrael wasiende utumwani, ila ile awamu ambayo walichukuliwa kwenda Babel, ilikuwa ni baada ya utetezi kushindikana. Mungu alimwambia Mikael, watu wako wamefanya dhambi. Mikael alijaribu kushawishi kwamba kwa kupitia watu wema wachache walioboki Israel, nchi yote iokolewe, lakini haikuwezekana, mashtaka yaliizidi haki (Katika Biblia utasoma habari za Nebuzaradani amiri wa jeshi la Nebukadreza, zama za Yeremia nabii, yapo yaliyofanywa na amiri huyu yalikuwa ni matokeo ya ushindani rohoni, na Israel kushindwa (Haya yameelezwa katika Yoma 77a Zohar col. 414)
*KILA MTU MWAMINI, ANA MALAIKA (Guardian angel)*
Mathayo 18 : 10
_*Angalieni msidharau mmojawapo wadogo hawa; kwa maana nawaambia ya kwamba malaika wao mbinguni siku zote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni*_
Waebrania 1 : 14
*_Je! Hao (malaika) wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?_*
Zaburi 34 : 7
*_Malaika wa Bwana hufanya kituo, Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa._*
Elimu ya kuhusu malaika, ni ndogo sana miongoni mwa wakristo wa mataifa (Gentile Christians), tofauti na Wakristo wayahudi (Judeo-Christians). Kuna malaika ambaye ni Guardian angel, huyu yuko kwa kila mwamini, yuko in charge, ingawa ni ukweli kwamba hakai kwao wakati wote, ni mhudumu tu... Na kunapotokea mambo yanayoashiria kuna vita inakujia si yeye peke yake atahusika kukushindania, bali vikosi vya kivita vya Mungu vitaachiliwa.
*VIKOSI (MAJESHI) VYA MALAIKA*
Malaika yule mhudumu, hausiki na mapigano, bali anaweza kuwa mjumbe wa kutoa taarifa kama una kabiliwa na mapigano, ili vikosi vije kukupigania. Idadi ya vikosi vya kukupigania, vitategemea na status yako kiroho, kimo cha cheo chako na hali yako na Mungu. Tukisoma katika Mathayo 26:53, Yesu anaongea kitu sensitive sana, kwamba au wadhani siwezi kumwomba Baba yangu akaniletea *SASA HIVI* majeshi 12 (kikosi cha malaika wa kupigana 72,000).
Kwa nini natumia sana neno upande wako, au upande wetu?
Tusome
2 Wafalme 6 : 16
*_Akamjibu, Usiogope; maana walio pamoja nasi ni wengi kuliko wale walio pamoja nao._*
Miongoni mwa visa mashuhuri vya ushindani wa rohoni ni hapa. Gehazi aliyaona yale majeshi yamezunguka kuwakabili tokea milimani. Lakini Elisha Ben'Shaphat alijua kwamba, yako majeshi ya giza yanayotenda kazi kwa kutumia jeshi la Shami la kimwili, lakini alitambua kwa wakati huohuo, kuwa majeshi ya Mungu yaliyoachiliwa kumtetea yeye yako mengi na kuwazidi nguvu yale majeshi ya giza. Ndio maana alipofunuliwa macho Gehazi aliyaona majeshi yenye magari ya moto yamemzunguka Elisha nabii. Bila kuchengesha, majeshi yale hayakuweko kwa ajili ya Gehazi, bali Elisha mwenyewe ndiye aliyekuwa na kimo kikubwa cha cheo rohoni, sio mwenye hofu na mashaka yule Gehazi. Kwa nini Jeshi la Washami, hawakuweza kumkamata Elisha, bali aliwapiga na upofu juu? Mafanikio yake yalitokea rohoni majeshi ya upande wake yaliyashinda yale ya giza. Wakati wa vita ya Israel na Yabini mfalme wa Kanaani, Debora na Baraka walishinda, kwa sababu vikosi vya malaika (nyota) vilipigana na vikosi vya kiroho alivyokuwa navyo Komando Sisera (Waamuzi 5:20), waliyashinda rohoni, huku nje Jemadari akabwagwa chini kwa kifo cha mbwa. Wakati wa vita vya wana wa Israel na Waamaleki, pale katika Kutoka 17, Musa alipoinua mikono 🙌🏽, aliyatia nguvu kwa kuomba majeshi yaliyopigana upande wa Yoshua dhidi ya ya majeshi yaliyosimama kiroho kuwakwamisha na safari kupitia taifa la Amaleki.
Mpendwa tambua kuwa, kuna ushindani mkali (hard wrestling) huko rohoni. Kama hutaishi kwa conscious hii, basi utakwama, utashindwa, utaanguka na kufa kama afavyo mpumbavu. Unaweza ukasimama sasa kama askari Bwana, hakikisha hautoi mwanya wa kambi ya adui kukushinda, usiruhusu dhambi kuyatawala maisha yako, ukoseapo kwa kufanya dhambi tubu mara moja na kuacha kabisa. Dumu katika kuomba (Pata muda ulirudie teba somo langu liitwalo *''KWA NINI KUOMBA"*, unapokuwa dhaifu kiroho, mwombe Mungu akusimamishe tena, hata wakati ambao utakuwa na udhaifu kiroho kushindwa kuvipiga vita vizuri, jitahidi usitende dhambi, kutoa nafasi ya malaika kufanya kufanya majukumu yao bila kushindwa. Jifunze kuwatumia malaika, kuwaagiza na kuwaelekeza, wao ni wahudumu wetu.
Mwl Proo
0762879363
0718922662
alltruth5ministries@gmail.com
No comments:
Post a Comment