*```TWEKA MPAKA VILINDINI```*
🇲 🇼 🇱 🇵 🇷 🇴 🇴
0762879363
0718922662
Haleluya!
Bwana Yesu Kristo asifiwe sana!🙋🏽
Leo Bwana kaweka Neno moyoni mwangu .Nalo ni hili
Luka 5 : 4
*_Hata alipokwisha kunena, alimwambia Simoni, Tweka mpaka kilindini, mkashushe nyavu zenu mvue samaki._*
PUT OUT INTO THE DEPTHS
Shetani na mawakala wake wote wanafurahia kuona tunabaki kwenye kina kifupi(shallower depth) ili waendelee kukufikia kwa kukuzuia kutoboza,kukukwamisha usifikie ukamilifu wa hatma na waendelee kukurudisha nyuma kila unapoonesha dalili ya kuinuka iwe kiroho,kielimu,kiuchumu etc etc
Farao alijua kwa wazi waisrael wakienda mbali sana(mpaka vilindini) hataweza kuwapata awatumikishe tena,hivyo aliwaruhusu waende ila anatoa conditionality kuwa msiende mbali sana:-
Kutoka 8 : 28
*_Farao akasema, Mimi nitawapa ruhusa mwende, ili mmchinjie dhabihu Bwana, Mungu wenu, jangwani; lakini hamtakwenda mbali sana; haya niombeeni._*
SASA HII CONDITION YA FARAO NDIYO HASA TABIA YA SHETANI NA WASAIDIZI WAKE,WANAWEZA KURUHUSU UFANYE MAMBO FULANI YA KIROHO LAKINI USIENDE MBALI SANA UBAKIE KWENYE SHALLOW-WATER ,USIFIKE VILINDINI WAKASHINDWA KUKUFIKIA.
KIPO KIWANGO KTK MAISHA YA KIROHO AMBAYO ADUI AKUCHEZEI TENA N KUKULETEALETEA MAANGUKO YASIYO NA MAANA AMBAYO HUTOKEA KWAKO IN *_CIRCULAR REPITITIONS_* YAANI EXACTLY ANGUKO ULILOANGUKA NALO MWAKA JANA(LIMEKUZONGA KWA UPESI) UMEANGUKA KWA LILELILE TENA,SABABU KUU NI NGUVU CHACHE(Mithali 24:10) ZINAZOTOKANA NA KUBAKI KTK KINA KIDOGO BADALA YA KUTWEKA MPAKA VILINDINI. MAJI KTK LUGHA ZA ROHONI/KINABII YANAWEZA KUASHIRIA ROHO MTAKATIFU,AU KAMA NI MAJI MAKUU/FLOODING YANAWEZA KUMAANISHA HATARI,MAJANGA NA MAJARIBU MAZITO,LAKINI MAJI YAKIWA KTK DEPTHS TOFAUTI YANAASHIRIA LEVELS ZA MAISHA KIROHO. KUNA WAKATI NILIENDA KUHUDUMU KWA NENO LA MUNGU MAHALI,ILA NILIFUNDISHA VITU VIKO JUU MNO KULINGANISHA NA UFAHAMU WA WATU,NILIPOTOKA HUKO ROHO AKANIONESHA KWENYE NDOTO,NIPO KWENYE KILINDI CHA MAJI NAWAVUTA WATU KWENYE KINA AMBACHO SIO SIZE YAO.
Tusome hapa
*Ezekiel 47*
*_3 Na alipotoka mtu yule, mwenye uzi wa kupimia mkononi mwake, kwenda masharikini, akapima dhiraa elfu, akanivusha maji yale; maji yakafika mpaka viweko vya miguu._*
*_4 Kisha akapima dhiraa elfu, akanivusha maji yale, maji yakafika mpaka magoti. Kisha akapima dhiraa elfu, akanivusha, maji yakafika mpaka viuno._*
*_5 Kisha akapima dhiraa elfu, yakawa mto nisioweza kuuvuka; maana maji yamezidi, maji ya kuogelea, mto usiovukika._*
KTK MISTARI HII HAPA JUU TUNA VIWANGO VITATU,BAADA YA YULE MTU(MALAIKA) KUPIKA DHIRAA ELFU ZA KWANZA(SHALLOW WATER) MAJI YALIMFIKIA KWENYE VIWEKO VYA MIGUU(FEET'S ANKLES) YAANI NI KIWANGO KISICHO NA KINA,NA WAKRISTO WENGI WANATEMBEA KTK MAJI YA VIWEKO VYA MIGUU AMBAPO MATENDO YA MWILI BADO YANA UDHIHIRISHO MKUBWA(GALATIA 5:19-21) UNAKUTA MTU KAOKOKA BUT ANA HASIRA HATARI(MHUBIRI 7:9) YAANI UKIGUSA TU ANAKUWASHIA MOTO WIKI TATU(EFES 4:26) TATIZO HAJAFUNIKIZWA NA YALE MAJI YAANI HAJATWEKA MPAKA VILINDINI KWA HIYO ANAOPARET KIMWILI ZAIDI.
KISHA YULE MTU(MALAIKA) AKAPIMA TENA DHIRAA ELFU MAJI YAKAFIKA MAGOTINI,LAKINI HAPO SIO MWISHO AKAPIMA TENA DHIRAA ELFU YAKAWA MTO ASIOWEZA KUUVUKA🏊🏽MAANA MAJI YAMEZIDI MAJI YA KUOGELEA NAAM MTO USIOVUKIKA🌊(VILINDINI)
NENO LA BWANA KWAKO NI HILI, *"TWEKA MPAKA VILINDINI"* KWA MAANA KUNA MAMVO YA KIROHO HUTAYAJUA,THERE IS A REALM OF THE SPIRIT YOU WILL NEVER OPERATE THROUGH MPAKA UTWEKE MPAKA VILINDINI,NA UTOKE KWENYE SHALLOWER DEPTH,
BIBLIA INASEMA KTK ZABURI 42:7
*_(NIV) DEEP CALLS TO DEEP_* Yaani kilindi chapigia kelele kilindi. Kuna mambo ya kiroho mpaka uwe vilindini na hayo mambo ya vilindini ya vilindini yatajifunua yenyewe kwako. Ukibaki unafanya mambo ya kiroho kwa namna ileile kwa kiwango kilekile,unabaki kwenye shallower water(kina kifupi/hauendi mbali) . Nilikuwa nilimsikiliza mtumishi mmoja wa Mungu ambaye ametweka mpaka kilindini,Yeye watu wote wanaokuja ili awahudimie kiroho kwa maombezi na uponyaji anawaona mara mbili tofauti👥Yaani anamwona mtu physically kwa mwili huu wa dunia lakini pembeni yake kama mita moja anamuona huyo mtu huyohuyo kwa macho ya roho ktk ulimwengu mwingine. Sasa ktk huyu mtu wa pembeni ndipo anaiona shida yake kwa kina na taarifa zote.Huenda umeileta kansa ipo stage ya mwisho,ila yeye alisema akimwangalia yule wa pembeni yako anajua kansa yako ilitokana na nini na na kama kuna shida au kifungo chochote anakiona ktk mwili wako ule wa pili,na akasema hayo mambo ukimhoji mtu mwingine ambaye hajawahi oparet in that realm atajibu tu kuwa ni uchawi etc akasema haya kamuulize mwingine anayeoparet ktk viwango vya vilindi kama hivi,na alifanya practical ya hilo jambo,yaani alisukuma hewani ambapo anamwona yule mtu wa pili na tukaona huyu mwingine ameyumba sana. Yuko mtumishi mwingine ambaye ametweka mpaka vilindini akitembea au akiwa ktk huduma madhabahuni pembeni yake anaona kama screen ya Tv 🖥📺ambapo mambo yote yanayoendelea ktk ulimwengu wa roho anayaona. Mnashangaa akisimama na ingawa anaeleza habari za mtu as if ametoka naye nyumbani ingawa mtu amekuja for the very first time(Sio ile ya Neno la maarifa) ila kiwango alichofikia kwa kutweka mpaka vilindini amepewa televisheni na miwani maalum👓📺 hadi raha,mambo wanaweza kuyafanya huko kijijini kwenu akawashuhudia kama yupo nao kulekule🏰. Sasa wengi wasioelewa haya mambo wakiona tuu hukimbilia kusema ni manabii wa uongo (NI KWELI WAPO,ILA ILI UPATE USAHIHI WA HILO JIPATIE SOMO LANGU LIITWALO, *_Roho Zidanganyazo_*)
Nilipopata ushuhuda wa Oral Roberts akiwa Uganda miaka mingi iliyopita kwa namna ambayo aliletewa kiwete ♿ambaye mguu kuanzia pajani haupo kabisa,lakini yeye kwa kuwa ametweka mpaka vilindini alijua kuna Spare organs ktk akiba ya Mungu ya kiungo chochote kile cha mwanadamu,kwa hiyo alitumiwa kufanya muujiza wa kuuleta mguu mpya ambao haukuwepo kabisa. HAKUNA HAJA YA KUSHANGAA ILI NI JUKUMU LETU LA KUTWEKA MPAKA KILINDINI.
Kama umekuwa na maombi ya saa moja,kwa nini wakati mwingine usiombe binafsi hata masaa nane kama una nafasi,Kwa nini usiamue hata kufunga na kuomba kwa muda ambao ni nje ya mazoea yako,Kwa nini usisome neno kwa kiwango ambacho hukuwahi kufanya? Nilikutana na Mchungaji Tosha toka kanda ya Ziwa,Yeye kwa miaka zaidi ya 25 amesoma Biblia zadi ya mara 25,Kila mwaka anamaliza Biblia yote mara moja,anaanza January mpaka September anakuwa amemaliza Sasa ana ufahamu wa Neno wa kiwango cha juu mno,pamoja na kwamba ni mwalimu wa kitaifa,mwalimu wa chuo cha Biblia lakini tabia hiyo ya kutweka mpaka kilindini imemfanya awe Mwalimu wa viwango vya kutisha sana
MPANGO MKAKATI
Panga kuongezeka nguvu ktk yote tangu sasa,Haupaswi kubaki na nguvu zilezile
*Zaburi 84 : 7*
*_Huendelea toka nguvu hata nguvu, Huonekana Sayuni kila mmoja mbele za Mungu._*
*Luka 1 : 80*(John the Baptist)
*_Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu rohoni, akakaa majangwani hata siku ya kutokea kwake kwa Israeli._*
*Luka 2:40* (Jesus)
*_Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu, amejaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake._*
Mwl Proo
0762879363(Whatsapp only)
alltruth5ministries@gmail.com
No comments:
Post a Comment