Sunday, December 3, 2017

ACHA MTUNGI WAKO, ACHA NYAVU ZAKO!

*ACHA MTUNGI WAKO, ACHA NYAVU ZAKO!.*

*_Mwl Proo_*
*_0762879363_*

©2016

Hallelujah!
Nawasalimu kwa jina kuu, Yesu!
Neno la Bwana linanielekeza kuwa divai mpya, kiriba kipya (New wine, new wineskin). Kuna shida ambapo watu wanataka kuyabeba mambo yao ya kwanza, yafit kwenye wokovu. There are things you can't carry them along with you, na bado ukawa na mahusiano mazuri na Mungu.

Tunawasoma wanafunzi wa Yesu, wengi walikuwa wavuvi, lakini walipoitwa kumfuata Yesu, iliwagharimu kuziacha nyavu zao.

Mathayo 4 : 20
*_Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata._*

Tunamsoma, mwanamke msamaria, alipokutana na Yesu, alikuwa radhi, kuachana utaratibu wake wa kawaida (Mtungi), na akaanza kazi ya uinjilisti mitaani.

Yohana 4 : 28
*_Basi yule mwanamke akauacha mtungi wake, akaenda zake mjini, akawaambia watu,_*

Iko mitungi, ziko nyavu ambazo lazima uziache. Huwezi tembea na Mungu kwa viwango, kama bado umekutana na Yesu, lakini bado nyavu zako na mitungi, umeishikilia.

BILA SHAKA MMESIKIA BAADHI YA WASANII WA BONGO MOVIES, BONGO FLEVA, NA WATU WENGINE AMBAO WAKO MAARUFU KATIKA JAMII (PUBLIC FIGURES), AMBAO WALIOOKOKA, HAWAKUDUMU, WAKARUDI DUNIANI NA KUWA WAPAGANI KULIKO MWANZO (WANA WA JEHANAMU X2). WATU HAO WENGI, WALIINGIA KWENYE SAFINA YA YESU, HUKU WAKITAKA ULE UMASHUHURI WAO, UENDELEE. WALIBEBA MITUNGI, HAWAKUWA RADHI KUACHA NYAVU ZAO. TABIA ZA KWANZA, USANII WA KWANZA, ULIOWAPATIA UMAARUFU, NI MITUNGI NA NYAVU, WAKITAKA KUSIMAMA, SHARTI WAKUBALI ZILE SIFA ZA KWANZA ZIFE (Yohana 12:24).

Huku kwa Yesu fahari yetu kubwa ni kumjua Yesu, sio kuonekana kwenye Tv (Yer 9:23-24, 1Kor 1:31).

Paulo mtume alikuwa na sifa tele, lakini alipoongoka, ali-terminate zile sifa za kwanza, ajipatie umashuhuri usiotokana na sifa zake za kwanza (Filipi 3:7-14. Makanisa yaliyopokea wale waitwao Stars, Superstars/Celebrites, walifanya kosa kubwa, kuendelea kuwapa *Recognition*, yaani kuwatambua kwa kazi zao za Mwanzo. Mtu ana wiki tatu, anapewa maiki🎀 kila siku madhabahuni, hali yeye ni recent convert (Mwongofu mpya), akajiona ni maarufu kanisani, kuliko washirika waaminifu wa miaka na miaka.  Ukweli ni kwamba, HATUPASWI KUMTAMBUA MTU KWA JINSI YA MWILINI, YAANI UINJINIA WAKO, UPROFESA WAKO, UWAZIRI WAKO, HAYO YATATAMBULIKA, LAKINI SIO KWENYE NYUMBA YA IBADA NA WOKOVU.

2 Wakorintho 5 :16a
*_Hata imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili....._*

πŸ‘†πŸ½πŸ‘†πŸ½πŸ‘†πŸ½Yaani ukitaka sifa zako za kuwa na PhD, ndizo zikupe umashuhuri kwa Yesu, ni kwamba umeamua kubeba mtungi, haujawa radhi kuziacha nyavu.

MTUNGI NA NYAVU, VYAWAKILISHA MAZOEA YAKO YA KWANZA, TABIA ZAKO ZA KWANZA. MWINGINE AMEOKOKA, LAKINI BADO TABIA ZA KUWA NA GIRLFRIEND NA BOYFRIEND, ANAZIENDELEZA. NI MUHIMU KUJUA HILI KUWA, KUWA HUKU KATIKA WOKOVU HATUNA MAHUSIANO YOYOTE YANAYOHUSISHA NGONO KABLA YA NDOA. NA HIYO NDIO TAFSIRI YA DUNIA IKITAJA MPENZI (BOYFRIEND NA GIRLFRIEND),  HUO NI MTUNGI AMBAO LAZIMA UUTUE. UKIISHA KUOKOKA UNALETEWA DIVAI MPYA, AMBAYO HAIKAI KATIKA KIRIBA CHA ZAMANI..

Luka 5 : 38
*_Lakini divai mpya sharti kutiwa katika viriba vipya._*

πŸ‘†πŸ½πŸ‘†πŸ½Huwezi kuokoka, then ukapewa karama na huduma za rohoni, ukiwa na mitungi na nyavu. Ulikuwa nyakati zote wakaa vijiweni na washikaji, unataka hiyo tabia ibakie tuu (wala usidai kwamba unawashuhudia injili), maana mazungumzo yao mabaya yanakuharibu wewe, na ukiona mataifa (masela wa kijiweni), wako huru kuongea mambo machafu mbele yako, ni wazi wewe hujawa balozi bado (2Kor 5:20). Ulikuwa na tabia wakati wote upo kwenye kubeti 🎲🎰🎯, sasa umejazwa Roho Mtakatifu, bado unataka ubakie na ratiba zako zilezile. Mungu anataka akutumie kwa kazi kubwa, lakini hakukuti katika position, maana moyo wako umeng'ang'ania mitungi na nyavu.

KAMA ULIKUWA NA MWANAUME AU MWANAMKE,  AMBAYE ALIKUWA MPENZI WAKO KWA MAANA ILE YA MNASHIRIKI HATA MAMBO MENGINE, KAMA WANANDOA, UKIOKOKA TU, MJULISHE KWAMBA SASA BASI, NIMEKUTANA NA YESU MIE. WALA HAKUNA MAMBO YA KUFEKI, KWAMBA SASA TUFUNGE NDOA YA BOMANI, AU SIJUI UMTIE USHAWISHI, KWAMBA ILI UNIOE NA WEWE OKOKA. HAIPASWI MTU AOKOKE ILI KUIFUATA NDOA, BALI MTU AOKOKE KWA KUWA AMEVUTWA NA WOKOVU WA YESU. ANAYE KUOKOKEA ILI AKUOE, ANAKUWA HAJAOKOKA, AMEKUFUATA WEWE BADALA YA KRISTO. KUENDELEZA MAPENZI NA MPENZI WAKO MPAGANI, NI MITUNGI UMEING'ANG'ANIA, YESU ANASEMA ACHA MTUNGI WAKO, ZIACHE NYAVU ZAKO, ILI ATEMBEE NAWE.

MUNGU AKUJALIE, KUTEMBEA KATIKA UPYA WA UZIMA. ANZA KUKAGUA MITUNGI AU NYAVU, ZILIZOSALIA, NA UZIACHE.

Mwl Proo
0762879363

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment