Friday, December 15, 2017

HERESIES IN CHRISTIAN HISTORY

MATERIALS BEYOND BIBLE

*PART ONE*
Narrated/Explored by Mwl Proo
0762879363
0718922662

*LEO KATIKA MATERIALS BEYOND BIBLE, TUTAFANYA SURVEY YA MAFUNDISHO POTOFU, KATIKA HISTORIA YA UKRISTO(HERESIES IN CHRISTIAN HISTORY)*

TUTAPITIA CHACHE KATI YA NYINGI ZAMA ZA MWANZO NA ZA KATI(EARLY AND MEDIEVAL PERIODS) NA KUNAPO MAJALIWA TUTAZITAZAMA HERESIES ZA 19/20th CENTURIES

NATAMANI KUCHAMBUA ZOTE KATI YA HIZI
*The Albigensians
*The Waldensians
*Adoptionism
*Arianism
*Docetism
*Macedoniansor/Pneumatomachians(Spirit Fighters)
*Melchisedechians
*Mornachianism
*Monothelism

BAADA YA KUJIFUNZA HERESIES ZITATUFUNGULIA MLANGO WA KUJIFUNZA ZILE HERESIES ZA KARNE ZA 19-20 PAMOJA NA  CURRENT HERESIES..

Neno "Heresy" linatokana na neno la kilatini 'haeresis' ambalo ni transliteration ya neno la kiyunani lenye maana ya "choosing,choice or course of action"  matumizi yake zama za Agano Jipya ilikuwa ni kama sect/division yaani dhehebu lililoweza kuhatarisha umoja wa wakristo . Badae neno hilo lilichukuliwa likiwa na maana ya kutoka katika ukweli yaani "Departure from Orthodoxy" ambapo neno Orthodoxy lilianza kutumika mara baada ya mwaka 100 A.D  likiwa na maana ya ukweli au right beliefs

Kanisa Katoliki walikuwa na makundi mawili ya Heresy (Material &Formal Heresy) ktk mjadala wangu nitaijadili hii ya Formal heresy ambapo mtu kwa kukusudia kabisa anashikamana na mafundisho yasiyo sawa kwa mambo ya imani yaani "The Wiful and Persistent adherence to an error in matters of faith" hili kwa mujibu wa kanisa Katoliki ilionekana ni dhambi haswa the grave sin iliyostahili adhabu ya 'ipso facto' yaani excommunication au kutengwa..kwao mambo ya imani walimaanisha zile DOGMAS zilizopitishwa na utawala wa juu the Infalliable Magisterium of the Church.

Katika zama za kati neno heresy lilikuwa na tafsiri ya "Kukosa usahihi-Error" yaani Obdurately held kwa hiyo mafundisho yote yaliyo onekana kuwa CONTRARY na "Revealed Truth" kweli ya Mungu kwa wanadamu kupitia Kanisa yalitajwa kama HERESIES... Haya yalichukiwa na kuogopwa

Mwandishi Mashuhuri aitwaye David Kirkwood anasema ktk kitabu chake cha "The Great Gospel Deception" kuwa hakuna mwalimu wa Biblia atasimama kujitaja anafundisha kinyume na Kweli,Ila atakuwa anayapuuzia baadhi ya maandiko ambayo ni muhimu na kuyageuza baadhi ya maandiko ili hadhira yake iamini

MSINGI MMOJA NAUJENGA KUWA.. UFUNUO BINAFSI HAUPASWI KUJENGEA FUNDISHO LA KANISA LA KRISTO...

YAANI KILE KINACHOITWA CHURCH DOCTRINE HAKIPASWI KUWA PRODUCT YA PERSONAL REVELATION AMBAYO INAWEZA KUWA CONTRARY NA UJUMBE MWINGINE WA NENO.. WAZEE WETU NA BISHOPS WALIFANYA KAZI KUBWA KUSHINDANA NA HERETICS ZISIENEE KAMA DONDA NDUGU KWENYE MWILI WA KRISTO

SASA TUNAANZA KUCHAMBUA SOME OF THE HERETICAL MOVEMENTS

HERESIES KTK ZAMA ZA MWANZO NA ZA KATI

1.) WAALBIGENIA/THE ALBIGENSIANS

jina lao lina chimbuko la mji wa kusini mwa ufaransa ambako ndiko walikuwa na nguvu zaidi wakiwa ni mwendelezo wa heretical movement nyingine ya Wamanikea/Manichaeans iliyostawi wakati wa Augustino wa Hippo (Karne ya 4/5)waumini wake walijulikana kama Paulicians huko Asia ndogo,Huku Balkans kama Bogomils huko Italy kama Patini na mwisho huko Ufaransa wakijulikana kama Cathari ..wote walikuwani Dualists wakishika kanuni za wema/ubaya (God vs Satan)
Hawa waliongeza kitu fulani(powerful ant-clerical twist) kutokana hizo principles of good and evil..walifundisha kuwa Yesu alitumwa duniani kwa principle of good.. lakini akafanyiwa trick na kuuawa na Wayahudi na Warumi. Na kuwa wale waliomuua walianzisha kanisa ili kuwapotosha watu kwa ile kanuni ya uovu ikiigiza kuwa ndicho kitu Yesu alitukwa kukiunda..Walienda mbali kwa kuwafanya watu wauabudu Msalaba yaani silaha ambayo waliitumia kumuulia Yesu.
Cathari walikuwa na makundi mawili "credentes-waumini  na clergy/perfecti watumishi wakamilifu the complete ones.. hii movement kanisa lilijitahidi kuizimisha kwa kuwataka wale Perfecti waje ktk midahalo na Orthodox clerics lakini hii njia haikfanikiwa maana Cathari were better debaters

Baadae Innocent III (1198-1216) akamuomba mfalme wa ufaransa Afanye vita dhidi ya heretics na chini ya utawala wa Simon de Montfort alifanikiwa kuwazuia na kuwashinda..

KWANZA NIWEKE SAWA KUWA NI SWALA GUMU KIDOGO KUYAHUKUMU MAFUNDISHO KUWA NI HERESY.. KWA KUWA HUENDA WENGINE HAWAONI KUWA HAYO MAFUNDISHO SIO YA KWELI... SWALA LA PILI NANI ANAYAHUKUMU AS HERETIC DOCTRINES.
KWA MFANO KATIKA EARLY CHURCH (100-476 A.D) BISHOPS WALIIFANYA HIYO KAZI KWA KUITISHA MABARAZA KADHAA NA KUHUKUMU MAFUNDISHO KADHA WA KADHA KUWA NI HERESIES.
MFANO BARAZA LA NIKEA 325A.D ;BARAZA LA CONSTANTINOPLE 380 A.D  YALIYOFANYA MCHUJO WA HERESIES NYINGI SANA

WAWALDENSIA/WALDENSIANS

Yuko mfanya biashara mmoja wa Kifrench ktk mji wa Lions aliyeitwa Pere Valdes kwa kingereza Peter Waldo 1173 alkuwa na msukumo wa kulinda kanisa lenye kufundisha kweli kwa kuubeba ujumbe wake kwenye mikusanyiko ya mijini.Wafuasi wake walikuwa na namna ya Waalbensia perfecti.. kusafir kwa makundi.. kuishi maisha ya kujinyima(austere style of life) nk Waldo alifanya mpako wa kuitafsiri Biblia kwa lugha ya Kifaransa.. orthodox clerics walipeleka malamiko kwa papa juu ya hawa Waldensia kutoka na kuishi kule kwa ufukara na umaskini kama dhihaki kwa watumishi(local clergy).Papacy Office ilijaribu kuwadhibiti Wawaldeninsia.Ghafla kanisa lilianza kujua kuwa kuna mafundisho potofu/heresy

The main heretical teaching ilikuwa apostolic poverty... waliamini utakatifu unapatika kwa kuwa maskini na yule muasisi wake Waldo ali-renounce mali zake zote na akawa akijulikana kama the Poor of Lyons

ADOPTIONISM

Hii ni moja kati ya heresy za mwanzo kabisa Walifundisha kwamba Yesu alizaliwa akiwa mwanadamu wa asili (Mere Man-Non Divine) na akaja kuwa ADOPTED kama mwana wa Mungu kutokana na kushukiwa na Roho juu yake..inasadikiwa kuanzishwa na mfanyabiashara wa ngozi huko Rumi aitwaye Theodotus Byzantium na baadae kuendelezwa na Paulo wa Samosata.. yule Theodotus alipewa ile adhabu ya ipso facto na Papa Victor,na yule Paulo alihukumiwa kuwa mpotofu na baraza la Antiokia(Synod of Antioch) 268 A.D Pia hii heretic movement ilijulikana kama Psilanthropism na Dynamic Mornachianism ambazo zilisadikika kuwa na misimamo ya Nestorianism

UAPOLINARI/APOLLINARISM

Hawa walifundisha kuwa Yesu alikuwa na mwili wa kibinadamu mwenye nafsi ya kawaida(lower soul=the seat of emotions) lakini alikuwa na ufahamu wa kimungu. Pia walifundisha kuwa roho za wanadamu zinazalishwa na roho zingine kama ilivyo miili yao..heresy hii ilianziwa na Apollunaris wa Laodicea aliyekufa mwaka 390 A.D lakini alitangazwa kuwa heretical teacher mwaka 381 wakati wa Baraza la Constantinople

ARIANISM

Walishika imani yote kuhusu uungu wa Yesu ,ila walikubali tu kuwa Yesu aliumbwa na Baba.. kwamba Yesu anao mwanzo wake(Not co-equal/co-eternal with the father) na hiyo ndio sifa ya jina Mwana wa Mungu .. haya mafundisho yaliasisiwa na Ariud (A.D 250-336) aliyeishi na kufundisha huko Alexandria,Misri. Baraza la kwanza la Nikea lilimtaja Arius kama mwalimu mpotofu(Heretical Teacher) na hili fundisho lilikuja kutafutiwa suluhu mwaka 381 huko Constantinople

DOCEITISM

Hawa walofundisha kuwa mwili wa Yesu haukuwa halisi aliposulubiwa,yaani Yesu alijionesha tu kuwa na physical bodu ili awe physically died lakini kiuhalisia hakuwa na mwili wa ulimwengu(incorporeal) Yaani Yesu ni pure spirit na asingeweza kufa kimwili... mafundisho yalihukumiwa na mabaraza kadhaa ingawa yalidumu kwa milenia hata wakati wa Cathari nao waliyaweka ktk imani yao..lakini heresy hii ilikufa wakati Albigensian Crusade (1209-1229)

MACEDONIANSOR PNEUMATOMACHIANS
(Spirit fighters)

Ktk kukubaliana na swala uungu lililopitishwa mwaka 325 A.D huko Nikea...hawa walikataa uungu wa Roho Mtakatifu ambalo wao waliona kuwa huo ni uumbaji wa Mwana,na kuwa Roho Mtakatifu ni mtumishi Wa Baba na Mwana.. liliamzishwa karne ya 4 na Bishop Macedonius I wa Constantinople na mthiolojia wao mkuu alikuwa Eustathius wa Sebaste.. hii Heresy ndio iliyopelekea kufanyiwe nyongeza kwenye ile Nicene Creed.... ikaongezwa sentensi hii ,"And in the Holy Spirit,the Lord,the Giver of Life,Who proceedeth from the Father,Who with the Father and the Son is equally worshipped and glorified,Who spake by the Prophets," wakati wa second ecumenical council..

MONARCHIANISM

Hii heresy ilitia mkazo uliopitiliza juu Mungu kutogawanyika(indivisibility of God the Father) ktk nafsi za utatu Non-Trinitarian iliyokuja kuzaa movements mbili either Sabellianism(Modalism) au Adoptionism..Mkazo wao ulikuwa ktk Monarchy of God kama thiolojia ya mashariki...na kuwa Mungu Baba ana chanzo pekee cha uungu(Unique Source of Divinity) ilihesabiwa kama heresy kwa vile ilivyokuwa extremely expressed.

MONOPHYSITISM /EUTYCHIANISM

Hawa walikuwa na imani kuwa uungu wa Kristo uliutawala na kuufunikiza ubinadamu wake ikiwa kinyume cha mtazamo wa Chalcedonia ambaye alisema Kristo ana asili mbili ya kiungu na kibinadamu au ule mtazamo wa Miaphysite walioshikilia msimamo kuwa Yesu alikuwa human nature na ile pre-incarnate divine nature..zimeungana pamoja kuwa Divine-Human nature
Heresy hii ilikataliwa mwaka 451 kwenye baraza la Chalcedonin...

Kwa sababu ya muda..tafuta ufafanuzi wa heretical movements kama

*Monothelitism
*Melchisedechians

Na zingine .
Ili sasa tupate kuangalia vitu vingine vya muhimu

KWA SASA NITARUKA HERESIES ZOTE ZA KARNE YA 15 HADI YA 20 MAANA NAJUA ZITAKUWA KATIKA MJADALA ULE ULIO KTK SERIES YA PASTOR PETER NAJUA HUKO TUTACHAMBUA HADI AKINA ELLEN GOULD WHITE

*NINAHAMIA KWENYE CURRENT HERESIES/CULTIC DOCTRINES*

NITAMCHAMBUA MHUBIRI MASHUHURI AMBAYE WENGI MNAMWAMINI LAKINI KUNA HERESIES KADHAA ..RUHUSUNI TUJIFUNZE HUYU NI BETH MOORE... KABLA YAKE NITAANZA NA LOCAL HERESIES ZILIZOPO TANZANIA

COMMON AND CURRENT HERETICAL TEACHINGS IN TANZANIA

Ktk utafiti nilioufanya Dar es Salaam kwa kukutana na watumishi wa Mungu nilikutana na Askofu Mwasota ili kuzidadisi imani potofu na haya mafundisho...

#1. FUNDISHO LA MEZA YA BWANA AMBAYO INAHUSISHA KUTUMIA DAMU HALISI(FLESH BLOOD) HII IMANI IMEZUKA DAR ES SALAAM  NA IMEANZA KUSHAMIRI KIDOGO..KTK UTAFITI WAKE WA AWALI ALIGUNDUA HAYA MAFUNDISHO YANATOKEA ZAMBIA ..NA ALISEMA KUWA HUKO ZAMBIA YALIPINGWA MPAKA NA SERIKALI..LAKINI KANISA HILO LIMEPATA USAJIRI HAPA DAR ES SALAAM(alitahadhalisha kuwa hii inahitaji utafiti zaidi)

#2.FUNDISHO KWAMBA RANGI NYEUSI YA KAVA/JARADIO LA BIBLIA IMEINGIZWA IKIWA NA NGUVU ZA GIZA. FUNDISHO HILI NI MASHUHURI KATIKA HUDUMA INAYOJULIKANA SANA THE POOL OF SILOAM CHURCH INTERNATIONAL.. NAJUA AMBAO NI WASHIRIKA WAKE MTA-REACT NEGATIVE  LAKINI MTAKUJA KUTETEA BAADA YA MJADALA.WASHIRIKA WA HII IMANI WAMEDIRIKI KUYAONDOA MAKAVA YA BIBLIA NA KUYAWEKA MAPYA KWA UFAHAMU WANGU FUNDISHO HILI NI HERESY

*#3. KUWATAKASA WANAWAKE KWA KUFANYA NAO NGONO*

HII IMELIPUKA DAR ES SALAAM NA KESI ZA WANAWAKE WENGI KURIPOTIWA KUWA WALIAMBIWA NA WATUMISHI(WENGI WAO NI MITUME NA MANABII) FULANI ,KWAMBA NJIA PEKEE YA KUWATAKASA NA KUWAKOMBOA NA LAANA NI KWA NJIA YA KUFANYA NGONO NA HAO WATUMISHI

Litaendelea......

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment