*UTUKUFU UNAWEZA KUONDOKA*
_*Mwl Proo*_
*0762879363*
Haleluya Haleluya!
Katika somo langu liitwalo, *"kuna tumaini katika toba, hata kama kosa ni kubwa"*, nilieleza kwa kina maneno kama Yerushalayim na Shekina, nikiuelezea utukufu kwa kina, sasa hapa ni kama mwendelezo.
Mungu anaitwa Mungu wa utukufu, Yesu Kristo anatajwa kama Bwana wa utukufu (Mdo 7:2, Yak 2:1), Kila anayempokea Bwana maishani mwake, na kumruhusu Mungu kuyatawala maisha yake. Utukufu wa Mungu unamshukia na kumkalia kama ambavyo, ulilishukia hekalu la Sulemani.
Tunafanya kosa kubwa sana, tunapojitahidi kuenenda kwa kuona👀 kuliko kuenenda kwa imani (2Kor 5:7). Ndugu msomaji ukiendelea kuangalia mitumba ya soko la Karume👚👕👨👨👧👦👖👘uliyovaa, na ku-calculate value yako kwa kiwango hicho, utaji-position mahala tofauti na viwango vyako. Wewe sio wa kawaida, umefanywa hekalu hai (1Kor 3:16, 6:19, 1Petro 2:5). Tofauti ya hekalu la Sulemani, ambalo ni jengo lenye ufu, ninyi wasomaji kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho (Living temples) 🏛🏛, Utukufu wa Mungu unawakalia kwa namna ya ajabu, kuliko lile jengo la mawe mafu.
Sasa wewe wakati unaona mitumba ya Manzese uliyovaa, Viumbe vya rohoni vinakuona umevikwa utukufu na mwangaza mkali 👼🏻👼🏻👼🏻👼🏻. (KUMBUKA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO TUNAONENAKANA KAMA MIANGA 💥💥💥💥 *Wafilipi 2:15*, HATA UKIWA BIZE KARIAKOO UNAZUNGUSHA BIASHARA ZAKO AS A MARCHING GUY/MACHINGA, BADO KULE ROHONI INAONEKANA NURU INATEMBEA). UKIWA NA UFAHAMU HUU MUDA WOTE, KURUDI NYUMA KIZEMBE SIO KAZI INAYOWEZEKANA. KUNA MAENEO HUTAENDA, KUNA MANENO HUTATAMKA, KUNA MAGRUPU YA WHATSAPP UTA-LEAVE (LEFT ), KWA ULE UTUKUFU UNAOKUKALIA. NA MAMBO MENGI YA SIRI UTAJITAKASA KABISA, DAUDI ANASEMAJE?
Zaburi 19 : 12
*_Ni nani awezaye kuyatambua makosa yake? Unitakase na mambo ya siri._*
*MOYO WA SOMO*
UTUKUFU WA MUNGU ULIOKUKALIA, UNAWEZA KUONDOKA. HILO NDILO NENO LA BWANA KWAKO MPENDWA.
Hosea 9 : 11
_*Naye Efraimu, utukufu wake utarukia mbali kama ndege,...*_ 🕊🕊🕊
KAMA HUTAJIFUNZA SIRI ZA KIROHO ZA KUJITUNZA KIROHO CHAKO, UTUKUFU UNAPUNGUKA NA KURUKA KAMA NDEGE 🐣.
NABII WA ROHO AITWAYE EZEKIEL, ALISHUHUDIA AKIWA KATIKA ROHO JINSI UTUKUFI WA MUNGU ULIVYOONDOKA HEKALUNI KWA STAGES. HAUKUONDOKA KWA MKUPUO. WALIPOJAZA VINYAGO, BWANA UTUKUFU WAKE HAUCHANGANYIKI NA VINYAGO. MAISHA YAKO YANAWEZA JAA VINYAGO, NA UTUKUFU SLOWLY UTA-LEAVE (LEFT) MAISHA YAKO, AMBAYO NI HEKALU HAI. UKICHEPUKA KWENYE NDOA UNAINGIZA KINYAGO, UKIFANYA DHAMBI YOYOTE NI KINYAGO, KUMBUKA SANAMU YA KWANZA KATIKA AGANO JIPYA, SIO HIZO ZINAZOCHONGWA NA KUCHORWA, BALI IBADA YA SANAMU/VINYAGO (KOLOSAI 3:5) IMETAJWA NI UASHERATI, UCHAFU, TAMAA MBAYA, MAWAZO MABAYA NA KUTAMANI HAYA NDIO YAMETAJWA YAKIWAKILISHA VINYAGO, KUNA DHAMBI ZINGINE ZIMETAJWA TU KAMA UCHAFU😤😤, KAMA BINTI UNATHUBUTU KUJIPIGA PICHA YA UCHI, NA KUMTUMIA YOUR BAE SIJUI BOO. HUO UNAITWA UCHAFU, UNAJITAHIDI KUMTAHADHARISHA, ETI UKITUMA POPOTE UTANIJUA MIMI NI NANI. KWA HIYO MUNGU NAYE ANAFICHWA KWA PASSWORDS ZA SIMU? 📱📱. HICHO KINYAGO KITAUONDOA UTUKUFU STEP BY STEP. TUSOME HAPA
Ezekieli 10 : 4 *_Utukufu wa Bwana ukapaa kutoka kwa kerubi yule, ukasimama juu ya kizingiti cha nyumba; nayo nyumba ikajazwa na lile wingu, na ua ulikuwa umejaa mwangaza wa utukufu wa Bwana._*
👆🏽👆🏽UTUKUFU ULISHINDWA KUBANANA NA VINYAGO HEKALUNI, UKATOKA UKAHAMIA KWENYE MAHALI PENGINE KWENYE KIZINGITI.
Ezekieli 10 : 18
_*Kisha huo utukufu wa Bwana ukatoka pale juu ya kizingiti cha nyumba, ukasimama juu ya makerubi.*_
👆🏽👆🏽👆🏽NA BAADAE HATA HAPO KWENYE KIZINGITI NAPO UKAPASHINDWA, UKIWEKA KINYAGO KIMOJA, UTUKUFU UTAJISOGEZA PEMBENI KIDOGO, UKIONGEZA VINYAGO, UTAENDA MBALI ZAIDI.
Ezekieli 11 : 23 *_Utukufu wa Bwana ukapaa juu toka katikati ya mji, ukasimama juu ya mlima wa upande wa mashariki wa mji._*
👆🏽👆🏽SASA ONA, TOKA KUKAA HEKALUNI, MPAKA UNAHAMIA MLIMANI😒. VYA NINI VINYAGO MPENDWA?? TABIA YA KUIBA VINYAGO UMEITOA KWA RAHELI? WANAOIBA VINYAGO, WANAFIA NJIANI!.
*HATARI KUU*
UTUKUFU UKIONDOKA HEKALUNI (MAISHANI MWAKO), WANAOANZA KUGUNDUA NI VIUMBE VILIVYOPO ROHONI. MAPEPO YOTE 👹👹👹👹, YANAONA MWANYA SASA, YALIKUSHINDWA MUDA MREFU SANA, WANASEMA DAH HUYO JAMAA ANA LANGO MOJA WAZI SASA. WENGI WALIOWEKA VINYAGO, WAKAPATWA NA MAJANGA, WANAMDHANIA MUNGU KAWAADHIBU, MARA NYINGI SIO ADHABU YA MUNGU, BALI UTUKUFU ULIOKUWA UNAWAZUIA MAADUI, HAUPO KWA HIYO MISHALE YA MOTO *FLAMMING ARROWS* 🏹🏹🏹🔥🔥🔥 YA ADUI, INAKUPATA SASA.
KWA NINI UNARUHUSU UTUKUFU UONDOKE?? MUNGU YUKO TAYARI, UKIWEKA MAMBO SAWA, UTUKUFU UTAIRUDIA NYUMBA YAKO MPENDWA...
Ezekieli 43 : 4
*_Na huo utukufu wa Bwana ukaingia ndani ya nyumba, kwa njia ya lango lile lielekealo upande wa mashariki._*
AHADI YA MUNGU KWAKO, SIO UTUKUFU KUPUNGUKA, BALI UTUKUFU KUWA ZAIDI YA ULE WA KWANZA (HAGAI 2:9)
MBARIKIWE SANA
Mwl Proo
0762879363
All Truth Group
alltruth5ministries@gmail.com
No comments:
Post a Comment