Saturday, December 2, 2017

KIKOMBE KINAFURIKA

*☕KIKOMBE KINAFURIKA☕*

*_Mwl Proo_*
*0762879363*

HALLELUJAH!!
Fuatana nami katika ufunuo huu, wa Roho. Neno kikombe kwa tafsiri ya kinabii (Prophetic symbolism), huwakilisha mapatilizo ya ghadhabu, pia humaanisha agano, huweza kumaanisha baraka (kulingana na utakavyo kiona, kama ni kwa ndoto au maono ya wazi), na kwa upande mwingine, huwakilisha hali ya kiroho kwa ujumla. Yupo rafiki yangu, aliyetamani kujijua maisha yake ya kiroho yakoje. Akiwa kwenye maombi ya kumuuliza Mungu, ghafula mbele yake akamwona malaika ameshika kikombe☕, kina maji safi/meupe yamejaa kama yanataka kumwagika, ikapotea hiyo picha. Maandiko yatakayo kusaidia kuthibitisha tafsiri ya kinabii ya *kikombe* (Yer 25:15, Isa 52:22, Ezek 23:33, Zabur 11:6,75:8, Math 26:39, 1Kor 10:16,20,11:25).

TUONDOKE NA TAFSIRI HIYO YA MWISHO YA KIKOMBE. DAUDI ALIJUA KATIKA ROHO, KIKOMBE CHAKE KINAFURIKA. UKISOMA ZABURI ZA DAUDI, MAANA NYINGINE SIO ZAKE. LAKINI UKISOMA ZILE ZABURI AMBAZO NI ZA DAUDI, UTAGUNDUA WAZI HUYU MTU KIROHO ALIFURIKA, USEMI WAKE WA IBADA, SALA ZAKE KINYUME NA MAADUI, SHUKRANI ZAKE BAADA YA KUSHINDA VITA, MASIMULIZI YA WEMA NA UKUU WA MUNGU, YALIVYOLETWA NA DAUDI KWA USHAIRI AU ZABURI, NI WAZI HUYU MTU ALIFURIKA KIROHO, HAKUWA MKAME, HAKUPUNGUKA KATIKA KIKOMBE CHAKE.

Zaburi 23 : 5b *_Umenipaka mafuta kichwani pangu, Na kikombe changu kinafurika._*

Maisha ya wakristo leo hii, yanatofautiana hapo tu. Kiwango cha kikombe kufurika, ndani ya watumishi, washirika binafsi, vinatofautiana, lakini baada ya kuokoka (kupakwa mafuta uwe wake), unayo kazi ya kuchochea ili kikombe kifurika ~*(tafuta somo langu liitwalo FANNING INTO FLAME/KUCHOCHEA, ili ujifunze siri zaidi)*~, Kwa hiyo mtu atakayejichochea kwa juhudi, na kujitahidi kukaa na Bwana, kikombe chake kitafurika.

☕ *WATU AMBAO VIKOMBE VIMEFURIKA, WANAKUWA FAIDA KWA WATU WENGINE.*
Yesu siku zake za duniani, kikombe kilifurika, wanafunzi wa Yesu, pamoja na uvivu wao wa kufunga (Luka 5:33-35), Kikombe cha Yesu, kilichofurika  kilikuwa kikiwamwagikia na wao, hivyo walikaa salama tuu.

☕ *WENYE VIKOMBE VILIVYO FURIKA, WANAPEWA NAFASI YA KUONA MAMBO YA WENGINE ZAIDI*
This is so practical and real. Bila shaka umeshuhudia hii, unakuta mtu so often times, Roho anakukonyeza mambo ya wengine tuu. Sizungumzii karama ya Neno la maarifa, lakini waliofurika vikombe vyao, wakilala wakiamka, wana jumbe za watu, kwamba, kamwambia fulani, afanye hiki asifanye kile, wanaona hali za kiroho za wengine, madhaifu ya wengine katika roho (SIO KWA HILA, PIA HUPEWA HEKIMA KUMJULISHA MHUSIKA BILA KUMKWAZA), ACHANA NA WALE WASANII, AMBAI MTU AKIANGUKA KWENYE UZINZI, WANASEMA MIMI NILISHAONESHWA😌, HAWAKUWAHI HATA KUMWONYA MBELE. KUNA WAKATI NILILALA NIKAMWONA MTUMISHI MWENZANGU KATIKA ROHO, AMEKONDA MNO, HADI SURA IMEKUWA NYEUSI. NIKAKUTANA NAYE NIKAMWELEZA, NAYE AKAKIRI HAPOHAPO, KWAMBA HAYUPO VIZURI KIROHO, MPAKA AMERUDIA KUANGALIA MIZIKI YA DUNIA KWENYE TV📺. IPO SIKU NILIKUWA NATAKA KUJILAZA SAA KUMI ALASIRI, KUJIANDAA KUKESHA USIKU, MUDA NAPANDA KITANDANI 🛌, HATA SIJAFUMBA MACHO, NILIYAONA MANENO YANAPITA HEWANI, NILIFANIKIWA KUYASOMA HARAKA HARAKA, YALIKUWA YANANIJULISHA KITU AMBACHO MTU KAKIWEKA KWENYE BEGI LAKE, NA KIUKWELI HAKIPASWI KUWEPO, HAPASWI KUWA NACHO KAMA MTU MKRISTO. NIKAAHIRISHA KULALA NIKAENDA KUFUNGUA BEGI LAKE, NIKAKIKUTA KWELI. MTU AMBAYE HAJAFURIKA ROHONI, HAJULISHWI YA WENGINE, ISIJE AKAJIVUNA NA KUMBE YEYE MWENYEWE ANA ISSUES NYINGI ZA KUFIX.

☕ *MTU AMBAYE KIKOMBE KINAFURIKA, ANAWEZA KUWA ANATEMBEA BARABARANI AU ANA-DRIVE, HUKU NAFSINI MWAKE ANAENDESHA IBADA. INAFANYIKA KWA NAMNA YA AJABU, PAMBIO ZITAIMBIKA HATA BILA SAUTI, AMAWEZA KUWA ANAPIGA HATUA 👣, HUKU ANASIKIA NAFSI YAKE INAHUBIRI UJUMBE ULIOMJAZA MOYONI. MTU HUYU ATAYASHINDA MENGI SANA, YANAYOWAJIA WANADAMU KUWAKOSESHA (Math 18:7-8).*

☕ *MTU AMBAYE KIKOMBE KINAFURIKA, UNAWEZA ONA TOFAUTI MUDA WA MAOMBI. UNAWEZA KUMSIKIA ALIKUWA ANAOMBA, GHAFULA MAOMBI NI KAMA ANAHUBIRI SASA (SIZUNGUMZII KUOMBA KWA SAUTI YA KUKOROMA KIINJILISTI NA KUWEKA NENO HALELOOOYA BADALA YA HALELUYA, HAPANA!). SIO KUHUBIRI BALI ANATABIRI, SIO KUTABIRI YA KUTAJA MATUKIO YAJAYO, LAKINI ANAONGEA VITU KWA MAMLAKA YA KIMUNGU, KAMA ANAUMBA MAMBO NA KUYATANGAZA, MAANA ALIYEFURIKA KIKOMBE HUFANYIWA KINYWA CHA MUNGU, ANAKUWA GOD'S SPOKESMAN (Yeremia 15:19).*

☕ *KIKOMBE KINAPOFURIKA, HUKAUKIWI NENO LA MUNGU*
Ni hatari kwa mhudumu wa madhabahu, kukaukiwa. Ukaanza kuwa bize kutafuta mahubiri ya ku-google bila ufunuo wa roho, ukawa bize kupitia diary za zamani tuu, kutafuta masomo, na hata kudiriki kuchakachua mahubiri ya wengine bila ku-acknoledge source. Ok hiyo sio kesi yangu hapa. Lakini kikombe kikifurika, hata kama utakuwa na sessions sita za kuhubiri kwa wiki, utaweza ku-manage hiyo ratiba mwaka mzima, bila marudio maaba kwa Mungu iko hazina isiyopungua, you just need to make sure, that your cup overflows. Unaweza usiwe mhudumu wa madhabahu kabisa, lakini asiyekaukiwa, mtamjua tuu. Ukiwa naye hawezi akaongea yote hakakosa vya Mungu, lazima tu ataweka habari za ufalme, maana zimekijaza kikombe chake (Luka 6:45). Na tukikaa na mtu ambaye hamna muda katika stori anajadili mambo ya ufalme, akimaliza habari za Donald Trump, kahamia habari za Chelsea⚽, akimaliza hizo, Anaanza ishu ya UKAWA vs CCM, akimaliza hayo ataanza simulizi za vipindi vya Tv, vya kidunia tuuu. Sijasema hayo mabaya, haswa yakifanywa kwa kiasi. Lakini you need to check out your inner treasury 👉🏽☕Umejaza nini? Unavyozijua habari za UEFA-Champions League, ndivyo unavyojua habari za Biblia? Tukikupa utueleze habari za Othiniel Bin'Kenaz na yule Kushan-Rishathaimu, utatueleza chochote?, Ukiona hata hayo majina wala stoi yao hujui inahusu nini, na wametajwa wapi katika Biblia, that is the real you, hazina yako inapunguka badala ya kufurika. Bwana akusaidie kama una haja ya kuponywa. Jikague huwa unapost vitu gani zaidi kwenye magrupu ya whatsapp? Kama vitu vya Mungu havitoki ndani yako kuwaendea watu, hiyo ni reflection ya aina ya hazina yako.

Luka 6 : 45
*_Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake._*

JE! TUKIPITIA TIMELINE/PROFILE YAKO KATIKA MITANDAO YA KIJAMII, UMEJAZA NINI? FOR YOUR INFORMATION, TWAWEZA JUA KAMA KIKOMBE KINAFURIKA, HATA KWA ULIYOJAZA KWENYE WALL YAKO YA FACEBOOK. IN SHORT, MTU AMBAYE KIROHO AMEFURIKA, ATAZINGATIA RATIO/UWIANO. YAANI MAMBO YA MUNGU YASIZIDIWE NA MENGINE, UKIWEZA KUAHIRISHA IBADA, ILI KUSHUHUDIA MTANANGE WA SIMBA NA YANGA, PALE NATIONAL STADIUM, WEWE UKO VIZURI KATIKA KUTOFURIKISHA KIKOMBE.WENYEWE UNAENDA HUKU UNAJISEMEA MOYONI, YESU NISAMEHE TU KWA KWELI 🌚!. HA HA HA HA YAANI HAKI UNAIJUA, HUTAKI KUITENDA (yakobo 4:17).

SASA UKIWA UMEJINGUA KIKOMBE HAKIFURIKI, AU KINAFURIKA UNATAKA KUMENTEINI HIYO HALI, USIACHE KUPITIA SOMO LA *KUCHOCHEA* NA MENGINE NILIYOFUNDISHA NAMNA YA KU-UPGRADE MAISHA YA KIROHO.

MBARIKIWE NYOTE

Mwl Proo
_Mjumbe wa Matengenezo_
0762879363

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment