🇦 🇱 🇱 🇹 🇷 🇺 🇹 🇭
*_Mwl Proo_*
0762879363 (calls/texts)
*MAOMBI NA HUDUMA NI MUHIMU SANA*
Once again,Bwana Yesu asifiwe sana wapendwa.
Kuna jambo la kutusaidia sana nililojifunza ktk maandiko. Kuwa *_maombi na huduma ni muhimu sana_*
TUJIFUNZE UFUNUO TOKA KWA MFALME SULEMANI
*1 Wafalme 2 : 35*
Kisha mfalme akamweka Benaya, mwana wa Yehoyada, *mahali pake juu ya jeshi;* na Sadoki, *kuhani,* mfalme akamweka mahali pa Abiathari.
Ameen,Sasa wapendwa mara baada ya Sulemani kushika hatamu,anatufundisha taasisi mbili nyeti kwenye *UFALME*(Maisha ya kiroho) . Naamini yeye kama mfalme kulikuwa na taasisi nyingi angeweza kushughulika nazo kwanza.Ila alipoingia tu aliondoa wale ambao hawafai tena kwa maana walishachakachua yaani Kamanda hatari Yoabu na kuhani Abiathari wa zama za babaye Daudi,kisha aka-replace akamweka Benaya bin Yehoyada ktk nafasi ya Jeshi ile ya Yoabu *(HII NI NAFASI INAYOWAKILISHA ULINZI KTK MAISHA YA KIFALME NA INAWAKILISHA MAOMBI KTK MAISHA YA KIROHO YA MWANA WA MUNGU)* Wako wanaosema ukiisha kuokoka hauhitaji kumbe kuomba ulinzi "they are right in saying", ila pia wanapaswa kuelewa how things operate in the spiritual realm. Wote mnaweza kuwa mmeokoka lakini msiwe na nguvu sawa,msiwe na idadi ya sawa ya majeshi yanayopigana upande wa kila mmoja,wote mkasema _"kwa jina la Yesu"_ isiwe na *effect/impact* sawa kwenu nyote. Watu walio kwenye *PRACTICAL MINISTRY* wanaelewa moja kwa moja,kunaweza kuwa na ngome au kifungo au jini au nguvu za giza/uchawi zimetaabisha weee,na watu wengine waliookoka wamesumbuka navyo kuvikamea au kuviharibu bila mafanikio,Lakini akaja tena mtumishi mwingine huenda hata asiombe ila kule kukaribia eneo la tukio kile kitu kikang'oka na kutoweka,Ukweli ni kwamba nguvu inayotenda kazi ndani yake ni kubwa(Efes 3:20) unaweza kuta kiasi cha majeshi ya Mungu yanayofanya kazi upande wake ni mengi kulingana na alivyoji-position ktk ufalme. Kumbuka habari ya Gehazi na Elisha bin Shafat,Gehazi ambaye ni mtumishi wa Nabii mwenye double portion anointing yeye pia alikuwa ni mwamini(kwa sasa ningemwita tena mlokole) lakini alipofunguliwa macho ya rohoni👁👁akaona majeshi yale hayajawazunguka wote ila yamemzunguka Elisha
*2 Wafalme 6 : 17*
*_Elisha akaomba, akasema, Ee Bwana, nakusihi, mfumbue macho yake, apate kuona. Bwana akamfumbua macho yule mtumishi; naye akaona; na tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote._*
Mungu ameahidi kuwafanya watumishi wake kuwa miali ya moto (Ebrania 1:7) Lakini kiasi cha zile blimestones of fire 🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥 zinazomzingira mtumishi haziwi sawa kwa wote itategemea ameji-position vipi ktk ufalme. NA UKWELI WA WAZI MAADUI ZETU WOTE KTK ROHO WANAZIFAHAMU TOFAUTI HIZI ZA NGUVU,KWA MARA YA KWANZA YESU KUFANYA HUDUMA KTK SINAGOGI NA WATU HAWAKUSHUHUDIA KAMWE MAPEPO KUWALIPUKA WATU JUST BY A SPEECH OF SERMON,LAKINI SHETANI ANTAMBUA KWA HARAKA SANA NANI MWENYE NGUVU(MARKO 1:24ff) Pepo wakapiga kelele katikati ya speech ya Yesu, *"tuna nini nawe?"*(what do you want with us?)👹👉🏾😭🔥(this is an utterace of surrendering),Kajifunze ngoma nzito iliyoletwa kwa wanafunzi ikagoma kwa Yesu ikayeyuka fasta (Mathayo 17:19,21) Nenda kajifunze pia kwa wana wa Skewa (Mdo 19:14-16) Pepo liliwajibu vyema *Yesu tunamjua,Paulo tunamfahamu,lakini ninyi ni akina nani?*
Wapendwa ngoja nimalizie habari za Sulemani ili tuendelee vyema na utamu. Sulemani akaifanya imara taasisi ya pili ya ukuhani,kwa kuwa Abiathari alichakachua then mfalme ak-replace nafasi hiyo kwa kumweka Sadoki(NAFASI HII KTK MAISHA YA KIROHO INAWAKILISHA HUDUMA ZA KIROHO ZA NAMNA ZOTE). Hivyo mfalme Sulemani kabla ya vyote aliona (ULINZI NA UKUHANI YAANI MAOMBI NA HUDUMA NI NUMBER ONE MISSION)
Sasa sisi tuliozaliwa upya(tuliookoka) tunayosifa ya kifalme(wafalme) na tunapaswa kuwa na ufahamu huo,tumepewa/tumeupokea ufalme,tumefanywa wafalme,tunapaswa kujifunza yote kwa sura ya kifalme
TUSOME MAANDIKO
*Waebrania 12 : 28*
*Basi kwa kuwa tunapokea ufalme usioweza kutetemeshwa, na mwe na neema, ambayo kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na unyenyekevu na kicho.*
*Luka 17 : 21*
*wala hawatasema, Tazama, upo huku, au, kule, kwa maana, tazama, ufalme wa Mungu umo ndani yenu.*
*Ufunuo 5 : 10*
*ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.*
*1 Petro 2 : 9*
*Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu.*
Luka 12 : 32 - *Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme.*
SASA NAZUNGUNZA NA NINYI WAFALME KTK UFALME WENU ULINZI NA UKUHANI(MAOMBI NA HUDUMA) NI MUHIMU SANA. HUU NI WITO KWA KILA MWANA WA MUNGU,KAMWE USIJARIBU KUACHA MAOMBI NA HUDUMA KWANI HII NI *KANUNI YA UFALME* Kabla sijaendelea nimetamani kunukuu kauli ya Bishop Deo Lubala aliyoitoa kwenye mkesha wa AFLEWO 8/7/2016 kuwa *UFALME WA MUNGU UPO KWA NAMNA MBILI(TWO ASPECTS) 1.PERSONAL OF JESUS 2.PRINCIPLES OF THE KINGDOM,AKASEMA HILO LA KWANZA(YAANI KUWA NA YESU) LITAKUHAKIKISHIA KUWA NA YESU MILELE, NA HILI LA PILI (KANUNI ZA UFALME) LINAKUSUDIA KUKUPA MAISHA YA USHINDI NA BARAKA HAPAA DUNIANI. Sasa humo ktk kundi la pili ndipo kuna utoaji,maombi,huduma etc etc
NIMEFURAHISHWA NA HIYO HOJA MAANA HIKI NINACHOTAJA LEO NI MIONGONI MWA KANUNI ZA UFALME
HAKUNA CHEO WALA MAJUKUMU DUNIANI YANAYOWEZA KUKU-EXEMPT ETI USIOMBE,MAOMBI HAYANA SUBSTITUTE(MBADALA) MAOMBI NI LAZIMA UOMBE, *HUWEZI KUOMBA KAMA HUOMBI* UKITOA PESA NYINGI KUSAPOTI MIKUTANO YA INJILI UNA HERI NA THAWABU LAKINI KAMWE SIO COMPENSATION YA MAOMBI,BADO KWA KANUNI ZA UFALME UNAPASWA KUWA NA BENAYA BIN YEHOYADA(MAOMBI) KTK UFALME WAKO. KUNA WATU KWA SABABU YA BIASHARA ZAO HAWAJITOI NAFSI ZAO KUFANYA HUDUMA ILA WANATUMA TU ZAKA NA KUTOA SAPOTI NYINGINE KANISANI,SASA MWANA WA MUNGU SADAKA ILI ILETE *SENSE* UNAPASWA KUJITOA WEWE KABLA YA PESA ZAKO, YAANI YOU NEVER FAST, YOU NEVER ATTEND OVERNIGHT PRAYER, UTAKUWA MANYAMA UZEMBE WA KIROHO (spiritually flabby),SADAKA YAKO ITAFUNGUA MLANGO FULANI WA BARAKA,LAKINI HAITAONGEZA MUSCLES 💪🏾💪🏾👊🏾NA KUNOA ZILE SILAHA ZAKO ZA VITA VYA ROHONI 🔫💣⚔🗡🛡NA HAPO NDIPO TUNAPOKUKUTA MENEJA MLOKOLE SEKRETARI WAKO KAPANDISHA PEPO👹 UNAPIGA SIMU KWA PASTA📞☎,AJE AKEMEE. MIMI NI MTUMISHI WA SERIKALI SIO MCHUNGAJI,LAKINI KTK TAASISI NILIYOPO IWE WAFANYAKAZI AU WALE TUNAWAHUDUMIA WAKIPATA SHIDA ZA KIROHO KAMA KULOGWA AU MAPEPO ,TUNAYASHUGHULIKIA NA KUMALIZA KESI,MAANA KANUNI ZA UFALME ZINAZINGATIWA.
SASA WAPENDWA WANGU NAWAAMSHA KWA KUWAKUMBUSHA *_"MAOMBI NA NA HUDUMA NI MUHIMU SANA"_*
MIONGONI MWA FAIDA KUBWA YA KUDUMU KTK MAOMBI NA HUDUMA NI KUTOKUWA NA MAISHA YA KIROHO YENYE ZIGZAG⚡⚡NA KUWA MBALI NA MAANGUKO, WALOKOLE WENGI WALIOPOTEZEA MAOMBI NA HUDUMA WAKAJIKUTA WAKO KWENYE GIZA LA NJE HUKO HADI DHAMBI ZIKAWA ZA KAWAIDA.NA INAPOKUJA SWALI, JE! ALIYEOKOKA ANAWEZA KULOGEKA (JIBU JEPESI,HAWEZI) ILA UKWELI NI KWAMBA MLOKOLE ASIYEZINGATIA KANUNI ZA UFALME(HASA KUDUMU KTK MAOMBI NA HUDUMA) IKIJA ATTACK AMBAYO NI KUBWA UNAWEZA KUMZOA (USIISHIE KUNUKUU KUWA UHAI WAKO UMEFICHWA......Kolosai 3:3) HAKIKISHA UNAFANYA HUDUMA YOYOTE,UKISHINDWA KUHUBIRI,FUNDISHA,IMBA KWAYA(HATA KAMA NI MENEJA WA BENKI) ,SHUHUDIA MITAANI KUHUSU YESU,PIGA VYOMBO VYA MUZIKI KANISANI NA HUDUMA ZOTE ZA KIROHO (HAA YOTE ILI KUJIDHILI,NA KUUTAWALA MUDA WAKO KIFALME,DUNIA ISIKUMEZE)
OMBI:
Katika jina la Yesu,Bwana akuondolee roho ya uzito,uvikwe wepesi, naam vazi la sifa
Ameeen
MBARIKIWE KWA JINA LA YESU
Mwl Proo
0762879363(whatsapp)
alltruth5ministries@gmail.com
No comments:
Post a Comment