🇦 🇱 🇱 🇹 🇷 🇺 🇹 🇭
*KWENDA MBELE MOJA KWA MOJA*
_Na Mwl Proo_
*0762879363*
Ezekiel 46
9.".....hatarudi kwa njia ya lango aliloingia kwalo, lakini atatoka kwa *kwenda mbele moja kwa moja.*"
NDUGU MPENDWA KTK BWANA,HAKUNA KITU KINA DISTURB POSITION YAKO KIROHO KAMA KUREJEA NYUMA BAADA YA KUIFAHAMU ILE KWELI NA KUOKOLEWA.
*KUREJEA NYUMA NI KUMKASIRISHA BWANA* 😡😡😡
Ezekiel 8:17
17 Basi, akaniambia, Umeyaona haya, Ee mwanadamu? *Je! Ni jambo dogo sana kwa nyumba ya Yuda, wayafanye machukizo wanayoyafanya hapa?* Kwa maana wameijaza nchi hii udhalimu, *_tena wamerejea nyuma ili kunikasirisha;_* na, tazama, wanaliweka tawi puani.
NDUGU WAPENZI WATU WENGI KWA KUTOJUA KANUNI ZA UFALME NA TARATIBU ZINAZOUONGOZA ULIMWENGU WA ROHO,WANADHANI NI NENO DOGO KUREJEA NYUMA WAKIWA TAYARI KWENYE NANGA YENYE SALAMA(EBRANIA 6:19) NA WAMEJAZWA MAARIFA YOTE YA MUNGU.
UKWELI NI KWAMBA ULIPOOKOKA ULIHAMISHWA KISHERIA TOKA KWENYE UFALME ULIOKUWA UKIKUMILIKI KWANZA(KISHERIA) KWA SABABU YA DHAMBI. UKAHAMISHWA NA KUFANYWA *KINGDOM CARRIER* YA UFALME HUU WA MUNGU. MAPENZI YA MUNGU KWAKO NI KWAMBA USIRUDI NYUMA TENA,BALI UWE NA MWENDO WA *KWENDA MBELE MOJA KWA MOJA* .
NILIKUWA NIKISOMA KITABU CHA RUTHU NIKAFUNDISHWA KITU
Ruth 1:20-21
21 *_Mimi nalitoka hali nimejaa, naye BWANA amenirudisha sina kitu, kwani kuniita Naomi, ikiwa BWANA ameshuhudia juu yangu, na Mwenyezi Mungu amenitesa?_*
22 *_Basi Naomi akarudi; pamoja na Ruthu Mmoabi, mkwewe; ambao walirudi kutoka nchi ya Moabu; nao wakafika Bethlehemu mwanzo wa mavuno ya shayiri._*
👆🏼👆🏼👆🏼👆🏼👆🏼NENO LA BWANA KTK MISTARI HIYO NI KWAMBA *"KAMA UKIRUDI NYUMA,THEN UKARUDI TENA,HAUWI SAWA KTK YOTE YALE YAHUSUYO POSITION KTK UFALME,KUNA KITU KINA-MISS* HUO NDIO UKWELI,NITAUELEZEA MBELE KIDOGO.
SASA TURUDI KTK KITABU, FAMILIA YA ELIMELEKI NA MRS WAKE NAOMI WALIONDOKA BETHLEHEMU(the city of bread🍞) BETHLEHEMU INA ASHIRIA NDANI YA WOKOVU,HALI NZURI YA KIROHO,UHUSIANO MZURI NA BWANA MUNGU(KUWA NDANI YA MILKI YA MUNGU) ...... LAKINI WATU HAWA WALIONDOKA BETHLEHEMU WAKAENDA KUKAA NCHI YA MOABU(UMOABUNI KUNAASHIRIA KUTOKA KTK HEMAYA YA MILKI YA MUNGU,KUACHA WOKOVU NAAM KUREJEA NYUMA) .
MIONGONI MWA ATHARI UNAZOZIPATA KWA WAKATI UKIWA UMEREJEA NYUMA NI PAMOJA NA KUPOTEZA VITU VYA THAMANI KTK MAISHA,IKIWEMO FURSA AMBAZO ZILIPANGWA KWA AJILI YAKO,MUNGU HATA KAMA ALIKUPANGIA BARAKA ZA NAMNA FULANI ANAZIHAIRISHA MCHANA KWEUPE.....
*Yeremia 18:9-10*
*_9 Na wakati wo wote nitakapotoa habari za taifa, na habari za ufalme, kuujenga na kuupanda,_*
*_10 ikiwa watatenda maovu mbele za macho yangu, wasiitii sauti yangu, basi nitaghairi, nisitende mema yale niliyoazimia kuwatendea._*
NAOMI ANASEMA ALIONDOKA AMEJAA NEEMA AMEREJEZWA HANA KITU,AKIWA UMOABUNI(NJE YA WOKOVU) ALIPOTEZA MUME NA WATOTO WAKE WAWILI👬 . NI MUHIMU UKUMBUKE MUNGU HAWATEMBELEI WATU HUKO UMOABUNI,NDIO MAANA WAKIWA HUKO ALISIKIA KUWA MUNGU AMEWATEMBELEA/AMEWAKUMBUKA WATU WAKE HUKO BETHLEHEMU NA KUWAPA CHAKULA,KUMBUKA PIA KUWA UKOSEFU WA CHAKULA BETHLEHEMU ILIKUWA SABABU YA WAO KUTOKA HUKO BETHLEHEMU. SHORTFALLS(MAPUNGUFU) ULIYONAYO NA UHITAJI USIKUONDOE BETHLEHEMU UKAENDA UMOABUNI,HUKU BETHLEHEMU AT ANY TIME "T" BWANA ANATUKUMBUKA (Ruth 1:6)
HOLD ON! SIJASEMA UKIREJEA NYUMA UTAKAPORUDI HUTAPOKELEWA, UTAPOKELEWA TENA KWA SHEREHE KABISA😊,ILA LEO NGOJA NIKUTAZAMISHE UFUNUO WA MWANA MPOTEVU(PRODIGAL SON)
MWANA MPOTEVU ALIPOZINGATIA MOYONI MWAKE(HE CAME BACK TO HIS SENSE) AKARUDI HOME KWA BABA,ALIPOKELEWA KWA KUFANYIWA KARAMU MPAKA NDAMA ALIYENONA ALIANGUSHWA🔪🐄,BUT I ASSURE YOU THE PRODIGAL SON WAS NO BETTER THAN THE BROTHER AT HOME,KWANI UKIREJEA NYUMA UNAKUWA KTK UFU⚰☠
*Luka 15:32*
*_32 Tena, kufanya furaha na shangwe ilipasa, kwa kuwa huyu ndugu yako alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana_*
Mwl Proo
WEWE AMBAYE UNADUMU UMESIMAMA(1KOR 10:12) WEWE AMBAYE UMEBAKI KWA BABA(ALWAYS WITH GOD) THAMANI YAKO KWA BABA(MUNGU) SIO KARAMU YA MAPOKEZI BALI VYOTE VILIVYO VYA MILKI YA BABA YAKO,NI VYAKO 👆🏼👈🏾👇🏽👉🏾
*Luka 15:25-31*
25 Basi, yule mwanawe mkubwa alikuwako shamba *(alikuwa busy na huduma ktk ufalme wa Mungu)* na alipokuwa akija na kuikaribia nyumba, alisikia sauti ya nyimbo na machezo.
26 Akaita mtumishi mmoja, akamwuliza, Mambo haya, maana yake nini?
27 Akamwambia, Ndugu yako amekuja, na baba yako amemchinja ndama aliyenona, *kwa sababu amempata tena, yu mzima.*(Unaweza rudi nyuma ukapotea kabisa,au unarudi umekatwa mkia🐄,utaruhusiwa kuingia zizini)
28 Akakasirika, akakataa kuingia ndani. Basi babaye alitoka nje, akamsihi.
29 Akamjibu baba yake, akasema, Tazama, mimi nimekutumikia miaka mingapi hii(anadumu ktk wokovu), wala sijakosa amri yako wakati wo wote (ukamilifu&uaminifu kwa Mungu), lakini hujanipa mimi mwana-mbuzi, nifanye furaha na rafiki zangu;
30 lakini, alipokuja huyu mwana wako aliyekula vitu vyako pamoja na makahaba, umemchinjia yeye ndama aliyenona.
*_31 Akamwambia, Mwanangu, wewe u pamoja nami sikuzote, na vyote nilivyo navyo ni vyako._*
👆🏼👆🏼👆🏼😋😋😋😋😋😋
NDUGU MPENDWA USIDIRIKI KUTENDA DHAMBI KWA KUSUDI(EBRA 10:26) WALE KAMWE USIWE NA RECORD YA KURUDI NYUMA (EBRA 6:4-6)
*NI BORA KUFA KULIKO KURUDI NYUMA*
*Yeremia 22:10,2:19*
10 Msimlilie aliyekufa, wala msimwombolezee(ambaye bado hajaitwa ktk neema hii ya ajabu),Bali mlilieni huyo aendaye zake mbali *(aliyerejea nyuma)* ;Kwa maana yeye hatarudi tena,Wala hataiona nchi aliyozaliwa.
"........ *ujue, basi, ukaone, ya kuwa ni jambo baya sana na uchungu, kuwa umemwacha BWANA, Mungu wako, na ya kuwa moyoni mwako hamna kunihofu*, asema Bwana, BWANA wa majeshi."
KITU KIMOJA AMBACHO WENGI HAWAELEWI ATHARI ZA KUREJEA NYUMA ZINAPINDUA MAMBO AMBAYO YANASIMAMIWA NA PRINCIPLES ZA ULIMWENGU WA ROHO,KWA MFANO HIVI UNAJUA NINI KINATOKEA KWA MALAIKA AMBAO/AMBAYE WAKO/YUKO IN CHARGE KWAKO?(Ebrania 1:14,Zabur 34:7) JE UNAJUA KUWA KUNA MALAIKA WA NURU AMBAO WAKO IN CHARGE KWA WATEULE NA WANAKUWA CAPTIVATED NA MAJESHI YA GIZA KWA SABABU YA WEWE KUTOKUWA KWENYE POSITION?
NDUGU YANGU INAWEZEKANA KABISA KUISHI MAISHA YA SAFATI YA WOKOVU KWA *_KWENDA MBELE MOJA KWA MOJA_*
Ktk Jina la Yesu pokea neema ya kutofia jangwani na uwezesho wa kwenda mbele moja kwa moja.
Mwl Proo
0762879363(whatsapp#)
alltruth5ministries@gmail.com
*_#teamantibackslidecombat#_*
No comments:
Post a Comment