*CHANGAMOTO YA NGUVU YA MWILI KWA KIJANA ALIYEOKOKA, NA NAMNA YA KUUSHINDA, ILI UISHI MAISHA YA USAFI NA KUMPENDEZA MUNGU*
_Mwl Proo_
*0762879363*
©2016
Bwana Yesu asifiwe..
Nianze kwa kusema, ukiona jambo linapokelewa na mwili kwa shangwe na bashasha, mara nyingi linakuwa sio zuri la kuifaa roho. Unaweza panga jambo fulani na ukausikia mwili unakupa support kubwa kumbe mwili ambao ni adui wa roho unajaribu kukukosesha. Kwa mfano unaweza kuamua kutoenda kukesha kanisani wakati kuna mkesha wa pamoja, na ukapata wazo wewe uombe tu chumbani kwako, ukasikia mwili umetoa *go ahead kwa mwendokasi*, kumbe kanisani ungeomba 6hours, lakini kwa kubaki chumbani, unagonga nusu saa kisha unakanyaga mbonji mpaka asubuhi ๐ด๐ด๐ . Mwili na roho vimesimama vikishindana daima (Galatia 5:17). Na katika umri wa ujana ambao mimi kwa mgawanyo usio rasmi lakini kwa kufundishia naweka miaka 16-32, ni wakati ambao mwili unakuwa katika *Climax*, ile nguvu ya mwili inakuwa kubwa mno, ndio maana Mungu anakutaka kwa wakati huo, na shetani naye anakutamani sanaaaaaa wakati huohuo.
Maombolezo 3 : 27
*_Ni vema mwanadamu aichukue nira Wakati wa ujana wake._*
KAMA UNAKUSUDIA KUWA VIZURI KWA MUNGU AU KWA ADUI, BADO MUDA SAHIHI WA KUITWAA NIRA EITHER YA KRISTO AU YA MAMBO MENGINE, NI KATIKA UMRI WA UJANA. MWANAUME MWENYE MIAKA 50 HUENDA HATA UKAMPELEKA DISCO KWENYE CASINO FULANI, ASI-FEEL KILE AMBACHO VIJANA WANA-FEEL. NGUVU YA MWILI YA VIJANA IKO JUU MNO, KAMA NI KUTENDA UOVU AU MAMBO MEMA, KWENYE UJANA NDIO HASWAAAAA MAHALI AMBAPO TUNAPASWA LEO KUPAANGALIA, ILI TUPATE FAIDA YA MAJIRA YA UJANA.
Mwanzo 8 : 21 - Bwana akasikia harufu ya kumridhisha; Bwana akasema moyoni, Sitailaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, *maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake;* wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya.
๐๐ป๐๐ป๐๐ป๐๐ป๐๐ป๐๐ปYaani kuanzia wakati wa ujana ndio mambo yanaanza kuvuruga.
Shetani anaitumia nguvu ya wakati wa ujanani, kuharibu maisha ya watu, kuwatoa kwenye makusudi ya kimungu waliyoandikiwa. Tatizo ni moja, vijana hawajatambua thamani kubwa ya wakati huo walio nao.
BIBLIA INASEMA, MWILI HUTAMANI UKISHINDANA NA ROHO (Gal 5:17), UNATAMANI NINI? MWILI TAMAA YAKE IPO JUU YA MAMBO YOTE YASIYO NA MANUFAA KWA ROHO. HAKUNA MWILI UNAOTAMANI KUFUNGA NA KUOMBA, MWILI UKIUWEKEA RATIBA KWAMBA ASUBUHI SAA MOJA SUPU, CHAPATI TANO NA CHAI YA MAZIWA ๐ฅ๐ฒ๐ฅ, UTAIPOKEA HII RATIBA KWA BASHASHA KUU, UNAWESA STUKA USINGIZINI UKAONA NI SAA NANE USIKU, MWILI UKAONA KAMA KUNACHELEWA KUKUCHA ILI UWAHI VILE VYAKULA. AND ITS VICE VERSA IS TRUE, MWILI HUOHUO, UKIUPANGIA RATIBA KUWA WIKI HII NI MFUNGO, UTATOA VIASHIRIA VINGI VYA KUSONONEKA MPAKA WAWEZA HISI DALILI ZA HOMA.
*NI MUHIMU KUTAMBUA HAYA YAFUATAYO*
HATA BAADA YA KUOKOKA MWILI UKIPEWA NAFASI UNAIZIDI ROHO NGUVU NA UNAANGUSHWA TU KAMA WASIOOKOKA. TUNAPASWA KUWA WAFU KWA HABARI YA DHAMBI (Rumi 6:11), LAKINI MWILI UKIPEWA NAFASI UNAAMKA TOKA USINGIZINI UKIWA NA *FULL MSHAWASHA*, NA LAZIMA UTAENDA NA MAJI. IMEFIKIA WAKATI TUNASHINDWA KUWAAMBIA WATU UZURI WA WOKOVU MAANA VIJANA WALIOKOKA WALINASWA NAO KWENYE NYAVU ZA TAMAA ZA MWILI, UJASIRI WOTE UKAWAISHA. KUNA MAHALI NIMESOMA KATIKA MTANDAO WAMEANDIKA, VITU VIFUATAVYO HUWEZI KUVIPATA KIRAHISI NCHINI TANZANIA :- (1.Binti Bikra, Vyeti vya Bashite etc etc). SIKUSUDII KABISA KULETA HUO MJADALA HAPA, LAKINI NILIFIKIRIA YAANI IMEFIKIA WAKATI HATA WALIOKOKA UKIULIZA NANI HAJAWAHI SHIRIKI NGONO, HUMPATI! TULITAZAMIA VIJANA WALIOOKOKA WOTE WAWE HAWAJAWAHI KUSHIRIKI NGONO LABDA WALE WALIOPITIA MAISHA HAYO KABLA YA WOKOVU. IKUMBUKWE KUNA UMUHIMU MKUBWA WA KUWA BIKRA SAFI WA KIROHO, NA WA KIMWILI KAMA HUJAOA NA KUOLEWA. HAYO YAPATE KATIKA SOMO JINGINE LIITWALO BIKIRA SAFI KWA LINK HII
( http://alltruthjohn1613.blogspot.com/2016/10/bikira-safi.html )
*SASA ILI TUSIENDELEE KUTESWA NA MWILI, HUKU TUKIANGUKA NA KUYAKOSA YALE TULIYOAHIDIWA, NI MUHIMU TUJIFUNZE NAMNA YA KUUSHINDA MWILI KABISA KABISA, MAANA TUPO HURU KATIKA KRISTO (Gal 5:13), NA TUNAZO NGUVU NYINGI (1Yoh 2:14), TUNAWEZA JUA SASA NAMNA YA KUELEKEZANA PA KUZITUMIA NGUVU HIZO.*
*YAFUATAYO NI MAMBO YATUPASAYO KUYAFANYA ILI KUUSHINDA MWILI KWAYO*
MWANADAMU AMEUMBWA NA SEHEMU TATU KUU, MWILI, NAFSI NA ROHO (1Thes 5:23). SASA VITA KUBWA IPO KATI YA MWILI NA ROHO, NA HUYU NAFSI ANASIMAMA KAMA REFEREE (Mwamuzi), KWA HIYO ILI KUWEZA KUSHINDA AU KUSHINDWA, INATEGEMEA HALI YA NAFSI. NAFSI IKIWA IMEJENGWA SANA, ROHO INASHINDA, NAFSI IKIWA IMEHARIBIWA MWILI UTAKUSHINDA TU. KWA HIYO SASA TUJUE NAMNA YA KUIJENGA NAFSI NA MAMBO YANAYOIHARIBU NAFSI. .ILI EITHER MWILI USHINDE AU USHINDWE KUKUANGUSHA
*1.)Kuijenga nafsi*
NAMNA YA KUIJENGA NAFSI*
Kumbuka kichwa cha ujumbe wetu
(1Korintho 14:4,Yuda 1:20,Ayubu 22:23 ,Yer 31:4
Neno "Jenga" ---- Edify (build/construct/instruct,improve morally/intellectually)
*Kama ilivyo sifa/tabia ya nafsi,inajengwa na zipo njia kadhaa za kuijenga
i.)Kukaa na BWANA (Awe rafikiako Isaya 41:8,Mithali 22:11Yoh 15:15)
Isaya 57:15,33:14-24
Zabur 15:1-5,24:3-6
ii.) Kunena kwa lugha/kuomba ktk Roho
>Kunena kwa lugha kuna upinzani mkubwa juu yake ,lakini hii ni _sponsored version_ ya kuijenga nafsi bila gharama (1Kor 14:4)
>Kuomba ktk Roho sio lazima useme kwa lugha za rohoni,unaweza ombs kwa lugha za wanadamu ila utagundua kuwa frequencies zimebadilika,mpangilio wa maneno umebadilika,uvuvio upo sio wa kawaida
Verse 39............ *Wala msizuie kunena kwa lugha*
Verse 18
*Namshukuru Mungu nanena kwa lugha zaidi ya ninyi nyote*
iii.)Mahubiri ya Neno la Mungu kwa wingi
>Sio aina zote za mahubiri zinajenga nafsi,ila yako aina ya mahubri/jumbe ambayo ni edification-based,yako mengine ni knowledge-based n.k
>Ni muhimu kuyasaka kwa bidii mahubiri yenye kujenga nafsi hadi ufike kiwango kizuri cha nafsi kujengwa.
>Ukiwa na neema ya kusoma vitabu vya watumishi wa Mungu,basi fanya hivyo ili ujengeke nafsini mwako
iv.)Kusoma neno la Mungu,kwa wingi (Intensive Bible Reading/Bible study)
Kol 3:16,Yoshua 1:8,Zabur 119:1-176,20,16,14,54,72,77,97,103,111,140,165
v.)Maombi yanayofanywa ktk hali ya kufunga(Fasting&Prayer)
2Kor 4:16,2Nyak 20:3,Ezra 8:21,Zabur 35:13,69:10,109,24.Yer 36:9,Dan 9:3,Yoel 2:12,Yona 3:5.Math 17:21,Luka 2:37,Mdo 13:2,Mdo 14:23,2Kor 6:5,11:27
vi.)Kutumia muda mwingi kwa BWANA, kwa mambo ya Mungu
Neh 9:3,Walitumia masaa 12 mbele za Bwana
Zabur 27:4,122:1,84:10,2,Mhubir 8:3a,1Yohana 3:19
NB
*Watu ambao wametoka kufunguliwa vifungo kama mapepo/majini,magonjwa sugu,hasa ya kurithi au wametoka kwenye vifungo vikubwa vya dhambi na uovu, wanapaswa kuwa mstari wa mbele ktk kujijenga nafsi*
*2.Kuiharibu nafsi*
*HAWA HAPA CHINI, NI MAADUI WANAOIHARIBU NAFSI YAKO, NA KUTOA NAFASI YA MWILI, UKUSHINDE*
*Katika sifa za nafsi tuliona ya kuwa nafsi inaweza kuhribiwa (Kutok 32:27) na kwa kuwa somo linasema "Nafsi iliyojengwa" ni dhahiri kuwa inaweza kuharibiwa
*Maadui wanaoiharibu nafsi wengi wao wanajua umuhimu wa nafsi
*A.)SHETANI*
Shetani akipata nafasi(Efes 4:27) anaweza kuiharibu nafsi kwa kiwango ambacho tiba yake inaweza kuwa na gharama kubwa au ngumu sana .
>Watumishi wake(mawakala/wachawi) Nafsi zao zimehribiwa na shetani,dhamiri zao zimekufa ili waweza kufaa kwa utumishi wa ufalme wa giza
>Hata wakristo ambao wanadumu na viroho vilivyoharibika muda mrefu,Shetani anaziharibu nafsi zao(Ufunuo 2:21)
>Na wale ambao adui akitqk kuwapoteza milele,awe nao Jehanamu,basi hufanya shambulio kubwa la kabisa la Nafsi
*B.)WAKUU WA GIZA/MAJINI(MAPEPO)*
*Kumbuka tunafanya vita na hili kundi (Efes 6:12) ,Wakuu wa giza/majini(mapepo) Wanatabia ya kujenga ngome kwenye fikra(nafsi),hizi ngome (vifungo) hziwi nyepesi kuangushwa mpaka upate maarifa .Ziko tabia chafu zinajengewa ngome(Addiction) -- 2Kor 10:4-7
Tabia zote mbaya zinajengewa ngome na hawa maadui ili kuharibu nafsi
•Uvutaji sigara๐ฌ
•Unywaji pombe๐บ
•Ugomvi/Hasira
•Kusagana/Kujisaga/Kujichua(Masturbation) utazamaji wa pornography etc etc Hizi haziitaji mtu aadhibiwe ili kuacha,wala sii mahali pa kutoa ushauri *NI SWALA LA KUANGUSHA NGOME/KUVUNJA/KUBOMOA NGOME*
*C.)WACHAWI/MAWAKALA WA SHETANI*
Hawa pia wanao uwezo wa kuteka nafsi,kuzitia vifungoni na wanaziharibu ili kuyaharibu maisha ya mtu
*Wanaweza kuitumikisha nafsi na asipopata msaada wa kiroho atapotea kabisa huyo mtu
*Wachawi ni wabaya sana wanakuwa na roho ya Shetani kwa level ya juu,wanaweza kuutenda ubaya kwenye nafsi hata bila sababu,mtoto anaweza kuwa na akili nyingi nafsini mwake,wanamfunga ili ashindwe(Kutok 22:18--- Msimwache mwanamke mchawi kuishi
*D.)MITUME NA MANABII (WA UONGO)*
Manabii/mitume wa uongo wanaweza kuharibu nafsi za watu kwa kuwalisha watu chachu (Mafundisho potofu)
Chachu--Luka 12:1/Yer 5:31
Nabii wa uongo anaweza kukuharibu nafsi jwa kukueleza mambo yanayopingana na kweli ya Mungu
>Mtu wa Mungu toka Yuda na yule nabii Mzee(1Falme 13:14-32)
>Nabii wa uongo Hanania (Yer 28:1-17)
>Nabii wa uongo (Bar-Yesu) Elima mchawi Mdo 13:8ff
*Yesu alipotoa tahadhari ya manabii wa uongo alijua namna wanavyoharibu nafsi (Math 7:15)
*Binafsi niliwahi msikia mtume fulani Dar akiwaruhusu washirika wafanye makosa fulani kwa kigezo kwamba atawatetea mbinguni
*Habari ya mtume mmoja huko Kenya aliyewaambia waumini wa kike wasivae underwears/pants ili Kristo awaingie๐๐
*E.)HALI YA MAISHA(NZURI AU MBAYA),MAKUZI/MALEZI*
Hali ya maisha ina mchango mkubwa ktk kuiharibu nafsi,nafsi ikajikinai au kuchoka n.k (Kumb 8:2-18/ Mithal 30:8--.*usinipe zaidi*)
*Yeshuruni alifanikiwa nafsi ikaharibika (Kumb 32:15
mifano ya watu kama Jack Pemba+Baba Juniour
MALI IKIONGEZEKA MSIIANGALIE SANA MOYONI zaburi 62:10
*F.) MAMBO UNAYOYARUHUSU KUINGIA NAFSINI KWA KUPITIA MILANGO YA FAHAMU*
*Milango ya fahamu macho,pua,ulimi,msikio na ngozi(Macho na masikio hasaa) ni milango mikubwa ya nafsi inayoingiza vitu,na uwe makini sana jinsi unavyosikiliza
Luk 8:18 Jiangalieni jinsi msikiavyo
Rumi 10:17 Basi imani chanzo chake ni kusikia.........)
Linda sana moyo(nafsi) --- Mithali 4:23,Kumbu 28:34(must read verse)
Zab 119:37,Mhub 10:6,1Yoh 5:17
>Ukipendelea kuona/kusoma/kusikia vitu vichafu,vitaharibu nafsi
•Magazeti ya Udaku
•Vipindi vya Tv visivyo na maadili unavyoviruhusu vinaenda nafsi n kujenga kitu kisicho cha kimungu
•Ukifuatilia riwaya na tamthilia za mapeni,nafsi yako utaundiwa kiu ya hayo mambo.
*Kwa hiyo ni lazima uweze kufanya filtering(mchujo),uweze ku-refrain (kujizuia) baadhi ya mambo ili nafsi isiharibiwe
*Ziko movie-series za kisasa za Zombies๐บ๐บ,movies za kichawi๐๐ฟ,Vimpires zimelenga kuharibu nafsi,hivyo lazima ujiponye nafsi.
*G.) WANAWAKE*
Wanawake ni miongoni mwa wenye uwezo wa kuziharibu nafsi. (kama msomaji na mwanamke kwake ibaki tu tahadhali anavyohusiana na jinsi (sex) tofauti... Mithali 31:3,
*Yezebel alimharibu nafsi Ahabu mfalme(soma habari za Naboth)
*Zereshi mke wa Haman alikuwa chanzo cha nafsi iliyojikinai ya Mmewe
>Usirefushe bila sababu mazungumzo na mwanamke (Mithal 7:21)
>Wanawake wanazo nguvu za kuiteka nafsi (Mithali 6:24-29
>Hata yeye.......(Nehemia 13:26)
>Usijione eti una nguvu sana (Mithali 7:10ff)
#Lakini pia unaweza kuwa na viwango ambavyo watu hata wakuone na wasichana hawawazi baya kabisa (Yohana 4:27)
NB:
*WATAWALA WANAWEZA KUZIHARIBU NAFSI*
1Falme 3:2(Mahali pa juu)
>Yeroboam mwana wa Nebati aliwakosesha wana wa Israel
>Watawala wanaweza kuwaingoza watu kinyume na Mungu na kuziharibu nafsi
Yer 5:31
>Wafalme wanaweza kushauriwa na wasaidizi ili kuziharibu nafsi za watu Mithali 29:12
Ili kujifunza kwa upana zaidi mambo haya ya kuhusu nafsi, basi fuata link hii, ujifunze kwa wakati wako mambo ya ziada
http://alltruthjohn1613.blogspot.com/2016/09/jinsi-ya-kuijenga-nafsi.html?m=1
No comments:
Post a Comment