*SEHEMU YA SOMO LA UMILELE (ETERNITY)*
By Mwl Proo
0762878363 (whatsapp)
0718922662
KWELI YOTE SERIES
Vipengele vitatu
*1.Hawa waliofufuliwa Mathayo 27:51-53 ni akina nani walitoka wapi kwenda wapi??*
*2.Nini hakika ya kuwa kila aliyewahi kuwa hai bado yupo mahali hata kama alifia tumboni?*
*3.Nini ukweli kuhusu yanayoendelea baada ya kifo (AFTERLIFE)?*
SASA JAMBO LA KWANZA NATAKA TUFAHAMU.. KILA MWANADAMU ALIYEPATA KUISHI, YAANI ALIKUWA NA PUMZI YA UHAI ILE NAFSI HAI (NEFESH), UJUE BADO YUKO HATA SASA.. HAKUNA ALIYEPATA NAFASI YA KUPOTEA ASIWEPO POPOTE...
Mbegu ziko hai ktk hali yake ya kuwa hai lakini kimsingi maisha/uhai wa kiumbe unaanza wakati wa mimba kutunga (CONCEPTION)!!.
FASIHI ZA KIYAHUDI ZINAMTAMBUA MALAIKA AITWAYE LAILAH, MWENYE KAZI YA KUUTIA UHAI KWA KILE KIUMBE MUDA WA MIMBA KUTUNGWA...
KWA MUJIBU WA JEWISH LITERATURE; UHAI WA MWANADAMU UNAANZIA WAKATI WA MIMBA KUTUNGWA (DURING CONCEPTION). NDIPO AMBAPO ROHO YA MTU INAKUWEPO NA KWA MSINGI HUO HATA MTU AKIFA AKIWA KIJUSI (EMBRYO), BADO KATIKA ROHO MTU HALISI
1 Wathesalonike 5 : 23 - Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili, bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.
SASA NIANZE KWA KUELEZA MWANADAMU AMEUMBWA KWA NAMNA YA AJABU NA KUTISHA (ZABURI 139:14)
MWANADAMU ANA
MWILI
NAFSI
ROHO
KTK 1THES 5:23; MWANZ 2:7
TUNAONA VIMETAJWA VYOTE
Mwili/Body (The outer carcass) Huu upo na mifumo yake na ndio unaurudi mavumbini
Soul (The driving force) hii hujumuisha Akili,utashi ,maamuzi na ina provide linkage kati ya mwili na roho
Spirit (The inner being/real person or personified breath of God)
Hivi vitu vitatu vina siri kubwa sana
BIOLOGY (SCIENCE) INAJADILI VIUMBE HAI HUSUSANI MWANADAMU, LAKINI WAO WAMEISHIA KUELEZEA NUSU KWA SABABU HAWAAMINI KATIKA MAMBO YA ROHO... NA HII ROHO NDIYO ILIYOFUNGIWA UMILELE... MAFUNDISHO KAMA YA SDA YAMEFANANA NA SCIENCE MAANA WAO WAMEKWAMA HAPA MWANZO 2:7 NA KUJUA KUWA KUNA NAFSI NA MWILI NA MTU AKIFA BASI HAKUNA KINACHOENDELEA (AFTERLIFE). HIVYO LEO SAYANSI ITATUSAIDIA KIDOGO MWANZONI LAKINI TUTAIACHA KATIKATI,
SWALI MOJA LA MSINGI JE WANYAMAπ΄ππππ WANA SEHEMU HIZO ZOTE TATU???
ROHO
NAFSI
MWILI ??
Wenzetu wayahudi wana hazina kubwa kuhusu maarifa ya Mungu Yehovah sema sisi tumenufaika kwa kumfahamu sana mwana wa Mungu Yesu Kristo
Huyu Malaika Lailah
Lailah is the angel of the night in
Jewish lore. She has been placed in charge of
conception and is appointed to guard over
spirits at their birth. Another thought states that
she fought for Abraham when he battled Kings.
Hajatajwa ktk Bible ila amehusika ktk matukio mengi ya Biblia
NAOMBA TWENDE KWENYE ETIMOLOJIA(Kujifunza maneno kwa lugha zake za asili)
NAFSI (SOUL)
Kiyunani psuche (breath/the soul) matamshi yake kifonetik ni psoo-khay hili ndilo neno Psyche(mind) inayotumika kwenye Psychology
Kilatini
Anima(the breath of life) or the vital force which animates the body and shows itself in breathing. Na kiebrania ni Nefesh
Roho/Spirit
Hebrew :Ruach
Greek: Pneuma
Hii roho ndio mtu halisi,mtu wa ndani au pumzi ya Mungu iliyofanyika mtu
Lakini mwili ambao unatajwa kama Basar (Kiebrania),au Soma (kiyunani) haya ndiyo mavumbi jina Adam maana yake mtu na neno hilo Adam linatokana na neno Adama=Udongo
SASA LEO TUTAJUA TOFAUTI YA HIVI VITU KIBIBLIA
NILISEMA KUWA YUKO MALAIKA WA MUNGU (LAILAH), ANAYEDILI NA KUWEKA ROHO DURING CONCEPTION YAANI KUTINGISHA MIMBA HII INATOKEA KILA MBEGU ZINAPOKUTANA NA YAI NA KULIRUTUBISHA... HII SIO LAZIMA IWE WANANDOA... HATA BINTI AKIBAKWA LILE TUKIO LA MBEGU KULIFIKIA YAI TUU HAPOHAPO MALAIKA HUSIKA MWAMINIFU KWA KAZI HIYO ANAHUSIKA NA HILI JUKUMU.
KUNA BINTI ALISHIKA UJAUZITO HUKO U.K KWA KUOGEA SINK AMBALO BABA YAKE ALILIONGEA BAADAE MADAKTARI WALIGUNDUA KIASI KIDOGO CHA SPERMS ZILIMWINGIA MAANA MBEGU ZA KIUME HUWA HAI HADI MASAA 48 ZIKIWA NJE
LEO NITAWASHANGAZA KIDOGO MWANADAMU
ANA MWILI (MZOGA WA NJE)
MAFSI (DRIVING FORCE)
NA ANA ROHO ... HII ROHO NDIO MTU HALISI AMBAYE HANA MWISHO WAKE NA HAKUNA ROHO ILIYOWAHI KUPOTEA TANGU KUUMBWA KWA ADAMU HATA SASA... WANADAMU WOTE WAPO HATA WALIOANGAMINZWA ZAMA ZA NUHU.
Sasa andiko la Eze 18:20 linasema roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa je ni roho au nini??
Kilichotaja roho ni Biblia ya Kiswahili kama ambavyo pahala pengi imechanganya Soul/Spirit/heart
Katika Vulgate (Latin Bible Version) pamendikwa "Anima" ambayo sio roho
SASA MNYAMA HANA ULE UTU WA NDANI AMBAO NDIO REAL BEING ULIOFUNGWA NA UMILELE..
MNYAMA ANA MWILI(BASAR) NA ANA NAFSI YA UHAI (NEFESH) ILA HANA RUACH/PNEUMA (Eternal being) YA ROHO ILE YENYE UMILELE WOTE
SYSTEMS ZA MWILI ZIKIGOMA AKAFA BASI NDIO MWISHO... LAKINI SIVYO KWA MWANADAMU KIFO KIKITOKEA KWA SABABU YOYOTE ILE, ROHO INATOKA AU INATOLEWA HAYO YOTE MAWILI NI SAHIHI...
SIKU MOJA KUNA PASTOR ALIWAHI KUSEMA MTU ANAWEZA BADO KUWA HAI HATA KAMA ROHO IMETOKA...WATU HAWAKUELEWA NA HAWAKUHOJI...LEO NITAFAFANUA
Muhubiri 3
_*11 Kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake; tena ameiweka hiyo milele ndani ya mioyo yao; ila kwa jinsi mwanadamu asivyoweza kuivumbua kazi ya Mungu anayoifanya, tangu mwanzo hata mwisho.*_
NASHAWISHIKA KUWA MBINGUNI HAKUNA WANYAMA, WALE WALIOPO (KAMA HII NI KWELI) HAWAJAPAA WALA KUFUFULIWA WALIUMBWA KWA UTUKUFU WA MUNGU HUKO
YONG CHO (KATIKA KITABU CHAKE CHA "HEAVEN IS REAL") AMESEMA ALIONA WANYAMA+VIUMBE KAMA SAMAKI
LAKINI KWA ULE MJI MPYA TWAAMBIWA WALA HAPANA BAHARI....UFUNUO 21:1ff
NO ANIMALS...HAKUNA WANYAMA (isaya 35:9)
Yah God has set eternity (umilele) in the hearts of men!! Ecc 3:11 NIV
Ni sisi wanadamu kati ya viumbe vya duniani, tumewekewa umilele..
BINADAMU NA VIUMBE HAI VINGINE MWISHO WAO NI KIFO...
HATA WATU MNAOFUATILIA SOMO HILI, KAMA YESU HATARUDI NDANI YA MIAKA 200 TOKA LEO TUWE NA HAKIKA WOTE TUTAKUFA.
NAPINGANA SANA NA ULE USEMI WA KILA NAFSI ITAONJA MAUTI...HILO SIO ANDIKO LA BIBLIA NI QURAN (Surat Imran Quran 3:185).. MSIMAMO WA BIBLIA NI HUU
1KOR 15:51-52
Mathayo 27:51-53
Ni moja kati ya aina za ufufuo
UFUFUO
Etimolojia yake:
1.)-Anhistemi
-Ageiro
2.) -Anastasis
-exana
SASA KATIKA MATHAYO 27 HUU UFUFUO UNAJULIKANA KAMA "ANABIOSKOMAI" YAANI (TRANSMIGRATION OF SOULS)
UFUFUO HUU ULIHUSISHA KUZIHAMISHA ROHO TOKA SEHEMU MOJA HADI NYINGINE.
SASA NIKUMBUSHE KUWA WATU WOTE WALIOKUFA KABLA YA KUFUFUKA KWA YESU, WENYE HAKI NA WASIO HAKI WOTE WALIENDA KUZIMU.
KISA CHA 1SAMWEL 28:7-18 TUMEKUWA NA UTETEZI WA KILOKOLE KUWA YULE HAKUWA SAMWELI HALISI, NA KUWA YULE MGANGA HAWEZI KUMRUDISHA NABII WA BWANA!!
SASA NASHAWISHIKA YULE ALIKUWA NI SAMWELI HALISI
KWA NINI?... DHAMBI YA ADAMU ILIMMILIKISHA SHETANI MAMLAKA JUU YA WANADAMU ... YULE MGANGA BIBI WA ENDORI ALIWEZA KUMPANDISHA SAMWELI TOKA KUZIMU...
SASA TUTAENDA KUJIFUNZA KUZIMU ILIKUWA NA MUUNDO GANI??
*KWELI KUHUSU KUZIMU (The idea of Hell)*
*kuzimu ni idea pana sana kuliko ambavyo wengi wanadhan8
*Watu wote waliokufa tangu enzi za Adamu walienda kuzimu!
*Shetani alikuwa na mamlaka kisheria juu ya roho za wanadamu, kwa sababu ya kosa la Adamu
*Lakini kuzimu tangu mwanzo ni mahali pa Shetani
Ezekiel 28:1-19
Isaya 14:9-23
Ibrahimu alikuwa kuzimu (Luka 16:19-26)
Samweli nabii alikuwa kuzimu (1Samwel 28:1-20)
MUUNDO WA KUZIMU:
SHEOL/HADES- The more neutral place Zaburi 16:10
ABUSSOS--Hili ni shimo kubwa la kuzimu lisilo na mwisho na hapa ndio makazi ya mapepo (Luka 8:31, Ufunuo 9:1-2)
CHASM -Kuzimu/Shimo kubwa linalotenga na mahali pengine nitafafanua vizuri (Luka 16:26)
TARTARUS (2Petro 2:4) this is the gloomy dungeon(gereza la chini lenye giza) ambapo malaika waliotenda dhambi walifungiwa (Yuda 1:6).
Lakini chanzo kingine kimedokeza, ndipo wanapoteswa waovu kwa sasa.
GEHENNA(Greek) GEHINNOM (Hebrew) Hii ndiyo sehemu ambayo ktk uislamu na ukristo ndipo waovu wanaenda... Ktk Quran inaitwa Jahannam ndipo mahali pa mateso for sinners and non-believers
Hili jina Jehanam linatokana na Bonde la mwana wa Hinomu yana Ben Hinomu, kuna transliteration fulani inayofanywa hadi kuitwa Jehanamu..
THERE IS A FINAL HELL MAARUFU KAMA JEHANAMU YA MOTO, HII NI SEHEMU TOFAUTI NA SEHEMU ZILIZOTANGULIA NI MAHALI PA MWISHO PA SHETANI, MALAIKA ZAKE NA WOTE AMBAO HAWATAONEKANA MAJINA YAO KWENYE KITABU CHA UZIMA (Na hata hilo jina Gehena linataja mahali hapa, kwa sasa hakuna aliyehukumiwa humu mpaka wakati wa *White Throne Judgement*).
UFUNUO 20:10
Mauti na kuzimu zitatupwa ktk ziwa la moto...Ufunuo 20:14
SASA WENYE HAKI WALIPOKUFA WALIENDA SHEOL, SEHEMU HII NI MASHUHURI KAMA ABRAHAM'S BLOSOM ... KILA SEHEMU MOJA NA NYINGINE ZILITENGWA NA MABONDE MAKUBWA, AMBAYO MTU HANGEWEZA KUVUKA KUHAMIA KWINGINE!!
DINI ZA DUNIANI HASA ZILE KUBWA YAANI
BAHA'I
BUDDHISM
CHRISTIANITY
FREEMASONRY
GOTHIC
GNOSTICISM
GRIMOIRES
HINDUISM
ISLAM
JAINISM
JUDAISM
MORMONISM
NATIVE AMERICAN
NEOPAGANISM/WICCA
SHAMANISM
SHINTO
SIKHISM
TAOSM
Dini zote hizi zina maelezo yao kuhusu nini kinaendelea baada ya kifo..
Mie nitachambua makundi mawili tu kwa leo...
KUNA SHERIA ZINAZOONGOZA MAMBO KATIKA ROHO, KWA HIYO SHETANI KWA SHERIA HIZO ALIMILIKISHWA VYOTE KWA KOSA LA MTU WA KWANZA.
WAKATI WA YESU KUJARIBIWA SHETANI ALIPRUVU HILO (LUKA 4:1-11). ALIMUONESHA YESU FAHARI YOTE YA DUNIA KWA DAKIKA MOJA.. AKAMWAMBIA HIVI VYOTE NI VYANGU NAMI HUMPA YEYOTE NIMTAKAE... SASA YESU HAKUBISHA KUWA SIO VYAKO HIVI ...INGAWA ANAJUA SHETANI HAKUUMBA HATA INZI , LAKINI YESU HAKUBISHA KWA KUWA KISHERIA ZILE ZA ROHONI ...SHETANI ALISEMA FACT!
IMANI ZOTE ZENYE MUUNGANIKO NA IBRAHIMU YAANI ABRAHAMIC FAITH HII NI PAMOJA NA UISLAMU, UKRISTO, NA JUDAISM ZINAAMINI KUHUSU BAADA YA KUFA KUNA MAISHA.. ZILE IMANI ZINGINE ZINAZOITWA DHARMIC FAITH IKIWEMO HINDUISM/BUDDHISM NAO WANAYO YAO!!
HAWA KWA MFANO WAHINDU WANA FUNDISHO LIITWALO SAMSARA YAANI REINCARNATION (REBIRTH), WAO HUAMINI MTU AKIFA ANAZALIWA TENA MAHALI PENGINE, YAANI KAMA ULIKUWA MTU MWEMA NA MKARIMU BASI UNAWEZA UKAZALIWA UKAWA MBUNGE AU WAZIRI AU MTU MASHUHURI. ILA KAMA ULIKUWA MTU MBAYA NA MUOVU ,BASI UTAZALIWA TENA UKIWA NI PAKA AU MBWA ππ SEHEMU INGINE. (Haya utayapata kwa kina kwenye somo langu, lisemalo _*"Imani ipi kati ya dini za dunia ni ya kweli?"*_
SASA JE UKRISTO UNASEMAJE???
*WHAT REALLY HAPPENS AT DEATH (Nini kinatokea muda mtu anakufa)*
Ni muhimu kukumbuka mtu halisi ni roho
Ndio maana utasikia kwenye msiba wanasema mwili wa marehemu...
Yaani yuko mwenyewe mtu halisi hayupo ila mwili wake tuu umebaki.
MAITI WA MTU ni lugha inayotumika kibiblia.
Hesabu 9 : 7 - Sisi tu hali ya unajisi kwa ajili ya maiti wa mtu; nasi tumezuiwa kwa nini hata tusipate kumtolea Bwana matoleo kwa wakati wake ulioagizwa, kati ya wana wa Israeli?
KWA MARA YA KWANZA TUNAKUTANA NA USEMI WA ROHO KUTOKA KWENYE KIFO CHA RAHELI
Mwanzo 35
17 Ikawa alipokuwa anashikwa sana na utungu, mzalisha akamwambia, Usiogope, maana sasa utamzaa mwanamume mwingine.
18 Ikawa hapo katika kutoa roho yake, maana alikufa, akamwita jina lake Benoni, lakini babaye alimwita Benyamini.
Maandiko tuliyosoma yanaonesha roho inatoka au inatolewa yote ni mawili ni halali kuyatumia. Roho haiguswi na mateso yanayoupata mwili. Aliyeliwa na simba au kukanyagwa na gari, roho inabaki bila madhara.
*Roho ikiona haiwezi kuutumia tena mwili (Body-the outer carcass) inatoka yenyewe...
HIZO SHUHUDA AMBAZO NITAZITUMIA SIO ZILE ZA WALOKOLE ZENYE UTATA-UTATA KIDOGO, NA WENGINE HATUWAAMINI LABDA AKINA NYISAKI, AKINA KULOLA AKINA DOMITILA ETC. SHUHUDA AMBAZO NINAZITUMIA NILIZITOA KWENYE KIPINDI CHA ABC NEWS AMBAO WANA KIPINDI KIITWACHO BEYOND BELIEF, AMBACHO WANAWAHOJI WATU WENYE VYETI VYA VIFO ILA ILITOKEA WAKAURUDIA UHAI
SHUHUDA ZA WALIOWAHI KUKATA ROHO, NA KURUDIA TENA MWILI WALIELEZA; ROHO INAWEZA KUBAKI HATA DAKIKA 15 IKIWA AROUND, ILA HAINA CONNECTION NA VISIBLE WORLD...
YAANI ANAWEZA AKAWA BADO YUPO KWA JUU, ANAONA ZILE HARAKATI ZA MANESI NA MADAKTARI YEYE AKIWA KWA JUU ANAUONA NA MWILI WAKE ILA HAWEZI KUUFUATA WALE KUWASILIANA NA ULIMWENGU HUU
HIYO WAMEISHUHUDIA WATU WATU KADHAA SIO WOTE DAK 15 ZINAFIKA ILA WENGI ROHO IKIJICHOMOA KWA MWILI UNAWEZA ONA HUU MWILI WAKO ULIOUVUA KAMA KOTI... SASA TUTAYAONA HAYO MBELE YA SAFARI
Ayubu 7 π
9 Kama vile wingu likomavyo na kutoweka,Ni vivyo huyo ashukaye kuzimuni hatazuka tena kabisa.
10 Hatarudi tena nyumbani kwake,Wala mahali pake hapatamjua tena.
OK MSIMAMO WA BIBLIA NI KWAMBA WATU WAKIFA WAKISHUKA KUZIMUNI HAWATAZUKA TENA ... HAWATARUDI NYUMBANI KWAO
NA HIYO ISAYA INATUJULISHA THERE IS A DISCONNECTION KATI YA WAFU NA WALIO HAI
SASA KABLA SIJAENDELEA NIWEKE SAWA ISHU YA MIZIMU/GHOSTS
Isaya 8 π
19 Na wakati watakapokuambia, Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunongona; je! Haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? Je! Waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai?
KWANZA KABISA... TUKIO LA YESU KUBADILIKA SURA (TRANSFIGURATION) LINATUTHIBITISHIA KUNA MAISHA BAADA YA KUFA...
TUKIWAONDOA HENOKO NA ELIYA KTK BIBLIA HAKUNA RECORD YA MWANADAMU MWINGINE AMBAYE HAKUFA YAANI ALIRITHI KUTOKUHARIBIKA KWA MWILI WENYE KUHARIBIKA KUBADILISHWA TU... LABDA KAMA WALIBADILISHWA MUDA WA KUTWALIWA AU TUAMINI SHULE YA FIKRA KUWA WALE MASHAHIDI WAWILI WA UFUNUO NI HAWA WATU...HILO LA UFUNUO TUTALICHEKI NEXT TIME
*MZIMU UNAKUWAJE?*
WAKO WATU WAMEUNGANISHWA NA UFALME WA GIZA KUTOKANA NA MIZIMU (ANCESTRAL SPIRITS) ... UTASIKIA MTU ANASEMA BABU KANITOKEA KANIAGIZA KUFANYA HILI NA LILE.. UKWELI NI KWAMBA, HAKUNA MTU ALIYEKUFA ANAPEWA HIYO NAFASI...
MIZIMU INATOKANA NA NINI?
KAMA MTU AMEKUFA LAKINI WAKATI WA UHAI WAKE ALIKUWA NA PEPO WACHAFU (DEMON-POSSESSED) AKAFA AKIWA HAJAFUNGULIWA KIFUNGO CHA πΉπΉπΉπΉ NDIPO WALE PEPO WANAFANYA IMPERSONATIFICATION KWA KUICHUKUA SURA YA YULE MTU NA KUWATOKEA JAMAA ZAO KWA MFANO WA YULE ALIYEKUFA... AFRICA HILI NI JANGA LA KIBARA... NILITUMIA MUDA MWINGI KUSOMA KUHUSU A.T.R (AFRICAN TRADITIONAL RELIGION), KULIKO UKRISTO SO NAELEWA HII ISHU SHETANI KAWAPIGA BAO WAAFRICA WENGI SANA... HADI LEO KUNA WATU WANATEKELEZA MAAGIZO ETI MAREHEMU MAMA ALIWAHI KUNITOKEA AKANIELEKEZA NIWE NAFANYA HILI... MUDA WANAENDELEA KUTII MAAGIZO THEY BECOME MORE AND MORE INITIATED KWA EVIL POWERS NA KUTESWA SANA... BILA WAO KUJUA CHANZO
KWENYE TUKIO HILO TUNAONA ELIYA (ALIYEPAA) NA MUSA (ALIYEKUFA) WOTE KWA PAMOJA WANAKUJA KUKUTANA NA YESU... (kumbu 34:5-6, math 17:2-3)
SWALI KAMA ELIYA ALITOKA MBINGUNI JE MAREHEMU MUSA ALITOKA MBINGUNI AU KULE SHEOL YA KUZIMU??
[12:37, 16/01/2016] mwl proo: *SEHEMU YA TATU*
(YANAYOENDELEA MARA BAADA YA ROHO KUTOKA)
HAPA TUTAJADILI KWA UPANA KWANZA... UWEZEKANO WA ROHO KUTOKUWEPO KTK MWILI LAKINI BADO IKAWA SIO KIFO... LAKINI PIA TUONE NA KUHUSU KIFO CHENYEWE HAPA NDIPO TULIPOISHIA LAST TIME!
ROHO KAMA MTU HALISI WA NDANI ANAWEZA AKAONDOKA WALA ISIMAANISHE KIFO...
TULIPEWA KISA HUMU CHA ROHO YA ELISHA KUAMBATANA NA GEHAZI INGAWA YEYE ALIKUWA AMEBAKI HOMEπ‘ KIMWILI...
SASA NISEME KUNA VIWANGO VYA KIUNGU TUNASHINDWA KUOPARET KWA KUWA HATUNA MAARIFA HUSIKA... KTK MAMBO HAYA YA NAFSI, ROHO NA MWILI HATA WACHAWI WAMETUZIDI WANA WA NURU MAARIFA. WACHAWI WENYE VIWANGO... WANAWEZA KUZIRUHUSU ROHO ZAO KUTOKA NJE YA MWILI WAKAENDA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO MAENEO YA MBALI NA BADAE WAKAIRUDIA MIILI YAO... HII NDIO ILE PSEUDO-SCIENCE.. MWAKA 1994 NILITEMBELEA KIJIJINI KWETU.. TUKIWA HUKO TULIKUWA TUNALALA NJE YA NYUMBA NA HUO NDIO UTARATIBU
SASA NILIKUTANA NA VISA VYA AJABU.. MVUA INAWEZA KUNYESHA USIKU WA MANANE MKASHANGAA MTU MWINGINE HATOKI ILA NI KAMA YUPO HAI... SASA WENYEJI WANAOELEWA WATAKUZUIA, " USIMWAMSHE HUYO HAYUPO" SASA WANAKUWA WANAJUA YULE MHUSIKA MWENYEWE KAUACHA MWILI WAKE NA ILE HUMAN-SPIRIT IMEENDA KAZINI. ELIMU YA MISUKULE INATUMIA SANA MAARIFA YA MWILI, NAFSI NA ROHO.. HATA PEPO WACHAFU WAKIMPAGAWA MTU WANAI-POSSESS NAFSI YAKE AMBAYO NDIYO DRIVING FORCE NA NDIO MAANA PEPO WAKIPANDA MTU HUTUMIA KINYWA CHAKE HUYO MTU NA VIUNGO VINGINE... LAKINI ROHO YA YULE ALIYEKAMATWA NA PEPO INAKUWA IMEFUNGWA KTK HALI FULANI JINSI YA KUELEZA NI KWAMBA MTU ANAKUWA "IN TRANCE" WENGI MARA BAADA YA PEPO KUTOKA AKIRUDI YEYE KTK UHALISIA ANAKUWA HAJUI YALIYOTOKEA.. UKIMHOJI KUMBUKUMBU ZAKE ZILIISHIA MUDA ANAANGUKA AU MUDA KAHISI KUSUKWASUKWA NA YULE PEPO
[12:37, 16/01/2016]mwl proo: JE NINI UKWELI KUHUSU HILI LA ROHO KUTOKUWA KTK MWILI... HATA KWA MATUMIZI YA UFALME WA MUNGU? TULIPASWA KUFUNGUKA FAHAMU KUWA UKITAKA KUFANYA MAJUKUMU FULANI NJE YA MWILI KWA UWEZO WA ROHO MTAKATIFU UNAWEZA KUUACHA MWILI UKAENDA ZAKO SEHEMU HUSIKA.. SEMA SHIDA YETU NI KUAMINI, KUKOSA MAARIFA NA HOFU!
MTUMISHI FULANI HAPA TANZANIA ALIWAHI KUSAFIRI KWA ROHO TOKA MWANZA HADI MBEYA BILA ✈ WALA π KWA NAMNA ILEILE YA MWINJILISTI FILIPO KTK MATEDO SURA YA 8 .. MARA NYINGI ANASEMA HAPENDI KUTOA USHUHUDA HUO MAANA WAPO WATAKAOACHA KUMWANI KABISA... SHIDA YETU NI KUAMINI... YUKO MCHUNGAJI ALIYENILEA MIAKA YA 2004 NIKIWA PUGU SEKONDARI ALINIAMBIA ALIWAHI KUFUATWA ANASAKWA AKAMATWE... AKAKAA KITANDANI AKASEMA ROHO NIFICHE WASINIONE.. WALIINGIA KWENYE CHUMBA CHAKE WANAANGALI PALE ALIPOKAA YEYE ANAWAONA ILA WANAJADILIANA HUMU HAYUPO... HAKUJIFICHA ALIKAA TU KWA WAZI KWENYE KITANDA
[12:41, 16/01/2016] proo: OK NIENDE KWENYE MATUKIO HALISI ZAIDI.. ROHO MTAKATIFU ALIKUSUDIA KUNIFUNDISHA HII KITU KABISA KABISA.. NAKUMBUKA TUKIO LA PILI MWAKA 2012 NIKIWA CHUONI.. ILIKUWA JUKAPILI MCHANA.. NILIONGOZANA NA WATUMISHI WA MUNGU WAWILI.. MWINJILUSTI MMOJA ALIKUWA KATIKATI KWA GHAFLA TUKAMUONA ANATABASAMU NA KUMUANGUKIA YULE MTU WA TATU NA MKONONI ALISHIKA BEGI LA LAPTOP NIKALIWAHI LISIDONDOKE.. TUKAMSAIDIA KWA KUMSHIKA HADI MAHALI ANAPOWEZA KUKAA.. KWA ZAIDI YA NUSU SAA TULIKAA NAYE AKIWA ANATUTAZAMA LAKINI HANA USHIRIKIANO NA CORPOREAL WORLD... YAANI SIMU YAKE ILIITA MFUKONI TULIITOA SISI KUIPOKEA.. BAADA YA NUSU SAA NI KAMA ROHO ILILEJEA... MIMI KWA MACHO YANGU NILISHUHUDIA MOVEMENT FULANI KTK MWILI WAKE HATA VIUNGO VYAKE KAMA MASIKIO PUA NA NGOZI ILISHAKE KWA NAMNA FULANI... THEN AKAANZA KUONGEA KWA UCHANGAMFU AKITUAMBIA WATISHI TWENDENI MULTIPURPOSE HALL ETC ETC.. TULINUIA TUSIMHOJI MASWALI.. TUKIWA TUMEKAA NAYE ROHO MTAKATIFU ALITUZUIA TUSIMPELEKE HOSPITALI YA CHUO WALA KURIPOTI
SIKU YA PILI NILIMHOJI JANA KULITOKEA NINI TUKIWA NJIANI... SASA HUU NDIO ULIKUWA MWANZO WA MIMI KUMTAKA ROHO WA KWELI ANIPE ELIMU HAPO.. AKASEMA HAJUI YALIOENDELEA HUKU NJE... ILA TUKIWA TUNATEMBEA ALIJIONA AMEBAKI PEKEAKE KTK ULIMWENGU MWINGINE NA AKAONA ANASHINDANA SANA NA MABAUNSA πͺπΌππΏ NA MUDA HUO TULIKUWA KTK MAANDALIZI KWENDA GOSPEL OUTREACH KTK KISIWA CHA MAFIA NA YEYE NDIO MHUBIRI... SASA KWA MAELEZO ALIYONIPA NA NILIPOENDA KUOMBA ROHO ANIFUNDISHE NDIPO NIKAHUNDUA ROHO YAKR ILITOKA KABISA TULIBAKI NA MWILI NA NAFSI(BASAR+NEFESH) ILA HAKUWA AMEKUFA NA ROHO YAKE ILIKUJA IKAUINGIA MWILI TENA.. NA MUDA HUO WOTE ZAIDI YA NUSU SAA ALIKUWA ANATAZAMA ILA HAKUTOMACHOπ³ BALI ILIKUWA NI KAMAANA☺ANATAZAMA KWA MBALI AS IF KUNA VITU DEEP ANA MEDITATE AU YUPO KTK YOGA. NAUNDA MSINGI ILI WATU TUJUE KUWA MARA BAADA YA ROHO KUUCHA MWILI HAIPOTEI BALI SASA UNAUINGIA ULIMWENGU HALISI WENYE MAMBO HALISI ZAIDI... WATU WANAOKUFA KILA SIKU WANA UELEKEO FULANI..
KUTOKA KTK VYANZO VYOTE VYA VIFO YAANI
1. BIOLOGICAL AGING
2. PREDATION
3. MALNUTRITION
4. DISEASE
5. SUICIDE
6. MURDER
7. ACCIDENTS OR TRAUMA RESULTING IN TERMINAL INJURY
KUTOKA VYANZO HIVI TAKWIMU ZINAONESHA WATU 150, 000 HUFA KILA SIKU DUNIANI AMBAYO KWA MIJIBU WA BENJAMIN FRANKLIN NI WATU 108 WANAKUFA KILA DAKIKA MOJA INAYOPITA... SASA ILI JAMBO NI SERIOUS HATUNA BUDI KUZAMA HAPA KUJIFUNZA SIO ILI KUJITIA HOFU BALI TULIJUE TUMAINI KUWA MTI UKIKATWA WAWEZA CHIPUKA(AYUBU 14:7ff)
TUKUMBUKE KIFO KWA SASA NDIO NJIA YA KUUINGIA UMILELE.. MWAKA 2007 NILIOTESHWA NDOTO ILI NIJIFUNZE ZAIDI.. NILIOTA NIMESIMAMA MLANGONI NIMEUMWA KICHWA NIMEANGUKA CHINI NA KUFA... THEN NIKAYASHUHUDIA BAADHI YA MAMBO AMBAYO HUTOKEA MTU AKITOA ROHO YAKE...
MARA YA MWISHO JUZI NILIFIKA MAHALI NILIPOELEZA KUWA WATU WAKIFA HAWANA NAFASI KURUDI TENA DUNIANI (LABDA AFUFULIWE, MAANA UFUFUO NI HALISI) UFUFUO UNA MAKUNDI MAWILI AMBAYO MECHANISM YAKE INAHITAJI VIWANGO TOFAUTI.. KUMFUFUA MTU AMBAYE HUU MWILI WAKE WA NJE UMEOZA NA KUMFUFUA MTU AMBAYE AMEITOA ROHO YAKE TU NA MWILI UPO SAWA KAZI IKO TOFAUTI HAPO... NA VIWANGO NI TOFAUTI.. AGANO LA KALE KUNA MIUJIZA MITATU YA KUFUFUKA NA AGANO NA AGANO JIPYA KUNA MIUJIZA SITA YA UFUFUO.. LAKINI ULE WA LAZARO KTK YOHANA 11 NI TOFAUTI NA YOTE MAANA MTU WA NJE ALIKWISHA DECOMPOSE!
INAENDELEA........
[12:58, 16/01/2016]mwl proo: SAWA YESU PIA ALILFUFUKA... ILA YESU INGAWA MWILI WAKE ULIMALIZA SAA 36 ILA HAUKUOZA... ILI UTIKIMIE UNABII..... ZABURI 16:10 UHARIBIFU(DECAY/DECOMPOSITION OF THE MATTER)
[12:58, 16/01/2016] proo: AYUBU 7:9 INATUONESHA UKWELI KUWA ALIYEKUFA HAPASWI KURUDI TENA... SASA OPTION YA KWANZA NI KUFUFUKA... YA PILI MTU ANAWEZA PEWA NAFASI KWA KUWA ALIKUFA NA KWENDA MAHALI PAZURI... KURUDI KWAKE NI EXCEPTIONAL CASE.. MUNGU ANAWEZA RUHUSU KWA KUSUDI MAALUM.. NA HII ATAIFANYA KWA WATU WAMEKOMAA ROHONI... HAPA TUSIJENGEE FUNDISHO MAANA NI RAHISI SANA SHETANI KUCHEZA DILI LA KUTUINGIZA KTK IMANI YA MIZIMU...
MUNGU HANA UPENDELO (RUMI 2:11, MDO 10:34) LAKINI IN A VERY RARE CASE ANAWEZA AKAITOA NAFASI KWA MTU AMBAYE HAKUWAHI KUIJUA NJIA... HII NI NADRA SANA ILA INAWEZA TOKEA HATA KAMA NI MARA MOJA KWA MILENIA SAWA TU.. NITAELEZA MATUKIO HAYA KWA USAHIHI WAKE .. NAJUA KUNA MAENEO TUTATOFAUTIANA BUT KTK NIPO TAYARI TUAPPLY FORMULA YA "AGREE TO DISAGREE"
[12:58, 16/01/2016]mwl proo: USHUHUDA WA KWANZA:
MIAKA SITA ILIYOPITA TULIKUWA NA MZEE WA KANISA MWAMINIFU SANA KWA MAMBO YA MUNGU.. KILA MTU ALITAMANI HALI YAKE YA KIROHO.. ALIKUWA NI ASKARI WA WANYAMAPORI WIZARA YA MALIASILI ILIMHAMISHIA MTWARA HUKO NDIKO UMAUTI ULIMKUTA.. WALIENDA KUKAMATA MAJANGILI WALIOKUWA NA NYARA ZA SERIKALI.. LAKINI WALE MAJANGILI WALIWAGEUKA NA KUWAITIA WIZI NA UJAMBAZI... HUYU MZEE WETI WENZAKE WAKAMKIMBIA... NA AKABAKI MWENYEWE THEN WANANCHI WAKAMSONGA WENGI SANA.. AKAPIGA RISASI JUU ILI WATAWANYIKE ILA WAO WALIAMINI NI JAMBAZI... WAKAMZIDI NGUVU WAKAMKATA KWA MAPANGA AKAFA..
WIKI MOJA BAADA YA MAZISHI MKEWE AMBAYE NAYE KIROHO ALIKUWA JUU SANA.. AKAWA ANAMHOJI MUNGU AKIWA IN GREAT AGONY ANAUGUA KUNAKOWEZA KUTAMKWA ILA ANAUGUA SANA.. MOYONI AKASIKIA GEUKA NYUMA.. AKAMUONA MME WAKE AMESIMAMA ... NA AKAZUNGUMZA NAYE.. HUYU MMEWE MAREHEMU AKAMWAMBIA HUNA HAJA YA KULIA ZAIDI MIMI NIKO HAI .... ILA TU SINA UWEZO KUJA HUKU MLIPO .. AKAMUONESHA HADI MAENEO AMBAKO ALIPIGWA MAPANGA NA YALE MAJERAHA YA MAUTI YANAONEKANA KUPONA.. SASA HAPO KUNA SIRI KUHUSU MWILI WA ROHO (1KOR 15:35-58
TUTAENDELEA BAADA YA MUDA... ENDELEA KUDAIJEST NA KUANDAA MASWALI
[12:58, 16/01/2016]mwl proo: 1Korintho 15 π
35 Lakini labda mtu atasema, Wafufuliwaje wafu? Nao huja kwa mwili gani?
36 Ewe mpumbavu! Uipandayo haihuiki, isipokufa;
37 nayo uipandayo, huupandi mwili ule utakaokuwa, ila chembe tupu, ikiwa ni ya ngano au nyingineyo;
38 lakini Mungu huipa mwili kama apendavyo, na kila mbegu mwili wake.
39 Nyama yote si nyama moja; ila nyingine ni ya wanadamu, nyingine ya hayawani, nyingine ya ndege, nyingine ya samaki.
40 Tena kuna miili ya mbinguni, na miili ya duniani; lakini fahari yake ile ya mbinguni ni mbali, na fahari yake ile ya duniani ni mbali.
41 Kuna fahari moja ya jua, na fahari nyingine ya mwezi, na fahari nyingine ya nyota; maana iko tofauti ya fahari hata kati ya nyota na nyota.
42 Kadhalika na kiyama ya watu. Hupandwa katika uharibifu; hufufuliwa katika kutokuharibika;
43 hupandwa katika aibu; hufufuliwa katika fahari; hupandwa katika udhaifu; hufufuliwa katika nguvu;
44 hupandwa mwili wa asili; hufufuliwa mwili wa roho. Ikiwa uko mwili wa asili, na wa roho pia uko.
45 Ndivyo ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha.
46 Lakini hautangulii ule wa roho, bali ule wa asili; baadaye huja ule wa roho.
47 Mtu wa kwanza atoka katika nchi, ni wa udongo. Mtu wa pili atoka mbinguni.
48 Kama alivyo yeye wa udongo, ndivyo walivyo walio wa udongo; na kama alivyo yeye wa mbinguni, ndivyo walivyo walio wa mbinguni.
49 Na kama tulivyoichukua sura yake yule wa udongo, kadhalika tutaichukua sura yake yeye aliye wa mbinguni.
50 Ndugu zangu, nisemayo ni haya, ya kuwa nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu; wala uharibifu kurithi kutokuharibika.
51 Angalieni, nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote tutabadilika,
52 kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.
53 Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa.
54 Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa kwa kushinda.
55 Ku wapi, Ewe mauti, kushinda kwako? U wapi, Ewe mauti, uchungu wako?
56 Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati.
57 Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.
58 Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana.
[13:06, 16/01/2016]mwl proo: USHUHUDA WA PILI :
USHUHUDA HUU WA NI WA BUDDHIST MONK(KUHANI WA KIBUDHA) AMBAYE ALIANZA HUDUMA KTK MAHEKALU YA KIDUBHA KUANZIA AKIWA NA MIAKA MITATU.. KWA KUWA ALIZALIWA NA KUKUTA WAZAZI WAKE NI PRIESTS KTK HAYO MAHEKALU... SASA ALIKUFA SIKU TATU LAKINI ALIPATA KUFUFUKA.. HAKUWAHI KUSIKIA HABARI ZA UKRISTO KWA NAMNA YOYOTE.. ZAIDI TUU KUJUA KUWA WAPO... NITATUMA LINK YA VIDEO YAKE YOUTUBE.. ILI MUIDOWNLOAD.. SASA KTK USHUHUDA WAKE NI KWAMBA NJIA YA KUWA NA UMILELE WA UHERI NA LAZIMA UWE NA YESU TUU.. MAANA KUZALIWA KWAKE KTK UBUDHA NA KUUJUA UBUDHA PEKEE HAKUKUMPA NAFASI YA KUHURUMIWA... NA HIVYO AKAWA NA UJUMBE KWA ULIMWENGU WA KIBUDHA... KUWA IKO NJIA..
INFACT WENGI WETU TUNAHISI WATU WOTE WANASIKIA MAMBO YA YESU MWOKOZI.. NINAO USHUHUDA WA MTUME MMOJA TOKA GHANA... AMBAYE BWANA ALIMPA AGIZO AKAMHUBIRI KUHANI MKUU WA KIBUDHA NCHINI THAILAND... ANASEMA ALIKUTA KUNA HEKALU KUBWA KAMA MTAA NA HUKO ALIKUTA WENGINE WAMEKAA KTK YOGA WIKI HATA 3 MTU HAKASIMAMA HADI ANAPATA CONNECTION YA KUWASILIANA NA SPIRITS ZA KIBUDHA... ALIONGOZWA NA WENYEJI HADI KTK CHUMBA CHA KUHANI MKUU NA ALITUMIA NAFASI KWA UJANJA MAANA NI KAMA ALIENDA ILI KUTOA RIPOTI YA UBUDHA UNAENDELEAJE AFRICA.... BUT ALIBEBA HABARI ZA YESU... ANASEMA ALIKUTA CHUMBA CHA KUHANI MKUU KINA UTUKUFU KABISA NA MOSHI WA MNG'AO... SASA ALIPOMTAKIA YESU YULE KUHANI ALISHTUKA NA KUMWAMBIA YULE MTUME TOKA GHANA... KUWA HAKUWA KULISIKIA HILO JINA KWA MIAKA 45 ILIYOPITA.. NI MFANO TU ULIMWENGU HUU NA MAENEO MENGINE.... MAANAKE HUYO KUHANI HATA HIZI KRISMAS ZINAPITA AKIWA HAZIJUI...
KWA HIYO NAFASI HII MUNGU KWA MAPENZI YAKE ANAWEZA KUITOA... LAKINI HATUWEZI KUJENGEA DOCTRINES HAPO ZAIDI YA ILE MWANADAMU AMEWEKEWA MARA MOJA KUFA NA BAADA KIFO HUKUMU..... EBRANIA 9:27
[13:06, 16/01/2016] proo: Watch "Buddhist monk Visited Hell, and came back to life after 3 days! (Part 2/2)" on YouTube - https://www.youtube.com/watch?v=24ThXPHM8iw&feature=youtube_gdata_player
[13:06, 16/01/2016] proo: ππΌππΌHIYO VIDEO INA DAKIKA 10 LAKINI UKIENDA HUKO YOUTUBE UTAIKUTA YENYE NUSU SAA NA UTAUPATA USHUHUDA KAMILI...
[13:06, 16/01/2016] proo: WATU AMBAO WALIWAHI KUFA NA WAKARUDI WALIKUWA NA SHUHUDA ZA KUFANANA SANAA..MIFANO KADHAA YA EVENTS ZINAFANANA WALIYOYAONA.. SASA KWA KUWA WENGI WANAJIANDAA KUZIKATAA SHUHUDA NAMI NACHEPUKA.. SILETI SHUHUDA ZA WALOKOLE TULIZOZIZOEA NA BAADHI YA SHUHUDA ZINA UTATA KWELI.... LAKINI NITALETA MAMBO AMBAYO WALIOSHUHUDIA WANAVYETI VYA KIDAKTARI KUTHIBITISHA THEY WERE CLINICALLY DEAD.. NILITAZAMA KTK TELEVISHENI YA KIDUNIA MWAKA 2010 IITWATO ABC NEWS WALIKUWA NA KIPINDI KIITWACHO BEYOND BELIEF.. WALIWAITA WATU AMBAO WALIKATA ROHO WAKARUDI PIA NA WALE WA NEAR-DEATH EXPERIENCES...
SASA KILA MMOJA KIVYAKE ILA WALIKUWA NA SOME SUITCASES... MIONGONI MWA WATU HAWA NI MISS MARY JO RAPIN.. ANA CHETI CHA CLINICAL DEATH ALITHIBITISHWA NA MADAKTARI KUWA ALIKUFA NA MWAKA 2003 SHE SUFFERED A BRAIN ANEURYSM IKAPELEKEA KIFO CHAKE... ILA ALITHIBITISHA KUWA "MUNGU ALIMWAMBIA GO BACK TO THE WORLD"
MTU WA PILI NI REV. DON PIPER OF PASADENA, CALIFORNIA PIA ALIAMBIWA NA MUNGU ARUDI DUNIANI.. WOTE WALIOHOJIWA WALIKUWA NA VITU VILIVYOLINGANA IKIWEPO YA ROHO ZAO ZILIPOIACHA MIILI WALIKAA WODINI KABLA YA KUONDOKA ALMOST 15MINUTES BAADHI YAO WALISEMA WALISHUHUDIA ZILE JITIHADA ZA WAUGUZI LAKINI WAO WALIKUWA KWA PEMBENI WAKITAZAMA NA BAADAE WALIONDOKA HAYO MAENEO
WALIYOYAONA NA YALIFANANA NI HAYA
A. UWEPO WA NURU ANGAVU SANA MARA ROHO ITOKAPO KTK MWILI
Hili nimelipata na ktk shuhuda zingine
B. UWEPO WA MALAIKA WANAOKUCHUKUA KUKUPELEKA UNAPOELEKEA
Nashawishika kuwa hii ni kwa wanaoenda pazuri..
*Wanaoenda pabaya hawana hiari ya kuchagua.. (REJEA KITABU CHA SAA 48 KUZIMU BY ALLEN ZANGMBOZI)
C. ) JAMBO LA TATU NI UWEPO WA MAHALI PAZURI SANA (A VERY BEAUTIFUL PLACE)
LENGO LA HAYA NI KUTUFANYA BADALA YA KUKIHOFIA KIFO, TUWE NA TUMAINI LA KWELI JUU YA YATAKAYOTEA KWA HAKIKA.. CHA MSINGI NI KWAMBA KAMA NI KUFA USIFE KIFO CHA OVYO CHENYE MATESO NA AIBU... KAMA YESU HATARUDI WITHIN THE NEXT CENTURY BASI UFE KIFO CHA MWENYE HAKI...
HESABU 23:10
NB:-
KWA UFAFANUZI WA MASWALA MENGINE MUHIMU YA SOMO HILI, JITAHIDI UPATE SOMO LANGU LA *MWILI WA ROHO*.
Mwl Proo
0762879363
alltruth5ministries@gmail.com
Ubarikiwe sana...umeniongezea maarifa
ReplyDelete