Tuesday, December 5, 2017

MWISHO MZURI

*MALIZA VIZURI*

*_mwlproo_*
*0762879363/0718922662*
HALELUYA HALELUYA!!
Wapenzi katika Bwana ujumbe huu umenitaharakisha, na imenifaa mimi na ninyi, kuuandika. Tusome hapa

Mhubiri 7 : 8a
*_Heri mwisho wa neno kuliko mwanzo wake,_*

Ndugu zangu, sipendi sana leo nijadili swala la hatma zilizowekwa tayari (predestination), kama nilivyowahi kueleza kwa sehemu katika moja ya masomo yangu. Ingawa jambo hilo lina ukweli kimaandiko, wako walioandikiwa hukumu tangu kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu, yaani wao ni vyombo vya ghadhabu. Na pia wako watu Mungu alishawachagua tangu asili, wao ni vyombo vya rehema. (Yuda 1:4, Rumi 8:29-30, 9:22,23). Sasa hilo nitaliezea wakati mwingine, lakini leo Bwana kanipa jambo hili la muhimu sana, nikuonye mbele kwamba *utafute kumaliza vizuri*

TUNAO WATU KATIKA HISTORIA ZA MAISHA YA SASA, AMBAO HAWAKUMALIZA VIZURI, PAMOJA NA RECORD NZURI YA MAISHA YAO YA ZAMANI. NA TUNAO AMBAO HAWANA RECORD NZURI LAKINI WALIMALIZA SAFARI VIZURI. INGAWA ITABAKI SIRI KWA MUNGU KUHUSU HALI YA MOYO YA HUYO MTU, MUDA ANAONDOKA. WAKO WATU AMBAO WALIWAHI FANYA HUDUMA YA KUTISHA, WALIFANYA GOSPEL CRUSADES AMBAZO ZILIVUNJA RECORD, LAKINI UMAUTI ULIWAKUTA WAKIWA WAMETOKA KUSHIKWA UGONI, FUMANIZI LA HATARI NA MKE WA MTU. HIYO SCANDAL ILIUNGANISHA MPAKA UMAUTI WAKE AKIWA HAJAWEKA MAMBO SAWA NA MUNGU WALA NA WANADAMU. NA WAKO WATU WALIISHI TU MAISHA YAO, LAKINI WALIKUJA KUMALIZA VIZURI. YUKO MTU MMOJA AMBAYE NI NDUGU YANGU WA DAMU, NILIPOELEZWA MWENENDO WAKE WA WIKI YA MWISHO KABLA HAJAFA, NIKAELEWA NAMNA ALIIMALIZA SAFARI. HAKUWA MWOKOVU KIVILE. LAKINI PAMOJA NA KUUGUA AKAPONA, LAKINI WIKI HIYO ALIYOFARIKI, ALIKUWA YUKO VIZURI, MWENYE AMANI TELE, MWENYE CHANGAMKO LA USO, AMEJAA IBADA, ANAIMBA TENZI ZA ROHONI KUCHWA KUTWA, KWA JUMA HILO TU, ALIKUWA AKIHIMIZA IBADA ZA NYUMBANI KILA JIONI, ALIKUWA AKIAMSHA WATU KUOMBA USIKU. HAKUYAFANYA HAYA KWA KUWA ANAUGUA, MAANA WIKI ALIYOFARIKI ALIKUWA YUKO ZAIDI YA MZIMA. LAKINI NAMNA ALIVYOMALIZA NA BWANA NASHAWISHIKA NDUGU YANGU HUYU, NITAMKUTA KWA BWANA. IKUMBUKWE ALIYEIAHI MAISHA YA UOVU TOKEA UJANANI, LAKINI MPAKA UZEENI, AKIYATENGENEZA MAMBO YAKE MWISHONI, HALIKUMBUKWI HATA MOJA KATIKA YALE MABAYA. NA MTU ALIYEISHI KWA KUJITENGA NA UOVU, AKAJA KUFANYA DHAMBI KATIKA KUMALIZIA SAFARI, HALIKUMBUKWI HATA MOJA KATIKA KAZI ZOTE ZILE NJEMA (AND THE LORD GOD IS SO JUST).

1.) Mwovu anayeghairi uovu wake

Ezekiel 18

*_21 Lakini mtu mbaya akighairi, na kuacha dhambi zake zote alizozitenda, na kuzishika amri zangu zote, na kutenda yaliyo halali na haki, hakika ataishi, hatakufa._*
_*22 Dhambi zake zote alizozitenda hazitakumbukwa juu yake hata mojawapo; katika haki yake aliyoitenda ataishi.*_

2.) Mwenye haki anayeharibu mwisho

Ezekiel 18

*_24 Bali mwenye haki atakapoghairi, na kuiacha haki yake, na kutenda uovu, na kufanya machukizo yote kama yale afanyayo mtu mwovu, je, ataishi? Katika matendo yake yote ya haki aliyoyatenda halitakumbukwa hata mojawapo. Katika kosa lile alilolikosa, naam, katika dhambi yake aliyoitenda, atakufa._*

Yuko mchungaji ninayemfahamu vizuri, amefariki mwaka 2015. Pamoja na kuyumbayumba kiimani miaka fulani. Lakini mwisho wake aliumaliza vizuri. Si wote watapata nafasi ya kuweka mamvo sawa nyakati zao za karibu na vifo, ndio maana somo hili pia litakupa mbinu ya kutokaa na *_suspended cases_*,  kiroho kimevamiwa and you are just in a suspense, hiyo ni hatari kubwa. Huyajui yanayoweza kuzuka katika siku moja tuu (Mithali 27:1). Mchungaji huyu alipoambiwa na madaktari bingwa kuwa hali yako ya ini (liver) lako imefikia stage ya mwisho ya kuharibika, haziwezi timia siku 21 ukiwa bado mzima. Naamini aliendelea kusihi uponyaji wa Bwana, maana anaongoza kanisa la maombezi, kwa hiyo yeye mwenyewe amekuwa akiwahudumia watu wa magonjwa hayo na ameshuhudia kwa mikono yake wakiponywa. Lakini huenda alikuwa akiwa na ushuhuda wa ndani, kuwa huu ni ugonjwa wa mauti yangu. Maana hizo wiki tatu alizokaa hoapitali alizitumia kusawazisha chochote chenye mushkeli. Niliambiwa na mchungaji msaidizi wake, kwamba alipiga simu kila mahali anapokumbuka kuna shida fulani, mpaka kwa askofu wake, anakumbuka kuna jambo waliwahi kwaruzana, naye alimpigia kufanya suluhu, ili asiwe na deni na mtu tena. Na siku anaondoka alijua kuwa leo hii naondoka, waliokuwepo wodini walieleza.

Sasa sifundishi bahati nasibu za kuvizia ukiwa maututi uweke mambo sawa, la hasha. Niteleza baadae kidogo..

*WATU AMBAO WALIKUWA NA MIANZO MIZURI, WAKAMALIZA VIBAYA KATIKA BIBLIA*

☄ MTU WA MUNGU TOKA YUDA (1Falme 13:1-32)
Tunasoma habari nzuri sana za huyu mtu wa Mungu/nabii ambaye hata jina lak halikutajwa. Pamoja na kutumika katika upako mwingi, kiasi kwamba hata akinyoshewa kidole, mkono unaganda. Pamoja na kutoa unabii very powerful katika madhabahu, alimaliza vibaya katika kutotii Neno la Bwana na kuuawa na simba🦁. Akamaliza na rekodi ya nabii asiyemtii Bwana bali nabii mzee (wa uongo).

☄ BALAAMU BIN BEORI
Huyu mtu amekuwa akiwatatiza watu kujua ni nabii wa Bwana au la. Wenfi wakisoma sura zile tatu za Hesabu 22, 23, 24, Wanamhisi kuwa ni nabii wa Bwana. Lakini huyu alikuwa mnajimu, mwenye elimu ya kijini na mchawi tu wa kawaida (Yoshua 13:22). Lakini pamoja na yale yote uyajuayo, Balaamu alikuwa na mwisho mbaya sana na aliuawa kwa upanga na waisrael wenyewe (Yuda 1:11, Ufunuo 2:14)

☄ YEHU
Huyu mtu hatari zaidi, aliyekuja na upako wa safishasafisha⚔🗡🏹 hakumaliza vizuri. Alitenda kazi nzuri nyingi, lakini mwiaho wake haukuwa mzuri (Hosea 1:4, 2Falme 10:29,31)

☄ YUDA ISKARIOTE
Huyu mtume mteule, alianza kama Thenashara aliyeaminiwa kiasi cha kuwa Chief Accountant wa Bwana Yesu, lakini safari yake iliishia Akaldema baada ya kujiua (Suicide). Mwisho haukuwa mzuri.

NDUGU YANGU MSOMAJI, NAOMBA USIPUUZIE, HAKUNA LOLOTE LINALOFANYWA  BAADA YA ROHO KUTENGANA NA MWILI, KUSAIDIA KUREKEBISHA RECORD YAKO YA MAISHA. WALA USIYADHARAU HAYA KWA KUWA MUDA HUU UPO KWENYE MFUNGO WA 21KAVU WALA SIKU 40, YAANI KAUWEPI UNAKOKAHISI UNADHANI NDIVYO HIVYO TUU UMEMALIZA SAFARI. HAPANA. VITA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO NI KUBWA KULIKO HUO MFUNGO WAKO, NI NEEMA TU YA MUNGU INAKUHIFADHI. NA NINAKUELEZA HAYA OUT OF GREAT EXPERIENCE, UNAWEZA MALIZA MFUNGO WAKO WA KAVU UKAANGUKIA KWENYE SCANDAL MOJA AMBAYO HAUTAAMINI, MPAKA UNAJIULIZA HIVI NI MIMI NILIYEFUNGA KAVU 14 MWEZI ULIOPITA? NI WEWE WEWE, WALA SI MWINGINE. SASA UNAPASWA KUJUA YAFUATAYO. HATA KAMA UKO MIONGONI MWA WALE AMBAO NI VYOMBO VYA REHEMA (AMBAO KWA MWISHO WAO HUENDA MUNGU AKAWAKUMBUSHA KAMA HEZEKIA, KUSEMA TENGENEZA MAMBO YA NYUMBA YAKO Isaya 38:1ff), LAKINI HATA KAMA SIVYO, BWANA ANAKUSAIDIA LEO, TAFUTA KUMALIZA VIZURI. USIDUMU NA DHAMBI, UKAIPOSTPONE TOBA, UZIMA HUU TULIONAO HAUKO YAKINI (JITAHIDI UPATE SOMO LANGU LA, *_"UZIMA WENU NI NINI?"_*). YUPO BINTI NILIYESOMA HABARI ZAKE KATIKA KILE KITABU CHA MAHOJIANO YA SAA 48 KUZIMU, SITAKI KUANZA KUKITETEA KITABU CHA KWELI AU CHA UONGO, LAKINI HOJA ILE NI YA MSINGI,  ALIMHOJI YULE BINTI AMBAYE ALIKUWA MWOKOVU MWENYE MOTO WA KIROHO🔥🔥, KUWA KWA NINI UPO HUKU. AKASEMA ALIANGUKA KWENYE UASHARETI SIKU YA GRADUATION YAKE YA CHUO. ALIPANGA ATATUBU AKIRUDU NYUMBANI. LAKINI AKIWA KWA BASI🚌 ALIPATA AJALI NA KUFA. AKAMALIZA SAFARI VIBAYA. NA PIA ALIANDIKA HABARI ZA MCHUNGAJI, SLIYETUMIA MICHANGO YA UJENZI KUFANYIA HARUSI YA MWANAE, KWA MPANGO KUWA ATAREJEZA BADAE, LAKINI KWENYE RIPOTI ALIONESHA PESA ZIMEFANYA KAZI ILIYOKUSUDIWA. KWA HIYO KUYAKAGUA MAISHA YA KIROHO NI JAMBO LA WAKATI WOTE. NIKIMNUKUU  BISHOP DEO LUBALA, ALISEMA MTU AKIWA MTUME AU MCHUNGAJI AU ASKOFU, HAMSHINDI SHETANI WALA DHAMBI, KWA SABABU YA HIYO NAFASI, BALI YEYE NAYE ANASHINDA KAMA WAAMINI WENGINE.

Mwl Proo
0762879363

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment