Friday, December 15, 2017

MAFARISAYO NA MASADUKAYO WALITOKEAJE?

*MATERIALS BEYOND BIBLE*

_By Mwl Proo_
0762879363

*YALIYOKUWAPO KUELEKEA AGANO JIPYA NA INJILI, (HISTORIA FUPI YA,PALESTINA)*


Palestina, tunamaanisha mashariki ya kati.
Kulikuwa na mfalme aitwaye Philip (323BC), na
mwanaye alikuwa Alexander Mkuu(mfalme
aliyekuwa na nguvu sana) dola yake ilijumuisha Ugiriki, Syria na maeneo ya Afrika
kaskazini. Alipokufa dola iligawanyika sehemu
mbili;
1.) Seleucid
2.) Ptolemaic (Egypty-199BC)


Mfalme Antiokas III aliushinda Ptolemaic
akautwaa..huyu aliwapa Israel haki nyingi na
upendeleo, aliujenga mji na hekalu, kukawa na
uhuru(autonomy).


Antiokas IV ajulikanae kama Epiphany (175BC), akauharibu mji wa Yerusalem na hekalu. Mwaka 167BC alichinja nguruwe madhabahuni na akaiinua sanamu yake iabudiwe, (wanahistoria wengi husema wayahudi waliita hilo ni chukizo la
uharibifu la Dan 9:27, Mark 13:14).


Wakazuka wazayuni wanaharakati (activists) waliopinga (Revolts). Mwanaharakati mmoja aitwate Mathias (wanawe John, Judas, Eleazer, Jonathan na Simon), huyu
Judas ndiye aliyepewa jina la utani Makabayo
hapo baadae.
Hawa walitumia style ya sokwe kivita (Guarrilla
Fighting), walitokeza mjini kushindana na
kukimbilia misituni. Na WAKASHINDA, hadi leo
Israel husherekea HANUKKAH ya jinsi hawa
activists wazayuni walivyoshinda...
Wakamteua Jaçîm (Alcimus) awe kuhani mkuu (159BC akafariki). Kukazuka vitabu vilivyofichika (Apocrypha), ikumbukwe agano la kale la kigiriki lilikuwepo tangu 250BC likujulikana kama Septuagint (Greek means the seventy) kutokana na 70 Scholars ndio maana ya neno hilo (lilitafsiriwa toka katika Tanakh, Hebrew Bible!.


Kutoka katika wana wanne Jonathan (hakuwa Mlawi) na akateuliwa kuwa kuhani, hiyo ikafanya watengane na kuwa na madhehebu matatu:-
-Pharisee
-Sadducees
-Essenes

*MAFARISAYO:*
💿Hawa hawapo connected na kuhani mkuu Zadok.
💿Waliamini israel wote waliitwa kuwa holy to God, na huo utakatifu watokana na ushikwaji wa Torah very strict.
💿Walifundisha sheria 603
💿Walikuwa maarufu kama watch dogs
💿Walikuwa watendaji wa karibu na serikali ya
Rumi, wakiitwa HABURAH
💿Kitabu chao kiitwacho HALAKAH kilileta
mkusanyiko uitwao MISHNAH na TOSEFTA

*WAANDISHI:*
Hili ni kundi la writers/clerks/secretaries. Waliandika katika Papyrus(ngozi za wanyama na majani yaliyokaushwa), hakukuwa na papers bali scroll-gombo la chuo

*MASADUKAYO:*
Hawa wana muunganiko na Sadoki kuhani mkuu, aliyeishi wakati wa Mfalme Daudi. (Hawa walikuwa wasomi-elites/aristocratic) na
walijitahidi sana kuishi kiyunani. Walikuwa na mtazamo tofauti na Mafarisayo kuhusu Torah, walitafsiri kwa kuweka vitu ambavyo havikutajwa na Torah.

💿 Walikuwa na vitabu vitano, waliamini ufufuo, lakini hawakuamini uwepo wa malaika (Mdo 23:8-9).
💿 Walikuwa na falsafa yao……
"The more you get, the more you will be corrupt"

*WAESENES (the separatest)*

Miongoni mwao ni mwanahistoria Josephus. Hawa ni watu wenye juhudi ya
kujifunza kwa moyo, waliishi kitawa (monastic
living). 

💿Walipinga sheria za kirumi. 

💿Wanahusika na magombo ya chuo ya Bahari ya Chumvi (Deadsea Scrolls). Walijiita wana wa nuru.


*ZEALOTS (walokole):*
Hawa ndio wale Guarrilla fighters, miongoni mwao ni yule Simon Zealot, walipigania uhuru, pia Judas (the commando) 200BC hadi 70A.D mwisho wa Revolts

*WAHERODIA:*
Hawa walikuwa wanasiasa (ikiwemo Herod the
Great)
Itaendelea…………………

alltruth5ministries@gmail.com

0718922662
0762879363

No comments:

Post a Comment