Saturday, December 30, 2017

DALILI ZA ROHO NA ZA NGUVU

*DALILI ZA ROHO NA ZA NGUVU*

🇲 🇼 🇱  🇵 🇷 🇴 🇴

0762879363

Jina la Bwana libarikiwe. Karibu tena katika mfululizo wa kujifunza kweli yote.

Neno la Bwana leo linasimama katika

1 Wakorintho 2 : 4
*_Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu,_*

Haleluya, leo nasukumwa moyoni kushughulikia mapokeo yasiyofaa,yanayotaka kulifanya kanisa la Kristo kusalia kama dini na hata ile injili ya kweli. 
Paulo mtume anawaandikia wakristo waliopo Korintho,kuwa ile injili aliyoihubiri kwao haikuwa ya maneno matupu,ili isije imani yao ikajengwa ktk maneno tu tena yenye kushawishi(yametungwa kwa hekima za kibinadamu) yenye *UKAME* bali Neno lake na kuhubiri kwake kuliambatana n dalili za Roho na za nguvu.
Neno la Ufalme kamwe halipaswi kuwa kavu lisilodhihirisha nguvu za Roho (Demonstration of Spirit's power). Mifumo ya dini inakawaida ya kubadili mtaala(Curriculum) wa Roho wa kweli na kuingiza ule wa kibinadamu. Mwaka 787 AD kule kwenye baraza la Nikea walipitisha mambo mengi yaloyozidi kuufanya Ukristo uwe ni dini tuu isiyo na dalili za Roho na za nguvu. Hilo ndilo baraza lilibariki sanamu za kanisani,liturujia,vipaimara vikaingizwa,kubatiza watoto wachanga na kitabu maalum cha sala(prayer book). Sasa watu waliopaswa kuomba ktk Roho Mtakatifu(Yuda 1:20) wanaletewa mfumo wa dini unaokinzana na mapenzi ya Roho. Mwishowe inabaki kuwa dini tuu,hata kutoa mapepo wachafu tu(ambalo ni jambo la kufanywa na watoto wa Sunday school ya watoto/Au waongofu wapya)  hakukuwahi kushuhudiwa kabisa. Na hata sasa mifumo ya makanisa inarejeza hali ileile.Ishara,ajabu na miujiza iliyopaswa kuambatana na Neno,imeenda likizo kwa sababu kuu mbili, 1. Jinsi watu walivyopokea mapokeo yasiyo sahihi(ili ishara zitendeke basi analetwa mhubiri mgeni/au unakuta mtu akijishughulisha n hizo dalili za Roho na za nguvu anahisiwa kutumiwa na roho zidanganyazo)
2.Watu hawan uzoefu wa ujuzi wa kutenda kazi hizo kwa sababu nao wanaiopokea injili kame (Wengi hutumia maelezo  kuwa Yohana Mbatizaji haijanukuliwa kama alifanya miujiza.

Mimi pamoja na juhudi ya kuifundisha kweli ya Mungu kama wito wangu ulivyo bado nikiacha kuyafundisha haya nitakuwa na *_imbalanced gospel_* maana hatusomi injili ya hivyo ktk maandiko.

TWENDE KTK MAANDIKO

1.AGIZO/NENO LA BWANA LINAAMBATANA NA ISHARA ZA KUTHIBITISHA

SAMWELI ALIPOMWAMBIA NENO LA MUNGU SAULI,ILIPASWA ISHARA IAMBATANE NALO

1 Samweli 9 : 27
*_Hata walipokuwa wakishuka mwisho wa mji, Samweli akamwambia Sauli, Mwambie mtumishi atangulie, (naye akatangulia), bali wewe simama hapa sasa, ili nikuambie neno la Mungu._*
👇🏽👇🏽👇🏽
Ishara iliyoambata na Neno

1Samwel 10

*_1 Ndipo Samweli akatwaa kichupa cha mafuta, akayamimina kichwani pake, akambusu, akasema, Je! BWANA hakukutia mafuta [uwe mkuu juu ya watu wake Israeli? Nawe utamiliki watu wa BWANA, na kuwaokoa na mikono ya adui zao; kisha hii itakuwa ishara kwako ya kuwa BWANA amekutia mafuta] uwe mkuu juu ya urithi wake._*
*_2 Utakapoondoka kwangu leo, utakutana na wanaume wawili karibu na kaburi la Raheli, katika mpaka wa Benyamini huko Selsa; nao watakuambia, Punda hao uliokwenda kuwatafuta wameonekana; na tazama, baba yako ameacha kufikiri habari za punda, anafikiri habari zenu, akisema, Nifanye nini kwa ajili ya mwanangu?_*

MUSA ALIPOPOKEA AGIZO,KULIPASWA KUWA NA ISHARA KUWA KWELI AMETUMWA NA MUNGU

KUTOKA 4
1 Musa akajibu akasema, Lakini, tazama, hawataniamini, wala hawataisikia sauti yangu; maana watasema, BWANA hakukutokea.
2 BWANA akamwambia, Ni nini hiyo uliyo nayo mkononi mwako? Akasema, Ni fimbo.
3 Akamwambia, Itupe chini; akaitupa chini, nayo ikawa nyoka; Musa akakimbia mbele yake.

5 ili kwamba wapate kusadiki ya kwamba BWANA, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amekutokea.

6 BWANA akamwambia tena, Sasa tia mkono wako kifuani mwako. Akautia mkono wake kifuani mwake; naye alipoutoa, kumbe! Mkono wake ulikuwa una ukoma, umekuwa mweupe kama theluji.
7 Akasema, Tia mkono wako kifuani mwako tena. Akautia mkono wake kifuani mwake tena, na alipoutoa kifuani mwake, kumbe! Umerudia hali ya mwili wake.

9 Kisha itakuwa wasipoamini hata ishara hizo mbili, wala kuisikiliza sauti yako, basi, yatwae maji ya mtoni uyamwage juu ya nchi kavu, na yale maji uyatwaayo mtoni yatakuwa damu juu ya nchi kavu.

SASA TUNAANZAJE KUIHUBIRI INJILI AU NENO LA MUNGU BILA UDHIHIRISHO WA NGUVU ZAKE KTK HILO NENO? MAANA UFALME HAUPO KTK NENO BALI NGUVU

1 Wakorintho 4 : 20 - *_Maana ufalme wa Mungu hauwi katika neno, bali katika nguvu._*

MITUME WALIENDA KUHUBIRI ILA NENO LIKIHUBIRIWA KWA USAHIHI LAZIMA ISHARA ZITALIFUATA ILI KULITHIBITISHA

Marko 16 : 20
*_Nao wale wakatoka, wakahubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithibitisha lile neno kwa ishara zilizofuatana nalo._*

KWA UPANDE WANGU SIKUBALIANI NA SWALA ZA KUHUBIRI NENO PASIPO ISHARA YOYOTE(ISAYA 7:11) INGAWA KWENYE SWALA LA UDHIHIRISHO WA NGUVU SHETANI BAADA YA KUONA WANA WA NURU HAWANA UJUZI/EXPERIENCE YA KUTOSHA,NAYE ANAPATUMIA HAPO HAPO KULETA ILE YA ULAGHAI (COUNTERFEIT) LAKINI HIZO ZA UONGO HAZIFANYI SISI TUACHE AU TUOGOPE,BECAUSE THAT WILL DO MORE HARM THAN GOOD(NA WAKRISTO AMBAO HAWAKUZOEZWA KUONA NA KUPOKEA MIUJIZA YAO,NDIO WAMEKOSA MSIMAMO WA IMANI(1kor 2:5) ,KILA WAKIONA TANGAZO LA MTUME NA NABII KWENYE TV 📺JUMAPILI WANAHAMIA HUKO,KWA HIYO WENGINE  KWA MWAKA MMOJA AMEKUWA MSHIRIKA KTK HUDUMA NA MAKANISA ZAIDI YA 10 ,KOSA SIO LAO NI WALE WALIOMLEA HAWAKUMJENGA KTK MSINGI,PIA MTU AMEKAA NA VIFUNGO VYAKE HASHUHUDIWI AKIHUDUMIWA MAANA WAHUDUMU WA MADHABAHU WAOGA,AU WALIPOKEA INJILI ISIYO NA DALILI ZA ROHO NA ZA NGUVU. NI KWELI WAKO WENYE KARAMA ZA MIUJIZA NA KUPONYA

1Kor 12
*_9 mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja;_*
*_10 na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha;_*

1 Wakorintho 12 : 28 *_Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha._*

KATIKA SOMO LANGU LA KARAMA NA HUDUMA NA HUDMA ZA ROHONI NITATOFAUTISHA ANAYEPONYA KWA KARAMA YA KUPONYA INKUWAJE NA ILE NYINGINE,MAANA ILI MAGONJWA YAPONE ILI ISHARA ZITENDEKE SIO LAZIMA UWE NA KARAMA HIZO, IKO  AMBAYO NI GENERAL KWA WAAMINI WOTE,KILA ALIYEAMINI KTK YESU ANAPASWA KUZITENDA,UKIWA MTAANI ,OFISINI UKIKUTA WENYE HAJA YA KUPONYWA WEKA MKONO L✋🏼KWA JINA LA YESU WATAGUSWA NA KUPONYWA,MUDA WATU WAMESUKWASUKWA NA PEPO WACHAFU TUMIA HUO MWANYA KUMDHIHIRISHA YESU WAKO, HIYO HAIHITAJI *_GO AHEAD_* TOKA KWA PASTOR,YAANI KAMA WAAMINI WOTE WANGEJUA HAYA ULIMWENGU UNGEPINDUKA

Marko 16 : 17

*_Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;_*

MUNGU AKISEMA ATAPONYA,NENO LAKE HALIANGUKI CHINI (2Falme 10:10)

Isaya 55 : 11

*_ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma._*

KANUNI ILIYOPO NI ULIHUBIRI NENO LA INJILI YA KWELI THEN UTENDE ISHARA,AJABU NA MIUJIZA. KUACHA KUFANYA HIVYO KUNAWAPA SHAVU WAHUNI WACHACHE WA KIBONGO WALE *FAKE* KUJIPATIA UMAARUFU ULIOMSTAHILI YESU. 
WAPENDWA NAOMBA KUWAJULISHA KUWA KILICHOKOSEKANA KWENU SIO MAOMBI,MAANA MAOMBI HAYO YA KUFUNGA MPAKA WILI TATU NA MIKESHA MINGI YA MAOMBI MLIYONAYO NI MIKUBWA NA MENGI MNO UKILINGANISHA NA NGUVU INAYOHITAJIKA ILI ISHARA,MIUJIZA NA AJABU ZITENDEKE,MMEKOSA TU UJUZI(AMBAPO INAWAFANYA KUWA WAOGA) NA ILE SHIDA YA MAPOKEO/TRADITIONS YASIYO SAHIHI. NIMEENDA KUHUDUMU MAHALI,WATU WAPO SAFI KTK NENO ILA HAWANA UZOEFU  WA KUTENDA KAZI(MIUJIZA NA UPONYAJI) WALIPOSHUHUDIA NAHUDUMIA KUPONYA WAGONJWA NA KUWAULIZA PAPO(INSTANT HEALING) NA WAKAKIRI KUPONA KABISA,WENGINE NDIO WAKAAMINI SIKU HIYO KUWA OOH KUMBE YESU ANAPONYA HATA SASA,WENGINE NI CHURCH ELDERS WAMETAMANI UPONYAJI WA YESU JUU YAO KITAMBO LAKINI HAYA MADINI YETU YAMEFICHA UFUNGUO WA MAARIFA (LUKA 11:52) ,SASA WENGINE WAKAANZA KUNIITA PRIVATE KUWA MIMI NINA HILI MTUMISHI,NA MIMI NINA HILI NIOMBEE,SASA MIFUMO YA DINI IMEWANYIMA WATOTO WA MUNGU CHAKULA CHAO CHA KUPOKEA MIUJIA NA UPONYAJI,NA WAKITHUBUTU KUFUATA MAHALI PENYE UJUZI WANAWATENGA NA MASINAGOGI.
INGAWA WATU WAKIAMINI TU BILA ISHARA WANA HERI YAO(YOH 4:48,20:29) LAKINI MSIKUBALI  KUWA NA IBADA KAME,ZISIZO NA DALILI ZA ROHO NA NGUVU,ILI WANAOSHAMBULIWA NA ADUI WAKIJA NYUMBANI WA BWANA VIFUNGO  VYA MAGONJWA AU KULOGWA,AU MATESO YA NAMNA ZOTE YAFUNGULIWE. NA NENO LA MUNGU LIKIHUBIRIWA KWA USAHIHI NA WAHUDUMU WAKIWA NA UJUZI HUO WA MATENDO YA MIUJIZA NA UPONYAJI BASI WAYATENDE HAYO
MAANA HII NI FORMULAR

1.PREACHING
2.PERFORMING MIRACLES

MATHAYO 4:17,23

Mathayo 4 : 17 
*_Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia._*

Mathayo 4 : 23
*_Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya ugonjwa na udhaifu wa kila namna katika watu._*

MTANISAMEHE KWA KUWA NIPO KINYUME NA MIFUMO YA DINI,HATA MAKANISA YETU YA KIPENTEKOSTE MENGI YAMEGEUKA KUWA YA DINI TUU,WATU WANAINGIA NA VIFUNGO VYAO NA MAGONJWA YAO NA KUONDOKA NAYO *_NO HEALING&MIRACLE MINISTRATION AT ALL_* NDIO MAANA WAJANJA WANAAMUA KUJA NA GEAR YA MIUJIZA NA KUFANYA UVUVI HARAMU WA KUVUA SAMAKI KWENYE MAKAPU YA WENGINE. WENGI WALIOANZA HUDMA ZAO KWA MSINGI WA MIUJIZA NA UPONYAJI HAWAJAENDA KUFANYA HTA CRUSADE AWAPATE MATAIFA,AMEWAVUA WASHIRIKA KWENYE MAKANISA YA KIPENTEKOSTE HAYO HAYO YALIYO YALIYOFUKIA NA KUZIZIKA DALILI ZA ROHO NA ZA NGUVU

ANZA SASA, BADILISHA MFUMO, EWE MHUDUMU TAFUTA UJUZI MAANA NGUVU/UWEPO WA BWANA UPO KTK IBADA  ILI APATE KUPONYA (LUKA 5:17). LAKINI CHANEL/TRANSMITTER INAKOSEKANA . WAKO AMBAO BWANA ATAKUJULISHA ANATAKA KUWAPONYA NA WENGINE UKIWAONA WANA SHIDA UNAPASWA KUZIRUHUSU NGUVU ZIWAHUDUMIE. ACHA MAZOEA NA UANZE KUTEMBEA KTK UJUZI WA ROHO,KUNA MAHALI NILIENDA KUHUDUMU KWA PRAISE AND WORSHIP NILIPO MALIZA  KUHUDUMIA SIFA NIKAULIZA WALIOINGIA WAGONJWA WAINUE MIKONO JUU NA WAANZE KUJICHEKI AFYA ZAO WANASIKIAJE MIILI YAO, WENGINE WAKABAKI KUSEMA MBONA HAJAOMBEA,TAYARI KATIKA KUIMBA WATU WALIKUWA WAMEPONYWA NA BWANA NAMI NILISHALIHISI HILO KATIKA ROHO, NDIO MAANA NIKAITISHA SHUHUDA.

MUNGU AWABARIKI KWA KUELEWA

Mwl Proo
0762879363(whatsapp only)

alltruth5ministries@gmail.com

Friday, December 29, 2017

TWEKA MPAKA VILINDINI

*```TWEKA MPAKA VILINDINI```*

🇲 🇼 🇱  🇵 🇷 🇴 🇴

0762879363
0718922662

Haleluya!
Bwana Yesu Kristo asifiwe sana!🙋🏽

Leo Bwana kaweka Neno moyoni mwangu .Nalo ni hili

Luka 5 : 4 
*_Hata alipokwisha kunena, alimwambia Simoni, Tweka mpaka kilindini, mkashushe nyavu zenu mvue samaki._*

PUT OUT INTO THE DEPTHS

Shetani na mawakala wake wote wanafurahia kuona tunabaki kwenye kina  kifupi(shallower depth) ili waendelee kukufikia kwa kukuzuia kutoboza,kukukwamisha usifikie ukamilifu wa hatma na waendelee kukurudisha nyuma kila unapoonesha dalili ya kuinuka iwe kiroho,kielimu,kiuchumu etc etc

Farao alijua kwa wazi waisrael wakienda mbali sana(mpaka vilindini)  hataweza kuwapata awatumikishe tena,hivyo aliwaruhusu waende ila anatoa conditionality kuwa msiende mbali sana:-

Kutoka 8 : 28

*_Farao akasema, Mimi nitawapa ruhusa mwende, ili mmchinjie dhabihu Bwana, Mungu wenu, jangwani; lakini hamtakwenda mbali sana; haya niombeeni._*

SASA HII CONDITION YA FARAO NDIYO HASA TABIA YA SHETANI NA WASAIDIZI WAKE,WANAWEZA KURUHUSU UFANYE MAMBO FULANI YA KIROHO LAKINI USIENDE MBALI SANA UBAKIE KWENYE SHALLOW-WATER ,USIFIKE VILINDINI WAKASHINDWA KUKUFIKIA.

KIPO KIWANGO KTK MAISHA YA KIROHO AMBAYO ADUI AKUCHEZEI TENA N KUKULETEALETEA MAANGUKO YASIYO NA MAANA AMBAYO HUTOKEA KWAKO IN *_CIRCULAR REPITITIONS_* YAANI EXACTLY ANGUKO ULILOANGUKA NALO MWAKA JANA(LIMEKUZONGA KWA UPESI) UMEANGUKA KWA LILELILE TENA,SABABU KUU NI NGUVU CHACHE(Mithali 24:10) ZINAZOTOKANA NA KUBAKI KTK KINA KIDOGO BADALA YA KUTWEKA MPAKA VILINDINI. MAJI KTK LUGHA ZA ROHONI/KINABII YANAWEZA KUASHIRIA ROHO MTAKATIFU,AU KAMA NI MAJI MAKUU/FLOODING YANAWEZA KUMAANISHA HATARI,MAJANGA NA MAJARIBU MAZITO,LAKINI MAJI YAKIWA KTK DEPTHS TOFAUTI YANAASHIRIA LEVELS ZA MAISHA KIROHO. KUNA WAKATI NILIENDA KUHUDUMU KWA NENO LA MUNGU MAHALI,ILA NILIFUNDISHA VITU VIKO JUU MNO KULINGANISHA NA UFAHAMU WA WATU,NILIPOTOKA HUKO ROHO AKANIONESHA KWENYE NDOTO,NIPO KWENYE KILINDI CHA MAJI NAWAVUTA WATU KWENYE KINA AMBACHO SIO SIZE YAO.

Tusome hapa

*Ezekiel 47*

*_3 Na alipotoka mtu yule, mwenye uzi wa kupimia mkononi mwake, kwenda masharikini, akapima dhiraa elfu, akanivusha maji yale; maji yakafika mpaka viweko vya miguu._*
*_4 Kisha akapima dhiraa elfu, akanivusha maji yale, maji yakafika mpaka magoti. Kisha akapima dhiraa elfu, akanivusha, maji yakafika mpaka viuno._*
*_5 Kisha akapima dhiraa elfu, yakawa mto nisioweza kuuvuka; maana maji yamezidi, maji ya kuogelea, mto usiovukika._*

KTK MISTARI HII HAPA JUU TUNA VIWANGO VITATU,BAADA YA YULE MTU(MALAIKA) KUPIKA DHIRAA ELFU ZA KWANZA(SHALLOW WATER) MAJI YALIMFIKIA KWENYE VIWEKO VYA MIGUU(FEET'S ANKLES)  YAANI NI KIWANGO KISICHO NA KINA,NA WAKRISTO WENGI WANATEMBEA KTK MAJI YA VIWEKO VYA MIGUU AMBAPO MATENDO YA MWILI BADO YANA UDHIHIRISHO MKUBWA(GALATIA 5:19-21)  UNAKUTA MTU KAOKOKA BUT ANA HASIRA HATARI(MHUBIRI 7:9) YAANI UKIGUSA TU ANAKUWASHIA MOTO WIKI TATU(EFES 4:26) TATIZO HAJAFUNIKIZWA NA YALE MAJI YAANI HAJATWEKA MPAKA VILINDINI KWA HIYO ANAOPARET KIMWILI ZAIDI.

KISHA YULE MTU(MALAIKA) AKAPIMA TENA DHIRAA ELFU MAJI YAKAFIKA MAGOTINI,LAKINI HAPO SIO MWISHO AKAPIMA TENA DHIRAA ELFU YAKAWA MTO ASIOWEZA KUUVUKA🏊🏽MAANA MAJI YAMEZIDI MAJI YA KUOGELEA NAAM MTO USIOVUKIKA🌊(VILINDINI)

NENO LA BWANA KWAKO NI HILI, *"TWEKA MPAKA VILINDINI"* KWA MAANA KUNA MAMVO YA KIROHO HUTAYAJUA,THERE IS A REALM OF THE SPIRIT YOU WILL NEVER OPERATE THROUGH MPAKA UTWEKE MPAKA VILINDINI,NA UTOKE KWENYE SHALLOWER DEPTH,

BIBLIA INASEMA KTK ZABURI 42:7

*_(NIV) DEEP CALLS TO DEEP_* Yaani kilindi chapigia kelele kilindi. Kuna mambo ya kiroho mpaka uwe vilindini na hayo mambo ya vilindini ya vilindini yatajifunua yenyewe kwako. Ukibaki unafanya mambo ya kiroho kwa namna ileile kwa kiwango kilekile,unabaki kwenye shallower water(kina kifupi/hauendi mbali) . Nilikuwa nilimsikiliza mtumishi mmoja wa Mungu ambaye ametweka mpaka kilindini,Yeye watu wote wanaokuja ili awahudimie kiroho kwa maombezi na uponyaji anawaona mara mbili tofauti👥Yaani anamwona mtu physically kwa mwili huu wa dunia lakini pembeni yake kama mita moja anamuona huyo mtu huyohuyo kwa macho ya roho ktk ulimwengu mwingine. Sasa ktk huyu mtu wa pembeni ndipo anaiona shida yake kwa kina na taarifa zote.Huenda umeileta kansa ipo stage ya mwisho,ila yeye alisema akimwangalia yule wa pembeni yako anajua kansa yako ilitokana na nini na na kama kuna shida au kifungo chochote anakiona ktk mwili wako ule wa pili,na akasema hayo mambo ukimhoji mtu mwingine ambaye hajawahi oparet in that realm atajibu tu kuwa ni uchawi etc akasema haya kamuulize mwingine anayeoparet ktk viwango vya vilindi kama hivi,na alifanya practical ya hilo jambo,yaani alisukuma hewani ambapo anamwona yule mtu wa pili na tukaona huyu mwingine ameyumba sana. Yuko mtumishi mwingine ambaye ametweka mpaka vilindini akitembea au akiwa ktk huduma madhabahuni pembeni yake anaona kama screen ya Tv 🖥📺ambapo mambo yote yanayoendelea ktk ulimwengu wa roho anayaona. Mnashangaa akisimama na ingawa anaeleza habari za mtu as if ametoka naye nyumbani ingawa mtu amekuja for the very first time(Sio ile ya Neno la maarifa) ila kiwango alichofikia kwa kutweka mpaka vilindini amepewa televisheni na miwani maalum👓📺 hadi raha,mambo wanaweza kuyafanya huko kijijini kwenu akawashuhudia kama yupo nao kulekule🏰. Sasa wengi wasioelewa haya mambo wakiona tuu hukimbilia kusema ni manabii wa uongo (NI KWELI WAPO,ILA ILI UPATE USAHIHI WA HILO JIPATIE SOMO LANGU LIITWALO, *_Roho Zidanganyazo_*)
Nilipopata ushuhuda wa Oral Roberts akiwa Uganda miaka mingi iliyopita kwa namna ambayo aliletewa kiwete ♿ambaye mguu kuanzia pajani haupo kabisa,lakini yeye kwa kuwa ametweka mpaka vilindini alijua kuna Spare organs ktk akiba ya Mungu ya kiungo chochote kile cha mwanadamu,kwa hiyo alitumiwa kufanya muujiza wa kuuleta mguu mpya ambao haukuwepo kabisa. HAKUNA HAJA YA KUSHANGAA ILI NI JUKUMU LETU LA KUTWEKA MPAKA KILINDINI.

Kama umekuwa na maombi ya saa moja,kwa nini wakati mwingine usiombe binafsi hata masaa nane kama una nafasi,Kwa nini usiamue hata kufunga na kuomba kwa muda ambao ni nje ya mazoea yako,Kwa nini usisome neno kwa kiwango ambacho hukuwahi kufanya? Nilikutana na Mchungaji Tosha toka kanda ya Ziwa,Yeye kwa miaka zaidi ya 25 amesoma Biblia zadi ya mara 25,Kila mwaka anamaliza Biblia yote mara moja,anaanza January  mpaka September anakuwa amemaliza Sasa ana ufahamu wa Neno wa kiwango cha juu mno,pamoja na kwamba ni mwalimu wa kitaifa,mwalimu wa chuo cha Biblia lakini tabia hiyo ya kutweka mpaka kilindini imemfanya awe Mwalimu wa viwango vya kutisha sana

MPANGO MKAKATI
Panga kuongezeka nguvu ktk yote tangu sasa,Haupaswi kubaki na nguvu zilezile

*Zaburi 84 : 7*

*_Huendelea toka nguvu hata nguvu, Huonekana Sayuni kila mmoja mbele za Mungu._*

*Luka 1 : 80*(John the Baptist)

*_Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu rohoni, akakaa majangwani hata siku ya kutokea kwake kwa Israeli._*

*Luka 2:40* (Jesus)

*_Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu, amejaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake._*

Mwl Proo
0762879363(Whatsapp only)

alltruth5ministries@gmail.com

UKWELI KUHUSU POMBE

*UKWELI KUHUSU KUNYWA POMBE!*
_By Mwl Proo_
0718922662/0762879363

KUNYWA POMBE NI DHAMBI KWA WATU MUNGU,HAKUNA UTETEZI WOWOTE WA KIBIBLIA. JAMBO LA KWANZA LUGHA YA KISWAHILI HAIKUWA NA MANENO YA KUTOSHA KUTAJA AINA ZOTE ZA DIVAI/MVINYO/VILEO. KTK ULIMWENGU WA ULE WA ZAMA ZA BIBLIA HUSUSANI UYAHUDI NA UYUNANI,WALIKUWA NA MANENO TOFAUTI KUTOFAUTISHA KINYWAJI HUSUKIA TOKA KWENYE ZAO LA ZABIBU. NI KAMA AMBAVYO CRUDE OIL IKIPITIA REFINING PROCESS HUTOA PETROL,DIESEL,KEROSENE ETC VIVYO HIVYO ZAO LA ZABIBU HUTOA DIVAI KILEO,DIVAI PURE JUICE,DIVAI DAWA ,ZABIBU KAVU ETC

*HAYA NI MAJINA YANAYO TOFAUTISHA AINA HIZO KAMA YANAVYOONEKANA KWENYE HEBREW BIBLE(TANAKH) NA GREEK BIBLE(SEPTUAGINT)*

1.Yayin(fermented/unfermented(
2.Tirosh (fresh juice )
3.Shekar (Strong drink/oinos)
4.Asis-(Isay 49:26,Yoel 1:5,Amo 9:13)
5.Ashishah
6.Chemer-foaming juice(all kinds of wine Isaya 27:2)
7.Chamar- fermented wine(Ezra 6:9,Dan 5:1-4)
8.Sobe -Mvinyo iliyochemshwa
9.Shemer-Mvinyo ya mabaki yaliyohifadhiwa
10.Nasek-Mvinyo iliyotolewa dhabihu
11.Mimsak-Divai iliyochanganywa(Isa 65:11)
12.Enab- (Hosea 3:1)
13.Chomet-Siki (vinegar)

KATIKA HIZI ZIPO AMBAZO NI DAWA ZA KUPAKA VIDONDA, TUYATAZAME HAYA MAANDIKO FROM OJB

PROV (Mithali) 31:6
|6| Give strong drink unto him that is ready to perish, and yayin unto those that be of bitter nefesh.

JH (Yohana) 2:10
|10| And the Rosh HaMesibba says to him, Everyone sets out the yayin hatov first, and when they have become drunk, he sets out the inferior; you have kept the yayin hatov until now. |11| This was the reshit

1TIM 5:23
|23| No longer drink only mayim, but use a little yayin because of your stomach and your frequent illnesses.

DIVAI ILIYOKUWA NI JUICE PURE NA HALALI KUNYWEWA BILA SHARTI NI TIROSH,INGAWA YAYIN NDIYO ILIKUWA THE MOST COMMON DIVAI. SASA HATUNA BUDI KUJUI DIVAI WAS A CUSTOMARY ACCEPTED DRINK, IT WAS COMMON FOR ITS RESTORATIVE AND REMEDIAL  PURPOSES, NDIO MAANA HATA HUU MSTARI WA MITHALI 31:6.ULIKUWA UNAJADILI KUWAPA KILEO WALIO KARIBU NA KUPOTEA,WATU AMBAO WALIKUWA EITHER WAMEPIGWA KWA MAWE AU WAMEKUTA NA HATARI NA WAPO KATIKA MAUMIVU KARIBU NA KUFA, WANAWAKE WALIKUWA NA TABIA YA KUWANYWESHA DIVAI HUSUSANI CHOMETS/AU SHEKARI KILEO CHENYE NGUVU,ILI WAPOTEZE FAHAMU WASISIKIE SANA YALE MAUMIVU HADI WANAPOKATA ROHO. INGAWA TUNAKUMBUKA MUNGU ALIWAKINGA WATU KADHAA WALE ALIOWATENGA KWA KUSUDI LAKE, MAKUHANI ETC,BILA SHAKA UNAKUMBUKA MKE WA MANOA AND ALL SUIT-STORIES. 
SASA LET ME CLEAR A DOUBT ON TIMOTHY. HUYU MCHUNGAJI TIMOTHEO ALIISHI KTK MJI WA EFESO, THE WATER OF THE CITY YALIKUWA SALTY AND HARD.WENGI HAWAKUWA WANAPENDELEA KUNYWA MAJI AKIWEMO TIMOTHEO, SASA KWA KUWA WATU WALIKAA HATA JUMA ZIMA BILA KUNYWA MAJI, WENGI WALIPATA SHIDA YA MATUMBO KATIKA MMENG'ENYO (CONSTIPATION), TIMOTHEO SUFFERED THE SAME. SASA PAULO ALIKUWA ANASHAURI "WATER THERAPY", AMBAPO WATU WALICHUKUA MAJI NA KUYACHANGANYA NA YAYINI KIDOGO ILI YAWE NA TASTE UWEZE KUNYWA. THE REASON BEHIND WAS NOT ULEVI, INGAWA BADO MSIMAMO WA MWISHO KUHUSU KILEVI NI "USIGUSE,USISHIKE,USIONJE" KOLOSAI 2:21
TUTAKUWA WAJINGA KAMA TUTALAZIMISHA UKRISTO WETU TUUFANANISHE NA ULIMWENGU WA KALE WA UJINGA (MATENDO 17:30) AMBAPO MUNGU HAKUWA AMEJIFUNUA KWA UKAMILIFU, WE ARE LIVING AT THE MAXIMUM REVELATION ERA

*_🍺🍻gonga tuu kama hupendi mbingu_*

alltruth5ministries@gmail.com

Wednesday, December 27, 2017

WALA HANA HABARI!!

*_WALA HANA HABARI_*

🇲 🇼 🇱  🇵 🇷 🇴 🇴

*0762879363* (whatsapp)

Nakusalimu katika jina kuu la Yesu Kristo. Mungu kuna anataka kusema nawe.

Hosea 7 : 9
~*_Wageni wamekula nguvu zake, naye hana habari; naam, nywele za mvi zimeonekana huko na huko juu yake, naye hana habari._*~

Hakuna hatari kama mambo ya hatari au yenye athari-hasi,yakawa yanafanyika kwako ukiwa ~```huna habari```~ ! NI HATARI SANA!

Ayubu 14 : 21  *_Wanawe hufikilia heshima, wala yeye hajui; Kisha wao huaibishwa, lakini yeye hana habari zao._*

👆🏼👆🏼Huyu mzazi kama angekuwa aware-of hiyo hali ya wanawe kuifikilia heshima huenda angesaidia hata kwa mawaidha ili wasishushwe viwango,lakini *hana habari*.

Kama Saphira angekuwa na habari ya kilichomkuta mmewe,angebadili msimamo,lakini alikuwa  *hana habari*.

Matendo ya Mitume 5 : 7
*Hata muda wa saa tatu baadaye mkewe akaingia, naye hana habari ya hayo yaliyotokea.*

Kuna maarifa umeyakosa,unafanya vitu kimakosa,vinakuzuia baraka zako lakini huna habari..

Mithali 5 : 6 - Hata asiweze kuiona njia sawa ya uzima; Njia zake ni za kutanga-tanga *wala hana habari.*

SASA UJUMBE WA MUNGU NI HUU. HAKUNA SIRI KTK ULIMWENGU WA MWILI ZINAZOBAKI KUWA SIRI KTK  ULIMWENGU WA ROHO,HATA ZILE ZINAZOITWA SEHEMU ZA SIRI SIO KTK ULE ULIMWENGU MWINGINE. RAFIKI YANGU MMOJA AMBAYE MACHO YAKE YA KIROHO 👁👁YAKO SHARP ALIINGIA KWA DALADALA 🚌 ALIKAA KARIBU NA BUS-CONDUCTOR(KONDA) ILA MACHO YAKE YA KIROHO YAKAONA SEHEMU ZA SIRI ZA KONDA ZIMEJAA MADONDA YA KUTISHA,INGAWA HAMJUI WALA HAWAJAI KUONANA  AKAMNONG'ONEZA NA KUMWAMBIA *_YESU ANAWEZA KUKUSAIDIA VIDONDA VYAKO VIKAPONA_* ALISHTUKA MAANA VIKO SEHEMU ZA SIRI NA HAJAMWAMBIA MTU
YAKO MAMBO MENGI UNAYAFANYA KWA SIRI,UKIWA UNADHANI UPO SIRINI KUMBE WALIOPO KTK ULIMWENGU WA ROHO WA NURU NA ULE WA GIZA WANAKUONA. UNATOA MWANYA KWA WALE MAADUI WENYE KUIHARIBU NAFSI *~hakikisha unapata somo langu liitwalo nafsi iliyojengwa pekee ndiyo inayoshinda~* WAWEZE KULA NGUVU ZAKO ZA KIROHO NA KUHARIBU YALE YA THAMANI ULIYOYARITHI KWA KUWA NDANI YA YESU.

TUURUDIE HUU MSTARI WA SOMO

Hosea 7 : 9  *_Wageni wamekula nguvu zake, naye hana habari; naam, nywele za mvi zimeonekana huko na huko juu yake, NAYE HANA HABARI._*

UNAPOKUWA KWENYE MAHALI PASIPO NA WATU(SOLITARY PLACE) SIO NAFASI YAKO YA KUFANYA YASIYOFAA.USIJIAMINISHE KWA KUWA UMEFUNGA MLANGO🚪🔐 UPO BAFUNI AU BEDROOM 🛀🏽🛌🖼🛋UKAONA HIYO NI NAFASI YAKO YA KUFANYA *~MASTURBATION~* (PUNYETO🙊) HAKUNA UNAYEMFICHA NDUGU,KUKAA GHETO NA KUJIFUNGIA ILI UTAZAME PORN-VIDEOS AU UKAWA NA JUHUDI ZA KUWEKA SECURITY CODES KWENYE KILA FOLDER LA 💻NA📱 HAKUNA UNAYE MFICHA ZAIDI YA KURUHUSU MAADUI WA KIROHO WALE NGUVU ZAKO *_WALA HUNA HABARI_*. HIVI KUKAA NA PICHA YA BINTI YUPO UCHI KWENYE ELECTRONIC DEVICES ZAKO INAKUFAIDIAJE KWA MFANO HATA UKIJITAHIDI KUIFICHA KWA KUTUMIA HIYO PICHA MAADUI WANAKULA NGUVU ZAKO NAWE HUNA HABARI,UNAJICHELEWESHA KUFIKIA VIWANGO VYAKO WALA HUNA HABARI, NGUVU ULIZOZIPATA PALE ULIPOSHIRIKI MAOMBI YA MFUNGO/FASTING YA MWEZI MZIMA NA ILE LEVEL/DARASA ULILOPANDISHWA KIROHO VYOTE VINALIWA MARA MOJA TU,ILIPOJIFICHA KUTAZAMA/KUINGALIA VIDEO YA UCHI (INTENTIONALLY) YAANI ULIPOKAA UKAHISI UNAIENJOY KULE KTK ULIMWENGU  MWINGINE ULIKUWA UNARUDISHWA DARASA AMBALO ULISHAVUKA NAWE HUNA HABARI,NI KAMA MFUNGO WA MAOMBI ILIKUWA UNAFANYA *_MARK TIME TUU_* , ETI KWA KUWA MPO NA MCHUMBA WAKO MAHALI PASIPO WATU AU PENYE GIZA,UKAHISI HUONWI NA HIVYO UKAJIHALISHIA KUFANYA USIYOPASWA UKADIRIKI HATA KUMPAPASA MATITI🙊,HUKUSALIMIKA BRO MACHO YA BWANA YALIWATAZAMA👀 (MITHALI 15:3,11) KWA MUNGU USIKU NA MCHANA VYOTE NI SAWASAWA,ULIPOTEND HAYO HAFU UMEJIKAZA KISABUNI,KUMBE WALE MAADUI WA KIROHO WANAKUFUATILIA WAPI UTAANGUKA,WALIUTUMIA MWANYA HUOHUO KULA NGUVU ZAKO WAKAKUFYONZA NA KUKUSAZA MKAME *_WALA HUNA HABARI_* NDIO MAANA YALE MAOMBI YENYE UVUVIO WA MWENDOKASI YAMEENDA LIKIZO,UKIJARIBU KUJIOMBESHA KWA NAMNA ILE UNACHOKA KWA DAKIKA 5 NA KUISHIA KUIKATA SAUTI TU.

*"YOUR PRIVACY(WHEN YOU ARE ALONE) SHOULD BE DEDICATED TO THE LORD"*
WAKATI UKIWA PEKE YAKO,NI WAKATI WAKO MZURI  WA KUENJOI UWEPO WA MUNGU,WENGI WALIOTEMBELEWA NA MUNGU(ANNUNCIATION=DIVINE VISITATION) ZILIWAKUTA WAKIWA PEKE YAO AT SOLITARY PLACES
NUHU ALIPOKEA MAELEKEZO YA KUJENGA SAFINA WHEN HE WAS AT SOLITARY PLACE,SO DID IBRAHIMU KULE MAMRE, YAKOBO PALE LUZ,NA USIKU ULE ALIOSHINDANA NA MALAIKA Mwanzo 32 : 24 - *Yakobo akakaa peke yake;* na mtu mmoja akashindana naye mweleka hata alfajiri. PIA MUSA KTK MLIMA HOREBU,GIDEON KTK UWANDA WA KUPURIA,SAMWELI HEKALUNI,MKE WA MANOA SHAMBANI N.K

UKIWA KTK USIRI(PRIVACY/ALONE) NI WAKATI WAKO WA KUENJOI UZURI WA MUNGU NA SIO KUJIFURAHISHA KWA UCHAFU KWA KITAMBO TU NA KUJIPATIA HASARA. TUMIA MUDA HUO KUOMBA,KUSOMA NENO,KUTAFAKARI WEMA WA MUNGU AU FANYA SHUGHULI ZAKO TU ZA KIJAMII

Marko 1 : 35
*Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko.*

FANYA MAAMUZI SASA,SEMA *_SASA BASI_*  SEMA *_YATOSHA SASA_* KUZUNGUKA KWENYE KAMLIMA KA KURUHUSU MAADUI WALE NGUVU ZANGU,SASA  AMUA KUSHTUKA. AZIMIA KUACHA MATENDO YA KWANZA,INAWEZEKANA KABISA. MUNGU YUPO TAYARI KUKUSAIDIA KTK MAISHA MAPYA UNAOYATAMANI AKUPE MIANZO MIPYA,ILI AKUTAKASA KABISA.NARUDIA TENA INWEZEKANA,MIMI NI KIJANA LAKINI SMARTPHONE NINAYOITUMIA📱 HAINA NGUVU KUNIZIDI HAIJAWAHI KUTUMIKA ETI KUINGIA G🌏🌍GLE KU-SEARCH VIDEO ZA NGONO NO NILIFANYA MAAMUZI NA KUSEMA NOO👐🏽,KAMA UNADHANI HUWEZI KUACHA MASTURBATION POKEA UKWELI HUU UNEWEZA UKAWEZA MARA MOJA TUU,NA HIYO NGUVU IPO JUU YAKO TANGU SAA HII,HIYO MICHEZO MICHAFU KAMA MASTURBATION NILIFANYA MAAMUZI MWAKA 2004 NIKIWA MWANAFUNZI WA SEKONDARI,HUU MWAKA WA 12 SIJAWAHI KUJARIBU WALA SITAKI TENA NACHUKIA(MITHALI 8:13) NAANZAJE KWA  MFANO?? YAANI NIFANYE HAYO HAFU NICHUKUE DIARY📕KUANZA✍🏽KUANDAA MAHUBIRI KAMA HAYA,HUO NI USANII WA FIRST CLASS

YESU KRISTO AKUTIE NGUVU TANGU SASAUNASULIWE KTK NGOME HIYO NA HIY NIRA IKATWE KWA JINA LA YESU,MAADUI WASIKUPATE HATA KUZILA NGUVU. YOU WILL NO LONGER BE UNAWARE(2KOR 2:11)

Mwl Proo
0762879363(whatsapp only)

alltruth5ministries@gmail.com

Sunday, December 17, 2017

FUNDISHO LA ZAKA/FUNGU LA KUMI

*NINI UKWELI KUHUSU FUNDISHO LA ZAKA/FUNGU LA KUMI*

©2015

Na
_Mwl Proo_
0762879363
0718922662

Nina wasalimu katika Jina la BWANA(Yesu) . Karibu tujifunze ili utoaji wetu uwe na maana sawa na kweli ya Injili.

SOMO LINA SEHEMU 12

I.)UTANGULIZI
II.)ETIMOLOJIA
III.)HISTORIA YAKE
IV.)ABRAMU NA YAKOBO
V.)ZAKA YA KILAWI(LEVITICAL TITHE)
VI.)TAFSIRI ISIYO SAHIHI KTK MALAKI 3
VII.)ZAKA KTK AGANO JIPYA
VIII.)LINI FUNDISHO HILI LILIINGIZWA?
IX.)NINI MSINGI WA UTOAJI KTK AGANO JIPYA(POST-CALVARY COVENANT)
X.)SHUHUDA ZA WALIOBARIKIWA
XI.)POSSIBLE GROUNDS TO JUSTIFY TITHING IN CHRISTIANITY
XII.)HITIMISHO

*I.) UTANGULIZI*
Kumekuwa na pande mbili zinazokinzana whether fundisho hili ni sahihi au sio sahihi ktk UKRISTO. Na tatizo kubwa lipo ktk msingi wa fundisho(Zab 11:3). Niseme kwamba UKRISTO SIO UYAHUDI INGAWA ULIANZA KAMA DHEHEBU NDANI YA DINI YA KIYAHUDI. Sasa ktk kuyachukua yale yaliyokuwa ktk dini ya KIYAHUDI(JUDAISM) kuyaleta ktk Ukristo inahitaji ufahamu mzuri wa kiroho wa kuweza kuchanganua ni nini ktk yale ya dini ya kiyahudi ambapo kuna (Maagizo ya Mungu+Utamaduni wa kiyahudi/traditions) Sasa lazima tujue kipi ni utamaduni na kipi ni agizo la Mungu endelevu(eternal moral principle).Utata umezuka ktk mambo mengi tu hasa inapofika kwenye kuyavusha mambo ya AGANO LA KALE KUYALETA KTK UKRISTO (Post-Calvary Covenant) Je tuyaache yote au tuyabebe yote? Kwa hiyo unakuta kila mtu anafundisha cha kwake maana mwingine akijaribu kuliset fundisho la MALIMBUKO kwa namna ileile ya Taurat anaona inakuwa ngumu au fundisho jingine lolote na hivyo kila watu ktk dhehebu lao hufundisha wanavyoona inafaa wao. Tunawezaje kupatata pure Christian Doctrine ktk maswala haya yote. Hatuwezi kama hatutarudi kwenye msingi ili kupata maarifa

*II.)ETIMOLOJIA*
Ktk historia ya neno zaka/tithe haikuwa na tafsiri ya sehemu ya kumi moja kwa moja. Kama ambavyo tutaona ktk sehemu ya tatu ya somo kuwa kiwango kiwango kilifanyiwa makaribisho ya chini(Rounded down) lakini sehemu ndogo yoyote ile ya ongezeka la pato (produce/income) na ndiyo maana ktk Kumbukumbu la torati 14:22-26 tunakutana na usemi wa ZAKA YA FUNGU LA KUMI
22 Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka.

Lakini tafsiri baadae ikawa ukizungumza TITHE/ZAKA UNAZUNGUMZIA SEHEMU YA KUMI(TENTH) ingawa tutaona ktk sehemu ya 5 ya somo kuwa jumla ya zaka ilikuwa ni <23% ktk Biblia. Sasa kietimolojia Neno la kiebrania Ma'aser linamaanisha zaka yaani sehemu ndogo(ya kumi) inayotolewa toka ktk increase ya produces na neno lilitumika ktk Septuagint(LXX) ni "Dekate" linalomaanisha moja kwa moja sehemu ya kumi. Neno hili Tithe/Tenth limetokea kwenye Old English "Teogopa" au Teopa(Western Saxon) na kijerumani "Teguntha" utoaji wa sehemu ktk mapato ilikuwa ni namna ambayo mataifa mengi yaliitumia hata kabla ya Sheria ya Musa(Mosaic Law) haya tutayaona ktk sehemu inayofuata lakini hata Yusufu akiwa Misri aliasisi sheria ya kutoa sehemu ya 5 ya mazao kwa Farao na sehemu ya 4 ilikuwa watu waitumie wenyewe(Mwanzo 41:34,47:24,26)

*III.)HISTORIA YA ZAKA(TITHING IN HISTORY)*

Utoaji wa zaka haukuanzia kwa Ibrahimu kama ambavyo wengi wanaotumia single source wanafundisha. Ktk Assyriological&Ancient Babylonian Literature tunaona kuwa hata mataifa ya kipagani ya vile vizazi baada ya Nuhu wote walikuwa wakitoa ZAKA kwa miungu(Waashuru walitoa zaka kwa mungu aitwaye *Anzu* na wale wababeli ya kale kwa mungu aitwaye *Merodaki*(Marduk)Wafalme walikuwa na local priests waliopokea Zaka ambazo ni sehemu ya kumi iliyo karibishwa chini. Kwa mfano Sheria iliwataka ktk nyara za vitani ktk kila mavazi 85 watoe zaka mavazi 8 na kwa kwa sababu hiyo ni kwamba ilikaribishwa chini maana mavazi hayo hayagawiki kwa kumi  bila sehemu.Sasa kwa wale wenye haki sana walitoa mavazi 9 Sheria hii ilikuwa na limitation kulingana na nyara.Lakini ikumbukwe pua Sheria ya Musa ilizingatia hilo wale waliokuwa na vitu pungufu hawakutoa zaka ya fungu la kumu.Mfano mtu mwenye ng'ombe chini ya 10 kiidadi hakutoa zaka (Lawi 27:32). Kwa hiyo tayari mataifa yenye kuabudu miungu yalikuwa yana utaratibu wa kutoa zaka kabla ya Abramu na kabla ya Sheria ya Musa

*IV.)ABRAMU NA YAKOBO*

Katika Mwanzo sura mbili  14&18  zinazungumza watu wawili kutoa sehemu ya kumi ya walivyopata(Abramu alitoa sehemu ya kumi ya kila nyara na Yakobo anaweka nadhiri kutoa fungu la kumi kama Mungu akimfanikisha ktk njia yake)

_a.)KUHUSU ABRAMU_

Maswali la matatu ya msingi kuhusu Abramu...i. Kwa nini alitoa sehemu ya kumi ii.Nani alimwagiza iii.alijifunza wapi

Maswali haya wahubiri wengi husema alifanya kwa hiari yake(Okey nice) inapofikia kuhoji alijifunza  wapi hatuwezi kukwepa ukweli kuwa Abramu(maana alikuwa bado hajatahiriwa wala hajapokea yale maagano yaliyopelekea kubadilishwa jina kuwa Ibrahimu swala la Mwanzo 12 Abram's call limezingatiwa) Lakini huyu Abram alilelewa ktk familia ya kipagani yenye kuabudu miungu kwa mzee Terah na ilikuwa kule Mesapotamia(Ancient Babylon) huko ndipo tulipoona hizo desturi za kutoa zaka zilikotokea nitaeleza haya sehemu ya 12 ya somo.
Katika Encyclopedia of Religion imeeleza kile alichofanya Abramu kinaitwa "Arab Custom of War" ndio maana alitoa sehemu ya kumi na vilivyobaki vyote hakuchukua hata uzi wala sindano wala gidamu vyote akampa mfalme wa Sodoma(Inaitwa Law of the Land) (NA HAKUNA NUKUU YOYOTE KUWA ALIWAHI KUFANYA HIVYO AU KUTOA TENA KWA OCCASION YOYOTE(one time recorded event)
_b.YAKOBO_
Kwa habari ya Yakobo ni ishu tofauti maswali yale ya kwanza yanaweza kujibika sema huyu alifanya _"VOWED TITHING"_ alijinadhirisha mwenyewe kuwa Mungu nikienda huko nikafanikiwa nitakutolea sehemu ya kumi.

*V.)ZAKA YA KILAWI(LEVITICAL TITHE)*

Sasa tumeingia kwenye moyo wa somo. Katika Hesabu 18 ndipo tunapoona swala la zaka kwa upana likielezwa. Sasa zaka hii ya kilawi na taratibu zake zitatula kuona kuwa haziwezi kuwa applied ktk UKRISTO AU KANISA kabisaa. Tutayaona hayo ktk sehemu ya saba ya somo. Zaka ya kilawi ilitokana na ukweli kwamba WALAWI HAWAKUPASWA KUMILIKI MALI(Should not own properties) na pia hawakupaswa kuwa na urithi kama makabila mengine. Na hivyo tuelewe kuwa ZAKA haikupelekwa kwa Makuhani toka waisrael bali zilikuwa zikipelekwa kwwnye miji ya walawi (Levitical cities) Hes 18:21 Kwa hiyo Wana wa Israel walipeleka Zaka kwenye miji ya walawi (10%) na wao Walawi walichukua 10%ya kile kilicho bora ktk Zaka ndicho walipeleka kwa makuhani kwa maana zaidi ya 80% hawakuwa makuhani ingawa kabila lao ndilo lililotengwa kwa utumishi huo. Kwa maneno mengine ni 1% ya maongeo ya watu ndiyo yaliyofika kwa kuhani. Ikumbukwe zaka ilikuwa ni kwa vile ambavyo vimezalishwa(produces) ndani ya ardhi takatifu ya Waisrael . Hakukuwa na zaka ya pesa ingawa pesa zimetajwa mara 44 toka Mwanzo mpaka mpaka wakati wa agizo la Musa lakini hakukuwahi kutolewa zaka ya pesa (Luka 11:42). Ile zaka ambayo walipewa kibali kuibadili iwe fedha nitatoa ufafanuzi na pia kuna mjadala mzuri unaojadili kwa nini yule Farisayo (Luk 18:12) alisema anatoa zaka ktk mapato yote. Jambo jingine la muhimu ni hili Zaka zilikuwa za aina 3. zinazofanya jumla ya Zaka ni 23% na sio 10%.Wanaofundisha kuhusu Zaka leo hii wanaangalia juujuu tuu bila kutanabaisha na kubainisha ktl zile aina tatu ipi wao hasa wanaifundisha kwa sababu zipi

Zaka aina ya kwanza ni ile ya 10% inayopelekwa ktk miji ya walawi (Lawi 27:30,Hesabu 18:21)
Zaka aina ya pili ndiyo ile ambayo walipaswa kuitunza kwa ajili Sikukuu ya Bwana kila mwaka wa tatu na walipeleka Yerusalem Kumbukumbu 26:12 12:6,14:22-27 Zaka hii nayo ni asilimia 10 ila wapokeaji walikuwa ni Walawi,Wageni,Wajane na Yatima
Na ipo ambayo ilipaswa kuhifadhiwa ndani kwa ajili ya maskini na makundi mengine ya marginalized hii ilikuwa Around 3% it makes a sum of around 23%{Deut 14:28-29} Wengi wanaofundisha zaka hawafafanui hizi zaka zinazoliwa na raia mpaka mtoaji

*VI) TAFSIRI YENYE MAKOSA KTK MALAKI 3:8-10*

Wahubiri wa Zaka ya fungu la kumi au wakristo wengi ukitaja tuu zaka wanapachika Malaki 3:8-10

Hiki ni kifungu kinachofanyishwa kazi isiyo yake

Zipo kanuni za kutafasiri maandiko (HERMENEUTIC PRINCIPLES) Zinatutaka tuulize vitu vya msingi nani aliandika na alimwandikia nani?Kulikuwa na nini hasa(Background&History) kulikuwa na muktadha upi(Context) Nabii huyu Malaki hakuwaandikia Israel wote ila uko ujumbe wa taifa lote pia..Aliwaandikia Makuhani (Mal 1:6ff,13-14) historia inaonesha hekaluni kulikuwa na chumba kikubwa(storeroom) kinatajwa ktk Nehemia 10:37,13:5) makuhani walikuwa wakiiba ktk vile vilivyopo kwenye storeroom na hata kuwasaidia wananchk wengine kuiba kwa kutoleta.Ikumbukwe raia walipeleka zaka kwa walawi nao walipeleka sehemu ya kumi bora ya ile sehemu ya kumi(1%) Makuhani pato lao kuu ualikuwa zaka bali ktk sadaka za hiari.Nao hawakutoa zaka tena kutoka ktk zile zaka bali walitoa kwa hiari kutoka ktk sadaka za hiari. Kwa hiyo nabii Malaki aliufunua uovu huo na akaagiza iletwe zaka kamili. Agizo la kuleta Zaka ktk kile chumba chenye ukubwa wa 10x20feet au 3x6metres halikuwa la Waisrael wote kwa kuwa zaka zao hazikupelekwa hekaluni na pia kwa kuwa zaka ilihusisha mazao ya ardhi na mifugo isingetosha kamwe kwenye ghala ya ukubwa huo kama Sitting room yetu .Hivyo ni muhimu kujifunza tafsiri sahihi ya maandiko ili mahubiri ya sahihi..

*VII)ZAKA KTK AGANO JIPYA*

Agano jipya halikatazi kutoa zaka ya fungu la kumi kama ambavyo pia haliagizi watu watoe(And the New Testament does not condemn Tithing). Kimsingi agano jipya limetaja zaka maeneo matatu kimsingi yaani
1.Mathayo 23:23/Luka 11:42
2.Luka 18:12
3.Ebrania 7:1-10,12

Maeneo mawili ya kwanza Yesu aliitaja akiwashutumu Mafarisayo kwa unafiki wao kisha e mfano wa Farisayo
Na baada ya hapo ipo ktk Ebrania 7 ikifanya mrejeo wa utoaji wa Sehemu ya kumi kwa Melkizedek na mstari wa 12&18 inaweka turning point na kwa msingi huo inaonesha kama ukuhani ukibadilika na sheria inabadilika..Haya tutayachambua ktk sehemu ya tisa ya somo. Kimsingi hakuna mtu anaweza akafundisha utoaji wa sehemu ya kumi kwa namna yoyote kwa kufuata Agano Jipya. Ninaposema Agano Jipya ni Post-Calvary Covenant... wengi wanatumia Mathayo 23:23b
*".....hayo imewapasa kuyafanya wala msiache yale mengine*
JE ANDIKO HI LITAWEZA KUHALALISHA FUNDISHO LA ZAKA. La hasha,Yesu ktk zama zake alikuwa ktk Jewish Religion&Tradition 100% Ingawa alileta tafsiri sahihi(Math 5:17) Sasa Post-Calvary Covenant sio Ndilo Agano Jipya... Wengi tukisema Agano Jipya wanawaza kitabu na zile nyaraka...Kumbe baada ya Yesu kuondoka Kanisa la kwanza lilikaa miaka karibu 30 hakukuwa na Injili wala nyaraka za mitume...Lakini Practically walikuwa ktk AGANO JIPYA ambalo Mungu alisema halitakuwa kama lile alilogana na mababa zao(Yer 31:31-40) sehemu ya tisa nitaeleza kwa kina haya yote.

*VIII.) LINI FUNDISHO HILI LA ZAKA LILIINGIZWA KTK UKRISTO?*

Wanahistoria wa kanisa wameeleza kwa kina kuhusu fundisho hili. Viongozi wa kwanza wa kwanza wa kanisa baada ya mitume(c95 hadi c200)AD hawakuwahi kukubali kuingiza fundisho hili maana waliliona kuwa 100% ni Jewish tradition. Hii haina maana kuwa hakuagiza Mungu.. Bali ktk yale maagizo yako ambayo hayawezi kuwa eternal moral principles maana yalikuwepo kwa muktadha fulani(Certainty of Context) So wazee wetu walijitahidi kujua kipi ni FUNDISHO LA UKRISTO kipi ni completely Jewish Tradition which not necessary to be incorporated in Christian Doctrine .Watu hawa Clement of Rome,Justin Martyr,Irenaeus na Tertullian hawakuruhusj fundisho hilo pamoja na kukubalina sana na swala la *UTOAJI* ila sio zaka ya kilawi.
Cyprian wa Cathage alijitahidi kwa bidii sana 250 A.D kuingiza swala la zaka bila mafanikio..Hata Karne ya nne ambapo UKRISTO ulipotambulika kisheria kama DINI bado hakukuwa na fundisho hilo. Mwaka 585 wakati wa baraza la Macon huko Ufaransa walijaribu tena bila mafanikio kuingiza zaka. ZAKA HAIKUWAHI KUWA FUNDISHO MPAKA MWAKA 777 AD Ambapo Emporer Charlemagne alipoipitisha kisheria kanisa kukusanya zaka (IKUMBUKWE WAKATI HUO KANISA LILIKUWA NI TAASISI YA SERIKALI) kwa sababu hiyo Catholic Church ikawa ina fundisho hilo mpaka wakati wa kuinuka kwa Uprotestanti Karne ya 15 ambapo wengi wa wale fathers of protestantism hawakukubaliana nalo pia,ingawa hawakuweza kuchuja mafndisho yote..mengi yaliendelea ktk uprotestant.Hata wahubiri wa kipentekoste ambao nawaita ni 4th Generation wakiwa ni zao toka kwenye uprotestanti lakini Karne ya 20 hawakuweza kuchuja sana kwa habari ya mafundisho ila kuwa na mkazo maeneo mihimu kama ujazo wa Roho Mtakatifu,karama za rohoni etc etc Hivyo hakuna muhibiri hata wa kipentekoste ambaye anaweza kutueleza nini msingi wake kufundisha hilo ktk Agano Jipya. Jibu walilo nalo nitalijadili sehemu ya 11

*IX.)NINI MSINGI WA UTOAJI KTK AGANO JIPYA(POST-CALVARY COVENANT)*

Msingi mkuu wa mambo mengi ktk Agano Jipya ni Imani na Upendo wa kumpenda Mungu ndio ulete msukumo wa matendo ya haki. Hakupaswi kuwa na shuruti ili ufanye kitu au vitisho kama baadhi ya wahubiri wanavyo tumia Malaki 3:8-10 kuwatishia *LAANA*  watu waliokombolewa toka kwenye  laana(Gal 3:13)
UTOAJI KTK AGANO JIPYA NI HIARI(inayotokana na kuenda Mungu na kufahamu kuwa unapaswa kutoa)

2Kor 9:7
7 Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.

SWALA LA KIASI GANI mtu anapaswa kuamua moyoni mwake kwa ukunjufu sio kutaja sadaka na viwango ambavyo wengine unakuwa umewalalia hasa.Na hata ile 10% sio kipimo cha kumpenda Mungu na tena hakuna usawa

2Kor 8
11 Lakini sasa timizeni kule kutenda nako, ili kama vile mlivyokuwa tayari kutaka, vivyo hivyo mkawe tayari na kutimiza, kwa kadiri ya mlivyo navyo.
12 Maana, kama nia ipo, hukubaliwa kwa kadiri ya alivyo navyo mtu, si kwa kadiri ya asivyo navyo.
13 Maana sisemi hayo, ili wengine wapate raha nanyi mpate dhiki;
14 bali mambo yawe sawasawa; wakati huu wa sasa wingi wenu uwafae upungufu wao, ili na wingi wao uwafae ninyi mtakapopungukiwa; ili mambo yawe sawasawa.
MISTARI HII INAJADILI EQUALITY
Mtu mwingine anafanya biashara ha kuingiza magari ya kifahari anapata milion 400 sasa wengi kwa fundisho la zaka..akitoa milion 40 ananihesabu kuwa na haki huku kabakiwa na milion 360 na kuna uhitaji zaidi ktk ufalme..na hivyo anaendelea kutoa sadaka shiling elfu1 akiamini ametimiza ile sheria ya zaka.Huu haupaswi kuwa msingi wa utoaji. Wengine imebidi wabuni sadaka mbali mbali kumbe ni matokeo ya kutotambua nini msingi hasa wa utoaji ktk Agano jipya.Wiki hii nimeongea na mshirika mmoja wa kanisa la Assemblies of God. Amesema kwao imeongezwa sadaka inaitwa *SADAKA YA MWANAKONDOO* ambapo mtu anapaswa kuahidi kiwango kikubwa at abnormal rate🤔💵💰 Sasa haya ni matunda tu ya kuoelewa msingi. Sadaka inapaswa kuwa hiari,ya binafsi na kwa nia ya kutaka kutoa kwa imani na kumpenda Mungu
Kutoka 35:5,21,2Nyak 29:31,Ezra 2:68,7:5,Zab 54:6

SACRIFICAL "FREEWILL" GIVING NDIO HASWAA MSINGI WA UTOAJI

*X.)SHUHUDA ZA WALIOBARIKIWA*

Shuhuda za waliobarikiwa walipotoa Zaka ya Fungu la kumi...halitoi mwanya wa kutengeneza fundisho. Maana GIVING AND RECEIVING ITSELF IS A PRINCIPLE (Mdo 20:35,Filip 4:15)

15 Nanyi pia, ninyi wenyewe mnajua, enyi Wafilipi, ya kuwa katika mwanzo wa Injili, nilipotoka Makedonia, hakuna kanisa lingine lililoshirikiana nami katika habari hii ya kutoa na kupokea, ila ninyi peke yenu.
NITAYELEZA HAYO KWA KINA KTK HITIMISHO

*XI.) GROUNDS ON WHICH I JUSTIFY TITHE*

Jambo la kwanza nieleze kuwa mimi natoa mafungu ya kumi ktk mapato yangu. Natoa kwa utaratibu wa kanisa letu tuliorithishwa ila sio kama fundisho au agizo kwa wakristo maana moyo wa kupenda Mungu sihesabu kile kuwa ni kitu kama ninavyojitoa nafsi yangu yote kwa Bwana na pia utoaji wa zaka ktk dhehebu ninaloabudu hautunyimi sisi wanafunzi wa Biblia kujifunza.
A.)Jambo la kwanza kuhusu kujaribu kueleza kwa namna gani naweza kui-justify tithe ni hii. Ingawa asili yake inatoka kwa mataifa ya kipagani hata kabla ya Abramu wala Sheria ya Musa..bado yale mataifa ya kipagani yaliyoishi baada ya Gharika ni muendelezo wa Uzao wa Nuhu.Sasa inasemekana watoto wa Nuhu walikuwa na maelekezo hayo toka Baba yao kuhus tabia ya kumtolea Mungu na pia sources nyingine zinaonesha Ile miungu iliyodai kupewa TITHE iliiga tabia/kanuni ya Mungu.Imumbukwe ibada za sanamu enzi za Nimrodi ni kitu ambacho wanadamu walifundishwa na wale malaika wasioilinda enzi na kuyaacha makao yanayowahusu(Yuda 1:6,2Petro 2:4) Sasa kama umesoma kwenye kitabu cha Henoko...ingawa wahubiri wengi wanapinga bila kufahamu, ila ni source of knowledge na waandishi wa Biblia walikisoma na kuuamini unabii wake(Yuda 1:14) Utagundua kuna mambo ambayo wale malaika 200 waliwafundisha wanadamu kimakosa.Ila vingine ni principles halisi za Mungu

B.) Namna ya pili ni hii kwa kuwa msingi tayari uliharibika(Zabur 11:3) at least basi njia hiyo inasaidia wakristo kujiepusha na choyo(Luk 12:15) maana wengi wakiachwa huru wanachagua vibaya *KUTOTOA KABISA* ingawa kutoa kwa sababu umeletewa mwinjilisti maalum wa muhimiza *UTOAJI* Akaweka na vitisho vingi vya kulaaniwa.Huo ni msingi usio  sahihi

*XII.)HITIMISHO*

Somo hili kamwe halilengi kupinga UTOAJI bali kufundisha msingi sahihi
*KUTOA/GIVING IS A MUST*

WATU WANAPASWA KUFUNDISHWA KUWA LAZIMA WATOE

WHY?
1.NI AGIZO(Luka 6:38)
2.ILI KAZI YA MUNGU ISONGE MBELE (1Kor 16:1-3)
3.ILI KUJIWEKEA HAZINA MBINGUNI(Math 6:19-21)
4.ILI KUPATA BARAKA ZA MWILINI HAPA DUNIANI(Filip 4:12-19)

ASANTE KWA KUFUATILIA NAAMINI UMEJIFUNZA MENGI

Mwl Proo
0762879363

alltruth5ministries@gmail.com

KAA NA LADHA YAKO WALA HARUFU ISIBADILIKE

🇦 🇱 🇱     🇹 🇷 🇺 🇹 🇭

*KAA NA LADHA YAKO WALA HARUFU ISIBADILIKE*

_Mwl Proo_
*0762879363*
0718922662

Haleluya!
Bwana analo Neno kwa ajili yetu leo, na neno lake kwako ni hili *_"kaa na ladha yako,wala harufu yako isibadilike"_*

*Yeremia 48 : 11*
*_Moabu amestarehe tangu ujana wake, naye ametulia juu ya sira zake, wala hakumiminwa kutoka chombo kimoja kutiwa chombo kingine, wala hakwenda kufungwa; kwa hiyo ladha yake anakaa nayo, wala harufu yake haikubadilika._*

UNAJUA SISI NI MATAWI TULIOPANDIKIZWA KTK SHINA JEMA YESU KRISTO(INGRAFTED BRANCHES) Warumi 11:11-24  Sasa ule umwitu unaondoka,kila mtu akikutana na Yesu anakuwa na *taste* na *smell* mpya ya namna yake,hiyo ladha na harufu imetokana na shina Yesu Kristo,Sasa Mungu anatazamia hiyo ladha yako ukae nayo na ile harufu isibadilike,bila kujalisha mabadiliko ya mazingira au mambo mengine.

Mimi ni mwalimu wa Jiografia,kuna kitu tunakiita *_River Regimes_* haya ni mabadiliko ya ujazo wa maji ya mto na tabia zingine za mto,kwa mfano mto Nile umeanzia ktk Ziwa Victoria,unasafiri mpaka Misri unakoenda kumwaga maji yake ktk bahari ya Mediterania. Huu mto ktk safari yake unabadili sifa(ladha na harufu) Ukienda kuupima huu mto hapo Uganda una kuwa na properties(sifa) tofauti na zile ambazo mto huu unazo unapofika Sudan(yaani hata Chemical composition yake hubadilika) ,unaweza kupima kiasi cha asidi/alkali kwa kutumia pH-scale ukahisi ni mto mwingine tena usiotoka Ziwa Victoria.

*MUNGU ANASHANGAA AKIONA UMEBADILIKA LADHA NA HARUFU*

*Yeremia 2 : 21*

*_Nami nalikuwa nimekupanda, mzabibu mwema sana, mbegu nzuri kabisa; umegeukaje, basi, kuwa mche usiofaa wa mzabibu-mwitu machoni pangu?_*

*Isaya 1 : 21*

*_Mji huu uliokuwa mwaminifu umekuwaje kahaba! Yeye aliyejaa hukumu ya haki; haki ilikaa ndani yake, bali sasa wauaji!_*

*UKIACHA KUKAA NA LADHA YAKO, NA HARUFU YAKO IKABADILIKA,HAUBAKI NA UTUKUFU SAWA*

1.Shetani alikuwa anakaa na ladha na harufu fulani ila akaacha kukaa nayo hata kubadili harufu yake

*Isaya 14*

*_11 Fahari yako imeshushwa hata kuzimu,Na sauti ya vinanda vyako;Funza wametandazwa chini yako,Na vidudu vinakufunika._*
*_12 Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni,Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi!Jinsi ulivyokatwa kabisa,Ewe uliyewaangusha mataifa!_*

*Ezekiel 28*

*_13 Ulikuwa ndani ya Adeni, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako, akiki, na yakuti manjano, na almasi, na zabarajadi, na shohamu, na yaspi, na yakuti samawi, na zumaridi, na baharamani, na dhahabu; kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako; katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari._*
*_14 Wewe ulikuwa kerubi mwenye kutiwa mafuta afunikaye; nami nalikuweka hata ukawa juu ya mlima mtakatifu wa Mungu, umetembea huko na huko kati ya mawe ya moto._*
*_15 Ulikuwa mkamilifu katika njia zako tangu siku ile ulipoumbwa, hata uovu ulipoonekana ndani yako._*

2.Taifa la Israel lilipoteza ladha na kubadili harufu wakati fulani

*Maombolezo 4*

*_1 Jinsi dhahabu ilivyoacha kung'aa?,Na dhahabu iliyo safi ilivyobadilika!Mawe ya patakatifu yametupwa mwanzo wa kila njia._*
*_2 Wana wa Sayuni wenye thamani,Walinganao na dhahabu safi,Jinsi wanavyodhaniwa kuwa vyombo vya udongo,Kazi ya mikono ya mfinyanzi!_*
*_3 Hata mbwa-mwitu hutoa matiti,Huwanyonyesha watoto wao;Binti ya watu wangu amekuwa mkali,Mfano wa mbuni jangwani._*
*_4 Ulimi wa mtoto anyonyaye wagandamana na kaakaa lake kwa kiu;Watoto wachanga waomba chakula,Wala hakuna hata mmoja awamegeaye._*
*_5 Wale waliokula vitu vya anasa wameachwa peke yao njiani;Wale waliokuzwa kuvaa nguo nyekundu wakumbatia jaa._*

*_7 Wakuu wake walikuwa safi kuliko theluji,Walikuwa weupe kuliko maziwa;Miili yao, walikuwa wekundu kuliko marijani,Na umbo lao kama yakuti samawi._*
*_8 Nyuso zao ni nyeusi kuliko makaa;Hawajulikani katika njia kuu;Ngozi yao yagandamana na mifupa yaoImekauka, imekuwa kama mti._*

PIA KTK MAANDIKO TUNASOMA WENGI WALIOACHA KUKAA NA LADHA ZAO NA KUBADILI HARUFU. LAKINI SASA TUYATATHMINI MAISHA NA SAFARI YETU, JE TUMEKUWA NA VARIATIONS KAMA ZA ULE MTO _"RIVER REGIME"?_ ,WENGI TASTE/SMELL ZIMEBADILIKA/SHWA ATI NA NDOA,KADIGRII KAMOJA ETC,HUYU ALIYEKUWA NGUZO YA HUDUMA FULANI CHECH AMEOA TU AKABADILI HARUFU,KUNA MABINTI WALIKUWA WAKIIMBISHA MAKANISANI ILA HIYO HUDUMA ILISITISHWA NA KUOLEWA,HUPASWI KUACHA KUIHUDUMIA NDOA KWA SABABU ZA KIHUDUMA NA PIA HAUNA SABABU YOYOTE YA KUACHA HUDUMA(MAMBO YOTE YAFANYIKE KWA UZURI NA KWA UTARATIBU-1kor 14:40),KUNA VIJANA WALITUMIKA VIZURI SANA WAKIWA TAASISI ZA ELIMU,ETI WALIPOPATA KAZI *_WAMEKOMAA HADI WAMEKOMA_*  WALISHASAHAUGI KAMA KUNA KITU KINAITWA HUDUMA NA KUJITOA KWA BWANA. WAMEBAKI NA HISTORIA TUU,TULIWAHI KUFANYA GOSPEL OUTREACHES MAENEO YENYE NGOME ZA UCHAWI,TULIKUWA TUNAFUNGA SANA AISEE TUKIWA CHUONI,MWINGINE ALIKUWA MWALIMU MZURI WA NENO,ILA KWA SASA HAKUMBUKI MARA YA MWISHO NI MWAKA GANI ALISIMAMA KUHUDUMU,ULIPOKUWA UNAHUDUMU ILIKUWA NJIA NYEPESI YA KUJIJENGA NAFSI YAKO PIA,KWA WALE WAHUBIRI NI MASHAHIDI KUWA KUNA MUDA UPO KWENYE DALADALA🚌LAKINI KWA KUWA KIKOMBE CHA ROHONI KIMEFURIKA UNAJISIKIA NAFSI YAKO UNAENDELEA KUHUBIRI, SASA HAYO UKAYAACHA NDIO MAANA IJAPOKUWA ULIZALIWA UPYA ILA UNAJIJUA UNAVYOSHINDANA NA MWILI,😃YAANI NGOMA YA DIAMOND PLATINUMS 🎤🎼🎹🎸IKIGONGA UNAANZA KUTIKISA KAMGUU THEN KAKICHWA THEN MOYO,KISHA UNAUDAUNLOD,KWELI WEWE KAKA MWINJILISTI ULIKUWA NI WA KUKAA NA WIMBO WA ALI KIBA KWENYE SIMU📱 YAKO? *UMEACHA KUKAA NA LADHA YAKO. HIVI SI WEWE ULIJAA MISTARI YA MOYO KAMA ULILISHWA BIBLIA,SASA MBONA LEO HATA KIFUNGU CHA MATHAYO 5:8 HUKIKUMBUKI KILE KIFUNGU ULICHOKIKARIRI TOKA MWAKA 1986 KWENYE SUNDAY SCHOOL YA WATOTO👶🏾,. YOU ARE NOW A BUSY BUSINESS MAN😱😱😱 WITO WAKO MKUBWA NI MAFANIKIO YA DUNIA HII🌍,NA KWA KUWA UMEKUWA MATERIALIST SASA UNAWAHI KUTUMA ZAKA KWA M-PESA ILI KUMVUNGA MCHUNGAJI ASIKUHOJI SANA KUHUSU YOUR ABSENTISM. NA MAKANISA YALIBADILI HARUFU, YAANI MSHIRIKA HAI SIO MWENYE KIROHO SAFI BALI ANAYETOA ZAKA HATA KWA KUTUMA TUU KWENYE NAMBA YA SIMU HUKU NI DODGER MZURI IBADANI,WAPENZI HII NI AJABU SANA. NILIENDA KANISA FULANI NIKAKUTA WALE WENYE AJIRA RASMI WAKO EXEMPTED KUJA IBADA ZA MID-WEEK DAYS, AKU😕 NANI KASEMA?? MIMI NI MTUMISHI WA
SERIKALI, ILA SIJAWAHI PATA SABABU YA KUHALALISHA KUKOSA IBADA YOYOTE, WEWE UNAYEFANYA FANYA OVERTIME ILI UPATE KALE KAELFU 40 USISINGIZIE KAZI WALA SERIKALI, NI WEWE ULIPOFANYA OPPORTUNITY COST YA IBADA NA ILE POSHO YA OVERTIME, .MUNGU ALIZIDIWA KETE.

NI NANI MTU YULE AMBAYE BAADA YA KUINULIWA ATABAKI NA QUALITIES ZAKE(LADHA/HARUFU)?  .MWAKA 2006 NILITEMBELEA IRINGA NIKAKUTANA NA JAJI MMOJA (LATE JUDGE UZIAH) WA MAHAKAMA YA RUFAA, ANAHUDHURIA IBADA ZOTE ZA MID WEEK DAYS, HADI MIKESHA YA VIJANA ANAKUJA ILI APATE MUDA WA KUTOSHA NA MUNGU TENA STYLE YAKE YA KUOMBA ILIKUWA ANALALA FLAT KIFULIFULI🚼,HUKU NJE YA KANISA KUNA SHANGINGI🚘ZILE ZA HERUFI MOJA SIJUI J25 NA MAASKARI. SASA HUYU JAJI ALIMENTEINI LADHA NA HARUFU PAMOJA NA KUINULIWA SANA MAANA  KIKWETE ALIMTEUA CHEO FULANI HIVI.

NB
UNAPOACHA LADHA YAKO NA KUBADILI HARUFU KAMA ULIKUWA SILVER OBJECT(CHOMBO CHA FEDHA UNAWEZA KUBADILISHWA UKAWA CLAY OBJECT (CHOMBO CHA UDONGO)  NA KUMBUKA THAMANI NA HESHIMA YA VYOMBO HAIFANANI (2TIM 2:20-21)

*PATA MUDA UTAFAKARI KUHUSU LADHA YAKO UNAKAA NAYO NA JE HARUFU YAKO HAIJABADILIKA?*

UNAYO NAFASI YA KUMLINGANA MUNGU, ILI AREJEZE ILE LADHA NA HARUFU YAKO.

Mwl Proo
0762879363(Whatsapp#)

alltruth5ministries@gmail.com

WEWE BWANA, NDIWE BABA YETU!

*WEWE BWANA, NDIWE BABA YETU!*

_*Mwl Proo*_
0762879363

Amani ya Mungu ipitayo akili zote, iwahifadhi!. Nawasalimu nyote kwa jina kuu la Yesu Kristo, Aliye Baba wa milele....

Mungu anaweza kujifunua kwako kulingana na ulivyo au unavyomjua (Zab 18:25-26). Leo Bwana alinijaza kweli hii, kuwa Yeye ni Baba (Our Abba Father). Nilipokuwa katika maombi ya usiku wa manane, nilitumia dakika tano kutamka sentensi *_"Wewe ni Baba yangu"_*, niliitamka until all my situations were inundated by the Truth, kuwa ninaye Baba. Niliamua kumtaja mpaka nafsi, roho na mwili vyote vijawe na hiyo kweli. Nilimtaja Baba yangu mpaka yale mambo yaliyotendeka hivi karibuni na kunishusha moyo, nayo yaka-salute👋🏾👋🏾. Na ingawa huwa ninakuwa na ratiba, nikimaliza maombi, huwa naanza vita katika ulimwengu wa roho, lakini leo nilipoenda kwa Mungu kama Baba, nilimaliza kuomba sikusikia haja tena, ya kufanya vita vya rohoni, My Papa is greater than all enemies out there (1Yoh 4:4), I just relaxed, nikaendelea kumfurahia Baba yangu.

Katika utamaduni wa kiyahudi, Baba/mababa ni kitu kina-matter mno. Na hivyo watu hutaja mababa as an ID, na kiburi kikuu ni pale wanapogundua kwa jinsi ya mwili wako connected na Ibrahimu na yale maagano (Abrahamic covenant).

Luka 19 : 9
*_............Leo wokovu umefika nyumbani humu, kwa sababu huyu naye ni mwana wa Ibrahimu._*

Mathayo 3 : 9
*_wala msiwaze mioyoni mwenu kwamba, Tunaye baba, ndiye Ibrahimu; kwa maana nawaambia ya kwamba Mungu aweza katika mawe haya kumwinulia Ibrahimu watoto._*

Yohana 8 : 39a
*_Wakajibu, wakamwambia, Baba yetu ndiye Ibrahimu!._*

YAANI WAYAHUDI ILIKUWA NONGWA, KILA UNACHOWAAMBIA, WAO DEFENCE YAO NI MOJA, TUNAYE BABA!! INGAWA HUYO BABA SI WA MILELE, WALA HAWEZI KUWA NAO KILA MAHALI. BILA SHAKA NA WEWE MSOMAJI UNAYE BABA WA KIROHO, HUENDA ANAKUGUSA MNO, KIASI KWAMBA UKIGUSWA TU UNAMTAJA HUYO FASTA, WELL AND GOOD!! HUENDA UNAYE BABA WA KIMWILI, ULIZALIWA KWAKE, KAMA AMBAVYO MIMI NILIKUWA NAYE, PAMOJA NA KUMPENDA NA KUMFURAHIA KAMA AMBAVYO UNAMFURAHIA SASA ULIYE NAYE, HUYO NAYE SI WA MILELE. SIKU NILIPOSIMAMA MBELE YA JENEZA⚰ NIKIMTAZAMA SURA YA BABA MZAZI, NDIPO NIKAJUA KUMBE NILIKUWA NAKUFURAHIA HAPA NYUMBANI, TUNAPIGA STORI ZA BIBLIA, KUMBE UNANIACHA, MAANA NAYE HAKUWA WA MILELE  (KAMA AMBAVYO ULIYE NAYE SI WA MILELE, HATA KAMA HE LOOKS SO YOUNG AND ENERGETIC 👨🏾💪🏾, IPITE MIAKA 20,30 ETC HE WILL GO), HII SIO KUKUTISHIA, BUT I WANT TO MAKE A TRADE-OFF, ILI TUMTAMBUE MWENYE UBABA WA MILELE YESU KRISTO, MUNGU MKUU NA MWOKOZI WETU (Isaya 6:9), AMETAJWA KAMA *_EVERLASTING FATHER_*

*MOYO WA SOMO*

Pamoja na kile kiburi cha Wayahudi, juu ya kuwa wana wa baba yao ibrahimu kwa jinsi ya mwili, nabii Isaya katika roho akatoa ukiri ambao mimi niliposoma, nafsi yangu ilivutwa kwa nguvu. Tusome;

Isaya 63 : 16
*_Maana wewe ndiwe Baba yetu, ijapokuwa Ibrahimu hatujui, wala Israeli hatukiri; wewe, Bwana, ndiwe Baba yetu, mkombozi wetu tangu milele ndilo jina lako._*

Isaya 64 : 8
*_Lakini sasa, Ee Bwana, wewe u baba yetu; sisi tu udongo, nawe u mfinyanzi wetu; sisi sote tu kazi ya mikono yako._*

HUYU NDIYE BABA TUNAWEZA KUJIJENGEA KIBURI KWA ADUI ZETU, MZEE WA SIKU AMBAYE HANA MWISHO WAKE. HATA WAZEE VIKONGWE 👴🏾👵🏿WA MIAKA 100/90 KWA HUYU NAO WANAJIVUNIA KUWA TUNAYE BABA.  ISAYA ANASEMA, KUWA HUYU IBRAHIMU TUNAYEJIVUNIA WALA HATUJUI, WALE YULE BABA WA TAIFA LETU ISRAEL(YAKOBO) HATUKIRI. MUDA ANAANDIKA HAYO ILIKUWA IMEPITA MIAKA 1300 TANGU IBRAHIMU AFE, LAKINI AKAJUA YUKO MUNGU ALIYE BABA, ANAYETUJALI HUYO NDIYE BABA YETU👈🏾.

*MUNGU KWA ROHO MTAKATIFU AMETUFANYA WANA (WE ARE ADOPTED AS SONS)*

Warumi 8 : 15
*_Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba._*

USIKUBALI KUISHI, NA MUNGU AKIWA KAMA BABA WA KAMBO KWAKO. HUYU NI BABA...FEEL HIM, UKIENDA KUFANYA MAOMBI UKIITA TU JINA BABA/AV/ABBA, UMHISI NDANI YAKO KABISA, UKIIMBA WIMBO WA KUABUDI AU KUSIFU, UKITAMKA BABA, MOYO WAKO UCHOMWE💘 NA FURAHA YA BWANA, KWAMBA UNAYE BABA. INFACT NIMESOMA MAFUNDISHO YA DINI ZOTE KUU ZA DUNIA ZILE 19, IDEOLOGY YA MUNGU KUWA BABA,TUNAIPATA HUKU KWETU TU; YAANI HAKUNA MUNGU ALIYE BABA ILA HUYU YEHOVAH BWANA ALIYEJIFUNUA KWETU KWA YESU KRISTO (YOH 1:18).

🔊 *HUYU BABA YETU, MACHO YAKE HAYATULII, YANAKIMBIA KIMBIA, ILI KUTULINDA* 👁👁
2 Mambo ya Nyakati 16 : 9a
*_Kwa maana macho ya Bwana hukimbia-kimbia duniani mwote, ili ajionyeshe mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake._*

Zekaria 4 : 10
*_naam, hizi saba ndizo macho ya Bwana; yapiga mbio huko na huko duniani mwote._*

AS THE MATTER OF FACT, MUNGU NI ROHO, YUKO KILA MAHALI (OMNIPRESENT GOD), LAKINI AMEAMUA KUTUMIA LUGHA YA KIBINADAMU (ANTHROPOMETAPHORIC LANGUAGE), ILI KUTIA MKAZO WA KAZI YAKE KAMA BABA. HUTASAHAULIKA HATA UTUPWE KIJIJINI, HUTAFICHIKA EVEN IN THE DEAD OF THE NIGHT. YEYE NI BABA, USIWE NA HOFU ✋🏾

🔊 *KWA NAMNA ILE-ILE BABA ANAYOMBEBA MTOTO MIKONONI, PIA MUNGU HUTUBEBA, MAANA YEYE NDIYE BABA YETU*

Kumbukumbu la Torati 1 : 31
*_na huko jangwani, ulipoona alivyokuchukua Bwana, Mungu wako, kama mtu amchukuavyo mwanawe, njia yote mliyoiendea, hata mkafikilia mahali hapa._*

BABA, HUYU AKIONA NJIA UIENDEAYO IKO ROUGH, IKO CROOKED, IMEJAA VALLEYS AND HILLS, ANAKUCHUKUA MIKONONI KWA NAMNA ILE-ILE AMBAYO BABA ANAKANYANYUA KATOTO KAKE👶🏽, ATATEMBEA YEYE ILI WEWE UEE SALAMA.

🔊 *BABA YETU, ANATUBEBEA MIZIGO, KILA SIKU, ILI TUSIWE OVERWHELMED*

Zaburi 68 : 19
*_Na ahimidiwe Bwana, Siku kwa siku hutuchukulia mzigo wetu; Mungu ndiye wokovu wetu._*

KUNA WATU, UNAKUTANA NAO, WAMEOKOKA, ILA WAKO HOI KIMAISHA NA KILA ANGEL YA MAISHA, MAANA MIZIGO YAO WAMEIBEBA WENYEWE, INAWALEMEA, LAKINI HUYA BABA ANASEMA, NJOONI KWANGU NINYI WENYE KULEMEWA....ANAZUNGUMZIA AINA ZOTE ZA MIZIGO, UMTWIKE YEYE ALIYE BABA, TENA YUKO BIZE MNO, AKIJISHUGHULISHA NA MAMBO YETU (1PET 5:7).

UKIISHA KUSOMA HUU UJUMBE, PATA DAKIKA HATA 10, JIFUNGIE UTANGAZIE MAZINGIRA YAKO YOTE NA HALI ZAKO ZOTE, KUWA UNAYE BABA. YAAMBIE MAGONJWA KUWA NINAYE BABA AITWAYE JEHOVAH RAHA (KUT 15:26), KIAMBIE KIFO, KUWA UNAYE BABA ANAITWA MKUU WA UZIMA NAAM YEYE NDIYE UFUFUO NA UZIMA (Mdo 3:15),
ZUNGUMZA NA HUZUNI, KUWA UNAYE BABA, ANAITWA MUNGU WA FARAJA YOTE (2KOR 1:3-11), ZUNGUMZA NA UMASKINI, KUWA UNAYE BABA, ANAITWA MCHUNGAJI MWEMA, HUTAPUNGUKIWA!

ANZA LEO KUMFURAHIA MUNGU, PEKEE ALIYE BABA. TEMBEA NJIANI UKIIMBA KUHUSU BABA YAKO HUYU, UKIMJUA HUYU UNARUHUSIWA KUJIVUNA (YER 9:24, 1KOR 1:31). YAANI HAPA WARINGISHIE MAADUI, NA MATAIFA WOTE, KUWA UNAYE BABA!!!! YAANI NIKIMTAMKA MUNGU NI BABA NAONA SURA YANGU INATENGENEZA SMILE 😊,NINASHUSHA PUMZI YA KUHISI RAHA 😉.

Lyrics By Don Moen 🎤🎼🎹🎸

*_I have known the Father's Cares for me. He's been goodX2,Through it all He is always there for me, God's been good to me.Through the storm, through the night,come what may, everything will be alright..._*

MUNGU BABA WABARIKI..

Mwl Proo
(Prosper Kadewele)
0762879363(ATG whatsapp group)

alltruth5ministries@gmail.com

MAOMBI NA HUDUMU; NI MUHIMU SANA!

🇦 🇱 🇱     🇹 🇷 🇺 🇹 🇭

*_Mwl Proo_*
0762879363 (calls/texts)

*MAOMBI NA HUDUMA NI MUHIMU SANA*

Once again,Bwana Yesu asifiwe sana wapendwa.

Kuna jambo la kutusaidia sana nililojifunza ktk maandiko. Kuwa *_maombi na huduma ni muhimu sana_*

TUJIFUNZE UFUNUO TOKA KWA MFALME SULEMANI

*1 Wafalme 2 : 35*

Kisha mfalme akamweka Benaya, mwana wa Yehoyada, *mahali pake juu ya jeshi;* na Sadoki, *kuhani,* mfalme akamweka mahali pa Abiathari.

Ameen,Sasa wapendwa mara baada ya Sulemani kushika hatamu,anatufundisha taasisi mbili nyeti kwenye *UFALME*(Maisha ya kiroho) . Naamini yeye kama mfalme kulikuwa na taasisi nyingi angeweza kushughulika nazo kwanza.Ila alipoingia tu aliondoa wale ambao hawafai tena kwa maana walishachakachua yaani Kamanda hatari Yoabu na kuhani Abiathari wa zama za babaye Daudi,kisha aka-replace akamweka Benaya bin Yehoyada ktk nafasi ya Jeshi ile ya Yoabu *(HII NI NAFASI INAYOWAKILISHA ULINZI KTK MAISHA YA KIFALME NA INAWAKILISHA MAOMBI KTK MAISHA YA KIROHO YA MWANA WA MUNGU)* Wako wanaosema ukiisha kuokoka hauhitaji kumbe kuomba ulinzi "they are right in saying", ila pia wanapaswa kuelewa how things operate in the spiritual realm. Wote mnaweza kuwa mmeokoka lakini msiwe na nguvu sawa,msiwe na idadi ya sawa ya majeshi yanayopigana upande wa kila mmoja,wote mkasema _"kwa jina la Yesu"_ isiwe na *effect/impact* sawa kwenu nyote. Watu walio kwenye *PRACTICAL MINISTRY* wanaelewa moja kwa moja,kunaweza kuwa na ngome au kifungo au jini au nguvu za giza/uchawi zimetaabisha weee,na watu wengine waliookoka wamesumbuka navyo kuvikamea au kuviharibu bila mafanikio,Lakini akaja tena mtumishi mwingine huenda hata asiombe ila kule kukaribia eneo la tukio kile kitu kikang'oka na kutoweka,Ukweli ni kwamba nguvu inayotenda kazi ndani yake ni kubwa(Efes 3:20) unaweza kuta kiasi cha majeshi ya Mungu yanayofanya kazi upande wake ni mengi kulingana na alivyoji-position ktk ufalme. Kumbuka habari ya Gehazi na Elisha bin Shafat,Gehazi ambaye ni mtumishi wa Nabii mwenye double portion anointing yeye pia alikuwa ni mwamini(kwa sasa ningemwita tena mlokole) lakini alipofunguliwa macho ya rohoni👁👁akaona majeshi yale hayajawazunguka wote ila yamemzunguka Elisha

*2 Wafalme 6 : 17*

*_Elisha akaomba, akasema, Ee Bwana, nakusihi, mfumbue macho yake, apate kuona. Bwana akamfumbua macho yule mtumishi; naye akaona; na tazama, kile kilima kilikuwa kimejaa farasi na magari ya moto yaliyomzunguka Elisha pande zote._*

Mungu ameahidi kuwafanya watumishi wake kuwa miali ya moto (Ebrania 1:7) Lakini kiasi cha zile blimestones of fire 🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥🔥 zinazomzingira mtumishi haziwi sawa kwa wote itategemea ameji-position vipi ktk ufalme. NA UKWELI WA WAZI MAADUI ZETU WOTE KTK ROHO WANAZIFAHAMU TOFAUTI HIZI ZA NGUVU,KWA MARA YA KWANZA YESU KUFANYA HUDUMA KTK SINAGOGI NA WATU HAWAKUSHUHUDIA KAMWE MAPEPO KUWALIPUKA WATU JUST BY A SPEECH OF SERMON,LAKINI SHETANI ANTAMBUA KWA HARAKA SANA NANI MWENYE NGUVU(MARKO 1:24ff) Pepo wakapiga kelele katikati ya speech ya Yesu, *"tuna nini nawe?"*(what do you want with us?)👹👉🏾😭🔥(this is an utterace of surrendering),Kajifunze ngoma nzito iliyoletwa kwa wanafunzi ikagoma kwa Yesu ikayeyuka fasta (Mathayo 17:19,21) Nenda kajifunze pia kwa wana wa Skewa (Mdo 19:14-16) Pepo liliwajibu vyema *Yesu tunamjua,Paulo tunamfahamu,lakini ninyi ni akina nani?*
Wapendwa ngoja nimalizie habari za Sulemani ili tuendelee vyema na utamu. Sulemani akaifanya imara taasisi ya pili ya ukuhani,kwa kuwa Abiathari alichakachua then mfalme ak-replace nafasi hiyo kwa kumweka Sadoki(NAFASI HII KTK MAISHA YA KIROHO INAWAKILISHA HUDUMA ZA KIROHO ZA NAMNA ZOTE). Hivyo mfalme Sulemani kabla ya vyote aliona (ULINZI NA UKUHANI YAANI MAOMBI NA HUDUMA NI NUMBER ONE MISSION)

Sasa sisi tuliozaliwa upya(tuliookoka) tunayosifa ya kifalme(wafalme) na tunapaswa kuwa na ufahamu huo,tumepewa/tumeupokea ufalme,tumefanywa wafalme,tunapaswa kujifunza yote kwa sura ya kifalme

TUSOME MAANDIKO

*Waebrania 12 : 28*

*Basi kwa kuwa tunapokea ufalme usioweza kutetemeshwa, na mwe na neema, ambayo kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na unyenyekevu na kicho.*

*Luka 17 : 21*

*wala hawatasema, Tazama, upo huku, au, kule, kwa maana, tazama, ufalme wa Mungu umo ndani yenu.*

*Ufunuo 5 : 10*

*ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi.*

*1 Petro 2 : 9*

*Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu.*

Luka 12 : 32 - *Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme.*

SASA NAZUNGUNZA NA NINYI WAFALME KTK UFALME WENU ULINZI NA UKUHANI(MAOMBI NA HUDUMA) NI MUHIMU SANA. HUU NI WITO KWA KILA MWANA WA MUNGU,KAMWE USIJARIBU KUACHA MAOMBI NA HUDUMA KWANI HII NI *KANUNI YA UFALME* Kabla sijaendelea nimetamani kunukuu kauli ya Bishop Deo Lubala aliyoitoa kwenye mkesha wa AFLEWO 8/7/2016 kuwa *UFALME WA MUNGU UPO KWA NAMNA MBILI(TWO ASPECTS) 1.PERSONAL OF JESUS 2.PRINCIPLES OF THE KINGDOM,AKASEMA HILO LA KWANZA(YAANI KUWA NA YESU)  LITAKUHAKIKISHIA KUWA NA YESU MILELE, NA HILI LA PILI (KANUNI ZA UFALME) LINAKUSUDIA KUKUPA MAISHA YA USHINDI NA BARAKA HAPAA DUNIANI. Sasa humo ktk kundi la pili ndipo kuna utoaji,maombi,huduma etc etc

NIMEFURAHISHWA NA HIYO HOJA MAANA HIKI NINACHOTAJA LEO NI MIONGONI MWA KANUNI ZA UFALME

HAKUNA CHEO WALA MAJUKUMU DUNIANI YANAYOWEZA KUKU-EXEMPT ETI USIOMBE,MAOMBI HAYANA SUBSTITUTE(MBADALA) MAOMBI NI LAZIMA UOMBE, *HUWEZI KUOMBA KAMA HUOMBI* UKITOA PESA NYINGI KUSAPOTI MIKUTANO YA INJILI UNA HERI NA THAWABU LAKINI KAMWE SIO COMPENSATION YA MAOMBI,BADO KWA KANUNI ZA UFALME UNAPASWA KUWA NA BENAYA BIN YEHOYADA(MAOMBI) KTK UFALME WAKO. KUNA WATU KWA SABABU YA BIASHARA ZAO HAWAJITOI NAFSI ZAO KUFANYA HUDUMA ILA WANATUMA TU ZAKA NA KUTOA SAPOTI NYINGINE KANISANI,SASA MWANA WA MUNGU SADAKA ILI ILETE *SENSE* UNAPASWA KUJITOA WEWE KABLA YA PESA ZAKO, YAANI YOU NEVER FAST, YOU NEVER ATTEND OVERNIGHT PRAYER,   UTAKUWA MANYAMA UZEMBE WA KIROHO (spiritually flabby),SADAKA YAKO ITAFUNGUA MLANGO FULANI WA BARAKA,LAKINI HAITAONGEZA MUSCLES 💪🏾💪🏾👊🏾NA KUNOA ZILE SILAHA ZAKO ZA VITA VYA ROHONI 🔫💣⚔🗡🛡NA HAPO NDIPO TUNAPOKUKUTA MENEJA MLOKOLE SEKRETARI WAKO KAPANDISHA PEPO👹 UNAPIGA SIMU KWA PASTA📞☎,AJE AKEMEE. MIMI NI MTUMISHI WA SERIKALI SIO MCHUNGAJI,LAKINI KTK TAASISI NILIYOPO IWE WAFANYAKAZI AU WALE TUNAWAHUDUMIA WAKIPATA SHIDA ZA KIROHO KAMA KULOGWA AU MAPEPO ,TUNAYASHUGHULIKIA NA KUMALIZA KESI,MAANA KANUNI ZA UFALME ZINAZINGATIWA.

SASA WAPENDWA WANGU NAWAAMSHA KWA KUWAKUMBUSHA *_"MAOMBI NA NA HUDUMA NI MUHIMU SANA"_*

MIONGONI MWA FAIDA KUBWA YA KUDUMU KTK MAOMBI NA HUDUMA NI KUTOKUWA NA MAISHA YA KIROHO YENYE ZIGZAG⚡⚡NA KUWA MBALI NA MAANGUKO, WALOKOLE WENGI WALIOPOTEZEA MAOMBI NA  HUDUMA WAKAJIKUTA WAKO KWENYE GIZA LA NJE HUKO HADI DHAMBI ZIKAWA ZA KAWAIDA.NA INAPOKUJA SWALI, JE! ALIYEOKOKA ANAWEZA KULOGEKA (JIBU JEPESI,HAWEZI) ILA UKWELI NI KWAMBA  MLOKOLE ASIYEZINGATIA KANUNI ZA UFALME(HASA KUDUMU KTK MAOMBI NA HUDUMA) IKIJA ATTACK AMBAYO NI KUBWA UNAWEZA KUMZOA (USIISHIE KUNUKUU KUWA UHAI WAKO UMEFICHWA......Kolosai 3:3) HAKIKISHA UNAFANYA HUDUMA YOYOTE,UKISHINDWA KUHUBIRI,FUNDISHA,IMBA KWAYA(HATA KAMA NI MENEJA WA BENKI) ,SHUHUDIA MITAANI KUHUSU YESU,PIGA VYOMBO VYA MUZIKI KANISANI  NA HUDUMA ZOTE ZA KIROHO (HAA YOTE ILI KUJIDHILI,NA KUUTAWALA MUDA WAKO KIFALME,DUNIA ISIKUMEZE)

OMBI:
Katika jina la Yesu,Bwana akuondolee roho ya uzito,uvikwe wepesi, naam vazi la sifa
Ameeen

MBARIKIWE KWA JINA LA YESU

Mwl Proo

0762879363(whatsapp)

alltruth5ministries@gmail.com

HALI YENU YA KWANZA!

🇦 🇱 🇱     🇹 🇷 🇺 🇹 🇭
*HALI YENU YA KWANZA*

*_Na Mwl Proo_*
0762879363
0718922662

BWANA YESU ASIFIWE SANA.

Somo hili halilengi kuwarudisha watu nyuma, Infact ni mimi ndiye nimefundisha somo lisemalo, *_Kwenda mbele moja kwa moja_* siku chache zilizopita. Lakini nilipata pia ufunuo juu ya hali za watu za mwanzo na za sasa ktk kupokea imani.

*Ufunuo 3:3*

Ufunuo wa Yohana 3 : 3 -  *_"Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu......"_*

Kuna hali ulikuwa nayo ulipoamini ndiyo hiyo Bwana anataka kusema nasi na anaidai.

Bila shaka kila mmoja wenu akijiangalia hali yake ya sasa, "in the first pace" atatoa hitimisho kuwa *"nimeongezeka sana ktk maarifa ya kiroho na kumjua Mungu"* sasa Bwana analo neno kwako,kuwa maarifa hayo mengi kama yangeambatana na ile hali yako ya kwanza ulipoamini "ungekuwa/utakuwa heri/bora sana".

*Ezekieli 36 : 11*

_Nami nitaongeza juu yenu mwanadamu na mnyama, nao watazidi na kuzaa; nami nitawakalisha watu ndani yenu, kwa kadiri ya *HALI YENU YA KWANZA*, nami nitawatendea mema kuliko mema ya mianzo yenu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana._

*KITU KTK HALI YAKE YA KWANZA(UPYA)*
Wapenzi hivi mnakumbuka namna kitu kikiwa ktk hali yake ya kwanza(upya)?
Kuna wakati nakumbuka nilinunua viatu fulani vipya vizuri sanaaa,na kwa sababu ya hali yake ya kwanza,nakumbuka niliviweka kabatini juu ya nguo zilizonyooshwa/pigwa pasi.Sasa ni viatu hivyo hivyo ambavyo muda ulifika hata mvunguni mwa kitanda havikustahili,kuna wakati nilikuwa navivulia kwenye ua wa nje na kuvificha kwenye maua kuepusha _bad smell_ ndani.
Je! unakumbuka upekee uliokuwa kwenye vazi jipya au suti yako ambayo ktk upya wake(hali ya kwanza) uliipeleke kwenye special laundry company ili ifanyiwe dry cleaning,na hata ukiisafisha nyumbani hauichanganyi na mavazi mengine. Je! unakumbuka gari jipya la hapo kwenu mlipolipa heshima ya kuliosha kila siku kwa maji safi,likiwa ktk hali yake ya kwanza,Je baada ya kuwa limechoka limepondeka kwa kugongwa mara nyingi,vipi ratiba ya kuliosha huko parking. Kumbuka vitu vyote ktk hali yake ya kwanza(upya).

INGAWA NI KWELI MTU ANALOENDELEA KUDUMU KTK WOKOVU ANAENDELEA KUTAKASWA NA KUFANYWA BORA,LAKINI IKO HALI YA KWANZA AMBAYO BWANA ACHUNGUZAYE MIOYO ANAIJUA NA ANAIDAI.

KIBIBLIA UPENDO WA KWANZA(UPENDO WA WAKATI WA UPOSO)  NI MKUBWA ZAIDI YA ULE WA BADAE,LAKINI MUNGU ANAUTAKA ULE UPENDO WA KWANZA WA WAKATI WA UPOSO NDIO UWE WA "LIFETIME"

*Yeremia 2 : 2*

Enenda ukalie masikioni mwa Yerusalemu, ukisema, *_Bwana asema hivi, Nakukumbuka, hisani ya ujana wako, upendo wa wakati wa uposo wako;_* Jinsi ulivyonifuata huko jangwani, katika nchi isiyopandwa mbegu.

*Ufunuo 2*

4 Lakini nina neno juu yako, *ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza.*
5 Basi, kumbuka ni wapi ulikoanguka; ukatubu, ukayafanye *matendo ya kwanza.* Lakini, usipofanya hivyo, naja kwako, nami nitakiondoa kinara chako katika mahali pake, usipotubu.

MUNGU ULE UPENDO WA KWANZA ANAUITA UPENDO WA WAKATI WA UPOSO,BILA SHAKA WANANDOA NA WALIOWAHI KUWA KTK UHUSIANO WA UCHUMBA BAADA YA UPOSO,UPENDO UNAFIKIA JUU KABISA,NDIPO WATU WANAKUWA KAMA WAMERUKWA NA AKILI HAWASIKII TENA,MNAKUMBUKA NYAKATI HIZO NA NAMNA AMBAVYO HATA MESEJI KUTOKA KWA PARTINER WAKO 📱💌📲UNAIONA YA MAANA SANA, UNAWEZA KUIONA MESEJI,UKAIWEKELEZA ILI UKATAFUTE POZI LA KUISOMA VIZURI UKIWA CHUMBANI🙈, ILA HUO UPENDO KUNA MUDA UNASHUKA,NA HALI YA KWANZA IKIISHA UNAWEZA JIBU MESEJI HATA HUJAISOMA MPAKA MWISHO NA UNAJIBU SHORTCUT TENA KWA HATA KWA KUTUMIA EMOJI (🙅🏽=NO) (😏=RACCA)

SASA MUNGU NAYE ANAUKUMBUKA UPENDO ULE ULIKUWA NAO ULIPOAMINI,KILE KICHO CHA BWANA,KULE KUUTIMIZA WOKOVU WAKO KWA HOFU NA KUTETEMEKA.
NILIKAA NA MCHUNGAJI FULANI WA EAGT(PSTR CHISSORO) AKATUSHUHUDIA KUHUSU MIKESHA WALIYOIFANYA MIAKA YA EARLY 1970's ,ALISEMA KWA WAKATI HUO MIKESHA KTK MAKANISA YA PENTEKOSTE ILIKUWA SIKU YA JUMAMOSI SIO IJUMAA KAMA NYAKATI HIZI,LAKINI WALIKESHA TOKA SAA MBILI USIKU MPAKA SAA MOJA ASUBUHI MWISHO,PIA WALIRUDI MAKWAO NA KUJA TENA IBADANI BAADA YA SAA CHACHE. TENA IKUMBUKWE CONTENT YA MKESHA WAO ULIKUWA NI MAOMBI YALE YA KIPENTEKOSTE YENYE UVUVIO MZITO WA ROHO 😪🙌🏽 ACHA HIZI *"DRY LANDS"*  ZETU ZA UNAOMBA HUKU UNACHUNGULIA MESEJI ZA WHATSAPP KIDOGO. SASA NAJARIBU KUIFIKIRIA HALI HII YA KWANZA,JINSI WALIVYOPOKEA,MAANA MIAKA MICHACHE IMEPITA NILIHUDHURIA MKESHA KANISA FULANI LA KISASA,NILIKUTA CONTENTS ZA MKESHA NI STAREHE FULANI,KULIKUWA NA MUDA MWINGI WA PERFORMANCES KAMA YOUTH DANCE TEAM,GUEST SINGERS WENGI MNO,PAMOJA NA KWAMBA MKESHA ULIANZA SAA NNE LAKINI SAA SABA NI BREAK TIME YA KUPATA ☕🍹🌮🌭🍞,MAOMBI NI YA KUBIPU "BEEP" ,NA KUNA MAHALI PENGINE NILIKUTA ILIKUWA TOO MUCH. MAANA HAPO KULIKUWA NA RATIBA NDANI YA MKESHA,KUANZIA SAA TISA NI MUDA WA KUANGALIA NIGERIAN MOVIE 📺📼,MAANA NGUVU NI CHACHE ZA KUOMBA (MITHALI 24:10) KWA NINI NIMETOA SHUHUDA HII??

*Yeremia 6 : 16*

*Bwana asema hivi, Simameni katika njia kuu, mkaone, mkaulize habari za MAPITO YA ZAMANI, I wapi njia iliyo njema? Mkaende katika njia hiyo, nanyi mtajipatia raha katika nafsi zenu. Lakini walisema, Hatutaki kwenda katika njia hiyo.*
*Ayubu 8 : 8*
Basi, uwaulize, tafadhali, vizazi vya zamani, Ujitie kuyaangalia yale baba zao waliyoyatafuta;

YAKO MAPITO YA ZAMANI AMBAYO BWANA ANAKUTAKA UYATAZAME,UNAJUA KUNA WAKATI ILIKUWA HATA WACHUMBA WAKITAKA KUONANA WANAENDA KUKUTANIA KANISANI,NA ZAMA HIZO MTU AKITAJWA AMEANGUKA KWENYE ZINAA,ILIKUWA KILIO NA KUSAGA MENO,NA WATU WALIJISALIMISHA WENYEWE,SASA ZAMA HIZI NI NYAKATI ZA HATARI,WACHUMBA WAKISHATANGAZA TUU,WAKO "OUTING" KILA WIKIENDI,WANAJIANGUSHA KWENYE UASHERATINI/UZINZI WEE KWA KIGEZO CHA "SHETANI ALIJIINUA"
SO WENGI WANAKAUSHA😷 MNAKUJA KUJUA BADAE,BAADA YA WEDDING💍💍MIEZI MITANO SITA BINTI KAJIFUNGUA WALA SIO "PREMATURE BIRTH" 
NI MUHIMU UKUE HATA UFIKIE KIMO CHA CHEO CHA UTIMILIFU KRISTO,LAKINI HUPASWI KUIACHA HALI YA KWANZA,ILE HALI AMBAYO MUDA WOTE ULIJIKUMBUSHA MOYONI KUWA "YESU ANARUDI TENA,SAA NISIYODHANI" IKAKUPA BIDII YA KUMZALIA BWANA MATUNDA. ILE HALI YA KWANZA YA MSIMAMO WA "NITENDEJE UOVU HUU NIMKOSE MUNGU"(Mwanzo 39:9) ILE HALI YA MWANZO YA KUTEGA ALARM CLOCK ⏰KUAMKA KUOMBA, ILE HALI YA KWANZA AMBAPO ULIKUWA UKIKAA WIKI NZIMA BILA KUFUNGA UNAJIHISI MDHAMBI 😰🙏🏾UNATUBU KWA KUGAAGAA CHINI CHUMBANI,YALE MAOMBI YA KUJIMIMINA MOYO KWA BWANA,SIO UCHANGA (1SAM 1:15) SAIV SI UNAFANYA MAOMBI YA KISOMI👔🎓👠,UNAOMBA HUKU UNAREKEBISHA TIE AU GAUNI LIKAE FRESH😀,NILIHUDHURIA IBADA FULANI HUKO KAWE,MUDA WORSHIP INAENDELEA NILIMUONA DADA MMOJA KAKAA 💺ALIFUNGUA POCHI NA KUTOA KITU KAMA KOPO LA LOTION AKAJIONGEZEA USONI,NILISHTUKA KIDOGO KUONA HILO(NDIO MAANA KUFUMBA MACHO KUNA FAIDA YAKE),TATIZO NI KWAMBA HALI YA KWANZA IKIONDOKA UNASAHAU MAMBO YA KUWA UPO MBELE ZA MUNGU (2SAM 6:21)

VIPI MPENDWA DO YOU STILL FEEL HIM(GOD) MOVING YOUR HEART KAMA MWANZO?

TUYAPITIE MAANDIKO YAFUATAYO

*Ezekieli 16 : 55*

Na maumbu yako, Sodoma na binti zake, watairudia hali yao ya kwanza, na Samaria na binti zake watairudia *hali yao ya kwanza,* na wewe na binti zako mtairudia *hali yenu ya kwanza.*

*Ezekieli 38 : 8*
Na baada ya siku nyingi utajiliwa; katika miaka ya mwisho, utaingia nchi iliyorudishiwa *hali yake ya kwanza,* baada ya kupigwa kwa upanga, iliyokusanywa toka kabila nyingi za watu, juu ya milima ya Israeli, iliyokuwa ukiwa wa daima; lakini imetolewa katika kabila za watu, nao watakaa salama salimini wote pia.

UNAPOGUNDUA HALI YA ZAMANI ILIKUWA NJEMA BASI KATA SHAURI NA AMUA KUYATENDA AU KUYAFUATA MATENDO YA KWANZA

Hosea 2 : 7 - Naye atawafuata wapenzi wake, lakini hatawapata; atawatafuta, lakini hatawaona; ndipo atakaposema, Nitakwenda nikamrudie mume wangu wa kwanza; kwa maana *hali yangu ya zamani ilikuwa njema kuliko hali yangu ya sasa.*

*Yeremia 33 : 11*
itasikilikana tena sauti ya furaha na sauti ya shangwe, sauti ya bwana arusi na sauti ya bibi arusi, sauti yao wasemao Mshukuruni Bwana wa majeshi, maana Bwana ni mwema, rehema zake ni za milele; na sauti zao waletao sadaka za shukrani nyumbani kwa Bwana. Kwa kuwa nitawarudisha wafungwa wa nchi hii *kama kwanza,* asema Bwana

*Yeremia 33 : 7*
Nami nitawarudisha wafungwa wa Yuda, na wafungwa wa Israeli, na kuwajenga *kama kwanza.*

*BWANA YUKO RADHI AKUFANYE TENA KWA KADRI YA HALI YAKO YA KWANZAA NA KUKUREJEZEA UPENDO WAKO WA WAKATI WA UPOSO(ULIPOAMINI)*

OMBI

Maombolezo 5 : 21 - Ee Bwana, utugeuze kwako, nasi tutageuka; *Zifanye mpya siku zetu kama siku za kale.*

Asante kwa kufuatilia, na Mungu wa mbinguni akuwezeshe ktk nia ya moyo wako, ya kumkaribia zaidi.

Mwl Proo
0762879363(whatsapp only)

alltruth5ministries@gmail.com

WALA HAKISHIKI KICHWA!

🇦 🇱 🇱     🇹 🇷 🇺 🇹 🇭

*WALA HAKISHIKI KICHWA*

*_Na Mwl Proo_*
0762879363

©2015

Shalom Aleichem!🙋🏽
Wapendwa ktk Bwana(Yesu Kristo) naomba niwashirikishe Neno la Uzima.

*Wakolosai 2 : 19 -*

*_wala hakishiki KICHWA, ambacho kwa yeye mwili wote ukiruzukiwa na kuungamanishwa kwa viungo na mishipa, hukua kwa maongeo yatokayo kwa Mungu._*

Yesu Kristo anatajwa pahala pengi ktk maandiko kama/kuwa ni  *KICHWA*

Angalia haya maandiko

*Waefeso 1 : 22 -*

*_akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe KICHWA juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo.._*

*Wakolosai 2 : 10*

*_Na ninyi mmetimilika katika yeye aliye KICHWA cha enzi yote na mamlaka._*

*Waefeso 4 : 15*

*_Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye KICHWA, Kristo._*

*Wakolosai 1 : 18*

*_Naye ndiye KICHWA cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote._*

*Waefeso 5 : 23*

*_Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni KICHWA cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili._*

NGOJA NIANDIKE KWA HERUFI KUBWA(Galatia 6:11)

MAANDIKO YAMETUTAJA SISI KUWA NI VIUNGO,SASA KWA SAYANSI YA KIMBINGU SHARTI KILA KIUNGO KIKISHIKE KICHWA,KIWE KIMEUNGAMANISHWA NA KICHWA ILI KIENDELEE KURUZUKIWA, KUUNGAMANISHWA NA VIUNGO ILI KIENDELEE KUKUA KWA MAONGEO YATOKAYO KWA MUNGU.

*Waefeso 2 : 21*

*_Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana._*

*Waefeso 4 : 16*

*_Katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadiri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo._*

*TURUDI KTK SAYANSI YA VIUMBE  YA DUNIANI*

Wale ambao mnakumbuka Biology kwa sehemu kuhusu *"BODY COORDINATION"* mtakumbuka vizuri swala Central Nervous System. Viungo vyote vinaweza kufanya vinavyofanya kama tu vimeungamanishwa na *KICHWA* . Ikitokea umemchoma mtu kwa sindano💉au kitu chochote chenye ncha kali,iwe umemchoma mguuni au mkononi au mtu akigusishwa moto ✋🏼🔥,Atashtuka na kutoa mkono au mguu kwa haraka sana. Sasa ukweli ni kwamba mkono hautaweza kutambua maumivu ya sindano wala muunguzo wa moto kama hakutakuwa na kushikama na *_KICHWA_* ,kisayansi ukimchoma mtu na kitu kama sindano,uko ujumbe/taarifa(Nerve impulse/message) inayotumwa very fast kwenda kwenye *KICHWA*(ubongo) ambapo huku KUTATAFSIRI HILO TUKIO NA HAYO MAUMIVU THE UJUMBE UNARUDISHWA KUWA UMECHOMWA NA SINDANO. NDIPO MTU ANAHISI CHA KUHISI NA ANAWEZA AKAUVUTA MKONO KWA HARAKA SANA. INGAWA UNAONA KINACHOTANGULIA KUONDOLEWA NI MKONO LAKINI TAARIFA YA KUCHOMWA💉NA AGIZO LA KUUONDOA MKONO LILITOKA KWENYE *KICHWA*

BAADHI YA TECHNIQUES ZA KITABIBU KTK UPASUAJI,NAMNA YA KUMFANYA HUYU   ANAYEFANYIWA UPASUAJI ASISIKIE MAUMIVU NI KU-DISTURB ILE NERVOUS SYSTEM ILI KICHWA(UBONGO) KISITAFSIRI MATUKIO YANAYOENDELEA,IWE NI SINDANO ZA KUTIA GANZI AU DAWA ZA UZINGIZI OR ANY ALCOHOLIC RECIPE ITAKAYOFANYA MUDA WA TUKIO MTU ASIWEZE KU-SENSE,LA SIVYO THEATRE KUNGEKUWA NA VILIO VYENYE KELELE KUU *(KAMA KUNA MAPUNGUFU KTK MAELEZO YANGU BASI WALE WENYE TAALUMA ZAO WATAWEKA SAWA,MAANA MIMI NI MTAALUMA WA TAALUMA TOFAUTI KABISA NA SAYANSI)*
LAKINI TUJIFUNZE,WATU WASIPOSHIKAMANA NA KICHWA YESU KRISTO WANAPATA GANZI KTK MIOYO/ROHO,NAFSI NA MIILI YAO NDIPO WANAPOWEZA FANYA KILA UBAYA NA MACHUKIZO YA UOVU

*Efeso 4:19*

*_19 ambao wakiisha kufa ganzi wanajitia katika mambo ya ufisadi wapate kufanyiza kila namna ya uchafu kwa kutamani._*

MTAFUTE MTU ALIYEPOOZA MKONO AU MGUU(PARALYSIS)  AMBAYE AMEPOOZA HASA,MWAMBIE  INUA MKONO HUU ULIPOOZA,ANA KUTA MAAMUZI ANAYAFANYA KICHWANI KWAMBA AUINUE LAKINI MKONO HAUJAUNGAMANISHWA,MPAKA ANAWEZA AKATUMIE MKONO MWINGINE KUUSAIDIE HUU *_USIO KISHIKA KICHWA_* UWEZE KUINUKA

NDUGU MPENDWA NENO LA BWANA NI HILI

UNAPASWA UBAKI UMEUNGANA NA KRISTO *_"(FULL CONNECTED)"_* NA YEYE ALIYE KICHWA,UPOOZA WA KIROHO UNAOFANYA UNA MEZWA NA DUNIA,NA KUUONA WOKOVU NI MZITO,NI KIASHIRIA CHA WAZI KUWA *"HUKISHIKI KICHWA"* TAWI LIKIKATWA TOKA SHINANI, HALIWEZI KUJIHUDUMIA LENYEWE HATA LIKAZAA🍊🍒🍎🍓, UWEZO WA KUPANGA MCHAKATO NA BINTI HADI AKAJA GHETO MKA-DUU 🙊🙊 UNADHANI ULIKUWA MCHAKATO MWEPESI?? AMINI NAKUAMBIA NI KAZI NGUMU KULIKO KUMTUMBUA RAISI WA NCHI MWENYE KINGA ZA KISHERIA,ILA ULIWEZA KUSIMAMIA STEP BY STEP HILO DILI BILA KUSIKIA KALE KAONYO KA NDANI YA DHAMIRI NA KILE KIDOLE CHA ROHO 👉🏾😾KILICHOKUWA KINAKU PIN-POINT NAFSINI,NI KWAMBA ULIKUFA GANZI(EFESO 4:19)  AMBALO NI TOKEO LA KUACHA KUKISHIKA KICHWA. JE WEWE AMBAE HAPO MWANZO, WEWE KINYWA CHAKO KILIJAA MANENO YA NEEMA KILA SAA HALELUYA,AMEN,UBARIKIWE LEO HII MISEMO YOTE YA KIDUNIA NDIYO IMEKUJAZA MOYO(LUKA 6:45),WEWE AMBAYE ULIPOKUWA UKIONA PICHA ZINAZOONESHA MAPAJA YA WADADA KWENYE GOSSIP MAGAZINES🗞📰ULITAMANI KUFUMBA MACHO🙈 LEO HII SMART PHONE YAKO📱📲 UMEIJAZA PORN VIDEOS NA NUDE PHOTOS KIBAO👙,WEWE AMBAYE ULIPOPIGA GOTI KUOMBA🛐🚼 TU ULISIKIA ATMOSPHERE NA NAFSI YAKO IMEKUWA *_INUNDATED_* NA UMANDE WA ROHO MTAKATIFU,SASA UNAISHI KWA SALA ZA KUOMBEA CHAKULA,WEWE ULIYEKUWA MFUATILIAJI WA VIPINDI TBN NA SASA UNAHISI VIPINDI VYA KWENYE TV ZA KIKRISTO VINABOA FULANI HIVI,WEWE AMBAE ULIJIKINGA NA MAMBO MACHAFU LAKINI KWA SASA UNA-LIKE KILA UKURASA WA FB WENYE MAMBO MACHAFU,UME-SUBSCRIBE KWENYE WEBSITES KADHAA ZENYE MAMBO YASIYOFAA,ULIOWA-FOLLOW INSTAGRAM NI CELEBRITES WENYE KUPOST PICHA ZA UTUPU WAO NA UDAKU UDAKU,KALE KAUWEPO KALIKUWA KAKIKUSHUKIA MUDA UNAOMBA KALISHAGA POTEAGA 5YEARS AGO,ILA UMEPOTEZEA TUU,UMEAMUA KUISHI BILA HAKIKA YA KUWA NA MUNGU,WEWE AMBAYE DHAMBI NA UDHAIFU MWINGINE ULISHA USHINDAGA ZAMANI,UMEUFUFUA TENA YAANI UMEYAJENGA ULIYOYABOMOA (GALATIA 2:18),ETI ULIPOOKOKA MKAKA ULISHAACHAGA KUJICHUA(MASTURBATION) HALAFU SAIV UMEIZINDUA HIYO TABIA HUKU UNAFANYA *"RECONSIDETATION"* NI DHAMBI AU SIO DHAMBI,UNACONCLUDE MWENYEWE, *"ITAKUWA SIO DHAMBI"* 😂😂,NI KWELI ULIANGUKA KWENYE UZINZI,ILA HAUPO TAYARI KUTUBU MAANA UNA-ORGANIZE DILI JINGINE LA KUDUU TENA,SO UNAPANGA RATIBA KUWA UTATUBU BAADA YA HIYO *_one more shot_*AS IF MUNGU NI ADMIN WA GRUPU LA WHATSAPP,KWAMBA AKIKULEFTISHA ATAKUADD TENA🌍

SASA SWALI NI HILI

*_"JE! BADO UNAKISHIKA KICHWA???_*

JE UNAWEZA KUJIJARIBU NA KUJITHIBITISHA KAMA BADO UMEKISHIKA KICHWA???? *2Korintho 13:5*

HEY BRETHREN,IT IS NEITHER TOO LATE NOR IMPOSSIBLE TO RECONNECT YOURSELF WITH THE HEAD,THERE IS ACCEPTANCE FOR YOU AT THE TABLE OF THE LORD,HIS MERCY IS GREATER THAN YOUR SIN.

*BAMBELELA KUJESU UZOTHOLA UTHANDO*
*UYABIZWA SONDELA UZOSINDISWA*😰 nimeongea kizulu kuonesha msisitizo, come back bhana

Mwl Proo
0762879363(whatsapp number)

alltruth5ministries@gmail.com

KWENDA MBELE MOJA KWA MOJA!

🇦 🇱 🇱     🇹 🇷 🇺 🇹 🇭

*KWENDA MBELE MOJA KWA MOJA*

_Na Mwl Proo_
*0762879363*

Ezekiel 46
9.".....hatarudi kwa njia ya lango aliloingia kwalo, lakini atatoka kwa *kwenda mbele moja kwa moja.*"

NDUGU MPENDWA KTK BWANA,HAKUNA KITU KINA DISTURB POSITION YAKO KIROHO KAMA KUREJEA NYUMA BAADA YA KUIFAHAMU ILE KWELI NA KUOKOLEWA.

*KUREJEA NYUMA NI KUMKASIRISHA BWANA* 😡😡😡

Ezekiel 8:17

17 Basi, akaniambia, Umeyaona haya, Ee mwanadamu? *Je! Ni jambo dogo sana kwa nyumba ya Yuda, wayafanye machukizo wanayoyafanya hapa?* Kwa maana wameijaza nchi hii udhalimu, *_tena wamerejea nyuma ili kunikasirisha;_* na, tazama, wanaliweka tawi puani.

NDUGU WAPENZI WATU WENGI KWA KUTOJUA KANUNI ZA UFALME NA TARATIBU ZINAZOUONGOZA ULIMWENGU WA ROHO,WANADHANI NI NENO DOGO KUREJEA NYUMA WAKIWA TAYARI KWENYE NANGA YENYE SALAMA(EBRANIA 6:19) NA WAMEJAZWA MAARIFA YOTE YA MUNGU.

UKWELI NI KWAMBA ULIPOOKOKA ULIHAMISHWA KISHERIA TOKA KWENYE UFALME ULIOKUWA UKIKUMILIKI KWANZA(KISHERIA) KWA SABABU YA DHAMBI. UKAHAMISHWA NA KUFANYWA *KINGDOM CARRIER* YA UFALME HUU WA MUNGU. MAPENZI YA MUNGU KWAKO NI KWAMBA USIRUDI NYUMA TENA,BALI UWE NA MWENDO WA *KWENDA MBELE MOJA KWA MOJA* .

NILIKUWA NIKISOMA KITABU CHA RUTHU NIKAFUNDISHWA KITU

Ruth 1:20-21

21 *_Mimi nalitoka hali nimejaa, naye BWANA amenirudisha sina kitu, kwani kuniita Naomi, ikiwa BWANA ameshuhudia juu yangu, na Mwenyezi Mungu amenitesa?_*
22 *_Basi Naomi akarudi; pamoja na Ruthu Mmoabi, mkwewe; ambao walirudi kutoka nchi ya Moabu; nao wakafika Bethlehemu mwanzo wa mavuno ya shayiri._*

👆🏼👆🏼👆🏼👆🏼👆🏼NENO LA BWANA KTK MISTARI HIYO NI KWAMBA *"KAMA UKIRUDI NYUMA,THEN UKARUDI TENA,HAUWI SAWA KTK YOTE YALE YAHUSUYO POSITION KTK UFALME,KUNA KITU KINA-MISS* HUO NDIO UKWELI,NITAUELEZEA MBELE KIDOGO.

SASA TURUDI KTK KITABU, FAMILIA YA ELIMELEKI NA MRS WAKE NAOMI WALIONDOKA BETHLEHEMU(the city of bread🍞) BETHLEHEMU INA ASHIRIA NDANI YA WOKOVU,HALI NZURI YA KIROHO,UHUSIANO MZURI NA BWANA MUNGU(KUWA NDANI YA MILKI YA MUNGU) ...... LAKINI WATU HAWA WALIONDOKA BETHLEHEMU WAKAENDA KUKAA NCHI YA MOABU(UMOABUNI KUNAASHIRIA KUTOKA KTK HEMAYA YA MILKI YA MUNGU,KUACHA WOKOVU NAAM KUREJEA NYUMA) .
MIONGONI MWA ATHARI UNAZOZIPATA KWA WAKATI UKIWA UMEREJEA NYUMA NI PAMOJA NA KUPOTEZA VITU VYA THAMANI KTK MAISHA,IKIWEMO FURSA AMBAZO ZILIPANGWA KWA AJILI YAKO,MUNGU HATA KAMA ALIKUPANGIA BARAKA ZA NAMNA FULANI ANAZIHAIRISHA MCHANA KWEUPE.....

*Yeremia 18:9-10*

*_9 Na wakati wo wote nitakapotoa habari za taifa, na habari za ufalme, kuujenga na kuupanda,_*
*_10 ikiwa watatenda maovu mbele za macho yangu, wasiitii sauti yangu, basi nitaghairi, nisitende mema yale niliyoazimia kuwatendea._*

NAOMI ANASEMA ALIONDOKA AMEJAA NEEMA AMEREJEZWA HANA KITU,AKIWA UMOABUNI(NJE YA WOKOVU) ALIPOTEZA MUME NA WATOTO WAKE WAWILI👬 . NI MUHIMU UKUMBUKE MUNGU HAWATEMBELEI WATU HUKO UMOABUNI,NDIO MAANA WAKIWA HUKO ALISIKIA KUWA MUNGU AMEWATEMBELEA/AMEWAKUMBUKA  WATU WAKE HUKO BETHLEHEMU NA KUWAPA CHAKULA,KUMBUKA PIA KUWA UKOSEFU WA CHAKULA BETHLEHEMU ILIKUWA SABABU YA WAO KUTOKA HUKO BETHLEHEMU. SHORTFALLS(MAPUNGUFU) ULIYONAYO NA UHITAJI USIKUONDOE BETHLEHEMU UKAENDA UMOABUNI,HUKU BETHLEHEMU AT ANY TIME "T" BWANA ANATUKUMBUKA (Ruth 1:6)

HOLD ON! SIJASEMA UKIREJEA NYUMA UTAKAPORUDI HUTAPOKELEWA, UTAPOKELEWA TENA KWA SHEREHE KABISA😊,ILA LEO NGOJA NIKUTAZAMISHE UFUNUO WA MWANA MPOTEVU(PRODIGAL SON)
MWANA MPOTEVU ALIPOZINGATIA MOYONI MWAKE(HE CAME BACK TO HIS SENSE) AKARUDI HOME KWA BABA,ALIPOKELEWA KWA KUFANYIWA KARAMU MPAKA NDAMA ALIYENONA ALIANGUSHWA🔪🐄,BUT I ASSURE YOU THE PRODIGAL SON WAS NO BETTER THAN THE BROTHER AT HOME,KWANI UKIREJEA NYUMA UNAKUWA KTK UFU⚰☠
*Luka 15:32*
*_32 Tena, kufanya furaha na shangwe ilipasa, kwa kuwa huyu ndugu yako alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana_*

Mwl Proo

WEWE AMBAYE UNADUMU UMESIMAMA(1KOR 10:12) WEWE AMBAYE UMEBAKI KWA BABA(ALWAYS WITH GOD) THAMANI YAKO KWA BABA(MUNGU) SIO KARAMU YA MAPOKEZI BALI VYOTE VILIVYO VYA MILKI YA BABA YAKO,NI VYAKO 👆🏼👈🏾👇🏽👉🏾

*Luka 15:25-31*

25 Basi, yule mwanawe mkubwa alikuwako shamba *(alikuwa busy na huduma ktk ufalme wa Mungu)* na alipokuwa akija na kuikaribia nyumba, alisikia sauti ya nyimbo na machezo.
26 Akaita mtumishi mmoja, akamwuliza, Mambo haya, maana yake nini?
27 Akamwambia, Ndugu yako amekuja, na baba yako amemchinja ndama aliyenona, *kwa sababu amempata tena, yu mzima.*(Unaweza rudi nyuma ukapotea kabisa,au unarudi umekatwa mkia🐄,utaruhusiwa kuingia zizini)
28 Akakasirika, akakataa kuingia ndani. Basi babaye alitoka nje, akamsihi.
29 Akamjibu baba yake, akasema, Tazama, mimi nimekutumikia miaka mingapi hii(anadumu ktk wokovu), wala sijakosa amri yako wakati wo wote (ukamilifu&uaminifu kwa Mungu), lakini hujanipa mimi mwana-mbuzi, nifanye furaha na rafiki zangu;
30 lakini, alipokuja huyu mwana wako aliyekula vitu vyako pamoja na makahaba, umemchinjia yeye ndama aliyenona.
*_31 Akamwambia, Mwanangu, wewe u pamoja nami sikuzote, na vyote nilivyo navyo ni vyako._*

👆🏼👆🏼👆🏼😋😋😋😋😋😋

NDUGU MPENDWA USIDIRIKI KUTENDA DHAMBI KWA KUSUDI(EBRA 10:26) WALE KAMWE USIWE NA RECORD YA KURUDI NYUMA (EBRA 6:4-6)

*NI BORA KUFA KULIKO KURUDI NYUMA*

*Yeremia 22:10,2:19*

10 Msimlilie aliyekufa, wala msimwombolezee(ambaye bado hajaitwa ktk neema hii ya ajabu),Bali mlilieni huyo aendaye zake mbali *(aliyerejea nyuma)* ;Kwa maana yeye hatarudi tena,Wala hataiona nchi aliyozaliwa.

"........ *ujue, basi, ukaone, ya kuwa ni jambo baya sana na uchungu, kuwa umemwacha BWANA, Mungu wako, na ya kuwa moyoni mwako hamna kunihofu*, asema Bwana, BWANA wa majeshi."
KITU KIMOJA AMBACHO WENGI HAWAELEWI ATHARI ZA KUREJEA NYUMA ZINAPINDUA MAMBO AMBAYO YANASIMAMIWA NA PRINCIPLES ZA ULIMWENGU WA ROHO,KWA MFANO HIVI UNAJUA NINI KINATOKEA KWA MALAIKA AMBAO/AMBAYE WAKO/YUKO IN CHARGE KWAKO?(Ebrania 1:14,Zabur 34:7) JE UNAJUA KUWA KUNA MALAIKA WA NURU AMBAO WAKO IN CHARGE KWA WATEULE NA WANAKUWA CAPTIVATED NA MAJESHI YA GIZA KWA SABABU YA WEWE KUTOKUWA KWENYE POSITION?

NDUGU YANGU INAWEZEKANA KABISA KUISHI MAISHA YA SAFATI YA WOKOVU KWA *_KWENDA MBELE MOJA KWA MOJA_*

Ktk Jina la Yesu pokea neema ya kutofia jangwani na uwezesho wa kwenda mbele moja kwa moja.

Mwl Proo
0762879363(whatsapp#)

alltruth5ministries@gmail.com

*_#teamantibackslidecombat#_*