*DALILI ZA ROHO NA ZA NGUVU*
🇲 🇼 🇱 🇵 🇷 🇴 🇴
0762879363
Jina la Bwana libarikiwe. Karibu tena katika mfululizo wa kujifunza kweli yote.
Neno la Bwana leo linasimama katika
1 Wakorintho 2 : 4
*_Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu,_*
Haleluya, leo nasukumwa moyoni kushughulikia mapokeo yasiyofaa,yanayotaka kulifanya kanisa la Kristo kusalia kama dini na hata ile injili ya kweli.
Paulo mtume anawaandikia wakristo waliopo Korintho,kuwa ile injili aliyoihubiri kwao haikuwa ya maneno matupu,ili isije imani yao ikajengwa ktk maneno tu tena yenye kushawishi(yametungwa kwa hekima za kibinadamu) yenye *UKAME* bali Neno lake na kuhubiri kwake kuliambatana n dalili za Roho na za nguvu.
Neno la Ufalme kamwe halipaswi kuwa kavu lisilodhihirisha nguvu za Roho (Demonstration of Spirit's power). Mifumo ya dini inakawaida ya kubadili mtaala(Curriculum) wa Roho wa kweli na kuingiza ule wa kibinadamu. Mwaka 787 AD kule kwenye baraza la Nikea walipitisha mambo mengi yaloyozidi kuufanya Ukristo uwe ni dini tuu isiyo na dalili za Roho na za nguvu. Hilo ndilo baraza lilibariki sanamu za kanisani,liturujia,vipaimara vikaingizwa,kubatiza watoto wachanga na kitabu maalum cha sala(prayer book). Sasa watu waliopaswa kuomba ktk Roho Mtakatifu(Yuda 1:20) wanaletewa mfumo wa dini unaokinzana na mapenzi ya Roho. Mwishowe inabaki kuwa dini tuu,hata kutoa mapepo wachafu tu(ambalo ni jambo la kufanywa na watoto wa Sunday school ya watoto/Au waongofu wapya) hakukuwahi kushuhudiwa kabisa. Na hata sasa mifumo ya makanisa inarejeza hali ileile.Ishara,ajabu na miujiza iliyopaswa kuambatana na Neno,imeenda likizo kwa sababu kuu mbili, 1. Jinsi watu walivyopokea mapokeo yasiyo sahihi(ili ishara zitendeke basi analetwa mhubiri mgeni/au unakuta mtu akijishughulisha n hizo dalili za Roho na za nguvu anahisiwa kutumiwa na roho zidanganyazo)
2.Watu hawan uzoefu wa ujuzi wa kutenda kazi hizo kwa sababu nao wanaiopokea injili kame (Wengi hutumia maelezo kuwa Yohana Mbatizaji haijanukuliwa kama alifanya miujiza.
Mimi pamoja na juhudi ya kuifundisha kweli ya Mungu kama wito wangu ulivyo bado nikiacha kuyafundisha haya nitakuwa na *_imbalanced gospel_* maana hatusomi injili ya hivyo ktk maandiko.
TWENDE KTK MAANDIKO
1.AGIZO/NENO LA BWANA LINAAMBATANA NA ISHARA ZA KUTHIBITISHA
SAMWELI ALIPOMWAMBIA NENO LA MUNGU SAULI,ILIPASWA ISHARA IAMBATANE NALO
1 Samweli 9 : 27
*_Hata walipokuwa wakishuka mwisho wa mji, Samweli akamwambia Sauli, Mwambie mtumishi atangulie, (naye akatangulia), bali wewe simama hapa sasa, ili nikuambie neno la Mungu._*
👇🏽👇🏽👇🏽
Ishara iliyoambata na Neno
1Samwel 10
*_1 Ndipo Samweli akatwaa kichupa cha mafuta, akayamimina kichwani pake, akambusu, akasema, Je! BWANA hakukutia mafuta [uwe mkuu juu ya watu wake Israeli? Nawe utamiliki watu wa BWANA, na kuwaokoa na mikono ya adui zao; kisha hii itakuwa ishara kwako ya kuwa BWANA amekutia mafuta] uwe mkuu juu ya urithi wake._*
*_2 Utakapoondoka kwangu leo, utakutana na wanaume wawili karibu na kaburi la Raheli, katika mpaka wa Benyamini huko Selsa; nao watakuambia, Punda hao uliokwenda kuwatafuta wameonekana; na tazama, baba yako ameacha kufikiri habari za punda, anafikiri habari zenu, akisema, Nifanye nini kwa ajili ya mwanangu?_*
MUSA ALIPOPOKEA AGIZO,KULIPASWA KUWA NA ISHARA KUWA KWELI AMETUMWA NA MUNGU
KUTOKA 4
1 Musa akajibu akasema, Lakini, tazama, hawataniamini, wala hawataisikia sauti yangu; maana watasema, BWANA hakukutokea.
2 BWANA akamwambia, Ni nini hiyo uliyo nayo mkononi mwako? Akasema, Ni fimbo.
3 Akamwambia, Itupe chini; akaitupa chini, nayo ikawa nyoka; Musa akakimbia mbele yake.
5 ili kwamba wapate kusadiki ya kwamba BWANA, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amekutokea.
6 BWANA akamwambia tena, Sasa tia mkono wako kifuani mwako. Akautia mkono wake kifuani mwake; naye alipoutoa, kumbe! Mkono wake ulikuwa una ukoma, umekuwa mweupe kama theluji.
7 Akasema, Tia mkono wako kifuani mwako tena. Akautia mkono wake kifuani mwake tena, na alipoutoa kifuani mwake, kumbe! Umerudia hali ya mwili wake.
9 Kisha itakuwa wasipoamini hata ishara hizo mbili, wala kuisikiliza sauti yako, basi, yatwae maji ya mtoni uyamwage juu ya nchi kavu, na yale maji uyatwaayo mtoni yatakuwa damu juu ya nchi kavu.
SASA TUNAANZAJE KUIHUBIRI INJILI AU NENO LA MUNGU BILA UDHIHIRISHO WA NGUVU ZAKE KTK HILO NENO? MAANA UFALME HAUPO KTK NENO BALI NGUVU
1 Wakorintho 4 : 20 - *_Maana ufalme wa Mungu hauwi katika neno, bali katika nguvu._*
MITUME WALIENDA KUHUBIRI ILA NENO LIKIHUBIRIWA KWA USAHIHI LAZIMA ISHARA ZITALIFUATA ILI KULITHIBITISHA
Marko 16 : 20
*_Nao wale wakatoka, wakahubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithibitisha lile neno kwa ishara zilizofuatana nalo._*
KWA UPANDE WANGU SIKUBALIANI NA SWALA ZA KUHUBIRI NENO PASIPO ISHARA YOYOTE(ISAYA 7:11) INGAWA KWENYE SWALA LA UDHIHIRISHO WA NGUVU SHETANI BAADA YA KUONA WANA WA NURU HAWANA UJUZI/EXPERIENCE YA KUTOSHA,NAYE ANAPATUMIA HAPO HAPO KULETA ILE YA ULAGHAI (COUNTERFEIT) LAKINI HIZO ZA UONGO HAZIFANYI SISI TUACHE AU TUOGOPE,BECAUSE THAT WILL DO MORE HARM THAN GOOD(NA WAKRISTO AMBAO HAWAKUZOEZWA KUONA NA KUPOKEA MIUJIZA YAO,NDIO WAMEKOSA MSIMAMO WA IMANI(1kor 2:5) ,KILA WAKIONA TANGAZO LA MTUME NA NABII KWENYE TV 📺JUMAPILI WANAHAMIA HUKO,KWA HIYO WENGINE KWA MWAKA MMOJA AMEKUWA MSHIRIKA KTK HUDUMA NA MAKANISA ZAIDI YA 10 ,KOSA SIO LAO NI WALE WALIOMLEA HAWAKUMJENGA KTK MSINGI,PIA MTU AMEKAA NA VIFUNGO VYAKE HASHUHUDIWI AKIHUDUMIWA MAANA WAHUDUMU WA MADHABAHU WAOGA,AU WALIPOKEA INJILI ISIYO NA DALILI ZA ROHO NA ZA NGUVU. NI KWELI WAKO WENYE KARAMA ZA MIUJIZA NA KUPONYA
1Kor 12
*_9 mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja;_*
*_10 na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha;_*
1 Wakorintho 12 : 28 *_Na Mungu ameweka wengine katika Kanisa, wa kwanza mitume, wa pili manabii, wa tatu waalimu, kisha miujiza, kisha karama za kuponya wagonjwa, na masaidiano, na maongozi, na aina za lugha._*
KATIKA SOMO LANGU LA KARAMA NA HUDUMA NA HUDMA ZA ROHONI NITATOFAUTISHA ANAYEPONYA KWA KARAMA YA KUPONYA INKUWAJE NA ILE NYINGINE,MAANA ILI MAGONJWA YAPONE ILI ISHARA ZITENDEKE SIO LAZIMA UWE NA KARAMA HIZO, IKO AMBAYO NI GENERAL KWA WAAMINI WOTE,KILA ALIYEAMINI KTK YESU ANAPASWA KUZITENDA,UKIWA MTAANI ,OFISINI UKIKUTA WENYE HAJA YA KUPONYWA WEKA MKONO L✋🏼KWA JINA LA YESU WATAGUSWA NA KUPONYWA,MUDA WATU WAMESUKWASUKWA NA PEPO WACHAFU TUMIA HUO MWANYA KUMDHIHIRISHA YESU WAKO, HIYO HAIHITAJI *_GO AHEAD_* TOKA KWA PASTOR,YAANI KAMA WAAMINI WOTE WANGEJUA HAYA ULIMWENGU UNGEPINDUKA
Marko 16 : 17
*_Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;_*
MUNGU AKISEMA ATAPONYA,NENO LAKE HALIANGUKI CHINI (2Falme 10:10)
Isaya 55 : 11
*_ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma._*
KANUNI ILIYOPO NI ULIHUBIRI NENO LA INJILI YA KWELI THEN UTENDE ISHARA,AJABU NA MIUJIZA. KUACHA KUFANYA HIVYO KUNAWAPA SHAVU WAHUNI WACHACHE WA KIBONGO WALE *FAKE* KUJIPATIA UMAARUFU ULIOMSTAHILI YESU.
WAPENDWA NAOMBA KUWAJULISHA KUWA KILICHOKOSEKANA KWENU SIO MAOMBI,MAANA MAOMBI HAYO YA KUFUNGA MPAKA WILI TATU NA MIKESHA MINGI YA MAOMBI MLIYONAYO NI MIKUBWA NA MENGI MNO UKILINGANISHA NA NGUVU INAYOHITAJIKA ILI ISHARA,MIUJIZA NA AJABU ZITENDEKE,MMEKOSA TU UJUZI(AMBAPO INAWAFANYA KUWA WAOGA) NA ILE SHIDA YA MAPOKEO/TRADITIONS YASIYO SAHIHI. NIMEENDA KUHUDUMU MAHALI,WATU WAPO SAFI KTK NENO ILA HAWANA UZOEFU WA KUTENDA KAZI(MIUJIZA NA UPONYAJI) WALIPOSHUHUDIA NAHUDUMIA KUPONYA WAGONJWA NA KUWAULIZA PAPO(INSTANT HEALING) NA WAKAKIRI KUPONA KABISA,WENGINE NDIO WAKAAMINI SIKU HIYO KUWA OOH KUMBE YESU ANAPONYA HATA SASA,WENGINE NI CHURCH ELDERS WAMETAMANI UPONYAJI WA YESU JUU YAO KITAMBO LAKINI HAYA MADINI YETU YAMEFICHA UFUNGUO WA MAARIFA (LUKA 11:52) ,SASA WENGINE WAKAANZA KUNIITA PRIVATE KUWA MIMI NINA HILI MTUMISHI,NA MIMI NINA HILI NIOMBEE,SASA MIFUMO YA DINI IMEWANYIMA WATOTO WA MUNGU CHAKULA CHAO CHA KUPOKEA MIUJIA NA UPONYAJI,NA WAKITHUBUTU KUFUATA MAHALI PENYE UJUZI WANAWATENGA NA MASINAGOGI.
INGAWA WATU WAKIAMINI TU BILA ISHARA WANA HERI YAO(YOH 4:48,20:29) LAKINI MSIKUBALI KUWA NA IBADA KAME,ZISIZO NA DALILI ZA ROHO NA NGUVU,ILI WANAOSHAMBULIWA NA ADUI WAKIJA NYUMBANI WA BWANA VIFUNGO VYA MAGONJWA AU KULOGWA,AU MATESO YA NAMNA ZOTE YAFUNGULIWE. NA NENO LA MUNGU LIKIHUBIRIWA KWA USAHIHI NA WAHUDUMU WAKIWA NA UJUZI HUO WA MATENDO YA MIUJIZA NA UPONYAJI BASI WAYATENDE HAYO
MAANA HII NI FORMULAR
1.PREACHING
2.PERFORMING MIRACLES
MATHAYO 4:17,23
Mathayo 4 : 17
*_Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia._*
Mathayo 4 : 23
*_Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya ugonjwa na udhaifu wa kila namna katika watu._*
MTANISAMEHE KWA KUWA NIPO KINYUME NA MIFUMO YA DINI,HATA MAKANISA YETU YA KIPENTEKOSTE MENGI YAMEGEUKA KUWA YA DINI TUU,WATU WANAINGIA NA VIFUNGO VYAO NA MAGONJWA YAO NA KUONDOKA NAYO *_NO HEALING&MIRACLE MINISTRATION AT ALL_* NDIO MAANA WAJANJA WANAAMUA KUJA NA GEAR YA MIUJIZA NA KUFANYA UVUVI HARAMU WA KUVUA SAMAKI KWENYE MAKAPU YA WENGINE. WENGI WALIOANZA HUDMA ZAO KWA MSINGI WA MIUJIZA NA UPONYAJI HAWAJAENDA KUFANYA HTA CRUSADE AWAPATE MATAIFA,AMEWAVUA WASHIRIKA KWENYE MAKANISA YA KIPENTEKOSTE HAYO HAYO YALIYO YALIYOFUKIA NA KUZIZIKA DALILI ZA ROHO NA ZA NGUVU
ANZA SASA, BADILISHA MFUMO, EWE MHUDUMU TAFUTA UJUZI MAANA NGUVU/UWEPO WA BWANA UPO KTK IBADA ILI APATE KUPONYA (LUKA 5:17). LAKINI CHANEL/TRANSMITTER INAKOSEKANA . WAKO AMBAO BWANA ATAKUJULISHA ANATAKA KUWAPONYA NA WENGINE UKIWAONA WANA SHIDA UNAPASWA KUZIRUHUSU NGUVU ZIWAHUDUMIE. ACHA MAZOEA NA UANZE KUTEMBEA KTK UJUZI WA ROHO,KUNA MAHALI NILIENDA KUHUDUMU KWA PRAISE AND WORSHIP NILIPO MALIZA KUHUDUMIA SIFA NIKAULIZA WALIOINGIA WAGONJWA WAINUE MIKONO JUU NA WAANZE KUJICHEKI AFYA ZAO WANASIKIAJE MIILI YAO, WENGINE WAKABAKI KUSEMA MBONA HAJAOMBEA,TAYARI KATIKA KUIMBA WATU WALIKUWA WAMEPONYWA NA BWANA NAMI NILISHALIHISI HILO KATIKA ROHO, NDIO MAANA NIKAITISHA SHUHUDA.
MUNGU AWABARIKI KWA KUELEWA
Mwl Proo
0762879363(whatsapp only)
alltruth5ministries@gmail.com