*KUHUSU YUSUFU ARIMATHAYA*
By Mwl Proo
©2017
Mtu huyu mwenyeji wa Arimathaya, ametajwa katika injili zote nne. Math 27:57, Mark 15:43, Luka 23:51, Yoh 19:38. Habari zake hazijaelezwa sana katika Biblia, maana Biblia haikueleza kila kitu. Kumbuka hili, theologically; *_The Bible does not contain all things, but it contains all things necessary for salvation._* Hivyo habari za ziada kuhusu mambo mengine, ziko katika vitabu vingine, kwa mfano stories kumhusu Yusufu huyu ziko zaidi katika kitabu cha matendo ya Pilato (Acts of Pilate) na Injili ya Nikodemu. Yaani habari zote zipo katika Apocryphal+Non-canonical references. Huyu ndiye aliye-donate sehemu ya kuzikwa Bwana, inaelezwa na wanahistoria wa karne ya tatu, kuwa alifia Glastonbury, United Kingdom. Mjadala mzito wa kithiolojia ni juu ya swala moja, Je yeye ndiye aliyeifikisha injili Uingereza, wako wanaodai kuna mitume waliahajenga kanisa kabla yake.
Katika injili ya Nikodemu, imeeleza mgogoro wake na Nikodemu. Ingawa Nikodemu alimsaidia kuuomba mwili wa Bwana kwa Pilato, lakini alipoenda kuuzika kwenye makaburi yake kukawa na mzozo. Yusufu alijitahidi kutafuta suluhu na Nikodemu, lakini mgogoro ukawafikia wazee wa kiyahudi, ambao walimkamata na kumtupa gerezani huyu Yusufu. Alifungwa gerezani wakalitia makufuli kibao๐๐๐๐๐๐ pande zote nne za gereza wakalilinda salama. Walipomtia gerezani alikwiasha waambia kuwa Yesu mliyemuua, atanitoa, na mabaya yenu yatawarudia. Walipoamka asubuhi kwenda gerezani, walilikuta limefungwa vizuri lakini Yusufu hakuwepo. Wakapata taarifa yuko kitaa huko Arimathaya. Wakatuma barua✉ ya kuomba radhi, wakimtaka waende awaeleze alitokaje?? Wazee wa kiyahudi walienda wakiwemo makuhani Caiphas na Annas. Akawasimulia kuwa akiwa amesimama katikati ya gereza anaomba usiku, kukatakea mwanga๐ฅakaanguka, mtu huyu alimsimamisha.. Na akamwagia maji toka utosini mpaka miguuni, akamwekea harufu ya manukato. Akambusu na kumwambia usiogope, amani iwe kwako. Yusufu akamuuliza wewe ni Eliya Nabii?? Akamwambia fumbua macho, mimi ni Yesu ambaye uliuhifadhi mwili wangu. Yesu akamchukua na kumwonesha mahali pale alipomlaza ⚰, kisha akamtoa gerezani akamsimamisha katikati ya nyumba yake huko Arimathaya akamwonya kwa siku arobaini usitoke huku Arimathaya, akamnyanyua na kumweka kutandani, yaani toka gerezani asubuhi alihamka home kwake ๐ก๐. Walipomwita wale wazee wa kiyahudi mbele ya makuhani, Yusufu alisimulia kila kitu. Akawaeleza kuwa Yesu alimjia kumtoa gerezani, lakini pia akaeleza kuwa Yesu alipofufuka, kuna watu walifufuka pia alieleza kitu chenye kulenga (Math 27:52-53) ingawa hiyo tunajua waliofufuka waliondolewa na kuuingia mji mtakatifu, maana ufufuo wa wakti ule uitwao *ANABIOSKOMAI*, Ulihusisha kuzihamisha roho toka Sheol kwenda Gan Aden, kama nilivyoelekeza katika somo langu la *UMILELE*. Lakini yeye alieleza juu ya waliofufuka wachache na wamendelea kuishi duniani, kipekee aliwataja CHARINUS na LENTHIUS, watoto wa yule SIMEONI wa Luka 2:25-35. Makuhani na wazee wa kiyahudi walifunga safari kwenda Arimathaya ili kuhojiana na watoto wa Simeoni waliofufuka katika ufufuo wa Yesu. And the story is completely interesting aisee...
NB:-
Vitabu kutokuwa katika list ya vile Canonical, haivifanyi kuwa vya uongo, bali katika vile vigezo vinne vya CANONIZATION kili-fail, kama nilivyoeleza katika somo langu la *JINSI YA KUITHIBITISHA BIBLIA KUWA NI YA KWELI*.
Barikiwa sana....
Mwl Proo
0762879363
Mungu akuzidishie neema mtumishi..ubarikiwe sana kwa masomo mazuri
ReplyDelete