Monday, November 20, 2017

MKONO ULIONYOSHWA

*MKONO ULIONYOSHWA(an outstretched arm)* ✋🏼

_By Mwl Proo_
0762879363(whatsapp)

Haleluya Haleluya!
Ziko nguvu za Mungu ambazo zimeambatana na ujumbe huu,unaposoma nguvu ya imani inayoongezwa kwa Neno hili,itaenda kuhusika kufungua🔓 kitu mahali.

Mkono wa Mungu,unaitwa mkono ulionyoshwa. Ni muhimu ujizoeze kujawa na Neno ndani yako ili upate usemi sahihi wa kutumia hasa ktk maombi,maana lugha ya Neno ndio lugha ya maombi,na hiyo inatambulika zaidi ktk ule ulimwengu mwingine wa roho. When you speak God's word back to Himself,When you declare what He declared and decree what He decreed,Unaleta matokeo ya mara moja maana hakuna hata kiumbe kimoja cha rohoni kisichojua kuwa hayo usemayo yaliamriwa na Mungu mkuu aliyeumba vyote,Shetani ktk kutengeneza arguments mbele za Yesu alisema *"maana imeandikwa atakuagizia malaika zake,mikononi mwao watakuchukua usije ukajikwaa mguu wako ktk jiwe"* Shetani alijua kuwa haya ni matamko ya Mwenyenzi Mungu (Zaburi 91:11ff) ndivyo ilivyo kwa viumbe vyote vya rohoni vinajua pia.
Sasa nakutambulisha juu ya Mkono ulionyoshwa

Zaburi 136 : 12
_*Kwa mkono hodari na mkono ulionyoshwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele.*_

MKONO KUNYOSHWA NI ISHARA YA KUWA TAYARI KUSAIDIA,TAYARI KUTETEA,TAYARI KUPIGANIA,TAYARI KUBARIKI,TAYARI KUKUTEGEMEZA,TAYARI KUKUINUA. MKONO WAKE BWANA HAUJAPUNGUA NA HAUJAKUNJWA NI MKONO ULIONYOSHWA.

Mithali 31 : 20 *_Huwakunjulia maskini mikono yake; Naam, huwanyoshea wahitaji mikono yake._*
👆🏼Ingawa andiko linataja sifa za yule mke mwema,nataka tuone kuwa kunyosha mkono ni ishara gani.

NAOMBA JITIE NIA NA MOYO,USOME HAYA MAANDIKO THEN TUENDELEE

Kutoka 6 : 6
_*Basi waambie wana wa Israeli, Mimi ni YEHOVA, nami nitawatoa ninyi mtoke chini ya mizigo ya Wamisri, nami nitawaokoa na utumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyoshwa, na kwa hukumu kubwa;*_

Yeremia 27 : 5
*_Mimi nimeiumba dunia hii, wanadamu na wanyama walio juu ya uso wa nchi, kwa uweza wangu mkuu, na kwa mkono wangu ulionyoshwa; nami nawapa watu kama inipendezavyo._*

Kumbukumbu la Torati 4 : 34 
*_Au Mungu amekwenda wakati gani akajitwalia taifa toka kati ya taifa lingine, kwa majaribu, na kwa ishara, na kwa maajabu, na kwa vita, na kwa mkono hodari, na kwa mkono ulionyoshwa, na kwa maogofya makuu, kama vile Bwana, Mungu wenu, alivyowatendea ninyi katika Misri, mbele ya macho yenu?_*

1 Wafalme 8 : 42  *_(maana watasikia habari za jina lako kuu, na za mkono wako ulio hodari, na za mkono wako ulionyoshwa); atakapokuja na kuomba kuielekea nyumba hii;_*

Ezekieli 20 : 34
_*nami nitawatoa katika mataifa, na kuwakusanya, na kuwatoa katika nchi mlizotawanyika ndani yake, kwa mkono hodari, na kwa mkono ulionyoshwa, na kwa ghadhabu iliyomwagika;*_

AMEN!
MKONO WA MUNGU ULIONYOSHWA NDIO ULIOTENDA AJABU ZOTE ULIZOZISOMA KTK MAANDIKO NA KUSIKIA POPOTE.MKONO HUO HAUJAKUNJWA WALA HAUJAPUNGUKA UMEJAA UTAYARI (READINESS) HATA SASA ILI UKUONEKANIE.

DAKIKA CHACHE KABLA SIJAANDIKA HAYA NILIKUWA NIKISOMA SHUHUDA ZA MWAKA 2014 KTK WEBSITE YA HABARI ISRAEL,NIKAKUTANA NA SHUHUDA NYINGI ZA ASKARI WALIOUONA MKONO WA MUNGU UMENYOOSHWA JUU YA ANGA LA ISRAEL ILI KUWAPIGANIA KWA BIDII

Yeremia 50 : 34  *_Mkombozi wao ni hodari; Bwana wa majeshi ndilo jina lake; yeye atawatetea kwa bidii, apate kuistarehesha nchi, na kuwasumbua wakaao katika Babeli._*

SASA IMERIPOTIWA HUMO KUWA TAKRIBANI MAKOMBORA YA ROCKET/MISSILES(ROCKET BOMBS 3,356 YALIRUSHWA NA HAMAS TERRORISTS HUKO GAZA KUELEKEA MAENEO MUHIMU ISRAEL  IKIWEMO TEL AVIV,ILITAZAMIWA YAUE MAMIA YA WATU KILA YANAPOTUA,LAKINI KATI YA MAKOMBORA 3356 NI MAKOMBORA 578 TUU AMBAYO MAJESHI YA ISRAEL (IDF) YALIFANIKIWA KUYATUNGUA KWA KILE KIZIMISHO KIITWACHO IRON DOME DETERRENT MARA KADHAA BETRI ZA HIVYO VIFAA ZILIFELI,KWA HIYO ASILIMIA 83% YA MAKOMBORA HAYAKUWEZWA KUZUILIWA. ASKARI WA IDF AITWAYE ARIEL SIEGELMAN ALISHUHUDIA KUWA ALIUONA MKONO WA MUNGU(ULE ULIONYOSHWA) UKIYASUKUMIA MAKOMBORA YENYE SPIDI SAWA NA UPEPO BAHARANI💣👉🏾🌊 ANASEMA JINGINE WALISHINDWA KULIZUIA NA LILIELEKEZWA KWENYE AIRPORT YA TEL AVIV🛫🛬ZIKIWA ZIMEBAKI SEKUNDE NNE ILI KOMBORA LILIPUE WATU NA ENEO HILO LA AIRPORT ULITOKEA UPEPO WA MASHARIKI AMBAO UKALISUKUMIA KOMBORA HILO BAHARINI,UNAJUA JAMBO LA AJABU RIPOT INAONESHA MAKOMBORA KARIBIA 2500 AMBAYO MASHINE YAO YA IRON DOME DETERRENT HAIKUWEZA KUYATUNGUA YALIUA WATU WANNE TU,HUKU ASKARI MMOJA AKIWA NA KAKOVU KA KUPANGUSA KWA PAMBA. SASA WAO WANAYO AHADI WANAYOISHIKA

Kumbukumbu la Torati 11 : 12
_*nayo ni nchi itunzwayo na Bwana, Mungu wako; macho ya Bwana Mungu wako, ya juu yake, tangu mwanzo wa mwaka hata mwisho wa mwaka.*_

SASA ISIJE IKAONEKANA NAJADILI SIASA ZA MASHARIKI YA KATI. TWENDE TUENDELEE,MKONO WA MUNGU HATA SASA UMENYOSHWA,KWA NINI TUNAKUWA NA HOFU/SHAKA? USISAHAU KUWA FEARS/DOUBTS ZINA-DEACTIVATE NGUVU YA NENO LA IMANI AMBAPO SASA HUURUDISHA NYUMA MKONO WA UTETEZI WA MUNGU. URUHUSU MKONO WA MUNGU ULIONYOSHWA JUU YA HUDUMA YAKO AMBAYO NI KAMA IMEKOSA *_PROGRESS_* INGAWA UNAYO HAKIKA KUWA MUNGU ALIKUITA,ILA NI KAMA UMESAHAULIKA, NDOA YAKO AMBAYO ADUI SHETANI ALIPATA MWANYA AKAIVURUGA HAIKO *_BEYOND REMEDY_* MUNGU ANAWEZA KUIFANYA MPYA KAMA MWANZO UKIURUHUSU MKONO WA MUNGU ULIONYOSHWA SIKU YA LEO,THAT WORST FAILURE IN ACADEMICS AND THAT DISCONTINUE; INATISHA KWAKO TUU, MUNGU KWAKE HILO NI JAMBO JEPESI SANA.JIZOEZE USIMWENDEE MUNGU NA SLOGANS ZA KICHOVU,MWAMBIE BWANA NIMEWEKEWA CARRY OVER YA COURSES TATU CHUONI,LAKINI JAMBO HILO NI JEPESI MACHONI PAKO.

2 Wafalme 3 : 18
*_Na jambo hili ni jepesi machoni pa Bwana; pia atawatia Wamoabi mikononi mwenu._*

Zekaria 8 : 6
*_Bwana wa majeshi asema hivi, Ingawa hili ni neno lililo gumu mbele ya macho ya mabaki ya watu hawa katika siku hizo, je! Liwe neno gumu mbele ya macho yangu? Asema Bwana wa majeshi._*

MUNGU KWA UPANDE WAKE,ANAJISIKIA UFAHARI MKUU KUKUTETEA  NA NDIO MAANA KWA MKONO WAKE ULIONYOSHWA ANATAKA KUSHUGHULIKIA HUO UGONJWA AMBAO  MADAKTARI BINGWA WA MUHIMBILI WAMEKU-REFER HOSPITALI YA APPOLOS INDIA. KWAO HUO NI UGONJWA UNAOASHIRIA KIFO KINA BISHA HODI MLANGONI. LAKINI KUMBUKA MAUTI IKIWAPANDIENI MADIRISHANI TUNAYE YESU ANAITWA MKUU WA UZIMA

Matendo ya Mitume 3 : 15
_*mkamwua yule Mkuu wa uzima, ambaye Mungu amemfufua katika wafu; na sisi tu mashahidi wake.*_

WALE WATU WALIOONA KIFO KINAWAKABILI KUTOKANA NA CHAKULA CHA SUMU,WAKAMLILIA MTU WA MUNGU KUWA *_mauti imo sufuriani_*🍲🍜 😭😭

2 Wafalme 4 : 40  *_Basi wakawapakulia hao watu ili wale. Ikawa, walipokuwa katika kula chakula, wakapiga kelele, wakasema, Mauti imo sufuriani, Ee mtu wa Mungu. Wala hawakuweza kula._*

LAKINI MAUTI SUFURIANI KWA MKONO WA MUNGU KUPITIA ELISHA BEN'HA SHAFAT ILIKOMESHWA. NDIVYO ITAKAVYOKUWA KWAKO UKIUAMINI MKONO WA BWANA ULIONYOSHWA BELIEVE THIS GOD'S OUTSTRETCHED ARM IS TAKING CARE OF YOUR SITUATION,HE WILL TURN IT AROUND. HE IS DELIGHTED IN THE WELLBEING OD HIS SERVANTS (ZAB 35:27) UKIMWAMINI KWA *_DIMENSION_* HII;ATATENDA KWAKO HIVYO,HE HAS NOT GIVEN UP ON YOU...ULIKUWA UNASUBIRIWA UAMINI TU,NA UURUHUSU MKONO WA MUNGU ULIONYWA JUU YA HALI ZAKO ZOTE

HAPO ULIPO KAMA NAFASI INARUHUSU SIMAMA ANZA KUUELEKEZA MKONO ULIONYOOSHWA KWENYE KILA UNALOLIONA KUWA NI ZITO LINAHITAJI *_DIVINE INTERVENTION_* NA LITASHUGHULIKIWA MARA MOJA,ONDOA MASWALI,WEWE AMINI TUU(MARKO 5:36) I CAN FEEL THAT POWER RIGHT NOW INANYOSHA KILA AMBAPO PALIPARUZWA,KILA BONDE LINAJAZWA SASA,KILA MLIMA NA KILIMA KTK MAISHA YAKO KINASHUSHWA NA KILA KILICHO POTOSHWA KINANYOSHWA  SASA (Luka 3:5) KWA JINA LA YESU RECEIVE THIS PROPHECY NOW,IT IS DONE!!!

AMEN AND AMEN!!!

Mwl Proo
0762879363
0718922662

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment