*KAMA KITU KISICHOKUWA*
*_(Less than nothing)_*
```Mwl Proo```
0762879363(whatsapp)
Bwana Yesu akubariki wewe usomaye (Ufu 1:3). Nakusalimu kwa jina kuu la Bwana na Mwokozi, Yesu Kristo!
Wewe ambaye uko na Mungu, yaani BWANA ni Mungu wako (Zab 144:15), maadui si kitu kwako. Vikao vyote vya kuzimu, vya wachawi, walozi, waganga na maadui wa kimwili wote, kila watakachopanga kitabatilishwa kwa kuwa upo na Mungu. Tusome;
Isaya 8 : 10
*_Fanyeni shauri pamoja, nalo litabatilika; Semeni neno, lakini halitasimama; Kwa maana Mungu yu pamoja nasi._*
Isaya 7 : 7
*_Bwana MUNGU asema hivi, Neno hili halitasimama wala halitakuwa._*
Wakati wowote unapaswa kujua kuwa ~*MAADUI SI KITU, UKIWA NA MUNGU*~, Wanayopanga kwa siri (Consipiracy), ili uuawe, ufe ghafula, ili upunguzwe kazi, ili usimamishiwe mshahara, ili uanguke dhambini, ili mambo yako yaharibike, unabaniwa na kufungiwa mlango wa fursa fulani, na kila aina ya hila; Mungu anasema yatabatilika, hayatakuwa, hilo shauri la maadui, litaanguka.
*```NB:```*
*```MUNGU AKIRUHUSU HILA YA MAADUI KUFANIKIWA, SI KWAMBA AMEKUACHA, DON'T TRY TO DROP OUT, JUST WATCH THE GAME. MUNGU ANAWEZA KURUHUSU HILA YA MAADUI KUFANIKIWA, MFANO KUKUFUKUZISHA KAZI, ILI AJITUKUZE SANA KWAO. YAANI AKIRUHUSU ESEKI KIFUKIWE NA KIFUSI, AU SITNA KIJAZWE KIFUSI NA MAADUI, UJUE ANAANDAA MPANGO KABAMBE WA KUKU-REHOBOTHI (Mwanzo 26:18-22). UMEFANYIWA HILA UKAFUKUZWA KAZI KWENYE KIWANDA CHA KUTENGENEZA VYOMBO VYA PLASTIC πΆ, HALAFU MUNGU ANAKUFUNGULIA MLANGO WA KAZI BOT, PESA ZINAPOZALIWA π·π°π΅π΄πΆπ³π§. ATAWAUMIZA VICHWA, WAONE JINA LAKO KWENYE GAZETI LA THE GUARDIAN, UPO KWENYE LIST YA KUITWA KAZINI BAADA YA USAILI.```*
*MOYO WA SOMO*
Liko andiko ambalo niliposoma katika lugha tofauti, kisha nikarudi kwenye kiswahili, nikagundua, wale wazee wetu walipata shida kuutafsiri huo mstari. Huu hapa....
Isaya 41 : 12 - *_Utawatafuta wala hutawaona wale wapiganao nawe; watakuwa si kitu; watakuwa kama kitu kisichokuwa, wale waliofanya vita juu yako._*
Watakuwa kama kitu kisichokuwa, baadhi ya tafsiri zimeweka, they will be reduced to nothing, nyingine wameandika they will be less than nothing, kijerumani wameweka *Null*, kirusi *Π½ΠΎΠ»Ρ* (Zero,empty/vacuum/of no importance/of no effect). Ok tuachane na tafsiri, cha msingi hapa ni hii kweli ya Mungu, wale wenye wanapanga vita, hila, wanakufanyia uadui....Ukiwa na Mungu tu (condition pekee), watafanywa kuwa kama kitu kisichokuwa. Haijalishi huku nje wanatishaje, Mungu anajua kuwa kwa hali ya kawaida, wanatisha, ndio maana akaahidi kukuokoa na mkono wao wenye kutisha (Yer 15:21). WEWE UNAWAONA WANATISHA, ILA MUNGU KWANZA ANAWAPUNGUZA SIZE.....
Isaya 7 : 4 *_ukamwambie, Angalia, ukatulie; usiogope wala usife moyo, kwa sababu ya mikia hii miwili ya vinga hivi vitokavyo moshi; kwa sababu ya hasira kali ya Resini na Shamu, na mwana wa Remalia._*
ππΌππΌππΌYAANI MAADUI WANA HASIRA π‘π‘, WAMEPAKI SILAHA KALI π£π«π‘π‘⚔. TUNAMWONA RESINI NA PEKA WANAJIANDAA KUIPIGA YERUSALEMU, LAKINI SILAHA ZAO NA HASIRA ZAO, HAZIWI KITU KWA MTU MWENYE MUNGU, MUNGU AKAWAITA HAO MAADUI WAWILI NI MIKIA TU, TENA NI VINGA VILIVYOTOLEWA MOTONI π₯, YAANI VIMEBAKI VINAFUKA MOSHI KAMA UTAMBI, NA UNAWEZA KUUUA MOTO HATA KWA MKONO AU MGUU. KWANZA KABISA KAULI HIYO YA MUNGU, INAKUONDOLEA HOFU.
JIFUNZE KUWAANGALIA MAADUI, KWA NAMNA MUNGU ANAWAONA. KWA MAANA TUNASHINDA KWA KUWA NA MUNGU, SIO KWA NGUVU ZETU NYINGI, MAANA KWA NGUVU HAKUNA ATAKAYE SHINDA (1Sam 2:9a, Zek 4:6).
KIJANA MDOGO AITWAYE DAUDI BIN JESSE. ALIPOSIKIA KWA SIKU 40, YULE MFILISTI ANAMTUKANA 1Sam 17:10) BWANA NA MAJESHI YA ISRAEL, AKASEMA NGOJA NIMTIE ADABU. HUKO GATHI KULIJAA MA-GIANTS KIBAO MASALIA WA MAJITU KAMA WALE WANEFILI, WANA WA ANAKI NA WAREFAI, NA HUYU GOLIATH ALITOKA HUKO, JITU MWENYR UREFU WA MITA TATU(FUTI TISA), CHUMA CHA MKUKI WAKE KILIKUWA KILO SABA, KOFIA YA SHABA KICHWANI MWAKE(HELMET) ILIKUWA NI KILO 57, ZAIDI YA MFUKO WA SIMENTIπ²πΎ. SASA DAUDI ALIONGEA NA HILI JITU KWA DHARAU, MKONONI ALISHIKA KOMBEO/SLINGSTONE, YAANI HATA HAYA MANATI TUNAYOWINDIA NDEGE, YANA UWEZO ZAIDI. ANAMWAMBIA YAANI WEWE LEO, NYAMA YAKO NTAWAPA NDEGEπππ, NA UKWELI WA ISAYA 41:12 TUNAUONA HAPA, ADUI MZOEFU WA VITA, ALITOLEWA KWENYE ROUND YA KWANZA KWA *T.K.O-Technical Knock Out*, KAJIWE KADOGO LAINI KAKAMWANGUSHA YULE JITU HATARI AMBAYE ALIKUWA NA VIUNGO ABNORMAL, NDIO MAANA HATA KAKAYE GOLIATH ANATAJWA KUWA NA VIDOLE 24. SASA AKAFANYWA KUWA KAMA KITU KISICHOKUWA, WHY? KWA KUWA ADUI SI KITU, UKIWA NA MUNGU. NDIVYO BWANA ATAKAVYOWATENDA ADUI ZAKO WOTE..WEWE CHAGUA TU KUWA UPANDE WA MUNGU, AMBAYE YEYE MWENYEWE ALISHACHAGUA KUWA UPANDE WETU BEFORE THE BEGINNING OF CREATION (RUMI 8:31)
Sasa huna haja ya kuhofia chochote....................mengine Roho wa Yesu akuongezee...
Mwl Proo
0762879363
All Truth Group
alltruth5ministries@gmail.com
No comments:
Post a Comment