Thursday, November 30, 2017

YESU KRISTO YUMO NDANI YENU, ISIPOKUWA MMEKATALIWA!

*YESU KRISTO YU NDANI YENU; ISIPOKUWA MMEKATALIWA!*

_*Mwl Proo*_
*0762879363*

Shalom Aleichem!✋🏾
Nilipoanza kutafakari tu, naandika nini, moyoni ukaja ujumbe kwa kasi ya ajabu. Nilipotafakari sehemu ya mambo yanayopaswa kuwemo, nikamwambia Bwana, _"Mbona hili jambo ni gumu😰!!"_. Lakini hii ni dawa ya kuponya. Wale ambao ni wa Mungu, wanakwenda kuponywa, hata kama walitanga-mbali (2Timothy 2:19). Leo pamoja na kuzungumza na Wakristo wasio wahudumu (Laities) lakini walengwa haswa ni wahudumu katika utumishi (Clergies).
Tunakutana na kauli moja ngumu hapa, tuisome kwa pamoja;

2 Wakorintho 13 : 5 *_Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa mmekataliwa._*

MANENO MAWILI YA MSINGI SANA, *JIJARIBUNI* NA *MMEKATALIWA*, NENO HILO JIJARIBUNI KATIKA BIBLIA YA KIEBRANIA KUMEANDIKWA _*BEDIKAH/BEDKOT*_ (בְּדִיקָה), AMBALO NI NENO MAALUM LA UCHUNGUZI WA UKE WA MWANAMKE KAMA KUNA DALILI YA DAMU YA SIKU ZAO (INTERNAL EXAMINATION OF VIGINAL CANAL). KWA MUJIBU WA MAFUNDISHO YA KIYAHUDI (JEWISH TALMUD) WALAWI 15:19-30, 18:19, 20:18) YENYE KUIFAFANUA TORATI, MWANAMKE ALIPASWA KUFANYA UCHUNGUZI/UKAGUZI SIKU SABA KABLA YA KUINGIA KATIKA _*NIDDAH (נִדָּה)/MENSTRUAL PERIOD/SIKU ZAO ZA HEDHI*_, NAYO ILIKUWA INAFANYIKA KWA UMAKINI MKUBWA, ILI KUEPUSHA UNAJISI NA KUTENGWA. MWANAMKE ALIPASWA KUNUNUA KITAMBAA MAALUMU CHEUPE (TAHARAH), AMBACHO ALIKITUMIA KWA NJIA YA VIDOLE, KUIKAGUA DAMU KWA NDANI SANA KABLA HAIJAONEKANA NJE. NA KILE KITAMBAA BAADA YA UKAGUZI KILIPELEKWA KWA RABI ILI AJIRIDHISHE. HAYA MAMBO NI KIVULI (EBRANIA 10:1, KOL 2:17) CHA UTAKATIFU (KEDUSHAH) WA KWELI WA SASA. MUNGU ALIKUWA ANAWAFUNDISHA USAFI WA KIMAHUSIANO/FAMILY PURITY _*(TAHARATH HAMISHPACHA/טהרת המשפחה )*_.
NENO LA PILI NI KUKATALIWA. NENO LILILOTUKIKA KUTAJA AINA YA KUKATALIWA HUKU NI *_REPROBATE_*, IKIWA NA MAANA YA KUWA *(DISAPPROVED BY GOD, BECAUSE YOU ARE DAMNED SINFUL)*, YAANI MUNGU ANAKUTAFAKARI NJIA ZAKO, THEN ANASEMA AAAH NO! 👐🏾WEWE HAPANA!!!!

Sasa kwa nini neno Bedikah limetumika, katika kuwataka watu wajijaribu/wajichunguze (examine)?. Ili kutia uzito, maana kuna uwezekano wa kukataliwa, hata kama ulikwisha itwa, usiwe mteule (Math 22:14). Paulo Mtume anatuonesha huo uwezekano;

1 Wakorintho 9 : 27 *_bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa._*

Pata picha namna ambavyo, wewe mtumishi unavyopiga kazi zito, saa nzingine unaletewa watu waliojengewa ngome nzito, deliverance zao zinakutoa jasho, washirika wanaondoka saa nane, wanakuacha upo mpaka saa kumi na mbili jioni, umekomaa na watu ambao, vifungo havifunguki kwa wepesi, koti la suti limeloa jasho kama umemwagiwa ndoo ya maji. Lakini eti siku ile, unamkumbusha Yesu, juu ya hizo kazi zote.. Naye anajibu......

Mathayo 7 : 23
*_Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu._*

Tena hatasema siwajui, bali sikuwajua; yaani mlikuwa mkiendelea na yote hayo ya huduma mkiwa mmekataliwa (hawajui).

Sikiliza mtumishi mwenzangu, huenda kuna wakati ulighafilika, ukajikwaa, ukaanguka labda katika uzinzi; the very day ulipoanguka, kabala hujaifikilia toba, ukaleta mgonjwa mwenye vifungo, ulipombandika mkono✋🏾, akafunguliwa mara moja. Ikakupumbaza, ukapotezea toba ya kweli (teshuvah), ukidhani may be God is just okey, with fornication. Kumbuka, miongoni mwa mambo yanasukuma kukataliwa, ni mrundikano wa dhambi zisizotubiwa *_(HAKIKISHA UNAPATA SOMO LANGU LIITWALO, "KUONDOLEWA KINARA")_*
Sasa kufunguliwa kwa wagonjwa na ile miujiza baada ya wewe kutoka katika hali ya usafi, haithibitishi kwamba uko 👍🏽na Mungu. Not all times ukianguka, Mungu atanyang'anya upako, No!. Baada ya anguko zito la Lusifa (Shetani kwa sasa), hakunyang'anywa nguvu kabisa, ingawa na aamini zililaaniwa maana aliji-disconnect na chanzo cha utukufu wote (Mungu). Sasa ndivyo ilivyo leo, tunao wahudumu wengi ambao walikwisha kataliwa, lakini wanaendelea zao na maombezi. Ile shwari waliyoipata baada ya kucheza rough (rafu) kiroho, iliwadanganya, Mungu hawezi ku-overlook dhambi, hajifanye hajaiona fulani hivi (Mdo 17:30), hayo aliyafanya zamani, sasa anawaamuru watu wote watubu *_(HAKIKISHA UNAPATA MASOMO YANGU HAYA MAWILI, ILI DOZI 💉💊IKAMILIKE 1.ASEMAYE KWELI KWA MOYO WAKE, NA LILE LA 2. SECOND CHANCE)_* Maana lengo ni kuponya na sio kuleta vitisho.

Hakuna hatari kama hii, yaani ulishawahi kuifahamu kweli, then ukaanguka mikononi mwa Mungu. Hilo ni jambo baya sana na uchungu

Waebrania 10 : 31
*_Ni jambo la kutisha kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hai._*

Yeremia 2 : 19
*_...ujue, basi, ukaone, ya kuwa ni jambo baya sana na uchungu, kuwa umemwacha Bwana, Mungu wako, na ya kuwa moyoni mwako hamna kunihofu, asema Bwana, Bwana wa majeshi._*

KUNA WATU WANAENDELEA NA HUDUMA, LAKINI KUNA WAKATI ALIMPA UJAUZITO BINTI WA KANISANI, AKATUBIA UZINZI, LAKINI ILI KULINDA HUDUMA ALIPOGUNDUA MIMBA ILIINGIA, AKAFANYA MAUJUZI WAITOE. SASA ANAENDELEA LAKINI YALE MAUAJI AMEYAFUKIA, KUMBE KUTOFANYA TOBA YA KWELI, KUKAFANYA BADO AWEKO HUKU NDANI, LAKINI KAKATALIWA. MWINGINE ALIMTENDA MAMBO YA HIANA MKE WA UJANA WAKE, MWINGINE AME-DIVORCE KWA SABABU FEKI FEKI, MARA NIMEFUNULIWA WEWE SIO MKE WANGU, MARA NILIWAHI KUKUFUMANIA (HAPO NAPO WAKRISTO TUMECHAKACHUA), YESU HAKUTOA SABABU YA KUMWACHA MKEO, KWA VIWANGO VYA UKRISTO, UNAWEZA MFUMANIA MMEO/MKEO KABISA KITANDANI NA MWANAMKE NA UKAAMUA BADO KUMSAMEHE. _*(HAKIKISHA UNAPATA SOMO LANGU LA NDOA YA KIKROSTO)*_, ILI MAMBO YAKAE SAWA HAPO.

*WITO WANGU KWA WATUMISHI WA MADHABAHU KAMA MIMI*
Badala ya kuendelea kuja kushtukizwa unaachwa, unayo nafasi JIJARIBU SASA (JIFANYIE BEDIKAH), VIPI HUJAKATALIWA? KUMBUKA DHAMBI HAISAMEHEWI KWA SABABU IMEPITA MIAKA SITA TANGU UIFANYE, BALI KWA TOBA YA KWELI (TESHUVAH), NA KAMA MTU HAJAFIKIA ILE LEVEL YA KUMKUFURU ROHO MTAKATIFU *_(ambako nimekufafanua katika lile somo la, "Mambo ya kiroho yakiharibika; Tengeneza")👈🏾Waweza jipatia hili somo katika mtandao_* BASI KAMA HUJAFIKIA HUKO, WAWEZA TUBU, UKAYATENGENEZA MAMBO YAKO. MAANA ULICHOFANYA KINASAMEHEKA, NA UKIISHASAMEHEWA NA KULIPA GHARAMA YA TOBA, BWANA MWENYEWE ATAKUTENGENEZEA MAMBO YAKO (2Nyakati 29:36).

*HITIMISHO*
*_```KAMA UNAHISI MOYONI MWAKO, MUNGU ALIKUWA ANASEMA NA WEWE, NA UNATAMANI KUYAWEKA MAMBO SAWA. TAFUTA SOMO LANGU LIITWALO, "KATIKA TOBA KUNA TUMAINI, HATA KAMA KOSA NI KUBWA MNO". LITAKUPA YAKUPASAYO UYAFANYE, NAWE UTAJIHAKIKISHIA UMILELE MZURI BAADA YA TAABU YA DUNIA HII, SIO UKAMALIZIA UMILELE WAKO KWENYE MOTO WA JEHANAMU🔥🔥.```_*

Mwl Proo
~*Mjumbe wa Matengenezo*~
0762879363 (whatsapp only)

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment