Thursday, November 9, 2017

ANITIMIZIAYE MAMBO YANGU

*ANITIMIZIAYE MAMBO YANGU*

Mwl Proo
0762879363(whatsapp#)

Ooh Haleluya Haleluya!

BILA SHAKA TUMEWAHI KUSIKIA NENO _*Godfather*_ ,NENO/JINA HILI HALINA UHUSIANO NA MUNGU BABA WA BWANA WETU YESU KRISTO,YAANI HII *_Godfather_* HAIMZUNGUMZII *GOD THE FATHER/FATHER-GOD* BADALA YAKE,JINA HILI LINAMZUNGUMZIA MTU FULANI HIVI MWENYE UWEZO WA KUKUTENGENEZEA MPANGO WAKO UTIKI✔,KWA MFANO UNA MJOMBAAKO AU YEYOTE AKUFAHAMUYE WIZARA YA FEDHA,AKAONA UMEMALIZA ZAKO SIJUI NI BBA-FINANCE  AKAKUCHONGEA DILI UPATE AJIRA(SHAVU) B.O.T(BENKI KUU), LABDA HUKUHITAJIKA,AU KULIKUWA NA WENYE QUALIFICATIONS NZURI KUKUZIDI ILA HUYO JAMAA YAKO KAWA _*Godfather*_ WAKO KUKUFANYIA MPANGO,NADHANI UMEPATA PICHA KAMILI YA HILI JAMBO. WATU WENGI WAMEKUWA NA *_Godfathers_* NA WAMEPATA KIBURI KWA SABABU AKIHITAJI MKOPO WA HESLB,AU AKIHITAJI KUPATA KIWANJA ENEO LA WAZI,AU AKIHITAJI PASSPORT,VISA,SCHOLARSHIP, ANAJUA ANAO WANAOMCHONGEA DILI NAYE HUWADHIHAKI WENGINEπŸ€”

LEO NAOMBA NIKUTAMBULISHE JAMBO LA MAANA SANA,ULIMWENGU HUU ULIOJAA KUPIGA MADILI TUU,ILI MAMBO YAKAE SAWA UNAMHITAJI MUNGU
Tusome:-

Zaburi 57 : 2 _*Nitamwita MUNGU Aliye juu, Mungu anitimiziaye mambo yangu.*_

Zaburi 138 : 8  _*Bwana atanitimilizia mambo yangu; Ee Bwana, fadhili zako ni za milele; Usiziache kazi za mikono yako.*_

YUKO MUNGU AMBAYE YEYE AKIKUCHONGEA MPANGO HAUKWAMI,MAANA YEYE HAKWAMI KAMWE. WALE WATU TUNAOWAWEKEA TUMAINI KWA SABABU YA VYEO,MUNGU ANAWAITA NI FIMBO YA MWANZI ULIOPONDEKA

πŸ‘‡πŸ½πŸ‘‡πŸ½

Isaya 36 : 6
_*Tazama, unaitumainia fimbo ya mwanzi huu uliopondeka, yaani, Misri, ambayo, mtu akitegemea juu yake, humwingia mkononi na kumchoma; ndivyo alivyo Farao, mfalme wa Misri, kwa wote wamtumainio.*_

SASA HIZI FIMBO ZA MWANZI ZILIZOPONDEKA _*(Godfathers)*_ AMBAZO WATU WANACHAGUA KUWAWEKEA TUMAINI,WENGI WAO NDIO WAMEUA HATA NDOTO KUBWA ZA KIMUNGU NDANI YA WATU. KWA KUWA WAO NI WANADAMU,WALIPONYOOSHA MIKONO YAO KUKUFANYIA MCHONGO(DILI) ILI UPITE KWENYE INTERVIEW KWA DILI,WAKAKUTAKA KIMWILI ILI WAKAMILISHE ULE MPANGO ULIOSALIA,NA KWA KUWA ULIKWISHA LOGWA NA PEPO LA UGODIFAZA HUKUKATAA UKAENDA KUIBANJUA AMRI YA MUNGU ILE ISEMAYO USIZINI *(Laa taazinu)*,  *_```NI ULIMWENGU HUU TU WA SIKU ZA MWISHO NDIO UNAOONA KUZINI IS CHEAPER THAN KAMSHAHARA KA LAKI 4```_* HATARI SANA,KILE UNACHOPOTEZA UNAPOZINI HAKIKARIBIANI THAMANI HATA KWA *0.000001%* NA UNACHOFAIDIKA NACHO,NDIO MAANA HUPASWI KUMWEKEA MWANADAMU TUMAINI
πŸ‘‡πŸ½πŸ‘‡πŸ½πŸ‘‡πŸ½

Mika 7 : 5  _*Msimwamini rafiki, msimwekee kiongozi tumaini; ilinde milango ya midomo ya kinywa chako ili mkeo alalaye kifuani mwako asijue habari.*_

MUNGU AKIKUFANYIA KAMPANGO KA KUKUPACHIKA MAHALI HATA KUCHANGANYIA NA HUZUNI KTK HIYO BARAKA (MITHALI 10:22) ,LAKINI YULE GODFATHER WAKO ALIKUFANYIA MPANGO UWE SEKRETARI KTK KAMPUNI KUBWA *_IN THE EXPENSE_* YA WEWE KUWA HAWARA(CONCUBINE) YAKE, HIYO NDIO HASARA KUU DUNIANI ITAKAYO KULETEA ILE HASARA YA NAFSI YAKO KWA ZAMA ZIJAZO

Zaburi 118 : 9 
*_Ni heri kumkimbilia Bwana. Kuliko kuwatumainia wakuu._*

JE HUKUJUA? HUKUSIKIA? KUWA MUNGU ANAO UWEZO WA KUFANYA UPATE HIYO AJIRA BILI WEWE KUFANYA NGONO? KUWA ZILE APPLICATIONS ZAKO ZA KAZI YUKO BWANA ANAYEHUSIKA NAZO AKUFIKISHE MAHALI PA MAPENZI YAKE MAKAMILIFU, IT HAS BEEN SAID, *_"GOD'S DELAY,IS NOT GOD'S DENIAL"._* TENA MUNGU HATA HAKAWII KIVILE (2PET 3:9) ,HUYU YEHOVA-YIRE UKIMTAMBUA KAMA BWANA MWENYE KUKUTIMIZIA(KUKUTENGENEZEA) MAMBO YAKO HUTAKAA KUCHAKACHUA MAANA YEYE NI LAZIMA TUU ATAKUTIMIZIA MAMBO YAKO UTAKAA UKIMNGOJA,MIONGONI MWA MAMBO YANATUNZA HALI NZURI YA KIROHO NI ILE UMEKAA MUDA WOTE UNAMTAZAMIA BWANA AFANYE JAMBO JIPYA (MIKA 7:7) HUTAKUWA RADHI KUCHAKACHUA. MKIBANDIKIWA TANGAZO OFISINI,KUWA TUPO KWENYE MPANGO WA KUPUNGUZA WAFANYAKAZI! YOU ARE NOT SHOCKED,ILA HIYO HOJA UNAIPELEKA KWA BWANA MKUBWA(YESU) UKIWA UNATABASAMU KWA MFANO WA HEZEKIA MFALME ALIYEIFUNUA ILE BARUA YA MATUKANO YA MFALME WA ASHURU SENAKERIBU NAWE VIVYO HIVYO UTAGONGANISHA MAMLAKA YA MUNGU NA YA OFISI,USHUHUDIE HIYO *_GAME_*, 

MNAKUMBUKA HABARI ZA RUTHU?  PATA NAFASI USOME RUTHU 2:5-23,HUU MCHONGO(DILI) ULIKUWA MONITORED NA MUNGU,NA HUYU BINTI WA KULA KWA KUOKOTA MASAZO YA BAADA YA MAVUNO AKABADILISHIWA FUNGU,AKARUHUSIWA AOKOTE KATI YA MIGANDA(MAZAO YASHAVUNWA YALE BORA YAKO PACKED) YEYE ANARUHUSIWA HATA HAYO NAYO ACHOMOE TUU NA BOSI MKUU BOAZI AKASEMA OLE WAKE MTU AMKATAZE. UNAMKUMBUKA YEHOYAKIMU??  (YER   52:31-34) GOD HIMSELF PIONEERED THE DEAL NA HIVYO ALIPATA KIBALI UTUMWANI ,BAADA YA MFALME EVIL-MERODAKI KUMTOA GEREZANI AKAANZA KUMLIPA ALLOWANCES ZISIZO HATA KWENYE BABYLONIAN SCHEME OF PENSION, ILI MRADI TU BWANA ABAKI KUWA NI MUNGU ATUTIMIZIAYE MAMBO YETU.
NILIPEWA USHUHUDA WA MFANYA BIASHARA AMBAYE UTAJIRI WAKE KILA BAADA YA MUDA INAMPASA AKAPIKIWE DAWA ZA KIGANGA KUYA-ACTIVATE MAJINI YA CHUMA ULETE ILI BIASHARA ZISIFE,SASA AKAONA MAMBO YANA-BANKRUPT HIVYO AKAWAHI KWA FUNDI(SANGOMA) HUKO BAGAMOYO LAKINI ALIPOFIKA KWENYE MAKAZI YA MGANGA BINGWA AKAKUTA UMATI WA WATU,WAKAMWAMBIA MGANGA AMEFARIKI NA LEO NI MAZISHI YAKE. ALIITUMAINIA FIMBO YA MWANZI ILIYOPONDEKA SASA SAA YAKE YA KUCHOMWAπŸ“ŒIMEFIKA. LAKINI HERI WALE WAMTUMAINIO BWANA,MUNGU SIO KAMA _*HUMAN-GODFATHERS*_ OUR GOD-JEHOVAH NEVER FAIL,MUDA WOTE INESHINDIKANA KUWAAMINI YEYE ANADUMU WA KUAMINIWA πŸ’―✔ HALELUYA

2 Timotheo 2 : 13  _*Kama sisi hatuamini, yeye hudumu wa kuaminiwa. Kwa maana hawezi kujikana mwenyewe.*_

INUKA SASA MTAZAME MUNGU BABA WA MIANGA,KILA KITU CHEMA UNACHOKIHITAJI CHATOKA KWAKE YEYE ASIYE BADILIKA,KWAKE HAKUNA KIVULI CHA KUGEUKAGEUKA (YAKOB 1:17,MAL 3:6) KAMA KUNA KAZI INASIMAMA KAMA KWAZO KTK UHUSIANO WAKO NA MUNGU TUPA KULEπŸ‘‰πŸΎπŸ‘‰πŸΎπŸ‘‰πŸΎπŸ‘‰πŸΎπŸ‘‰πŸΎπŸ‘‰πŸΎ,KAMA NI MAHUSIANO(MCHUMBA) ANAKUWA KUWA KWAZO LA MAISHA YAKO YA KIROHO MWAMBIE PITA KULE πŸ‘‰πŸΎπŸ‘‰πŸΎπŸ‘‰πŸΎπŸ‘‰πŸΎπŸ‘‰πŸΎπŸ‘‰πŸΎπŸ‘‰πŸΎ

HAPA DUNIANI WALA MBINGUNI HAKUNA CHA KUPENDEZA ILA KUWA NA MUNGU,NA UWE NA UHUSIANO MZURI (ZABURI 73:25),KUSIWE NA KITU CHOCHOTE CHA KUKUTENGA NA UPENDO WAKE(RUMI 8:35) ALWAYS STAY TUNED,STAY CONNECTED MAANA YUKO MUNGU ATAKAYE KUTIMIZIA MAMBO YAKO.

Nimemaliza kwa leo.πŸ€—

Mwl Proo
0762879363

alltruth5ministries@gmail.com

No comments:

Post a Comment